Hamna kitu kama hicho kaka ...bukoba haiwezi jengewa international airport.sana sana wanahamisha hii iliyopo kwenda kujenga Mpya ... international airport haiwezi jengwa Kila mkoa .Kuna factor muhimu za kujengewa international airport.idadi ya abiria,pamoja na mizigo,.au sababu za kiserikali(msalato airport). mwanza tayari ishafikia vigezo hivi .. haiwezekani Mwanza wawe na international airport,na bukoba pia wawe na international airport....
Kitu kingine maendeleo ya mji hayaletwi na uwanja wa ndege tu ..kama ingekuwa hvyo kiwanja Cha ndege Cha iringa Yale maeneo ya nduli pangekuwa bonge la mji ..au uwanja wa KIA maeneo ya pale hai ingekuwa bonge la mji
Mzee hebu jaribu kufikiria vzr..faida za airport ya kimataifa na faida ya stendi ya mabasi.
Hebu tuangalie stendi za mabasi mpya Tanzania na mafanikio yake..hiv kweli zinawanufaisha wananchi kwa ukubwa unaotakiwa?hiv hiz stendi kibaha, korogwe, njombe, kigoma, singida, dodoma, bariadi, tanga, songea nk zote si mpya na zimejengwa kwa mabillion ya shillings..vip hiz halmashauri zimeweza hadi sasa kufaidisha at least asilimia 50 ya wakazi wa mji huo?
Kuwa na Airports kubwa sehemu moja si big issue sana.....issue ni mipango na mikakati...
Wakulima wa kahawa, maua, na mazao yanayokuwa exported yanatumia uwanja wa KIA kwenda moja kwa moja nje...
Ukijegww uwanja mkubwa omkajunguti sio tu utawanufaisha wasafiri bali hata wakulima kadhaa wa mkoa wa kagera na mikoa jirani...
Kajunguti ilikuwa suala la muda ...maana plan yake ilikuwepo toka 1996 huko...na juzi wameanza tena kurudisha mpango wa kuwalipa fidia wakazi wa eneo hilo waondoke....it means airport itajengwa tu
Kuwa na stendi nzr na ya kuvutia hakukunufishi wew mkulima wa pamba mkoani kwako...lakin international airport inaweza kuwa msaada kwako na mazao yako...
NB...Airport ni jina tu...sio big deal kwamba serikali inashindwa kujenga kila mahali..ni runway tu na technology tu ya kutua ndege ndo inayohitajika....
Halafu hawajengi airport ili baadae pazungukwe na mji...tena Airport inabidi ziwe mbali na makazi ya watu kabisa..just why maeneo ya airport hayapaswi kukua miji mikubwa...