Hii nchi vivutio vipo vingi sana ila siku wakiacha mambo ya kuangalia Jiji moja tu bas tutafika mbali sana lakin haya mambo ya Kila kitu dar ni upuuzi mtupu
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAOFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAAHALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO
Toggle navigation
Kituo kikubwa cha ukaguzi wa magari kujengwa katika Halmashauri ya Mji Makambako
Tarehe Iliyowekwa: August 11th, 2022
Na. Lina Sanga
Kituo kikubwa cha ukaguzi wa magari kinatarajiwa kujengwa katika Halmashauri ya Mji Makambako,kitachotumika kufanya ukaguzi wa magari yote yanayoelekea mbeya na Songea.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mhe. Makame Mbalawa alipokuwa akitoa salamu kwa wakazi wa Halmashauri ya Mji Makambako leo,waliofika kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Mbalawa amesema kuwa eneo la ujenzi wa kituo hicho lenye ukubwa wa hekta 200 limechukuliwa na jumla ya mil. 870 zimelipwa fidia kwa wamiliki wa maeneo hayo na mil. 2.9 Wizara inajipanga kuwalipa wamiliki walio baki.
Ametoa wito kwa wamiliki wa maeneo hayo ambayo yamechukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho,wanaostahili kulipwa fidia kwa mujibu wa sheria watalipwa kwani fedha zao zipo hawatadhulumiwa.
Ameongeza kuwa jumla jumla ya bil. 2.2 zimetolewa kwa ajili ya matengenezo ya barabara za mjini na Serikali itaendelea kuleta fedha hizo kadri inavyowezekana ili Mji wa Makambako uondokane na Vumbi kwa kujenga barabara za lami.
Video
TEHAMA ni Msingi wa Taifa Endelevu, Tuitumie kwa Usahihi na Uwajibikaji . Makambako TC, 2021
Makambako Town Council Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako Simu ya mezani: 026-2730044 Simu ya Kiganjani: 0785635383 Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAOFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAAHALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO
Toggle navigation
Wananchi 18 eneo la soko la kimataifa Makambako,kufanyiwa uthamini kwa ajili ya malipo ya fidia.
Tarehe Iliyowekwa: January 5th, 2023 Na. Lina Sanga
Njombe
Tamko hilo limetolewa leo na Waziri wa Uwekezaji,Biashara na Viwanda, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji katika mkutano wa saba wa baraza la biashara, Mkoa wa Njombe lililofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe , na kuwakutanisha wafanyabiashara wote wa Mkoa wa Njombe ili kusikiliza na kujadili changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
Mhe. Kijaji amesema kuwa Wananchi hao ambao hawakufanyiwa uthamini wa maeneo yao wakati wa uthaminishaji wa awali na kushindwa kulipwa fidia ya maeneo yao , Wizara imeanza kufanyia kazi suala hilo ili kumalizana na wananchi hao , ili pindi wadau wa kujenga soko hilo watakapo patikana ujenzi uanze mara moja bila kikwazo chochote.
Amesema kuwa endapo ujenzi wa soko hilo la Kimataifa na bandari kavu katika Halmashauri ya Mji Makambako ukikamilika,utasaidia kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa katika Mkoa wa Njombe na wananchi wataweza kunufaika na kujipatia maendeleo.
Ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya nchini kusimamia Sekta binafsi katika maeneo yao na kuzilea ili zikue na kutokuwa kikwazo katika ukuaji wa Sekta hizo ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Samia Suluhu Hassan kwani Sekta binafsi ndizo zimebeba uchumi wa taifa.
Video
TEHAMA ni Msingi wa Taifa Endelevu, Tuitumie kwa Usahihi na Uwajibikaji . Makambako TC, 2021
Makambako Town Council Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako Simu ya mezani: 026-2730044 Simu ya Kiganjani: 0785635383 Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.