dyuteromaikota
JF-Expert Member
- Apr 30, 2013
- 5,936
- 8,345
Alichukua hatua gani kurekebisha kabla hajahama?
Opposition parties hapa Africa ni tofauti unavyofikiria wewe. Kwenye Demokrasia kuna mazuri yanayofanywa na chama tawala inatakiwa opposition parties waunge mkono na serikali inapokosa waikosoe. Nchi nyingi za ulaya huwezi kuona chama cha upinzani kinatoa kejeli na matusi kwa kiongozi aliyeko madarakani.
Reuters)
Obama’s family leaves Italy
Read Less
First lady Michelle Obama left Italy with her daughters, Malia and Sasha, as well as her mother, Marian Robinson. During their stay the Obama family visited the Milan Expo.
June 21, 2015 | 5:41 PM EDT
Mfano wa hapo juu familia ya Rais Obama walienda Italia kutembea kwa gharama ya walipa kodi wa Marekani lakini hakuna kiongozi wa chama cha upinzani alitoa tamko la kulalamika. Hapa serikali imejenga Airport Chato ambayo ipo Tanzania imekuwa tatizo kubwa. Kwa msimamo na speed ya serikali ya awamu ya tano Opposition parties Tanzania zitakufa natural death.
Ww kichwa, no doubt about itAwali ya yote naomba kuchukua nafasi kumshukuru Mwenyezi Mungu kutujalia zawadi ya uzima tulio nao.
Bila kupoteza muda, napenda kusema kuwa nimemsikia Ndg Kafulila kupitia (voice note) akithibitisha kuwa ndiye aliyetoa tamko la kujiengua toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Kimsingi sina tatizo na yeye kutoka kwani ni HAKI yake kikatiba kufanya maamuzi aliyoyafanya na hivyo sina PINGAMIZI lolote katika hilo.
Ndg Kafulila anasema kupitia tamko lake kuwa ataujulisha umma ni chama gani atajiunga nacho hivi karibuni, kitu ambacho binafsi naona hakina haja kwani tayari maudhui ya andiko lake yanabainisha ni chama gani atajiunga nacho.
Sasa kama sina tatizo na Ndg Kafulila ku-exercise haki yake kikatiba, kwanini natoa maoni yangu kuhusiana na suala lake la yeye kuondoka Chadema?
Nimeamua kutoa maoni yangu kutokana na ukweli kuwa SIKUBALIANI na hoja kuu ya Ndg kafulila kuwa UPINZANI SIO TENA JUKWAA SALAMA LA KUENDESHA VITA DHIDI YA UFISADI. Adai hii imetokana na vyama vya upinzani kupigwa ganzi (japo hajasema nani kavipiga ganzi na kwanini avipige ganzi) na hivyo UFISADI SIO TENA AJENDA KUU YA UPINZANI.
Labda nisema tu kuwa Ndg Kafulila ni ama kaamua kupotosha umma kwa makusudi au hajui ni nini maana ya VYAMA VYA UPINZANI, lakini pia hajui AJENDA KUU ya vyama hivyo nchini! Kifupi tu ni kwamba, UFISADI haujawahi kuwa na kamwe hauta kuwa AJENDA KUU ya vyama vya upinzani si tu kwa Tanzania, bali duniani pote. Hii inatokana na tafsri ya upinzani lakini pia wajibu wake katika Demokrasia ya mfumo wa vyama vingi duniani.
Naomba nitumie maandiko kadhaa kulithibitisha hili nisemalo, nitaanza na mmoja wa wanasiasa wakongwe na machachari nchini New Zealand, na huyu sio mwingine ila ni Dakta Donald Thomas Don Brash. Dakta Brash alipata kuwa Gavana wa Benki Kuu ya New Zealand, Kiongozi wa Kambi Rasmi Bungeni, Kiongozi wa vyama vya National Party na ACT Party kwa nyakati tofauti. Yeye aliwahi kusema, naomba nimnukuu;
“The Opposition’s main role is to question the government of the day and hold them accountable to the public…. Opposition represents an alternative government, and is responsible for challenging the policies of the government and producing different policies where appropriate.”
Naomba nitoe tafsiri (sio rasmi) Kazi kuu ya upinzani ni KUHOJI serikali iliyoko madarakani na kuifanya iwajibike kwa umma….Upinzani unawakilisha serikali MBADALA na unawajibika kutoa changamoto kwenye sera za serikali na hivyo kutoa sera tofauti/mbadala pale inapowezekana.
