Kafulila Asipotoshe Umma

Kafulila Asipotoshe Umma

Awali ya yote naomba kuchukua nafasi kumshukuru Mwenyezi Mungu kutujalia zawadi ya uzima tulio nao.

Bila kupoteza muda, napenda kusema kuwa nimemsikia Ndg Kafulila kupitia (voice note) akithibitisha kuwa ndiye aliyetoa tamko la kujiengua toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Kimsingi sina tatizo na yeye kutoka kwani ni HAKI yake kikatiba kufanya maamuzi aliyoyafanya na hivyo sina PINGAMIZI lolote katika hilo.

Ndg Kafulila anasema kupitia tamko lake kuwa ataujulisha umma ni chama gani atajiunga nacho hivi karibuni, kitu ambacho binafsi naona hakina haja kwani tayari maudhui ya andiko lake yanabainisha ni chama gani atajiunga nacho.

Sasa kama sina tatizo na Ndg Kafulila ku-exercise haki yake kikatiba, kwanini natoa maoni yangu kuhusiana na suala lake la yeye kuondoka Chadema?

Nimeamua kutoa maoni yangu kutokana na ukweli kuwa SIKUBALIANI na hoja kuu ya Ndg kafulila kuwa UPINZANI SIO TENA JUKWAA SALAMA LA KUENDESHA VITA DHIDI YA UFISADI. Adai hii imetokana na vyama vya upinzani kupigwa ganzi (japo hajasema nani kavipiga ganzi na kwanini avipige ganzi) na hivyo UFISADI SIO TENA AJENDA KUU YA UPINZANI.

Labda nisema tu kuwa Ndg Kafulila ni ama kaamua kupotosha umma kwa makusudi au hajui ni nini maana ya VYAMA VYA UPINZANI, lakini pia hajui AJENDA KUU ya vyama hivyo nchini! Kifupi tu ni kwamba, UFISADI haujawahi kuwa na kamwe hauta kuwa AJENDA KUU ya vyama vya upinzani si tu kwa Tanzania, bali duniani pote. Hii inatokana na tafsri ya upinzani lakini pia wajibu wake katika Demokrasia ya mfumo wa vyama vingi duniani.

Naomba nitumie maandiko kadhaa kulithibitisha hili nisemalo, nitaanza na mmoja wa wanasiasa wakongwe na machachari nchini New Zealand, na huyu sio mwingine ila ni Dakta Donald Thomas Don Brash. Dakta Brash alipata kuwa Gavana wa Benki Kuu ya New Zealand, Kiongozi wa Kambi Rasmi Bungeni, Kiongozi wa vyama vya National Party na ACT Party kwa nyakati tofauti. Yeye aliwahi kusema, naomba nimnukuu;

“The Opposition’s main role is to question the government of the day and hold them accountable to the public…. Opposition represents an alternative government, and is responsible for challenging the policies of the government and producing different policies where appropriate.”

Naomba nitoe tafsiri (sio rasmi) Kazi kuu ya upinzani ni KUHOJI serikali iliyoko madarakani na kuifanya iwajibike kwa umma….Upinzani unawakilisha serikali MBADALA na unawajibika kutoa changamoto kwenye sera za serikali na hivyo kutoa sera tofauti/mbadala pale inapowezekana.

Dakta Brash anaongeza kusema, namnukuu; “…one of the most important jobs of the Opposition is to constantly question the Government. Any Government has to remain answerable to the public at all times, and a good Opposition can put the spotlight on serious issues and have them resolved quickly”.

Tafsiri (sio rasmi) Moja ya kazi muhimu za upinzani ni kuendelea kuhoji serikali bila kuchoka, Serikali yeyote inapashwa kuendelea kuwajibika kwa umma muda wote, na upinzani mzuri unaweza kumulika/kuibua mambo na hivyo kurekebishwa kwa haraka.

