Zaidi ya kilimo kaka njombe kuna uwekezaji upi mpya na kumbuka Bei ya mazao inapanda na kushuka na uwekezaji wa viwanda vingi makambako huo ndo utaongeza maradufu hayo mapato unayo yaona na kupitia hayo mapato madogo tayari wamelipa eneo fidia ya kujenga stendi kubwa ya mabasi pale kipagamo na zoezi la ujenzi mkandarasi anaanza mwez wa saba na kumaliza mwez wa 12 kitu tayar serikali kuu Sasa imelipa fidia eneo la ujenzi one stop centre pale idofi jilan na mpaka wa mkoa wa iringa na njombe pia imelipa fidia eneo la ujenzi soko la kimataifa pale mashujaa wamebaki watu kumi na tano kumaliziwa kazi iendelee na pia kuna ujenzi wa kiwanda cha madawa chini ya msd kwaajili ya ku supply nchi za SADC kazi bado inaendelea pale idofi ,kiwanda cha kusindika nyama pale kihanga wanamalizia kufunga mitambo ,ujenzi wa soko kubwa la mazao pale kiumba inaendelea hiyo ni baadhi tu ya miradi ya serikali ambayo inaendelea kutekelezwa ndani ya halmashaur ya mji wa makambako na ya watu binafsi na makampuni hiyo tumeiweka kando kidogo maana ni mingi mno muda unaongea
Ni kweli kabisa hayo unayosema na jiografia ya Makambako ina support viwanda kwa sababu ni tambarare na iko junction.
Sasa baba unatakiwa ujue kwamba roho ya Mkoa na Mji wa Njombe ni kilimo anuwai na licha ya kuwa Mazao kuwa na ups and downs Kwenye bei ukweli unabakia pale pale kwamba wakulima wa Mazao wanapata kipato kikubwa kuliko vibarua wa viwandani.
Pili kiwanda kinaweza kuwa 1 kikalipa pesa moja tuu kwa mwaka.ya ushuru lakini Mazao ya kilimo na misitu ni mwaka mzima.Pili kilimo cha Njombe sio sawa na.Sumbawanga kwamba watu wanategemea kudra za Mungu.
Mkoa wa Njombe una watu wenye pesa naaggressive wa biashara na kilimo Chao ni kilimo cha kisasa kwa hiyo quality ya Mazao itaamua bei na kuzuia bei isiporomoke zaidi.
Makambako hadi mje kufikia mapato ya Njombe ni miaka mingi Sana ijayo,Kumbuka Njombe imetoka chini around 2.5 bln(2015) hadi kuwapita Tunduma,Mafinga (2019) na kwa mwaka huu (2020/21) biashara zimefunguka utaona mwenyewe mkuu,7bln zote zinaenda kutumika kwa wananchi wa Njombe TC.
Na uhakika by 2025 Njombe itafikisha mapato ya ndani 10 bln maana ndio kwanza take off ya investments ya Mazao ya Kilimo hasa parachichi,ufugaji wa kisasa na Vannila bado,na kufungua miundombinu kufungua miundombinu ya barabara inayoendelea aisee mambo yatanoga Sana.
Hapa kila mtu ashinde mechi zake mkuu.