Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,818
- 11,993
Shule ya Singi Keza Wilayani Ngara, hatihati kufungwa kwa Ukosefu wa Vyoo unaopelekea mazingira ya shule kuwa Magumu Kufundisha na kujifunzia.
Mbunge wa Jimbo la Ngara Ndaisaba George Ruhoro, ametoa Mil 3 kutengeneza vyoo vya dharura ili Shule isifungwe. Ruhoro amesema shule ni ya miaka mingi kwani imejengwa kipindi cha vita ya pili ya Dunia hivyo imechoka inahitaji ukarabati mkubwa sio wa vyoo tu.
==========
KAGERA: SHULE YA MSINGI HAINA VYOO
Wanafunzi na Walimu wa Shule ya Msingi Keza iliyopo Wilayani Ngara wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa kutokana na uhaba wa huduma hizo.
Baada ya kipande cha video kusambaa mitandaoni ikiwaonesha Wanafunzi na Walimu wakilalamikia hali ya shule hiyo, Mbunge wa Jimbo la Ngara, Ndaisaba George Ruhoro amesema “Nilifika shuleni nikatoa Tsh. Milioni 3 ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo ambayo ilitolewa kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya dharura na Ths. Milioni 15 ya vyanzo vya ndani vya Halmashauri.”
Ameongeza kuwa tayari ujenzi unaendelea na kuongeza “Shule ya Keza ilijengwa Mwaka 1945 wakati wa Vita vya Dunia, miundombinu inatakiwa kufanyiwa maboresho.”