Kafulila Kuendelea na ubunge?

Naona maoni ya wengi yanafanana kabisa lakini ukweli ni kuwa kama Kafulil kavuliwa uanachama automatically na ubunge hana. Sababu zieshaelezwa na wengi waliochangia.

Hii itabaki kuwa changamoto kwa siku za usoni.
 
Kafulila anaweza kukata rufaa mahakamani, pamoja na yote atavuta muda mpaka kesi imalizike mwaka na ushehe utakuwa umepita....
 
Jibu ni rahisi tu ukiangalia sifa za kugombea ubunge, moja wapo ni kuwa mwanachama wa chama cha siasa kilichokupendekeza kugombea nafasi hiyo. Kwa kuvuliwa uanachama, Kafulila anakosa sifa ya kuwa Mbunge. Hapa ndipo 2naona umuhimu wa mgombea binafsi, pia umuhimu wa kufuta suala la chaguzi ndogo za Ubunge na udiwani.
Katika kesi kama hii, kundi la watu wasiofikia mia moja, litaipa gharama serikali kufanya uchaguzi mdogo Kigoma Kusini bila kujali hali ngumu ya uchumi tunayokabiliana nayo.
Kama vipi sheria zibadilishwe tu aliyeshika nafasi ya 2 achukue jimbo.

Naungana na wewe 100%
 
Mbona naona tuko page moja, Kafulila ikithibitika kavuliwa uanachama basi mbona ni simple tu na Ubunge hana!! Simple and clear!!!

Mama mdogo, clearance hii umeipata kwenye nini? Nisaidie mwenzio niko kwenye lindi la mawazo.
 
Wanajamvi

Ngoja pia nitumie fursa hii kujibu swali la tofauti kati ya mgombea binafsi na mgombea huru, mgombea binafsi (Private Cnadidate) anapitia chama cha siasa, kwa mujibu wa sheria ya vyama na ya uchaguzi, maana yake ni kwamba anadhaminiwa na chama husika kupitia barua ya utambulisho rasmi kwamba ameteuliwa na chama hicho, mgombea huru (Independent candidate) yeye hapitii chama chochote anajidhamini mwenyewe.....kwa hiyo haya maneno tusiyatumie interchangeably, Mkuu soma Ibara ya 71 ya Katiba, umeshajuzwa vya kutosha.......itasaidia siku nyingine usiulize tena...ataachama chama ni pamoja na kufukuzwa maana hatakuwa na mdhamini kwa ubungee wake tena..
 
Naona maoni ya wengi yanafanana kabisa lakini ukweli ni kuwa kama Kafulil kavuliwa uanachama automatically na ubunge hana. Sababu zieshaelezwa na wengi waliochangia.

Hii itabaki kuwa changamoto kwa siku za usoni.

Kwa hiyo inatosha tu kugeuza sifa za mbunge kwamba kinyume chake siyo mbunge? :smash:.
 
Kafulila, jiunge na timu ya makada wa Chadema (Chini ya Dr Slaa) kusambaza operesheni Sangara sehemu zilizobaki nchini hapa!

then,2015 tuangalie kinachoendelea! unasemaje?
 
Mnapoambiwa vikundi hivi havifai(vyama) watu hawaelewi haya ndio matokeo yake ona sasa chama hakiangalii kundi la wananchi waliomwamini awawakilishe bali kinaangalia masirahi ya mtu mmoja aitwae m/kiti. Kwani mbatia ni nani hata awazidi wananchi wa kigoma kusini? Wananchi hawakuchagua chama walichagua mwakilishi(mbunge). Kafulila aende akaweke pingamizi haraka mahakamani. Pia katiba mpya itambue wagombea binafsi la sivyo taifa litakuwa linapoteza fedha nyingi ktk chaguzi ndogo kila mara, pia mbatia kama m/kiti uwe na uvumilivu kwa unaowaongoza kwani mawazo kugongana ni hali ya kawaida sio unakimbilia kufukuza uwanachama wenzako utajikuta unabaki na ndiyo bwana mkubwa wote! Hiyo siyo siasa.
 
mbunge anapoteza ubunge wako anapokoma kuwa mwanachama wa chama cha siasa kilichompeleka bungeni
 
Kafulila fanya maamuzi magumu Mkuu achana na kukata rufaa ili tu ubaki chini ya mwenyekiti usiyemuunga mkono! Maana utakuja kuwa mtumwa!
 