Dakta Brash anaongeza kusema, namnukuu; “…one of the most important jobs of the Opposition is to constantly question the Government. Any Government has to remain answerable to the public at all times, and a good Opposition can put the spotlight on serious issues and have them resolved quickly”.
Tafsiri (sio rasmi) Moja ya kazi muhimu za upinzani ni kuendelea kuhoji serikali bila kuchoka, Serikali yeyote inapashwa kuendelea kuwajibika kwa umma muda wote, na upinzani mzuri unaweza kumulika/kuibua mambo na hivyo kurekebishwa kwa haraka.
Lakini pia kwa mujibu wa Taasisi ya Kidemokrasi ya Afrika (Africa Democratic Institute) inasema wajibu wa upinzani katika Demokrasia ni mkubwa sana. Taasisi hii inabainisha baadhi ya kazi/wajibu wa upinzania kuwa ni pamoja na:-
To hold governments accountable (Kuiwajibisha Serikali);
To serve as a credible alternative to the ruling government (Kuwa mbadala wenye kuaminika/thabiti dhidi ya serikali inayotawala);
To promote and stimulate debates in parliament (Kukuza na kuchochea mijadala bungeni);
To be a training ground for future leaders (Kuwa eneo la mafunzo kwa viongozi wa baadaye);
Kwa upande mwingine, mwandishi Sheetal Kumari wa India, anaandika kama ifuatavyo:-
The Opposition parties play a very significant role in a democracy as representatives of the people…to safeguard their interests….The opposition act as watch dog’ of a the system.
Tafsiri (sio rasmi) Vyama vya upinzani vina jukumu muhimu sana katika Demokrasia kwa kuwa wawakilishi wa watu/umma ili kulinda maslahi yao….Upinzani ni mlinzi katika mfumo.
Sio hao tu, pia msomi Julius Kiiza, PhD; kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, katika ‘pepa’ yake ya Wajibu wa Upinzani katika Demokrasia, Kiiza (kama anavyopenda kuitwa) pamoja na mambo mengine anaandika.
“…opposition parties perform several important functions. These include; promoting responsible and reasoned debate. Opposition parties hold the government to account for its commissions or omissions. Parties present a viable alternative to the incumbent government by designing alternative ideas, principles and policies for governing society. Should the party in power let the voters down, the ‘government-in-waiting’ takes over the reign of power – through free and fair elections.”
Kiza anendelea kuandika; “Parties act as a training ground for future leaders, parties strengthen the culture of democracy within the party and the political community in general (by, for example, promoting open debate during delegates’ conferences, promoting intra-party democratic elections and ensuring accountable use of party finances). Parties work with the Electoral Commission, the mass media and civil society organizations to monitor and improve the quality of voter registration, civic education and electoral transparency.
Tasfri (sio rasmi) ya maneno ya Kiiza
...vyama vya upinzani vinafanya kazi kadhaa muhimu. Hizi ni pamoja na; kukuza mijadala na hoja zenye kuleta uwajibikaji. Vyama vya upinzani vinaiwajibisha serikali katika maelekezo na makosa yake. Vyama vinajinadi kama mbadala unayofaa na fanisi dhidi ya serikali iliyoko madarakani katika kubuni mawazo, kanuni na sera mbadala zenye kuongoza umma. Kama itatokea chama tawala kikawaangusha wapiga kura, 'serikali inayosubiri' huchukua madaraka kupitia chaguzi huru na za haki.
Sasa nikirejea kwenye hoja yangu, ukisoma hayo maandiko na mengine mengi tu, hakuna hata moja linalosema kuwa AJENDA KUU YA UPINZANI NI UFISADI. Hivyo kwa wanaotumia maneno kama hayo ya Ndg Kafulila pale wanapoamua kuondoka upinzania, ama wanaamua kudanganya ama hawajui wajibu/agenda kuu ya upinzani ni nini.
Ni vema watoe sababu zengine lakini sio sababu zisizo na mashiko na tena ni MFU kama hizo za aina ya Ndg Kafulila. Lakini pia ukisoma maandiko hayo, na mengine mengi ambayo sikuyanukuu, hakuna mahali panasema njia ya upinzani kuiunga mkono serikali iliyoko madarakani ni kuondoka upinzani na kujiunga chama tawala, kama ingelikuwa ni hivyo. Basi upinzani na wajibu wake utakuwa hauna maana.
Mimi nadhani ni sahihi sana kwa wewe unaona vyuma vimekaza na unaona njia rahisi ni kukimbilia chama tawala, basi ondoka tu, USIUPOTOSHE UMMA. Au kama umeshindwana na wenzio ndani ya chama na ukaona njia sahihi ni wewe kuachana nao, basi ondoka tu, ukipenda kimya kimya au kwa kelele lakini USIUPOTOSHE UMMA. Na kama umeahidiwa CHEO, PESA nk basi we nenda tu kachukue lakini USIUPOTOSHE UMMA.
NAOMBA KUWASILISHA
Dickson Ng’hily
European Zone Coordinator – ACT Wazalendo
22/11/2027
Africa ina safari ndefu kufikia Demokrasia kamili. Kwani kila chama inakiona chama kingine Adui mkubwaHapa UK, waziri Priti Patel alilazimishwa ku-resign simply kaenda safari binafsi Israel ambayo kimsingi sio tatizo ila kitendo chake cha kukutana na viongozi wa Israel including their Prime Minister bila kujulisha Serikali yake ya Uingereza lilikuwa ni kosa kubwa sana kiasi cha kulazimishwa ku-resign...Lakini pia Waziri Boris Johnson alipata shinikizo la ku-resign baada ya kauli yake Bungeni kuwa mwanamama Nazanin alikwenda Iran kufundisha waandishi wa habari. Kauli ambayo ilisababisha mwanamama huyo kuitwa mahakamani tena. Ilibidi aombe msamaha bungeni kwa kauli yake na kuahidi kulishughulikia ikiwa nia pamoja na kwenda Irani baadaye mwezi huu kushughulikia jambo hilo.
Priti Patel forced to resign over meetings with Israeli officials.
Calls for bungling Boris Johnson to resign over gaffe that could land Brit five more years in Iranian jail, Nazanin Zaghari-Ratcliffe was summoned to court where Johnson's comments were cited as proof that she was engaged in "propaganda against the regime".
Umedandia uzi, hujaelewa chochoteKweli kabisa . Chama hakiwezi kununuliwa na LOWASA halafu kikaendelea kuufanya UFISADI kuwa ajenda kama zamani.
Aliyenunua kivuko cha Dsm-Bagamoyo aliwahi kuwajibika? Aliyeuza nyumba za serikali akajiuzia nyumba kibao kienyeji tena zingine akagawa kwa mdogo wake na Zingine kwa hawala huku akizaa na Shemeji yake kinyume cha maadili je? Aliwajibika? Zile bilion 252 zilipotea wizara ya ujenzi kwa kuwalipa makandarasi hewa ni nani aliwajibika? Kuzuiwa kwa ndege Canada ni nani wa kuwajibika?Kwani serikali haipaswi kuwajibika unapotokea ufisadi? Mbona akina Mlongo waliachia ngazi baada ya escrow, sio kuwajibika huko? Naomba nieleweshwe maana ya neno 'kuwajibika'
Sawa, things are supposed to be like that, ila kwa takriban miaka kadhaa huko nyuma CHADEMA wenyewe kama model ya upinzani nchini walisimama kidete na hoja ya ufisadi kama agenda kuu ktk kuipinga CCM na serikali yake na kwa kweli iliwasababishia Political positive Impact ktk Mass mobilization, sasa ukilinganisha na msimamo wa CHADEMA ya sasa huoni hii ina create grounds za mashiko ktk tuhuma za Kafulila dhidi ya upinzani?.
Wana njaa sana ni vigeugeu Madalali wa siasa wenye Dili la kuwanunua Wapinzani wamepoteza pesa zao bure kabsa.Sijawahi kuona material candidate wa mageuzi toka Kigoma. Records zinawahukumu.
Msome jamaa, either hujasoma au hujaelewaKumbuka Kafulila anaposema wapinzani ana maana ya CHADEMA kwa sababu anaamini vyama vingine sio wapinzani bali ni matawi ya CCM na CHADEMA!
Kafulila alikuwa mwanachama wa CHADEMA , Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA kwenye dibaji/utangulizi inasema Ufisadi ndio tishio kubwa kabisa la mustakabali wa nchi yetu. Ndio kusema tukitaka tutoke hapa tulipo ni lazima tuukatae na tupambane na ufisadi.
Nmekuwekea sehemu ya utanguliza wa Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA.
‘’Hivi karibuni Rais wetu, Jakaya Mrisho Kikwete, aliulizwa na waandishi wa habari wa Jijini Paris, Ufaransa kwamba “Nchi yako ina utajiri mkubwa wa maliasili, inakuwaje Watanzania ni masikini wa kutupwa?” Alijibu, kwa furaha na kwa kujiamini, “Hata mimi sijui sababu; ninajiuliza kila siku swali hilo lakini sijapata jibu!’’ Huyo ndio dereva wa gari tulilopanda; hajui anakotoka wala aendako. Sote tunaelewa hatari ya kupanda gari ambalo dereva wake hajui anapoenda. Kama Rais wa nchi hajui sababu kwa nini nchi yetu ni maskini atawezaje kupambana na huo umaskini? Hata hivyo, CHADEMA hatuamini kwamba Rais Kikwete hajui chanzo cha umaskini katika nchi yetu. Rais Kikwete anajua chanzo cha umaskini wa nchi yetu lakini hawezi kukitaja kwa kuwa yeye mwenyewe ni sehemu ya tatizo hilo''.
''Kuna sababu tatu zilizosabisha nchi yetu ifike hapa ilipo, nazo ni: ufisadi, ufisadi na ufisadi. Ufisadi ndio tishio kubwa kabisa la mustakabali wa nchi yetu. Ndio kusema tukitaka tutoke hapa tulipo ni lazima tuukatae na tupambane na ufisadi’’.
Kwa mantiki hii, ajenda kuu ya CHADEMA ilikuwa ni kupambana na Ufisadi. Kwa sasa wameachana na ajenda yao kuu.
Aliyenunua kivuko cha Dsm-Bagamoyo aliwahi kuwajibika? Aliyeuza nyumba za serikali akajiuzia nyumba kibao kienyeji tena zingine akagawa kwa mdogo wake na Zingine kwa hawala huku akizaa na Shemeji yake kinyume cha maadili je? Aliwajibika? Zile bilion 252 zilipotea wizara ya ujenzi kwa kuwalipa makandarasi hewa ni nani aliwajibika? Kuzuiwa kwa ndege Canada ni nani wa kuwajibika?
Bashite alitaja List ya wauza Unga ( blackmail) akajichumia mali mpaka akachukua magari ya watuhumiwa na mali zao zingine na kala 10% nyingi kwani kila kazi kubwa Mtukufu kamweka mbele anapiga 10% Ufisadi hautakwisha CCM mpaka akina Grace Mugabe watakapozeeka na kufariki.Je mpaka sasa hivi huo ufisadi umefanyiwa kazi??Nani mpaka sasa amefungwa kwa ufisadi au rushwa.Akina Lugumi na wale wa TRA imeshindikana kuwashtaki kwa sababu kuna aliyetaka yale yafanyike na ni kiongozi mkuu wakiendelea kuguswa utumbo utakata.
Hakuna vita ya ufisadi wala rushwa hapo ni changa la macho tu.Ila Muda ndiyo mchawi mkuu wa kila jambo.Kuna watu watahama hapa JF
Uko sahihi sana ingawa hakuna CHADEMA inachoweza kufanya kuzuia CCM/serikali inayotumia hazina ya taifa na nguvu za dola kuua upinzani zaidi ya kutegemea mshikamano wa wananchi wote kupinga hujuma hiyo inayolielekeza taifa kwenye mfumo wa udikteta kamili.
Na NAKUHAKIKISHIA CCM/serikali ikifanikiwa kuua upinzani makini nchini, watakaolia na kusaga meno si CHADEMA, NCCR, ACT na CUF pekee bali hata wana-CCM wenyewe. Tena hao ndio watalia zaidi huku wakisakamwa na aibu ya kuendekeza uovu na ujinga usiomithilika. Kwa kifupi hakuna atakayekuwa salama nchini. Soma historia ya Hitler alipoanzia hadi kuishia. Hakuanza kama mtu wa ovyo ovyo.
Yaliyowapata Nape na Lissu ni kidokezo tu cha mwelekeo wa hiyo CCM inayojengwa leo hii kwa kuua sauti makini ya upinzani (voice of objective dissent). Tusisahau kuwa sauti ya upinzani husaidia hata ndani ya chama tawala. Magufuli mwenyewe alifurahia harakati za Kafulila kuhusu Escrow acc scandal. Leo yeye hataki kabisa sauti ya aina hiyo isikike kwenye utawala wake kiasi cha kutumia pesa za umma na nguvu ya dola kuzima upinzani. It’s up to all Tanzanian’s to wake up and smell the coffee!
Bashite alitaja List ya wauza Unga ( blackmail) akajichumia mali mpaka akachukua magari ya watuhumiwa na mali zao zingine na kala 10% nyingi kwani kila kazi kubwa Mtukufu kamweka mbele anapiga 10% Ufisadi hautakwisha CCM mpaka akina Grace Mugabe watakapozeeka na kufariki.
Wanasajili vyama kibao makusudi ili wawe wanavichonganisha wakati vinagombana wao wanatumia fursa hiyo hiyo kuwanunua wanachama wa upinzani.Africa ina safari ndefu kufikia Demokrasia kamili. Kwani kila chama inakiona chama kingine Adui mkubwa
Kwa mujibu wa polepole upinzani ni mawazo mbadala hivyo upinzani ni kuwa na mawazo tofauti na watawala hivyo kazi ya upinzani cii moja kama anavyopotosha kafulilaKumbuka Kafulila anaposema wapinzani ana maana ya CHADEMA kwa sababu anaamini vyama vingine sio wapinzani bali ni matawi ya CCM na CHADEMA!
Kafulila alikuwa mwanachama wa CHADEMA , Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA kwenye dibaji/utangulizi inasema Ufisadi ndio tishio kubwa kabisa la mustakabali wa nchi yetu. Ndio kusema tukitaka tutoke hapa tulipo ni lazima tuukatae na tupambane na ufisadi.
Nmekuwekea sehemu ya utanguliza wa Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA.
‘’Hivi karibuni Rais wetu, Jakaya Mrisho Kikwete, aliulizwa na waandishi wa habari wa Jijini Paris, Ufaransa kwamba “Nchi yako ina utajiri mkubwa wa maliasili, inakuwaje Watanzania ni masikini wa kutupwa?” Alijibu, kwa furaha na kwa kujiamini, “Hata mimi sijui sababu; ninajiuliza kila siku swali hilo lakini sijapata jibu!’’ Huyo ndio dereva wa gari tulilopanda; hajui anakotoka wala aendako. Sote tunaelewa hatari ya kupanda gari ambalo dereva wake hajui anapoenda. Kama Rais wa nchi hajui sababu kwa nini nchi yetu ni maskini atawezaje kupambana na huo umaskini? Hata hivyo, CHADEMA hatuamini kwamba Rais Kikwete hajui chanzo cha umaskini katika nchi yetu. Rais Kikwete anajua chanzo cha umaskini wa nchi yetu lakini hawezi kukitaja kwa kuwa yeye mwenyewe ni sehemu ya tatizo hilo''.
''Kuna sababu tatu zilizosabisha nchi yetu ifike hapa ilipo, nazo ni: ufisadi, ufisadi na ufisadi. Ufisadi ndio tishio kubwa kabisa la mustakabali wa nchi yetu. Ndio kusema tukitaka tutoke hapa tulipo ni lazima tuukatae na tupambane na ufisadi’’.
Kwa mantiki hii, ajenda kuu ya CHADEMA ilikuwa ni kupambana na Ufisadi. Kwa sasa wameachana na ajenda yao kuu.
Hata CCM sio mahala salama kutwa wanatishiana kupora kati za uanachama wa CCM hata Spika wa Bunge ndungai amewahi kutishiwa kuporwa uanachama wa CCM endapo atatoa uhuru kwa Wapinzani Bungeni, CCM ya sasa ni ya kidikteta sana ngoja kafulila akajionee huko maana anapenda Majungu na fitna atawakuta wenye Phd za Uzushi ndipo atajutia baadae.
Grace Mugabe hafai ni mtu Hatari sana lakini hakuna mabaya yasiyo na mwisho ipo simu watafeli na kupata Aibu kubwaMpaka leo,akija kwenye kampuni yako akitaka bilini moja ukimnyima anaenda TRA na kukufungia biashara hata kama huna utaenda kukopa ili umpe na wakati mwingine unapata kesi za uhujumu uchumi refer Manji