heshimuni wapiga kura jamani!!! huwezi kuwatukana watu wa kwenu na kisha ukataka kuwa mbunge wao!!
mengine story!!
Nakubaliana na ulichozungumza mkuu, neno kwa neno!
kafulila alifukuzisha kazi watu wasio na hatia,mungu amempa mshahara wake sahihi,akalime mawese.
:crying: Ni afadhali kukosa Ubunge kuliko kuwa R.I.P. Ukiwa hai unaweza kujaribu wakati ujao au maisha sio lazima uwe Mbunge. Aidha, R.I.P inawapa shida hata wasiohusika-familia.Escow team hawajamuweza Zitto tu, Deo (RIP) kapumzika, sasa Kafulila
Na hao waliomnyenyekea zzk na kumlamba miguu wako wapi!?Malipo ni hapahapa Duniani ZZK alimpigania sana huyu dogo 2010 aingie Bungeni likini alichomfanyia zzk kinajulikana,watu wa Kigomba aliwatukana mpaka wakamzomea ilitegenea wampe kura? Na zaidi ni kile kitendo cha kuwafukuzisha watu wasio na hatia kazi kwa bifu tu la kuwanyima mafisadi vitaru vya gesi Muhongo kaondolewa wizara nyeti mpaka sasa umeme wa kusuasua kwa fitina za huyu jamaa mi nashukuru sana kama kweli kakosa
Hajatukana alisema alichofikiri ni sahihi kuwaambia wenzake,si wakati wa kuanzisha chama kwa ajili ya watu wa Kigoma tu.Haya Chama kimeanzishwa kimeambulia kiti kimoja,Mkoa wote umeurudisha CCM,lazima tukapime akili zetu.
Hana umuhimu wowote zaidi ya unafiki na ujasiriamali wa kisiasa.
Mbunge gani anayelipwa ili kwenda kutetea bungeni waliomlipa.
Kuna wabunge kama Mnyika ambao taifa linawahitaji sana.
Kafulila ni simba anayevaa ngozi ya kondoo.
He's good for nothing.
Na hao waliomnyenyekea zzk na kumlamba miguu wako wapi!?
Mkuu, huu ni wakati wa mabadilko na kwa mtu mwenye uwezo na akili kama za kafulila hawezi kupotea kwenye wakati muhimu kama huu. Utaniambia!
Mbona hujiulizi ACT chenye umri wa miezi kimepata wapi pesa za kufanyia kampeni na kuweka wagombea nchi nzima. Mbona akina TLP hawajafanya hayo !!Mbali na Mbatia ni wapi NCCR-Mageuzi wameshinda kwenye huu uchaguzi? Baada ya kupata hela za Lowassa Mbatia kajipa cheo cha msemaji mkuu wa CHADEMA na kusahau chama chake! Chama kina miaka 20 kwenye ulingo wa siasa lakini kimesimamisha wagombea wachache kuliko ACT yenye miezi michache kwenye siasa za Tanzania! Aibu!
Nimesikiliza namna mkurugenzi wa uchaguzi jimbo la Uvinza kwa Kafulila (zamani kama Kigoma kusini) alivyotangaza matokeo kibabe kwa kweli nimeumia sana! Alitangaza usiku akiwa peke yake just imagine!! Hata wafuasi wenyewe wa CCM wakabaki kushangaa!!
Kama majumuisho ya fomu Kafulila aliongoza inakuwaje wapindue kibabe? Huu mfumo wa BVR haukutoa haki na Kikwete alaumiwe kwa kupora haki!! Majimbo yote ya upinzani wameshinda kwa jasho kwenye uhesabuji wa kura, why?? Hii nchi haina demokrasia na kutafuta kitu hicho kwa njia ya kura ni kujidanganya!!
Wahenga walinena 'elimu haina mwisho'. Uchaguzi huu umekuwa mwalimu kwangu. Mimi siku zote nikifikiri itikadi kali za ukabila ziliishafifia katika taifa hili. Kumbe sikuwa sahihi! Nimerejea shule.kafukuzwa kwenye chama cha wapare, siunaona hata mbatia hakujishughulisha nae, badala ya kuoa mchagga yeye kaoa mnyiramba, haoni mwenzie wenje aliyeoa mchagga wanampigania kufa na kupona.
heshimuni wapiga kura jamani!!! huwezi kuwatukana watu wa kwenu na kisha ukataka kuwa mbunge wao!!
mengine story!!