Kagoda Agriculture Ltd: Another BOT scandal


Dr. Slaa,

Kwa nini mapaka sasa hivi hamjafanya maandamano nchi nzima kupinga huu uhalifu unaofanywa na Serikali na CCM? Je, mtaungana na CUF kwenye maandamano waliyopanga, na pengine mtoe hotuba?

Tatizo nini? Mbona wafadhili wengi wako tayari kuwasaidieni.
 
Ningekuwa na uwezo ningekwenda niwaombe madaktari wapime Ubongo wa viongozi wa CCM,usikute hamna kitu.Tukawa tunawalaumu bure.
...Teh! teh! tehhhhhh!! Malila, sisi tunawaita Hamnazo hawa"
 


Mara Manji, mara Rostam sasa mtatupoteza kabisa maboya. Serikali na iseme sasa au ikae kimya milele kwani kama tume imeundwa kama uchunguzi umefanyika, kama ripoti imetolewa sasa kwa nini inatuweka kiaina namna hii.

Ungozi wa nchi uangalie sana nyakati. Hizi ni nyakati ambazo watu walio wengi wanathamini sana manufaa ya jumla na sii binafsi na nyakati hizi wameongeza uelewa. Wanajua udanganyifu na hata usanii katika maswala nyeti ya nchi. Pls pls jamani viongozi fanyeni maamuzi sahihi muda muafaka wananchi wanavunjika moyo sana huku chini.
 
Mkuu Dr Slaa, Nikushukuru kwa namna ya kipekee kabisa ktk kuwatetea, kuwahurumia na pia kuwaelimisha Watanzania... Mungu akulinde na abariki kazi za mikono yako till the end of time inshaallah.
Mahali ambapo nchi yetu imefikia ni patamu sana na inahitajika force kubwa zaidi kuweza ku-break-even! ama kwa hakika wapambanaji mmefanyakazi kubwa sana!... mchango wangu mdogo sana ni kwa wana JF wote wenye uwezo wa kuchapisha na kusambaza leaflets zenye kueleza uozo wa ufisadi uliotopea wa viongozi na mafisadi wote na kusambaza ktk kila pembe ya jamhuri yetu hii yenye utajiri lukuki ilihali tu- masikini fukara wa kunuka...
Nina uhakika vijarida vikisambazwa kwa wingi hadi shule za chekechea, pasi na shaka watanzania wataamka kutoka ktk usingizi mzito wa unyonge waliopuliziwa miaka lukuki...
 

MiratKad,

Naomba unieleweshe. Hao wafadhili wengi ni wakinanani?
 

Dr.W.Slaa nashkuru kwa mchango wako..ni vema pia ukaweka wazi iman yako juu ya vyama unavyohisi ni Pandikizi..."Kuuficha ni sehem ya ufisadi"..kwani watanzania wanatakiwa wajue ni chama gani ktk vyama Upinzani ni Dodoki au Pandikizi....Uvijataje hivi vyama kama ulivyotaja list ya Mafisadi...ili Watz wajue Moja...Bahati mbaya kila ukikutana na Mpinzani au kiongozi wa Upinzani anasema maneno hayohayo...
 
Hivi hawa wahindi mbona katika kila ufisadi wapo,hawafikishwi mahakamani wanalindwa na viongozi wa chama na serekali kwa kutumia kodi zetu.Hii maana yake nini !.
Ukugusa EPA,Radar,Richmond ni wahindi wametamalaki.

Tusitafute visingizio. Ni "wamatumbi" wenzetu ndio ambao wanafungua milango yote hiyo. Walaumiwe wanaowalinda.
 
Hivi nani alituchagulia jina TANGANYIKA na ni nini maana yake? Inawezekana tumelaanika kuanzia jina hadi matendo...! TANGANYIKA = DANGANYIKA.
 
MiratKad,

Naomba unieleweshe. Hao wafadhili wengi ni wakinanani?

Wapo watu ambao hata si wabongo lakini wanahuzunishwa na tabia za wazi za viongozi wa serikali ambao ni wahuni wakisiasa. Wangependa kusaidia lakini wanashindwa pa kuanzia na wanataka wananchi wenyewe waanze na watake mabadiliko kwa vitendo.

Ndio maana nikauliza tatizo haswa ni nini?? Kwa nini wameshindwa hata kuandaa maandamano ya Kupinga vitendo hivyo vya wizi na uhalifu wa wazi?

.........Kwa hisani ya Ole L, (Kutoka T Daima).....

