Kafulila Asipotoshe Umma

Kafulila Asipotoshe Umma

Awali ya yote naomba kuchukua nafasi kumshukuru Mwenyezi Mungu kutujalia zawadi ya uzima tulio nao.

Bila kupoteza muda, napenda kusema kuwa nimemsikia Ndg Kafulila kupitia (voice note) akithibitisha kuwa ndiye aliyetoa tamko la kujiengua toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Kimsingi sina tatizo na yeye kutoka kwani ni HAKI yake kikatiba kufanya maamuzi aliyoyafanya na hivyo sina PINGAMIZI lolote katika hilo.

Ndg Kafulila anasema kupitia tamko lake kuwa ataujulisha umma ni chama gani atajiunga nacho hivi karibuni, kitu ambacho binafsi naona hakina haja kwani tayari maudhui ya andiko lake yanabainisha ni chama gani atajiunga nacho.

Sasa kama sina tatizo na Ndg Kafulila ku-exercise haki yake kikatiba, kwanini natoa maoni yangu kuhusiana na suala lake la yeye kuondoka Chadema?

Nimeamua kutoa maoni yangu kutokana na ukweli kuwa SIKUBALIANI na hoja kuu ya Ndg kafulila kuwa UPINZANI SIO TENA JUKWAA SALAMA LA KUENDESHA VITA DHIDI YA UFISADI. Adai hii imetokana na vyama vya upinzani kupigwa ganzi (japo hajasema nani kavipiga ganzi na kwanini avipige ganzi) na hivyo UFISADI SIO TENA AJENDA KUU YA UPINZANI.

Labda nisema tu kuwa Ndg Kafulila ni ama kaamua kupotosha umma kwa makusudi au hajui ni nini maana ya VYAMA VYA UPINZANI, lakini pia hajui AJENDA KUU ya vyama hivyo nchini! Kifupi tu ni kwamba, UFISADI haujawahi kuwa na kamwe hauta kuwa AJENDA KUU ya vyama vya upinzani si tu kwa Tanzania, bali duniani pote. Hii inatokana na tafsri ya upinzani lakini pia wajibu wake katika Demokrasia ya mfumo wa vyama vingi duniani.

Naomba nitumie maandiko kadhaa kulithibitisha hili nisemalo, nitaanza na mmoja wa wanasiasa wakongwe na machachari nchini New Zealand, na huyu sio mwingine ila ni Dakta Donald Thomas Don Brash. Dakta Brash alipata kuwa Gavana wa Benki Kuu ya New Zealand, Kiongozi wa Kambi Rasmi Bungeni, Kiongozi wa vyama vya National Party na ACT Party kwa nyakati tofauti. Yeye aliwahi kusema, naomba nimnukuu;

“The Opposition’s main role is to question the government of the day and hold them accountable to the public…. Opposition represents an alternative government, and is responsible for challenging the policies of the government and producing different policies where appropriate.”

Naomba nitoe tafsiri (sio rasmi) Kazi kuu ya upinzani ni KUHOJI serikali iliyoko madarakani na kuifanya iwajibike kwa umma….Upinzani unawakilisha serikali MBADALA na unawajibika kutoa changamoto kwenye sera za serikali na hivyo kutoa sera tofauti/mbadala pale inapowezekana.

Dakta Brash anaongeza kusema, namnukuu; “…one of the most important jobs of the Opposition is to constantly question the Government. Any Government has to remain answerable to the public at all times, and a good Opposition can put the spotlight on serious issues and have them resolved quickly”.

Tafsiri (sio rasmi) Moja ya kazi muhimu za upinzani ni kuendelea kuhoji serikali bila kuchoka, Serikali yeyote inapashwa kuendelea kuwajibika kwa umma muda wote, na upinzani mzuri unaweza kumulika/kuibua mambo na hivyo kurekebishwa kwa haraka.

