Write your reply...Aisee kwa kasi ya sasa ya mabadiliko katika mji wa shinyanga hakika mji utakua mbali sana ndani ya miaka mitatu.Baadhi ya miradi inayoendelea ni ujenzi wa kisasa wa stendi za mabasi madogo,bajaji nakupumzikia katika maeneo ya kalogho,soko kuu,kambarage,mataa,lubaga sokoni nk.ujenzi wa soko kuu,soko la kisasa kambarage na ngokolo mitumbani,ujenzi shopping mall eneo la mazingira center,soko la machinga eneo jiran na ccm wilaya,stendi ya mkoa ibadakuli,maegesho ya maloli trm jirani na veta,ujenzi wa ukumbi wa mikutano wakimataifa,ujenzi wa mahoteli mbalimbali maeneo ya lubaga,majengo mapya,bushushu na butengwa bila kusahu hoteli ya nyota 5 inayojengwa sambamba na uwanja wa mpira na michezo wakisasa vya fresho.Bila kusahau ujenzi wa uwanja wa ndege mkubwa.Vyuo vinavyopandishwa kua vyuo vikuu ni chuo cha biashara na ushirika kizumbi{muccobs kizumbi campus}na chuo cha afya kolandoto nk.miradi ni mingi sana na imeshaanza kujengwa,kwa aliepita shinyanga hivi karibuni ameona mabadiliko makubwa.