Lakini pia kwa mujibu wa Taasisi ya Kidemokrasi ya Afrika (Africa Democratic Institute) inasema wajibu wa upinzani katika Demokrasia ni mkubwa sana. Taasisi hii inabainisha baadhi ya kazi/wajibu wa upinzania kuwa ni pamoja na:-

To hold governments accountable (Kuiwajibisha Serikali);
To serve as a credible alternative to the ruling government (Kuwa mbadala wenye kuaminika/thabiti dhidi ya serikali inayotawala);
To promote and stimulate debates in parliament (Kukuza na kuchochea mijadala bungeni);
To be a training ground for future leaders (Kuwa eneo la mafunzo kwa viongozi wa baadaye);

Kwa upande mwingine, mwandishi Sheetal Kumari wa India, anaandika kama ifuatavyo:-
The Opposition parties play a very significant role in a democracy as representatives of the people…to safeguard their interests….The opposition act as watch dog’ of a the system.

Tafsiri (sio rasmi) Vyama vya upinzani vina jukumu muhimu sana katika Demokrasia kwa kuwa wawakilishi wa watu/umma ili kulinda maslahi yao….Upinzani ni mlinzi katika mfumo.

Sio hao tu, pia msomi Julius Kiiza, PhD; kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, katika ‘pepa’ yake ya Wajibu wa Upinzani katika Demokrasia, Kiiza (kama anavyopenda kuitwa) pamoja na mambo mengine anaandika.

“…opposition parties perform several important functions. These include; promoting responsible and reasoned debate. Opposition parties hold the government to account for its commissions or omissions. Parties present a viable alternative to the incumbent government by designing alternative ideas, principles and policies for governing society. Should the party in power let the voters down, the ‘government-in-waiting’ takes over the reign of power – through free and fair elections.”

Kiza anendelea kuandika; “Parties act as a training ground for future leaders, parties strengthen the culture of democracy within the party and the political community in general (by, for example, promoting open debate during delegates’ conferences, promoting intra-party democratic elections and ensuring accountable use of party finances). Parties work with the Electoral Commission, the mass media and civil society organizations to monitor and improve the quality of voter registration, civic education and electoral transparency.

Tasfri (sio rasmi) ya maneno ya Kiiza
...vyama vya upinzani vinafanya kazi kadhaa muhimu. Hizi ni pamoja na; kukuza mijadala na hoja zenye kuleta uwajibikaji. Vyama vya upinzani vinaiwajibisha serikali katika maelekezo na makosa yake. Vyama vinajinadi kama mbadala unayofaa na fanisi dhidi ya serikali iliyoko madarakani katika kubuni mawazo, kanuni na sera mbadala zenye kuongoza umma. Kama itatokea chama tawala kikawaangusha wapiga kura, 'serikali inayosubiri' huchukua madaraka kupitia chaguzi huru na za haki.

Sasa nikirejea kwenye hoja yangu, ukisoma hayo maandiko na mengine mengi tu, hakuna hata moja linalosema kuwa AJENDA KUU YA UPINZANI NI UFISADI. Hivyo kwa wanaotumia maneno kama hayo ya Ndg Kafulila pale wanapoamua kuondoka upinzania, ama wanaamua kudanganya ama hawajui wajibu/agenda kuu ya upinzani ni nini.

Ni vema watoe sababu zengine lakini sio sababu zisizo na mashiko na tena ni MFU kama hizo za aina ya Ndg Kafulila. Lakini pia ukisoma maandiko hayo, na mengine mengi ambayo sikuyanukuu, hakuna mahali panasema njia ya upinzani kuiunga mkono serikali iliyoko madarakani ni kuondoka upinzani na kujiunga chama tawala, kama ingelikuwa ni hivyo. Basi upinzani na wajibu wake utakuwa hauna maana.

Mimi nadhani ni sahihi sana kwa wewe unaona vyuma vimekaza na unaona njia rahisi ni kukimbilia chama tawala, basi ondoka tu, USIUPOTOSHE UMMA. Au kama umeshindwana na wenzio ndani ya chama na ukaona njia sahihi ni wewe kuachana nao, basi ondoka tu, ukipenda kimya kimya au kwa kelele lakini USIUPOTOSHE UMMA. Na kama umeahidiwa CHEO, PESA nk basi we nenda tu kachukue lakini USIUPOTOSHE UMMA.