Lakini pia kwa mujibu wa Taasisi ya Kidemokrasi ya Afrika (Africa Democratic Institute) inasema wajibu wa upinzani katika Demokrasia ni mkubwa sana. Taasisi hii inabainisha baadhi ya kazi/wajibu wa upinzania kuwa ni pamoja na:-

To hold governments accountable (Kuiwajibisha Serikali);
To serve as a credible alternative to the ruling government (Kuwa mbadala wenye kuaminika/thabiti dhidi ya serikali inayotawala);
To promote and stimulate debates in parliament (Kukuza na kuchochea mijadala bungeni);
To be a training ground for future leaders (Kuwa eneo la mafunzo kwa viongozi wa baadaye);

Kwa upande mwingine, mwandishi Sheetal Kumari wa India, anaandika kama ifuatavyo:-
The Opposition parties play a very significant role in a democracy as representatives of the people…to safeguard their interests….The opposition act as watch dog’ of a the system.

Tafsiri (sio rasmi) Vyama vya upinzani vina jukumu muhimu sana katika Demokrasia kwa kuwa wawakilishi wa watu/umma ili kulinda maslahi yao….Upinzani ni mlinzi katika mfumo.

Sio hao tu, pia msomi Julius Kiiza, PhD; kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, katika ‘pepa’ yake ya Wajibu wa Upinzani katika Demokrasia, Kiiza (kama anavyopenda kuitwa) pamoja na mambo mengine anaandika.

“…opposition parties perform several important functions. These include; promoting responsible and reasoned debate. Opposition parties hold the government to account for its commissions or omissions. Parties present a viable alternative to the incumbent government by designing alternative ideas, principles and policies for governing society. Should the party in power let the voters down, the ‘government-in-waiting’ takes over the reign of power – through free and fair elections.”

Kiza anendelea kuandika; “Parties act as a training ground for future leaders, parties strengthen the culture of democracy within the party and the political community in general (by, for example, promoting open debate during delegates’ conferences, promoting intra-party democratic elections and ensuring accountable use of party finances). Parties work with the Electoral Commission, the mass media and civil society organizations to monitor and improve the quality of voter registration, civic education and electoral transparency.

Tasfri (sio rasmi) ya maneno ya Kiiza
...vyama vya upinzani vinafanya kazi kadhaa muhimu. Hizi ni pamoja na; kukuza mijadala na hoja zenye kuleta uwajibikaji. Vyama vya upinzani vinaiwajibisha serikali katika maelekezo na makosa yake. Vyama vinajinadi kama mbadala unayofaa na fanisi dhidi ya serikali iliyoko madarakani katika kubuni mawazo, kanuni na sera mbadala zenye kuongoza umma. Kama itatokea chama tawala kikawaangusha wapiga kura, 'serikali inayosubiri' huchukua madaraka kupitia chaguzi huru na za haki.

Sasa nikirejea kwenye hoja yangu, ukisoma hayo maandiko na mengine mengi tu, hakuna hata moja linalosema kuwa AJENDA KUU YA UPINZANI NI UFISADI. Hivyo kwa wanaotumia maneno kama hayo ya Ndg Kafulila pale wanapoamua kuondoka upinzania, ama wanaamua kudanganya ama hawajui wajibu/agenda kuu ya upinzani ni nini.

Ni vema watoe sababu zengine lakini sio sababu zisizo na mashiko na tena ni MFU kama hizo za aina ya Ndg Kafulila. Lakini pia ukisoma maandiko hayo, na mengine mengi ambayo sikuyanukuu, hakuna mahali panasema njia ya upinzani kuiunga mkono serikali iliyoko madarakani ni kuondoka upinzani na kujiunga chama tawala, kama ingelikuwa ni hivyo. Basi upinzani na wajibu wake utakuwa hauna maana.

Mimi nadhani ni sahihi sana kwa wewe unaona vyuma vimekaza na unaona njia rahisi ni kukimbilia chama tawala, basi ondoka tu, USIUPOTOSHE UMMA. Au kama umeshindwana na wenzio ndani ya chama na ukaona njia sahihi ni wewe kuachana nao, basi ondoka tu, ukipenda kimya kimya au kwa kelele lakini USIUPOTOSHE UMMA. Na kama umeahidiwa CHEO, PESA nk basi we nenda tu kachukue lakini USIUPOTOSHE UMMA.

NAOMBA KUWASILISHA

Dickson Ng’hily
European Zone Coordinator – ACT Wazalendo
22/11/2027
Nasubiri Dickson Ng’hily ahamie CCM nitacheka sana
 
Kumbuka Kafulila anaposema wapinzani ana maana ya CHADEMA kwa sababu anaamini vyama vingine sio wapinzani bali ni matawi ya CCM na CHADEMA!

Kafulila alikuwa mwanachama wa CHADEMA , Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA kwenye dibaji/utangulizi inasema Ufisadi ndio tishio kubwa kabisa la mustakabali wa nchi yetu. Ndio kusema tukitaka tutoke hapa tulipo ni lazima tuukatae na tupambane na ufisadi.

Nmekuwekea sehemu ya utanguliza wa Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA.

‘’Hivi karibuni Rais wetu, Jakaya Mrisho Kikwete, aliulizwa na waandishi wa habari wa Jijini Paris, Ufaransa kwamba “Nchi yako ina utajiri mkubwa wa maliasili, inakuwaje Watanzania ni masikini wa kutupwa?” Alijibu, kwa furaha na kwa kujiamini, “Hata mimi sijui sababu; ninajiuliza kila siku swali hilo lakini sijapata jibu!’’ Huyo ndio dereva wa gari tulilopanda; hajui anakotoka wala aendako. Sote tunaelewa hatari ya kupanda gari ambalo dereva wake hajui anapoenda. Kama Rais wa nchi hajui sababu kwa nini nchi yetu ni maskini atawezaje kupambana na huo umaskini? Hata hivyo, CHADEMA hatuamini kwamba Rais Kikwete hajui chanzo cha umaskini katika nchi yetu. Rais Kikwete anajua chanzo cha umaskini wa nchi yetu lakini hawezi kukitaja kwa kuwa yeye mwenyewe ni sehemu ya tatizo hilo''.

''Kuna sababu tatu zilizosabisha nchi yetu ifike hapa ilipo, nazo ni: ufisadi, ufisadi na ufisadi. Ufisadi ndio tishio kubwa kabisa la mustakabali wa nchi yetu. Ndio kusema tukitaka tutoke hapa tulipo ni lazima tuukatae na tupambane na ufisadi’’.

Kwa mantiki hii, ajenda kuu ya CHADEMA ilikuwa ni kupambana na Ufisadi. Kwa sasa wameachana na ajenda yao kuu.
Ufisadi wa MTU hushughulikiwa na serikali km mtu huyo atakuwa nje ya cc.m
Lkn akiwa bado yupo huko anaitwa mzalendo,
Tafsiri ni
Chama chenu ni mwanvuli na pango la kuwalinda mafisadi,
Ref.Mr Nyaa landu
 
Upinzani sio mahali salama.....well and good. Angeondoka na mkewe basi.
Hata CCM sio mahala salama kutwa wanatishiana kupora kati za uanachama wa CCM hata Spika wa Bunge ndungai amewahi kutishiwa kuporwa uanachama wa CCM endapo atatoa uhuru kwa Wapinzani Bungeni, CCM ya sasa ni ya kidikteta sana ngoja kafulila akajionee huko maana anapenda Majungu na fitna atawakuta wenye Phd za Uzushi ndipo atajutia baadae.
 
Mama usipotoshe! Katambi hakuwa na nafasi kubwa kwenye chama? Mwigamba alikuwa mdogo ndani ya ACT? Waseme ukweli tu kwamba vyuma vimekaza hivyo wanatafuta pa kupumlia!!
Mbona unamsahau mama Anna mngwila
 
Kama CCM wanpiga vita ufisadi basi kwa moyo mweupe kabisa watuambie yafuatayo, ni nani alye lalamikiwa na marehemu S. Stta kuwa amehujumu shirika la reli hadi kufikia kuagiza vichwa vibovu vya treni na kuvitelekeza bandarini , ni nani huyo na sasa ana wadhifa gani serikalini, ni nani aliye uza nyumba za serikali hovyo hovyo hadi zingine kuwapa ndugu zake na wapenzi wake , ni nani huyo na sasa yuko chama gani na ana wadhifa gani, watuambie ni akina nani waliotumia vibaya hela za walipa kodi wa nchi hii katika mchakato wa wa rasimu ya katiba mpya, hao ni akina nani na wako wapi kwani hawajui kuwa watanzania wana wadai mabilion ya shilingi walio hongana kwenye mchakato huo, hao nao watuambie wako chama kipi. Yapo mengi tu nchi hii bado wananchi wengi tu wanachangia visima vya maji ya kunywa na ngedele hilo hawalioni, nchi hii huduma za Afya zime zorota kiasi kwamba watu wapanga foleni kwenye meli ya madkatari toka china utadhani wako loliondo kwenye kikombe cha babu, mikopo kwa ajili ya elimu imekuwa shida mnata watu wasipate elimu ujinga utawale ili muendelee kuwa ibia vizuri rasilimali za Taifa. Acheni zenu hizo mna sema mnapambana na rushwa huku nyie ndio vinara wa wa kutoa hiyo rushwa, semeni ukweli hongo za ajira mmetoa ngapi katika kipindi hiki cha serikali ya awamu tano na bado mmetoa ahadi kuhonga wangapi. Watanzania tunayaona yote haya jaribuni kuwa hata na mshipa wa AIBU.
Dadadadeki!!!
We jamaa!!
Unamiakili km Mimi,
Ulichoongea ni km mkuki
Utumwa wa kimahaba na mkumbo juu ya mtu huyo ndo utafanya wasikujibu,ama wapotoshe uzito wa swali ulilouliza,
Kimoyo moyo wanajua,
Safi sana mkuu,
 
Chukua mfano wa Patrobas unadhani angepewa jukumu gani zaidi ili abaki kwenye chama? Mwenyekiti wa Taifa wa Youth wing??? Halafu useme hawapewi majukumu? Ukweli ni kuwa wameahindwa majukumu.
Kwa hyo ndo kusema kaenda alikoenda ili kupewa nafasi na jukumu,
Upinzani ni zaidi ya kutaka majukumu
 
mnasema magufuli kakomesha ufisadi, awamu hii kwa hiyo ufisadi siyo ajenda kuu kwa vyama pinzani simple logic, labda kama ufisadi unaendelezwa na away hii ya mtukufu magu
Kula gwala mkuu,hakika haupo humu kimakosa
 
Ufisadi wa MTU hushughulikiwa na serikali km mtu huyo atakuwa nje ya cc.m
Lkn akiwa bado yupo huko anaitwa mzalendo,
Tafsiri ni
Chama chenu ni mwanvuli na pango la kuwalinda mafisadi,
Ref.Mr Nyaa landu
Ukiwa ndani ya CCM hata ukiiba nguo za Mtukufu au kinana au Bashite ukauza utaitwa mzalendo na wale waliobuni mladi wa kuwanunua Wapinzani wao kula cha juu 10% kwa sasa wanaitwa mashujaa huko CCM, Udalali wa siasa Ukiwa CCM unaitwa mzalendo, imetengwa Bajeti kubwa sana kwa ajili ya kuwanunua Wapinzani na waliopewa Dhamana ya kuvuruga upinzani wanapiga Ufisadi hiyo pesa ya Umma, watanzania wanalipa kodi kisha pesa zao anapewa Msajili na akina Lipumba bure bure kwa kazi ya kudhoofisha upinzani inauma na inakera sana lakini hakuna mabaya yasiyo na mwisho na mwisho wa ubaya ni Aibu.
 
Awali ya yote naomba kuchukua nafasi kumshukuru Mwenyezi Mungu kutujalia zawadi ya uzima tulio nao.

Bila kupoteza muda, napenda kusema kuwa nimemsikia Ndg Kafulila kupitia (voice note) akithibitisha kuwa ndiye aliyetoa tamko la kujiengua toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Kimsingi sina tatizo na yeye kutoka kwani ni HAKI yake kikatiba kufanya maamuzi aliyoyafanya na hivyo sina PINGAMIZI lolote katika hilo.

