Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
Mchambuzi, mwenyekiti, Katibu Mkuu, mjumbe wa secretariat wakiyasema hayo, ni nani anapaswa kubadilika katika chama? Au kwa lugha ingine ni nani anayearibu katika chama?
Always, tatizo la chama cha siasa huwa haliwi wanachama bali ni huwa ni viongozi; CCM isn't spared na ukweli huu - uongozi wa chama ni tatizo kubwa sana kwani chama kinaendeshwa na personalities za viongozi, sio kwa kuendana na values zilizopo kitaasisi. Ndio maana Kinana performs better than makamba or mukama; kolimba was better than the rest, nyerere was better than the rest katika nafasi ya uenyekiti, n.k, n.k. Ufanisi ccm utaboreshwa kwanza kwa ku decentralize decision making za chama ngazi za chini. Pili, kwa kutenganisha kofia ya mwenyekiti na rais huku mwenyekiti akizuia na katiba ya chama kutogombea urais akiwa katika uenyekiti na kwa miaka mitano baada ya kumaliza muda wake wa uenyekiti, na uchaguzi wa mwenyekiti uwe wazi na wa ki demokrasia kila baada ya miaka mitano. Kwa mtazamo wangu, kutenganisha kofia ya urais na uenyekiti kwa maelezo hayo juu huku pia decentralization in decision making ikishuka chini, tutaondokana na tatizo alilosema mwalimu kwamba kutenganisha kofia hizi ni kutayumbisha nchi. Kwa hoja ya Mwalimu, then kuvitenganisha ni "desirable" but not "preferable". It will only be preferable ikiwa mabadiliko niliyojadili hapo juu, in my humble view, yatatokea.
Lakini swali lako linanipa swali kwamba - nani yupo karibu kikazi na hawa mawaziri kuweza kubaini madhaifu yao - mwenyekiti au katibu mkuu? Je inawezekana source ya kinana kubaini mapungufu ya mawaziri ni kutokana na kufanya ziara nchi nzima?
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums