Kafulila: Nimerejea CHADEMA rasmi leo

Kafulila: Nimerejea CHADEMA rasmi leo

Zunguka zunguka chama chetu cha ccm kinakusubili uje na siri zetu nzito tulizokutuma
 
Karibu sana mheshimiwa!! Sasa hapa utamu unazidi pale lisu, hapa kafulila kule zito!! Watu wanozungumza kwa kuwa na facts na sio yale mapompoma!! Ikiwekwa rege wao ni kucheza tu hata dj akiweka blues wao hawajui bado wako kwenye rege tu
 
Namshukuru Mungu kwa siku ya leo kurejea CHADEMA rasmi. Kwa heshima kubwa Namshukuru Mungu kwa tukio la leo. Namshukuru sana Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa heshima kwa kunikabidhi kadi mbele ya kikao muhimu cha Kamati Kuu leo jijini Mwanza. Ninaawaahidi wanachadema na wazalendo wote mnaopigania mabadiliko ya taifa hili kuwa nitatumia nguvu na akili yangu kuchangia mabadiliko tunayoamini! Ni wito wangu kwa wazalendo wote tuunganishe nguvu CHADEMA kuliokoa taifa letu linalopita nyakati ngumu kiuchumi na majaribu makubwa kiuongozi.
Mmmmhhh naona Kafulila ameamua kula matapishi yake. Kajiunga na chama chenye watuhumiwa wa ufisadi!ana roho ngumu sana. Njaa itatupeleka pabaya wajameni. Hajatueleza kwa nini amemuacha bwana Mbatia peke yake. Au ndio kampeni za kuua vyama dhaifu kama nccr. Mungu atuhurumie
 
Ila apunguze ukigoma .... (ubishi ) usio na tija
na kujiona ni bora.... atulie na kujenga chama... namkubali sana huyu jamaa tatizo tu ni Kale ka UKigoma ajakaacha.... Kafulila this time kaache Malagalasi tafadhali..... karibu nyumbani....
Je Kafulila aliyekabidhiwa kadi na Mbowe leo ni yule yule aliyemtuhumu Mbowe kuwa alimuua Wangwe au ni mwingine? Tena akapanga maandamano Dar wakati viongozi wa CHADEMA wakiwa Tarime kwa kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge kufuatia kifo cha Wangwe. Na yote hayo lengo ni kuonyesha Mbowe hafai kuwa mwenyekiti na kuwa Zitto alitakiwa achukue uenyekiti. Kama ndio Kafulila huyo huyo basi wengine hatuiwezi siasa
 
Nakumbuka Kafulila alikua anaponda sana chadema. Sasa sijui chadema hii imebadilika kidogo au vipii. Au kwa sababu wale watuhumiwa wa ufisadi wamemkamatisha samsin
 
Namshukuru Mungu kwa siku ya leo kurejea CHADEMA rasmi. Kwa heshima kubwa Namshukuru Mungu kwa tukio la leo. Namshukuru sana Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa heshima kwa kunikabidhi kadi mbele ya kikao muhimu cha Kamati Kuu leo jijini Mwanza. Ninaawaahidi wanachadema na wazalendo wote mnaopigania mabadiliko ya taifa hili kuwa nitatumia nguvu na akili yangu kuchangia mabadiliko tunayoamini! Ni wito wangu kwa wazalendo wote tuunganishe nguvu CHADEMA kuliokoa taifa letu linalopita nyakati ngumu kiuchumi na majaribu makubwa kiuongozi.

Mnafiki karejea kwao.
 
Kama angepata ubunge angehamia CHADEMA? Jibu hapana.

Kwa nini anadhani CHADEMA ni bora kuliko NCCR-Mageuzi wakati ukisimamishwa kugombea na NCCR-Mageuzi unapigiwa kampeni na vyama vilivyoko Ukawa.

Kwa hiyo anatupa ujumbe kuwa NCCR-Mageuzi limebaki jina tu ndani ya UKAWA.

Nini hatima ya Ukawa nchini? Au ndio kama yale madai yanayosema Tanganyika imevaa koti la Muungano!

Kwa sasa CHADEMA imevaa koti la Ukawa!
Kama Msindai angepata ubunge angerudi CCM? Jibu Hapana. Na wale wenye "mkia" mbona mkubwa wao kateuliwa balozi? Hivi mnajielewa kweli?

Ni muhimu ukafahamu kwamba ndoto kubwa kuliko zote ya ukawa ni kuwa chama kimoja cha siasa lakini CCM haitaki hilo litokee ndio maana ilipitisha Sheria maalum ya vyama vya siasa (1992) ambayo inapiga marufuku vyama kuungana,badala yake kushirikiana tu. CCM inajua kwamba muungano wa vyama vya siasa ni kifo kwake.