Ndg Kafulila anasema kupitia tamko lake kuwa ataujulisha umma ni chama gani atajiunga nacho hivi karibuni, kitu ambacho binafsi naona hakina haja kwani tayari maudhui ya andiko lake yanabainisha ni chama gani atajiunga nacho.

Sasa kama sina tatizo na Ndg Kafulila ku-exercise haki yake kikatiba, kwanini natoa maoni yangu kuhusiana na suala lake la yeye kuondoka Chadema?

Nimeamua kutoa maoni yangu kutokana na ukweli kuwa SIKUBALIANI na hoja kuu ya Ndg kafulila kuwa UPINZANI SIO TENA JUKWAA SALAMA LA KUENDESHA VITA DHIDI YA UFISADI. Adai hii imetokana na vyama vya upinzani kupigwa ganzi (japo hajasema nani kavipiga ganzi na kwanini avipige ganzi) na hivyo UFISADI SIO TENA AJENDA KUU YA UPINZANI.

Labda nisema tu kuwa Ndg Kafulila ni ama kaamua kupotosha umma kwa makusudi au hajui ni nini maana ya VYAMA VYA UPINZANI, lakini pia hajui AJENDA KUU ya vyama hivyo nchini! Kifupi tu ni kwamba, UFISADI haujawahi kuwa na kamwe hauta kuwa AJENDA KUU ya vyama vya upinzani si tu kwa Tanzania, bali duniani pote. Hii inatokana na tafsri ya upinzani lakini pia wajibu wake katika Demokrasia ya mfumo wa vyama vingi duniani.

Naomba nitumie maandiko kadhaa kulithibitisha hili nisemalo, nitaanza na mmoja wa wanasiasa wakongwe na machachari nchini New Zealand, na huyu sio mwingine ila ni Dakta Donald Thomas Don Brash. Dakta Brash alipata kuwa Gavana wa Benki Kuu ya New Zealand, Kiongozi wa Kambi Rasmi Bungeni, Kiongozi wa vyama vya National Party na ACT Party kwa nyakati tofauti. Yeye aliwahi kusema, naomba nimnukuu;

“The Opposition’s main role is to question the government of the day and hold them accountable to the public…. Opposition represents an alternative government, and is responsible for challenging the policies of the government and producing different policies where appropriate.”

Naomba nitoe tafsiri (sio rasmi) Kazi kuu ya upinzani ni KUHOJI serikali iliyoko madarakani na kuifanya iwajibike kwa umma….Upinzani unawakilisha serikali MBADALA na unawajibika kutoa changamoto kwenye sera za serikali na hivyo kutoa sera tofauti/mbadala pale inapowezekana.

Dakta Brash anaongeza kusema, namnukuu; “…one of the most important jobs of the Opposition is to constantly question the Government. Any Government has to remain answerable to the public at all times, and a good Opposition can put the spotlight on serious issues and have them resolved quickly”.

Tafsiri (sio rasmi) Moja ya kazi muhimu za upinzani ni kuendelea kuhoji serikali bila kuchoka, Serikali yeyote inapashwa kuendelea kuwajibika kwa umma muda wote, na upinzani mzuri unaweza kumulika/kuibua mambo na hivyo kurekebishwa kwa haraka.

Lakini pia kwa mujibu wa Taasisi ya Kidemokrasi ya Afrika (Africa Democratic Institute) inasema wajibu wa upinzani katika Demokrasia ni mkubwa sana. Taasisi hii inabainisha baadhi ya kazi/wajibu wa upinzania kuwa ni pamoja na:-

To hold governments accountable (Kuiwajibisha Serikali);
To serve as a credible alternative to the ruling government (Kuwa mbadala wenye kuaminika/thabiti dhidi ya serikali inayotawala);
To promote and stimulate debates in parliament (Kukuza na kuchochea mijadala bungeni);
To be a training ground for future leaders (Kuwa eneo la mafunzo kwa viongozi wa baadaye);

Kwa upande mwingine, mwandishi Sheetal Kumari wa India, anaandika kama ifuatavyo:-
The Opposition parties play a very significant role in a democracy as representatives of the people…to safeguard their interests….The opposition act as watch dog’ of a the system.

