Si zamani sana 2018-2022, mji ule ni mdogo na haujachangamka ukitembea kutoka pale NMB mpaka stendi ya zamani mji umeisha, sehemu za starehe ni chache kuna La chalz, nyuma yake kuna Lamori pamoja na Serengeti mji mzima. Kuna wakati nilikuwa nakuja mpaka Madaba. Ukiwauliza watu wa Madaba wana prefer zaidi kwenda Njombe kuliko Songea. Wanasema Njombe iko vizuri kwenye biashara wengine walikuwa wanaenda mpaka Makambako. Bei Makambako na Njombe zipo chini ukilinganisha na Songea na bidhaa nyingi zaidi zinapatikana sehemu hizo kuliko Songea.
Wenye maduka yao pale Madaba walikuwa wanaenda Njombe na Makambako kufanya manunuzi.
Hotel nzuri Njombe ni nyingi kuliko Songea.