Kagame tells Kikwete "I will hit you......"

Kagame tells Kikwete "I will hit you......"

Status
Not open for further replies.
vita ya nini? Kagame hawezi kuanzisha vita hata siku moja, is he that suicidal? JK nae aache ku-seek cheap populairity kwa kujifanya anawashauri majirani, waache? Ndo maana Obama, na miguvu yake na ukubwa wa nchi yake alikataa kutaja nchi kwa majina. Na akasema wanaofanya makosa waadhibiwe (FDLR). Sasa JK anaandikiwa ma speech na anasoma eti anawashauri watu, mbona UN haijawahi kuiambia Rwanda ikapatane na FDLR? We have to respect sensitivity of other countries.But this is a minor issue, why blahallo! Alafu Kagame na ka nchi kake, na vulnerability ya ukabila aliaanzishe na Tanzania, atakuwa anaumwa!
Tatizo langu inawezekana hii issue hatuijua kiundani sana sisi JK ndiye anayejua na ndio maana hajibu. Kama amiri jeshoi mkuu alipaswa kumjibu kagame yeye na sio sisi, tulitakiwa tumwambie amjibu. Nina wasi wasi tunapopaona sio penyewe issue inawezekana ilianza zamani na itelejensia zao hawa watu wawili
 
Dah, mbona hueleweki sasa, msimamo wako ni upi? Mimi nafikiri simplemind yupo sawa kwamba wananchi hivi sasa wamepoteza imani na majeshi yetu. Badala ya majeshi kuendelea kuwa rafiki wa watu, ndiyo hayo yanatumika hivi sasa kupiga na kuumza watu huko Mtwara na hata Arusha. Hivi ikianza vita, wananchi hawatawaunga mkono maadui kama walivyofanya waganda wakati wa vita na Tanzania? Mimi naunga mkono wazo la kwamba huu si wakati muafaka kufikiria vita. Maana huo uzalendo tunaotaka wananchi waonyeshe ndiyo huo unadhulumiwa na serikali. Kwa hakika usitegemee wananchi wa Arusha wanaopigwa mabomu na polisi watakuwa upande wa polisi. Definitely watawasupport maadui. Lets not even dream about war kwa sasa.
Kaa chini!
 
Hivi ile ishu ya Malawi imeishia wapi??

Noma ni pale mtakapolianzisha na Kagame yule Mama analianzisha kule chini, can we fight in two fronts?? Intelijensia wetu akina Rama Ighondu watatujuza...
 
Kwani tatizo ni nini hapa? Sipendi uongozi wa Jakaya kwa vipindi vyote akiwa madarakani kama Rais wa Tanzania. lakini, kutukanwa na kanchi kadogo kama Rwanda is disgusting!! Kisa Jakaya ametaka peace talks and negotiations kwa nchi zile zilizo katika vita ndani ya maziwa makuu.

Jeuri ya kagame ya kupigana vita vya mstuni, anataka kutuletea sie? Hii haikubaliki hata kidogo...

Israel,UK,Qatar, Netherlands, sweden, norways etc ....ni vinchi vidogo sana ila mziki wake unajulikana duniani...Hembu tengua kauli yako y audogo wa nchi.
 
The problem with Kagame is his failure to see the final score..He might inflict great damages to Tanzania but Rwanda would be wiped out km UN hawatawahia piga Kipenga km ile vita ya Israel na Hizbolah.
 
Hee jamani punguzeni hasira .....relax, relax na hizi habari za vita wengine tuko huku Benaco-Ngara sasa mnatuathiri kisaikolojia maana vita havina macho eti.
 
Intelligence war! Kijana acha kupiga mayowe watayaona wenyewe!!
 
Look at this fool.Ajaribu aone jinsi watanzania tutakavyoungana kumfunza adabu and dump him huko lake Tanganyika.Na sisi tumekua wapole mno maana mimi ningemuonyesha cha moto.Hakuna cha intetnational community!