Tafsiri (sio rasmi) Vyama vya upinzani vina jukumu muhimu sana katika Demokrasia kwa kuwa wawakilishi wa watu/umma ili kulinda maslahi yao….Upinzani ni mlinzi katika mfumo.

Sio hao tu, pia msomi Julius Kiiza, PhD; kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, katika ‘pepa’ yake ya Wajibu wa Upinzani katika Demokrasia, Kiiza (kama anavyopenda kuitwa) pamoja na mambo mengine anaandika.

“…opposition parties perform several important functions. These include; promoting responsible and reasoned debate. Opposition parties hold the government to account for its commissions or omissions. Parties present a viable alternative to the incumbent government by designing alternative ideas, principles and policies for governing society. Should the party in power let the voters down, the ‘government-in-waiting’ takes over the reign of power – through free and fair elections.”

Kiza anendelea kuandika; “Parties act as a training ground for future leaders, parties strengthen the culture of democracy within the party and the political community in general (by, for example, promoting open debate during delegates’ conferences, promoting intra-party democratic elections and ensuring accountable use of party finances). Parties work with the Electoral Commission, the mass media and civil society organizations to monitor and improve the quality of voter registration, civic education and electoral transparency.

Tasfri (sio rasmi) ya maneno ya Kiiza
...vyama vya upinzani vinafanya kazi kadhaa muhimu. Hizi ni pamoja na; kukuza mijadala na hoja zenye kuleta uwajibikaji. Vyama vya upinzani vinaiwajibisha serikali katika maelekezo na makosa yake. Vyama vinajinadi kama mbadala unayofaa na fanisi dhidi ya serikali iliyoko madarakani katika kubuni mawazo, kanuni na sera mbadala zenye kuongoza umma. Kama itatokea chama tawala kikawaangusha wapiga kura, 'serikali inayosubiri' huchukua madaraka kupitia chaguzi huru na za haki.

Sasa nikirejea kwenye hoja yangu, ukisoma hayo maandiko na mengine mengi tu, hakuna hata moja linalosema kuwa AJENDA KUU YA UPINZANI NI UFISADI. Hivyo kwa wanaotumia maneno kama hayo ya Ndg Kafulila pale wanapoamua kuondoka upinzania, ama wanaamua kudanganya ama hawajui wajibu/agenda kuu ya upinzani ni nini.

Ni vema watoe sababu zengine lakini sio sababu zisizo na mashiko na tena ni MFU kama hizo za aina ya Ndg Kafulila. Lakini pia ukisoma maandiko hayo, na mengine mengi ambayo sikuyanukuu, hakuna mahali panasema njia ya upinzani kuiunga mkono serikali iliyoko madarakani ni kuondoka upinzani na kujiunga chama tawala, kama ingelikuwa ni hivyo. Basi upinzani na wajibu wake utakuwa hauna maana.

Mimi nadhani ni sahihi sana kwa wewe unaona vyuma vimekaza na unaona njia rahisi ni kukimbilia chama tawala, basi ondoka tu, USIUPOTOSHE UMMA. Au kama umeshindwana na wenzio ndani ya chama na ukaona njia sahihi ni wewe kuachana nao, basi ondoka tu, ukipenda kimya kimya au kwa kelele lakini USIUPOTOSHE UMMA. Na kama umeahidiwa CHEO, PESA nk basi we nenda tu kachukue lakini USIUPOTOSHE UMMA.

NAOMBA KUWASILISHA

Dickson Ng’hily
European Zone Coordinator – ACT Wazalendo
22/11/2027

Umeongea vyema sana.NA mbaya zaidi Chama Tawala hakijaelewa nini maana ya UPINZANI/Vyama vingi kwao maana yake kuu ni UADUI.

NB😛eleka article yako kwenye gazeti wengi wapate kuelewa maana halisi ya upinzani
 
Waha wana matatizo
 
Kwani serikali haipaswi kuwajibika unapotokea ufisadi? Mbona akina Mlongo waliachia ngazi baada ya escrow, sio kuwajibika huko? Naomba nieleweshwe maana ya neno 'kuwajibika'
 
Ukiwa ndani ya CCM hata ukiiba nguo za Mtukufu au kinana au Bashite ukauza utaitwa mzalendo na wale waliobuni mladi wa kuwanunua Wapinzani wao kula cha juu 10% kwa sasa wanaitwa mashujaa huko CCM, Udalali wa siasa Ukiwa CCM unaitwa mzalendo, imetengwa Bajeti kubwa sana kwa ajili ya kuwanunua Wapinzani na waliopewa Dhamana ya kuvuruga upinzani wanapiga Ufisadi hiyo pesa ya Umma, watanzania wanalipa kodi kisha pesa zao anapewa Msajili na akina Lipumba bure bure kwa kazi ya kudhoofisha upinzani inauma na inakera sana lakini hakuna mabaya yasiyo na mwisho na mwisho wa ubaya ni Aibu.
Naaaaam kaka,
Halafu eti
Mniombeeee
 
Good analysis. Hawa njaa inawasumbua. Mtu mwenye akili timamu na usie njaaa huwezi kuhama chama kwa sababu za kijinga. Haya majitu yanakera kweli kweli.
 
Effectively katika maslahi gani ya taifa? Hasi au chanya?
Mfano mtu kama Polepole sasa hivi waweza kumuita ni faida kwa taifa?

Mtani wnagu naye naona vyuma vimekaza,muelimishe ataelewa
 
Hujasema agenda ya vyama vya upinzani hapa Tanzania ni nn. So ufisadi sio inshu ya kuzungumziwa? Na kwann wanaogopa kilizungumzia

AMeeleza vizuri sana msome upya tena na tena ndiyo nyie akina Kafulila unaulizwa 1+2 ngapi unajibu 2+1 ngapi
 
Vijana wanaingia upinzani hawapewi majukumu Kwa kuwa uongozi uko mikononi mwa wachache. Waache wajitafutie chimbo watakakotumika effectively

Mtani acha hizo rafiki,hivi upinzani unafursa gani ya kumpa kijana ambaye ni mwanachama wa Chama cahke au kiongozi wa chama chake??Ni bora wakati mwingine kumtrain asiyeenda shule kuliko hawa wenye degree zao
 
nadhani agenda ya ifisadi ndo agenda kubwa iliyofanya kuvifikisha vyama vingi na ata ivi vya kwetu hapo vilipofika bila kupambana na ufisadi utapata wapi utawala bora utaweza wapi kukusanya kodi bila kukusanya kodi hizo huduma muhimu unazoitaji kuwaletea wananchi wako fedha utatoa wapi mimi nafikili mtu kutoa mawazo yake na hali anayoiona ktk chama atokacho si vibaya ni maoni yake na ujinga mkubwa tulionao tumejikita sana na kununuliwa mkiimanisha njaa lakini amtaki kujikita ktk utafiti kuwa kuna nini hasa kinafanya hawa wanasiasa wanahama vyama lipo tatizo na moja ya tatizo viongoz wengi wa hivi vyama awataki kukubar kukosolewa na hili si hapa kwetu tu ni nchi nyingi za ki afrika hapa kwetu kumeibuka tatizo kubwa kuwa kila atoae mawazo yake anaambiwa njaa amenunuliwa n.k huu ni upuuz ambao watu wengi wamelishwa vichwani mwao na watawala wa vyama nani kansa mbaya

Chuki iliyojengeka kwenye itikadi za siasa.Uoga wa wanasiasa hasa pale linapokuja swala la kuhoji.Awamu ya tano haitaki kuhojiwa na haitaki upinznai kabisa kabsia kwa hiyo njia rahisi ni kuua upinzani au kuwaondoa dunia hii
 
Kiongozi, hiyo ilikuwa ni typing error na nimeisharekebisha...ni sawa na mahali niliandika upinzania badala ya upinzani, nimejitahidi kufanya mabadiliko. Hao wasamehe bure tu...

Hebu liweke badiko lako kwa Kiswahili bila kuchanganya na kiingereza naona kuna watu wanapiga fyuuuuuuuuuuu maana wanatoka kapa kabisa
 
Back
Top Bottom