Maandamano haya ni nyeti na kila Mtanzania anayeipenda nchi yetu anatakiwa atoe mchango wake wa kuandamana.Hakuna aliyeambiwa atoe pesa zake.Fungeni biashara kwa masaa mawili kudai haki zenu. Kufunga biashara kwa lisaa limoja mawili haisababishi wewe kulala njaa lakini ukiwapuuza viongozi wenye kuipenda nchi yako usijekushangaa siku moja unachapwa bakora ndio upate huduma.Ninachoomba tu haya maandamano yasiitwe ya CUF kwa vile kuna migogoro mingo inayohusisha uongozi wa nchi hii na chama cha CUF.Utashangaa watabadili kuyaita maandamano ya kupindua nchi. Mimi nawajuwa viongozi wa CCM na Serekali hii ya Tanzania ni watu wa hila.Wameiga tabia za Wazungu wao waliowawekeza.Wazungu ni watu wa hila na wameshawaambukiza kina Makamba hadi hawakumbuki hata wananchi waliowapatia kura kule mbalamo.Mimi sikuamini kuwa Mwalimu akifariki ndio tutafanyiwa mambo ya aibu namna hii.Nashauri kila Mtanzania awe mtoto wa Shule,Mfanyakazi wa Serekali,Mkulima,Mchimba madini,Muongoza watalii,Taxi dereva,Mchuuzi wa soko,muuza nyama,Dereva wa mabasi ya abiria atoke kushiriki maandamano.Kila mtu na bango lake.
Mfano mabango yaandikwe hivi.
1.WATOTO WA SHULE - Fedha za mafisadi zimerudisha elimu nyuma.
2.WAKULIMA - Fedha za mafisadi zimepandisha bei za pembejeo.
3.MADINI - Fedha za mafisadi zimemaliza madini yetu bila tija.
4.WAONGOZA WATALII - Fedha za mafisadi zinamaliza wanyama pori wetu bila faida.
5.WACHUUZI SOKONI - Fedha za mafisadi zimetuulia biashara ya ndani.
6.MADEREVA - Fedha za mafisadi zimepandisha bei za nauli.
7.WAFANYAKAZI - Fedha za mafisadi zimepunguza ari ya utumishi kazini.nk
 
Toka vita vikali vya Richimonduli vilipofikia kumpumzisha Waziri Mkuu Lowassa, kulikuwa na swali kubwa sana of what Rostam played, Rostam alijua kuwa baada ya Lowassa pressure itakuwa kwake, kwa hiyo alichofanya ni kuyahamisha makampuni yake yote kwenye mikono ya Manji ambaye ni patner wake sana in crime,

Baaada ya kumaliza uhamishaji ndio akaanza kupiga makelele kuwa yuko clean, na mpaka akamtwanga Mtikila na akajaribu kila njia kumpaka Spika, na moja ya mashirika yake Rostam aliyompa Manji ni Kagoda, na pia hata Ze-Comedy walinunua pamoja kumzuia Mengi na makali ya Ze - Comedy na mafisadi.
 
vyama pandikizii alivyosema dr slaa ni kama ifuatavyo


1. NCCR MAGEUZI YA JAMES MBATIA NA AKINA SUNGURA

2. KILE CHAMA CHA MTU ANAITWA PAUL KYARA

3.
4.
5
PIA KUNA NGO FEKI NA PANDIKIZI KAMA

1. CEGODETA LILE LA THOMAS NGAWAIYA LA KUJIKOMBA KWA CCM
2.
3

ENDELEA KUJAZA LIST
 
Gazeti la Mwanahalisi la leo limeandika habari inayomhusisha RA na fedha nyingine za EPA kiasi kwa kutumia majina ya wafanyakazi wake. Kampuni iliyotumika ya Afritainer inatumia contact sawa na Kagoda na hiyo ndio inamuunganisha RA moja kwa moja na Kagoda.
 

Attachments

  • RostamTena.jpg
    37.1 KB · Views: 278
Last edited by a moderator:
JK anasubiri Yesu aje amuhakikishie kuwa RA ni fisadi.

Yebo Yebo,

JK anajua kwamba RA kachota hizo pesa maana ilikuwa mipango yao wote. Labda alichozidiwa JK ni kwamba RA alichota nyingi zaidi na kuziingiza kwenye biashara zake na kuwagawia chache CCM.

Mimi niko convinced JK anajua hilo suala ndani mpaka nje. Huu ni ujambazi wa mchana
uliofanywa na CCM na serikali yao. Kilichofanyika ni sawa na baba kuiba uji wa mtoto wake, hivi kweli hii mijitu ina akili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…