Ben nakuheshimu sana tena ni kamanda mzuri; Lakini unaijua team yako ya ushindi kwa undani? Je unamjua kwa undani huyo unaemwita Fool?
au kwakuwa tuna eneo kubwa kuliko Rwanda na yamkini tunajeshi kubwa kuliko yeye? au tunajiamini sana na kuwa na hamu ya vita kwasababu ya kuwa na mapumziko ya muda mrefu bila kujipima?
 
i think this idiot general is dreaming
 
Rwanda ni nchi huru kama ilivyo Tanzania na wana haki zote za kumaliza shida zao bila kuingiliwa na taifa linguine lolote nje yao,hivyo wanaona ni dhihaka kuzungumza na adui yao na wana haki pia ya kukutaa ushauri wowote sawa sawa na kuunganisha ndoa usiyo ijuakwa undani kwani siri inaendelea kubaki ndani ya nyumba husika na anaweza kutoka mmoja wao kati ya wanandoa akapakaza mbaya kwa mwenza kama huna busara uta conclude. Mwacheni Kagame na nchi yake ila akithubutu sasa kuvamia hapo ndipo tumwoshe kuwa sisi ni nani
 
I beg to differ with most members.
Naona wengi wamekimbilia kusema Rwanda ipigwe...well, ni alama nzuri ya uzalendo!
Najua wengi wetu tunapima uwezo wa jeshi letu kwa reference ya vita ya Uganda ya 1978/79!
Naomba niwajuze kwamba kushinda vita ni function ya ushirikiano kati ya jeshi na raia.
Jeshi parse haliwezi kuperform kwa ufanisi wa 90% bila back up ya raia.

Tukumbuke enzi ya nduli vijana mitaani walikuwa wanajitolea kwa kupiga training ya mgambo ya wiki mbili then wanaenda front-line huku wakiwa na ari ya juu sana, wakitamani kufika kwa adui na kuanza vitendo.

Pia tujikumbushe enzi hizo raia kwa kupitia vijiji vya Ujamaa vya wakati huo walikuwa wanachangia ng'ombe, mbuzi mahindi na vyakula vingine viende MSITARI WA MBELE , na matendo hayo yalikuwa yanafanywa kwa uzalendo usio hata na chembe ya shaka.

Turudi zama hizi basi, na tujiulize maswali yafuatayo:

-Je mambo yaliyofanyika wakati ule kama yalivyosemwa hapo juu yanawezekana kwa sasa?

-Je kuna uwezekano wa vijana wetu kujitoa na kwenda mgambo na kusonga msitari wa mbele kwaajili ya mapenzi na nchi yao?

.-Je kuna uwezekano mkubwa wa raia kutoa akiba zao za mahindi (kama at all zipo), kwaajili ya kuuwezesha msitari wa mbele?

-Je kwa hali ya mahusiano yaliyopo sasa kati ya majeshi yetu na raia, tutegemee mutual support ambayo ni reliable?

-That rope which was once holding us together is like no longer existing.

-Kwa enzi hizi kuna Watanzania wenzetu wanaitwa MAGAIDI...are we still one under the umbrella of Tanzania?

-Nijuavyo mimi kutokana na maadili kupungua sn nchini(toka kwa viongozi hadi kwenye vyombo vya usalama) kuna hatari ya loophole ya vita kutumika kinyume na matarajio, aidha kwa baadhi ya viongozi au wanajeshi kutaka kujitajirisha kwa kufanya looting ya mali za umma na kuzificha kusikojulikana-this is serious!

Tunaposhabikia vita tuapply na 3rd dimension ya tendo hilo.
Nothing is the same in our country!
 
Hakika Leo mimeamini Beni saanane wewe ni mzalendo,kuanzia Leo naahidi kukuheshimu sana!you are great my bro,Kagame na apigwe tuuuu!

jamaa kumbe ni mzalendo bana,mengine haya ya siasa za humu tukiweka kando...
 
Kwa kweli hii haivumiliki ni lazima Wizara ya mambo ya nje itoe kauli kwa kudhalilishwa kwa kiti cha urais wa JMT...
Hawa Wanyarandwa tuliwahifadhi wakati wa machafuko halafu leo hii Kagame analeta utoto....ni utoto kwa sababu jambo aliloshauriwa ni la AMANI wala si la shari....

Muda ukifika JWTZ itarudisha heshima tunayostahili maana nafikiri majirani zetu wamesahau mabavu yetu
 
kwahyo na wewe unaamini jk kakosea kutoa ushauri?kwani wewe m2 akikushaur jambo huwa unagombana nae?
Hili liwe fundisho JK usiwe
unaandikiwa kila kitu, wewe huwa unasema akili ya kwaambiwa changanya
na yako. we kila unachoambiwa na kuandikiwa unakubali tu, Hongera sana
Kagame.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom