Kafulila Kuendelea na ubunge? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kafulila Kuendelea na ubunge?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpui Lyazumbi, Dec 18, 2011.

 1. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Wakuu heshima kwenu, kulingana na habari zilivyo ni dhahiri kwamba Mbunge Kafulila kavuliwa uanachama wake. Jambo hili limenisukuma kuyapitia makabrasha kadhaa kuona kama kwa kuvuliwa uanachama ndugu kafulila ataukosa ubunge automatically. Kuna utata nimeupata sambamba na ule wa mbunge wa Arumeru mashariki bwana Sumari ni mbunge ama la. Imani yangu naiweka hapa jamvini kwa ufafanuzi iwapo huu sasa ndo ukomo wa kafulila kuwa mbunge. Nimepitia katiba yetu haisemi kwa uwazi juu ya ukomo wa mbunge kama ilivyo kwa nafasi nyingine kama vile rais, makamu wa rais, waziri mkuu n.k. Swali langu linabaki palepale -Kafulila ataendelea na ubunge licha ya kuvuliwa uanachama?
   
 2. n

  nyuki dume JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hawezi kuendelea kuwa mbunge tena endapo atakuwa amevuliwa uanachama kwa sababu aliogembea kiti cha ubunge kupitia chama hicho.
   
 3. A

  Apta Kayla JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 326
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jibu ni rahisi tu ukiangalia sifa za kugombea ubunge, moja wapo ni kuwa mwanachama wa chama cha siasa kilichokupendekeza kugombea nafasi hiyo. Kwa kuvuliwa uanachama, Kafulila anakosa sifa ya kuwa Mbunge. Hapa ndipo 2naona umuhimu wa mgombea binafsi, pia umuhimu wa kufuta suala la chaguzi ndogo za Ubunge na udiwani.
  Katika kesi kama hii, kundi la watu wasiofikia mia moja, litaipa gharama serikali kufanya uchaguzi mdogo Kigoma Kusini bila kujali hali ngumu ya uchumi tunayokabiliana nayo.
  Kama vipi sheria zibadilishwe tu aliyeshika nafasi ya 2 achukue jimbo.
   
 4. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160

  Huo ukomo wa mbunge umetajwa wapi? Mimi nieona utata tu kama kwa sumari pale arumeru bana.
   
 5. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,865
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Uchaguzi wa Tanzania unaambatana na kuwa mwanchama wa chama cha siasa kilichoandikishwa na kutambulika rasmi kwa msajiri wa vyama vya siasa. Kwa mantiki hii diwani, mbunge na rais wakitimuliwa na vyama vyao, basi wanakuwa wamepoteza udiwani, ubunge au urais wao. Hata hivyo sarakasi za kisiasa zinaweza chezwa kama ilivyofanyika kwa madiwani wa Manispaa wa Arusha, lakini mwishowe sheria ikichukua mkondo wake sharti aliyefukuzwa anapoteza nafasi yake, na nafasi inatangazwa na tume ya uchaguzi kuwa iko wazi, na uchaguzi unatakiwa kufanyika!!! Hivyo kafulila anaelekea kuwa mbunge mstaafu / mfukuzwa!!!
   
 6. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Kafulila aligombea na akapata. Wapi ukomo wa hii kitu maana saa hizi hajaomba kugombea mkuu. Lete ukomo hapa,
   
 7. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Kuhusu Rais hata ukinisoma nimeeleza kuwa katiba yetu imetaja ukomo wa rais, majukumu yake na uwazi wa kila namna. Lete hapa ukomo wa mtu kuwa mbunge na siyo sifa za kuchaguliwa, mbona tunachanganya vitu hapa?
   
 8. Wa kusoma

  Wa kusoma JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,315
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Sasa we vp? Umekuja hapa kuomba uelekezwe manake hujui sasa unaelezwa ukweli ulivyo hlf unaleta ubishi we mwe.u au? Wewe umeshaambiwa kafulila alikuwa mbunge wa jimbo la kigoma kusini kupitia tiketi ya nccr sasa kafukuzwa na mle bungeni hamna mbunge au waziri mkuu, spika, mwanasheria, mawaziri n.k wote wana vyama vyao sasa kafulila atakuwa mbunge wa chama gani? Katiba iliyopo hairuhusu mgombea binafsi unataka ueleweshwe namna gani? We kweli mb.rula, hatuna muda wa kubishana na wewe hapa kama kafulila ni ndgu yako ujue imekula kwako.
  Lkn wanajamvi vp khs zile mil90 alizokopwa kununu gari atazilipaje? Sijui RA naye kama alirudisha.
   
 9. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Umegusia sifa za kuchaguliwa kuwa mbunge. Wote tunajua baada ya uchaguzi unawakilsha wananchi wote bila kujali vyama vyao vya siasa ama kikundi fulani. Sina undugu wowote na kafulila wala lengo langu siyo ubishi, pitia katiba na uniletee uwazi hapa kuhusu ukomo wa mbunge baada ya hapo niendelee na mambo mengine. Kama hilo hutalifanya ujue tuna safari ndefu kuhusu katiba yetu na katika hili nimegusia jimbo la arumeru mashariki mbunge wao ni nani? Kuwa mvumilivu twende pamoja mkuu.
   
 10. U

  UMUGANE Member

  #10
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sifa ya kwanza ya mtu kuwa mbunge ni kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Ndo maana TZ haina mgombea binafsi. Hivyo kafulila hatakuwa na chake tena. Angalizo: Katika mabadiriko ya katiba yajayo lazima suala hili likaangaliwe kwa umakini maana kwa sasa, mbunge huwajibika zaidi kwa chama kulilo kwa wananchi.
   
 11. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #11
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Jamini ni muhimu wagombea binafsi kuwekwa kwenye katiba la sivyo mambo yanayomkuta mbunge machachari Kafulila yataendelea. Hana tena sifa za kuwa mbunge
   
 12. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #12
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,078
  Likes Received: 7,293
  Trophy Points: 280
  Tulishajadili hili suala la mshindi wa pili kuchukua kiti,
  Magamba wakadai kua siyo ligi ya mpira wa miguu hii!!
  Kusema ukweli inasikitisha sana kwamba ugomvi wa Kafulila na Mbati, Taifa linaingia gharama zingine za uchaguzi!!
  Yaani leo Mwenyekiti akigombana na mmoja wa wancahama wake hata kwa issue personal tu, basi Taifa linaingia gharama!!
  Suluhisho la huu upuuzi ni mgombea binafsi tu!!
  Mbunge aruhusiwe kujitoa chama but asiruhusiwe kujiunga na chama kingine mpaka uchaguzi mkuu!!
  Au akitaka kujiunga na chama basi akubali kupoteza ubunge/udiwani!!
   
 13. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #13
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Hujanisoma kabisa.
   
 14. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #14
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Ni mchakato mrefu,mpaka mbatia amuandikie barua Spika,na kama kafulila ajafungua kesi ya kuappeal basi atapoteza ubunge lakini navyomjua kafulila lazima afungue kesi ya kupinga kufukuzwa kwake na kesi hiyo inaweza enda hata miaka 6,pili anaweza akashinda kesi na kuendelea kua mwanachama,mpaka sasa kafulila bado mbunge wa kigoma kusini,si unakumbuka sakata la RA,aliachia ngazi lakin spika alisema ajapokea barua yeyote kutoka kwa ra so yeye anamtambua mb mpaka atakapompa barua ya kurizain,same as kafulila mpaka mbatia apeleka barua kwa spika na kama kafulila akifungua kesi basi ataendelea kua mbunge mpaka mahakama itavyoamua kwamba amefukuzwa uanachama kialali
   
 15. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #15
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  David Kafulila, usijali simama kwa yale unayoamini ni ya kweli bila kujali uko bungeni au nje ya bunge. Kuna watanzania wengi tu ambao wanachangia ujenzi wa nchi yetu kisiasa na kiuchumi lakini hawako bungeni. Keep it up
   
 16. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #16
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  :focus:
   
 17. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Ukomo wa ubunge siyo lazima utajwe kwenye Katiba, lakini kama uwepo wa ubunge unatokana na Katiba ukomo wake unatokana pia na moja au vyote vya vigezo ku'cease' kuwepo. Mfano, chama anachotoka mbunge kikifutwa automatically ubunge unakoma, mbunge akifa au akipata maradhi yanayomfanya asimudu tena kazi yake ya ubunge, akiamua kubadili uraia wa nchi, ikijulikana kuwa umri wake ni chini ya miaka 18, nk.
   
 18. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #18
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,865
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Mbona naona tuko page moja, Kafulila ikithibitika kavuliwa uanachama basi mbona ni simple tu na Ubunge hana!! Simple and clear!!!
   
 19. J

  Joshua Bukuru Member

  #19
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 25
  Kuna tofauti kati ya kuvuliwa uanachama na kufukuzwa uanachama. Nijuavyo mimi, ukivuliwa uanachama unaweza ukarudishiwa uanachama wako endapo chama kitakuwa kimeridhishwa na mwenendo wako. Wakati huo chama kinakuwa kinakuchunguza na endapo hakiridhishwi hatua inayofuata ni kufukuzwa. Hatua ya kufukuzwa haina msamaha na kama ni mbunge automatically unapoteza sifa ya kuwa mbunge pale tu chama chako kitakapomwandikia barua spika kumjulisha kuwa jimbo fulani lipo wazi.
  Sasa hii ya Kafulira haiko wazi maana habari hizi ni za kupikwa na vyombo vya habari na chama chake hakijatangaza kumvua au kumfukuza uanachama. Tuvute subira kidogo!
  Kama ni kuvuliwa uanachama, ataendelea na shughuli zake za kuwawakilisha wapiga kura wake hadi pale maamuzi ya mwisho yatakapo fanywa na chama chake. Bado ataendelea kuwa mbunge na atahudhulia vikao vyote vya bunge na vya kamati za bunge. Mpiganaji huyo hawezi kutoweka kwenye siasa za uwakilishi maana alichaguliwa na wapiga kura wake kwa upambanaji wake wa kuelewa matatizo ya watu wake na ni si chama chake.
   
 20. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #20
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Kauli kama hizi ndizo zinazotusumbua, kwa nini unashindwa kutaja jambo zito kama hili katika sheria mama. Kwenye hali kama hii tunamalizanaje? Maana kwa ujumla hayo ni mawazo yako tu.
   
Loading...