NAOMBA KUWASILISHA

Dickson Ng’hily
European Zone Coordinator – ACT Wazalendo
22/11/2027
Hakuna upinzani pasi na elimu au pesa umemuongelea dkt thomas wa newsland huyu tu anakuonesha kuwa ni msomi na alikuwa gavana tayari anauwezo wa kielimu na pesa,Tz upinzani unaungwa na walalahoi matatizo chungu nzima elimu ndiyo hamna kabisaaaa umbumbumbu mwingi,NASISITISHA HAKUNA UPINZANI WA KWELI PALIPO NA NJAA NA UMASKINI KAMA TZ
 
Ni ukweli kuwa upinzani una majukumu mengi kwa ustawi wa Taifa. Lakini kwa Kafulila na baadhi yetu wengine kilichotushawishi kusapoti upinzani ni jinsi walivyotumia nguvu na ujasiri mwingi kuupinga na kupambana na ufisadi nchini.

Sasa huyu Kafulila anapoona hii agenda imefutika katika vyama vya upinzani na kwa bahati mbaya mafisadi wanapoona moto utawawakia wakibaki chama tawala wanahamia upinzani na kupewa usalama yeye Kafulila ameshindwa kuvumilia kubaki upinzani.

Hajasema upinzani hauna jukumu nchi hii bali tu kuachana na agenda ya ufisadi kumemchefua Kafulila kiasi cha kuamua kuachana nao. Tumwache ana haki yake kikatiba.
 
Kiukweli kabisa watu wamepigwa na butwaa
Na hata wanachokijadili hakieleweki na hakielelkezeki tena.

Kama mtakubali turudisheni mpira kwa kipa tujipange hii turnover sio ya kawaida, kuziba masikio ni kupoteza muda, UKAWA kuna mahali wanamakosa yanayohitaji overhaul au review.

Kuwashambulia waliotoka au wanaotoka Bado sio jibu watz wanataka ubunifu zaidi kutoka upinzani
 
Awali ya yote naomba kuchukua nafasi kumshukuru Mwenyezi Mungu kutujalia zawadi ya uzima tulio nao.

Bila kupoteza muda, napenda kusema kuwa nimemsikia Ndg Kafulila kupitia (voice note) akithibitisha kuwa ndiye aliyetoa tamko la kujiengua toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Kimsingi sina tatizo na yeye kutoka kwani ni HAKI yake kikatiba kufanya maamuzi aliyoyafanya na hivyo sina PINGAMIZI lolote katika hilo.

Ndg Kafulila anasema kupitia tamko lake kuwa ataujulisha umma ni chama gani atajiunga nacho hivi karibuni, kitu ambacho binafsi naona hakina haja kwani tayari maudhui ya andiko lake yanabainisha ni chama gani atajiunga nacho.

Sasa kama sina tatizo na Ndg Kafulila ku-exercise haki yake kikatiba, kwanini natoa maoni yangu kuhusiana na suala lake la yeye kuondoka Chadema?

Nimeamua kutoa maoni yangu kutokana na ukweli kuwa SIKUBALIANI na hoja kuu ya Ndg kafulila kuwa UPINZANI SIO TENA JUKWAA SALAMA LA KUENDESHA VITA DHIDI YA UFISADI. Adai hii imetokana na vyama vya upinzani kupigwa ganzi (japo hajasema nani kavipiga ganzi na kwanini avipige ganzi) na hivyo UFISADI SIO TENA AJENDA KUU YA UPINZANI.

Labda nisema tu kuwa Ndg Kafulila ni ama kaamua kupotosha umma kwa makusudi au hajui ni nini maana ya VYAMA VYA UPINZANI, lakini pia hajui AJENDA KUU ya vyama hivyo nchini! Kifupi tu ni kwamba, UFISADI haujawahi kuwa na kamwe hauta kuwa AJENDA KUU ya vyama vya upinzani si tu kwa Tanzania, bali duniani pote. Hii inatokana na tafsri ya upinzani lakini pia wajibu wake katika Demokrasia ya mfumo wa vyama vingi duniani.

Naomba nitumie maandiko kadhaa kulithibitisha hili nisemalo, nitaanza na mmoja wa wanasiasa wakongwe na machachari nchini New Zealand, na huyu sio mwingine ila ni Dakta Donald Thomas Don Brash. Dakta Brash alipata kuwa Gavana wa Benki Kuu ya New Zealand, Kiongozi wa Kambi Rasmi Bungeni, Kiongozi wa vyama vya National Party na ACT Party kwa nyakati tofauti. Yeye aliwahi kusema, naomba nimnukuu;

“The Opposition’s main role is to question the government of the day and hold them accountable to the public…. Opposition represents an alternative government, and is responsible for challenging the policies of the government and producing different policies where appropriate.”

Naomba nitoe tafsiri (sio rasmi) Kazi kuu ya upinzani ni KUHOJI serikali iliyoko madarakani na kuifanya iwajibike kwa umma….Upinzani unawakilisha serikali MBADALA na unawajibika kutoa changamoto kwenye sera za serikali na hivyo kutoa sera tofauti/mbadala pale inapowezekana.

Dakta Brash anaongeza kusema, namnukuu; “…one of the most important jobs of the Opposition is to constantly question the Government. Any Government has to remain answerable to the public at all times, and a good Opposition can put the spotlight on serious issues and have them resolved quickly”.

Tafsiri (sio rasmi) Moja ya kazi muhimu za upinzani ni kuendelea kuhoji serikali bila kuchoka, Serikali yeyote inapashwa kuendelea kuwajibika kwa umma muda wote, na upinzani mzuri unaweza kumulika/kuibua mambo na hivyo kurekebishwa kwa haraka.

Lakini pia kwa mujibu wa Taasisi ya Kidemokrasi ya Afrika (Africa Democratic Institute) inasema wajibu wa upinzani katika Demokrasia ni mkubwa sana. Taasisi hii inabainisha baadhi ya kazi/wajibu wa upinzania kuwa ni pamoja na:-

To hold governments accountable (Kuiwajibisha Serikali);
To serve as a credible alternative to the ruling government (Kuwa mbadala wenye kuaminika/thabiti dhidi ya serikali inayotawala);
To promote and stimulate debates in parliament (Kukuza na kuchochea mijadala bungeni);
To be a training ground for future leaders (Kuwa eneo la mafunzo kwa viongozi wa baadaye);

Kwa upande mwingine, mwandishi Sheetal Kumari wa India, anaandika kama ifuatavyo:-
The Opposition parties play a very significant role in a democracy as representatives of the people…to safeguard their interests….The opposition act as watch dog’ of a the system.

Tafsiri (sio rasmi) Vyama vya upinzani vina jukumu muhimu sana katika Demokrasia kwa kuwa wawakilishi wa watu/umma ili kulinda maslahi yao….Upinzani ni mlinzi katika mfumo.

Sio hao tu, pia msomi Julius Kiiza, PhD; kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, katika ‘pepa’ yake ya Wajibu wa Upinzani katika Demokrasia, Kiiza (kama anavyopenda kuitwa) pamoja na mambo mengine anaandika.

“…opposition parties perform several important functions. These include; promoting responsible and reasoned debate. Opposition parties hold the government to account for its commissions or omissions. Parties present a viable alternative to the incumbent government by designing alternative ideas, principles and policies for governing society. Should the party in power let the voters down, the ‘government-in-waiting’ takes over the reign of power – through free and fair elections.”

Kiza anendelea kuandika; “Parties act as a training ground for future leaders, parties strengthen the culture of democracy within the party and the political community in general (by, for example, promoting open debate during delegates’ conferences, promoting intra-party democratic elections and ensuring accountable use of party finances). Parties work with the Electoral Commission, the mass media and civil society organizations to monitor and improve the quality of voter registration, civic education and electoral transparency.

Tasfri (sio rasmi) ya maneno ya Kiiza
...vyama vya upinzani vinafanya kazi kadhaa muhimu. Hizi ni pamoja na; kukuza mijadala na hoja zenye kuleta uwajibikaji. Vyama vya upinzani vinaiwajibisha serikali katika maelekezo na makosa yake. Vyama vinajinadi kama mbadala unayofaa na fanisi dhidi ya serikali iliyoko madarakani katika kubuni mawazo, kanuni na sera mbadala zenye kuongoza umma. Kama itatokea chama tawala kikawaangusha wapiga kura, 'serikali inayosubiri' huchukua madaraka kupitia chaguzi huru na za haki.

Sasa nikirejea kwenye hoja yangu, ukisoma hayo maandiko na mengine mengi tu, hakuna hata moja linalosema kuwa AJENDA KUU YA UPINZANI NI UFISADI. Hivyo kwa wanaotumia maneno kama hayo ya Ndg Kafulila pale wanapoamua kuondoka upinzania, ama wanaamua kudanganya ama hawajui wajibu/agenda kuu ya upinzani ni nini.

Ni vema watoe sababu zengine lakini sio sababu zisizo na mashiko na tena ni MFU kama hizo za aina ya Ndg Kafulila. Lakini pia ukisoma maandiko hayo, na mengine mengi ambayo sikuyanukuu, hakuna mahali panasema njia ya upinzani kuiunga mkono serikali iliyoko madarakani ni kuondoka upinzani na kujiunga chama tawala, kama ingelikuwa ni hivyo. Basi upinzani na wajibu wake utakuwa hauna maana.

Mimi nadhani ni sahihi sana kwa wewe unaona vyuma vimekaza na unaona njia rahisi ni kukimbilia chama tawala, basi ondoka tu, USIUPOTOSHE UMMA. Au kama umeshindwana na wenzio ndani ya chama na ukaona njia sahihi ni wewe kuachana nao, basi ondoka tu, ukipenda kimya kimya au kwa kelele lakini USIUPOTOSHE UMMA. Na kama umeahidiwa CHEO, PESA nk basi we nenda tu kachukue lakini USIUPOTOSHE UMMA.

NAOMBA KUWASILISHA

Dickson Ng’hily
European Zone Coordinator – ACT Wazalendo
22/11/2027
Sawa, things are supposed to be like that, ila kwa takriban miaka kadhaa huko nyuma CHADEMA wenyewe kama model ya upinzani nchini walisimama kidete na hoja ya ufisadi kama agenda kuu ktk kuipinga CCM na serikali yake na kwa kweli iliwasababishia Political positive Impact ktk Mass mobilization, sasa ukilinganisha na msimamo wa CHADEMA ya sasa huoni hii ina create grounds za mashiko ktk tuhuma za Kafulila dhidi ya upinzani?.
 
Kafulila njaa imemtoa huko! Upinzani na njaa kichwani??? Sasa ananyemelea u DC wameshamwambia jitoe akili upate ulaji japo miaka hii 3 ukijipanga kurudi jimboni! Njaaaaa hakuna lingine
Si mmesikia mbwa mtembea bure c sawa na mkaa bure ameamua atembee huenda akaokota mfupa lakini
ajitizame mkia mbona kama umekatwa
 
Kafulila aliweza kuwa kiongozi kwa sababu wananchi walitaka mabadiliko lakini siyo kwa sababu alikuwa na uwezo. Sidhani kama anaelewa dhana ya chama cha upinzani.
Unamzungumzia Kafulila yupi huyu aliyeibua na Ku sacrifice maisha yake dhidi ya tuhuma nzito za Escrow au?
 
Awali ya yote naomba kuchukua nafasi kumshukuru Mwenyezi Mungu kutujalia zawadi ya uzima tulio nao.

Bila kupoteza muda, napenda kusema kuwa nimemsikia Ndg Kafulila kupitia (voice note) akithibitisha kuwa ndiye aliyetoa tamko la kujiengua toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Kimsingi sina tatizo na yeye kutoka kwani ni HAKI yake kikatiba kufanya maamuzi aliyoyafanya na hivyo sina PINGAMIZI lolote katika hilo.

Ndg Kafulila anasema kupitia tamko lake kuwa ataujulisha umma ni chama gani atajiunga nacho hivi karibuni, kitu ambacho binafsi naona hakina haja kwani tayari maudhui ya andiko lake yanabainisha ni chama gani atajiunga nacho.

Sasa kama sina tatizo na Ndg Kafulila ku-exercise haki yake kikatiba, kwanini natoa maoni yangu kuhusiana na suala lake la yeye kuondoka Chadema?

