Mbunge David Kafulila amemjia juu Waziri Mkuu Pinda Bungeni hivi sasa akimtuhumu kuwa ndio mzigo namba moja katika Serikali ya JK! Amesema mawaziri kadhaa wametajwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuwa ni mizigo serikalini, lakini ukweli ni kwamba mzigo unaanzia kwa Waziri Mkuu kwa kuwa hachukua hatua panappohitajika, haheshimiwi na wala haogopwi na mawaziri na watumishi wa ngazi za utendaji! Akasema endapo Waziri Mkuu haheshimiwi basi ni bora aogopwe ili mambo yaende!!