@mpui,..mi bado cjaelewa kinachokutatza, soma kwa makini ibara ya 67 uisome pamoja na ibara ya 71 (1) (f) ya katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania..pili rejea ishu ya madiwani wa arusha kupitia CHADEMA. Nadhani utaelewa.
 
labda wa Mbagala
Akamuulize zitto kabwe akiwa anawania uenyekiti ...mpenipole mdogo wangu alifwata mkumbo bila kusoma nyakati
Kwishne tukutane kijiweni songambele
 
Mwenzenu aliliiiiiii kuaaaaaaachana na ubunge analia kuachana na zile lakimbili mbili per day
loh
 
Jibu ni rahisi tu ukiangalia sifa za kugombea ubunge, moja wapo ni kuwa mwanachama wa chama cha siasa kilichokupendekeza kugombea nafasi hiyo. Kwa kuvuliwa uanachama, Kafulila anakosa sifa ya kuwa Mbunge. Hapa ndipo 2naona umuhimu wa mgombea binafsi, pia umuhimu wa kufuta suala la chaguzi ndogo za Ubunge na udiwani.
Katika kesi kama hii, kundi la watu wasiofikia mia moja, litaipa gharama serikali kufanya uchaguzi mdogo Kigoma Kusini bila kujali hali ngumu ya uchumi tunayokabiliana nayo.
Kama vipi sheria zibadilishwe tu aliyeshika nafasi ya 2 achukue jimbo.
Kaka hapo kwenye bluu tuhakikishe tunashiriki katika maoni ya katiba mpya ingawa sheria yake ilichakachuliwa
 
Mkuu mbunge anaingia kwa ticketi ya chama hivyo akivuliwa uanachama anakosa sifa ya kuwa mbunge! Ndio maana hakuna wagombea binafsi!
 
Hawezi kuendelea kuwa mbunge tena endapo atakuwa amevuliwa uanachama kwa sababu aliogembea kiti cha ubunge kupitia chama hicho.
Ni maajabu kwa sababu wananchi waliompeleka bungeni.sio.waliomkataa ni kikundi cha watu.wasiozidi.arobaini.na wala hawatoki.jimboni kwake
 
Sasa we vp? Umekuja hapa kuomba uelekezwe manake hujui sasa unaelezwa ukweli ulivyo hlf unaleta ubishi we mwe.u au? Wewe umeshaambiwa kafulila alikuwa mbunge wa jimbo la kigoma kusini kupitia tiketi ya nccr sasa kafukuzwa na mle bungeni hamna mbunge au waziri mkuu, spika, mwanasheria, mawaziri n.k wote wana vyama vyao sasa kafulila atakuwa mbunge wa chama gani? Katiba iliyopo hairuhusu mgombea binafsi unataka ueleweshwe namna gani? We kweli mb.rula, hatuna muda wa kubishana na wewe hapa kama kafulila ni ndgu yako ujue imekula kwako.
Lkn wanajamvi vp khs zile mil90 alizokopwa kununu gari atazilipaje? Sijui RA naye kama alirudisha.

Hii lugha ya ukali na matusi ni lugha ya chama fulani kinachovaa magwanda ya khaki.
 
Kauli kama hizi ndizo zinazotusumbua, kwa nini unashindwa kutaja jambo zito kama hili katika sheria mama. Kwenye hali kama hii tunamalizanaje? Maana kwa ujumla hayo ni mawazo yako tu.

Nadhani hujasoma katiba vizuri.

71- (1) Mbunge atakoma kuwa mbunge na ataacha kiti chake katika bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:
(a) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya katiba hii.


Halafu kasome
67-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika katiba hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa mbunge endapo:
(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa

Kwa maelezo hayo, ni dhahiri kuwa Kafulila kwa kufukuzwa katika NCCR, siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa, kama asingekuwa mbunge, na angekuwa anagombea leo nafasi ya ubunge, basi asingekuwa na sifa za kuweza kuchaguliwa, kwa sababu siyo mwananchama wa chama cha siasa aliyependekezwa na chama, kama katiba inavyotamka.
 
Ni vyema pia kutofautisha kati ya mgombea huru (independent candidate) na mgombea binafsi (private candidate) kwa Tanganyika wagombea wote ni private maana wanadhaminiwa na vyama vyao kwa muji u wa Ibara ya 67 kama ilivyofafanuliwa hapo juu
 
Back
Top Bottom