Nini hatima ya ukawa nchini? Pengine ungeuliza je - nini ni hatima ya CCM ya sasa, CCM inayojitambua kwamba ni dhaifu na isiyo na political legitimacy,inayojitambua kwamba haiwezi survive bila nguvu ya dola kupora mamlaka ya nchi.

Leo kama njia ya kukabiliana na kifo cha chama chenu ambacho hakipo mbali, mpo mstari wa mbele kushirikiana na msajili wa vyama vya siasa pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kumaliza ukawa. Kazi kubwa inafanyika kuwatumia akina Lipumba et al.

Juhudi hizo hazitafanikiwa. Sana sana kitakachotokea ni CCM kusambaratika kuelekea 2020 kwani humo ndani mmechanganyikiwa kwa sababu yule ambae wakubwa walimtaka, hakupita. Uchaguzi wa chama mwaka huu utaandamana na utitiri wa wagombea wengi kwa Mara ya kwanza katika historia ya chama chenu. Mtasingizia ni kukomaa kwa demokrasia lakini ukweli ni kwamba mmevurugwa. Kila la kheri katika kutenganisha kofia mbili.

Kama kawaida, tutarudi kukumbushana haya.
 
Kafulila mtu wa migogoro.Pale atakapo tangaza nia ta kugombea uenyekiti ndipo mtamjua kafulila ni nani
Kwani sababu zilizomfukuzisha chadema zimeondoka?Muulizeni mama Tanzania anamjua vizuri kafulila
 
Namshukuru Mungu kwa siku ya leo kurejea CHADEMA rasmi. Kwa heshima kubwa Namshukuru Mungu kwa tukio la leo. Namshukuru sana Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa heshima kwa kunikabidhi kadi mbele ya kikao muhimu cha Kamati Kuu leo jijini Mwanza. Ninaawaahidi wanachadema na wazalendo wote mnaopigania mabadiliko ya taifa hili kuwa nitatumia nguvu na akili yangu kuchangia mabadiliko tunayoamini! Ni wito wangu kwa wazalendo wote tuunganishe nguvu CHADEMA kuliokoa taifa letu linalopita nyakati ngumu kiuchumi na majaribu makubwa kiuongozi.

Karibu Nyumbani, karibu Nyumba kuuuubwa ya mabadiliko Mh Kafulila! Tunajua uwezo wako na ari yako ya mabadiliko ya kweli, karibu ujiunge na makamanda wa ukweli tulisongeshe jahazi la mabadiliko, mchango wako unahitajika zaidi wakati huu kuliko wakati mwingine wowote kutokana na ombwe kubwa la kiuongozi linalopotia taifa letu
 
Namshukuru Mungu kwa siku ya leo kurejea CHADEMA rasmi. Kwa heshima kubwa Namshukuru Mungu kwa tukio la leo. Namshukuru sana Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa heshima kwa kunikabidhi kadi mbele ya kikao muhimu cha Kamati Kuu leo jijini Mwanza. Ninaawaahidi wanachadema na wazalendo wote mnaopigania mabadiliko ya taifa hili kuwa nitatumia nguvu na akili yangu kuchangia mabadiliko tunayoamini! Ni wito wangu kwa wazalendo wote tuunganishe nguvu CHADEMA kuliokoa taifa letu linalopita nyakati ngumu kiuchumi na majaribu makubwa kiuongozi.
Karibu home Kaka
 
Alitimuliwa baada ya kumpinga mbowe. Kakosa ubunge karudi. (Uchu wa madaraka.) Zito kamkalia kooni anashindwa kupumua.
 
Kama angepata ubunge angehamia CHADEMA? Jibu hapana.

Kwa nini anadhani CHADEMA ni bora kuliko NCCR-Mageuzi wakati ukisimamishwa kugombea na NCCR-Mageuzi unapigiwa kampeni na vyama vilivyoko Ukawa.

Kwa hiyo anatupa ujumbe kuwa NCCR-Mageuzi limebaki jina tu ndani ya UKAWA.

Nini hatima ya Ukawa nchini? Au ndio kama yale madai yanayosema Tanganyika imevaa koti la Muungano!

Kwa sasa CHADEMA imevaa koti la Ukawa!
Hapana mkuu naona ni bora ili tuwe na chama kimoja kikubwa kuliko utitiri wa vyama ikiwezekana hta kina mbowe waivunje chadema na mtatiro aivunje cuf waunde chama kimoja chenye nguvu maana Ukawa haupo kisheria na katiba mpya ambayo ingeweza kutambua coallition za kisiasa ndo imeota mbawa so naona ni kma transition ya kuelekea chama kimoja cha upinzani bara na zanzibar.
 
Back
Top Bottom