Nimeamua kutoa maoni yangu kutokana na ukweli kuwa SIKUBALIANI na hoja kuu ya Ndg kafulila kuwa UPINZANI SIO TENA JUKWAA SALAMA LA KUENDESHA VITA DHIDI YA UFISADI. Adai hii imetokana na vyama vya upinzani kupigwa ganzi (japo hajasema nani kavipiga ganzi na kwanini avipige ganzi) na hivyo UFISADI SIO TENA AJENDA KUU YA UPINZANI.

Labda nisema tu kuwa Ndg Kafulila ni ama kaamua kupotosha umma kwa makusudi au hajui ni nini maana ya VYAMA VYA UPINZANI, lakini pia hajui AJENDA KUU ya vyama hivyo nchini! Kifupi tu ni kwamba, UFISADI haujawahi kuwa na kamwe hauta kuwa AJENDA KUU ya vyama vya upinzani si tu kwa Tanzania, bali duniani pote. Hii inatokana na tafsri ya upinzani lakini pia wajibu wake katika Demokrasia ya mfumo wa vyama vingi duniani.

Naomba nitumie maandiko kadhaa kulithibitisha hili nisemalo, nitaanza na mmoja wa wanasiasa wakongwe na machachari nchini New Zealand, na huyu sio mwingine ila ni Dakta Donald Thomas Don Brash. Dakta Brash alipata kuwa Gavana wa Benki Kuu ya New Zealand, Kiongozi wa Kambi Rasmi Bungeni, Kiongozi wa vyama vya National Party na ACT Party kwa nyakati tofauti. Yeye aliwahi kusema, naomba nimnukuu;

“The Opposition’s main role is to question the government of the day and hold them accountable to the public…. Opposition represents an alternative government, and is responsible for challenging the policies of the government and producing different policies where appropriate.”

Naomba nitoe tafsiri (sio rasmi) Kazi kuu ya upinzani ni KUHOJI serikali iliyoko madarakani na kuifanya iwajibike kwa umma….Upinzani unawakilisha serikali MBADALA na unawajibika kutoa changamoto kwenye sera za serikali na hivyo kutoa sera tofauti/mbadala pale inapowezekana.

Dakta Brash anaongeza kusema, namnukuu; “…one of the most important jobs of the Opposition is to constantly question the Government. Any Government has to remain answerable to the public at all times, and a good Opposition can put the spotlight on serious issues and have them resolved quickly”.

Tafsiri (sio rasmi) Moja ya kazi muhimu za upinzani ni kuendelea kuhoji serikali bila kuchoka, Serikali yeyote inapashwa kuendelea kuwajibika kwa umma muda wote, na upinzani mzuri unaweza kumulika/kuibua mambo na hivyo kurekebishwa kwa haraka.

Lakini pia kwa mujibu wa Taasisi ya Kidemokrasi ya Afrika (Africa Democratic Institute) inasema wajibu wa upinzani katika Demokrasia ni mkubwa sana. Taasisi hii inabainisha baadhi ya kazi/wajibu wa upinzania kuwa ni pamoja na:-

To hold governments accountable (Kuiwajibisha Serikali);
To serve as a credible alternative to the ruling government (Kuwa mbadala wenye kuaminika/thabiti dhidi ya serikali inayotawala);
To promote and stimulate debates in parliament (Kukuza na kuchochea mijadala bungeni);
To be a training ground for future leaders (Kuwa eneo la mafunzo kwa viongozi wa baadaye);

Kwa upande mwingine, mwandishi Sheetal Kumari wa India, anaandika kama ifuatavyo:-
The Opposition parties play a very significant role in a democracy as representatives of the people…to safeguard their interests….The opposition act as watch dog’ of a the system.

Tafsiri (sio rasmi) Vyama vya upinzani vina jukumu muhimu sana katika Demokrasia kwa kuwa wawakilishi wa watu/umma ili kulinda maslahi yao….Upinzani ni mlinzi katika mfumo.

Sio hao tu, pia msomi Julius Kiiza, PhD; kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, katika ‘pepa’ yake ya Wajibu wa Upinzani katika Demokrasia, Kiiza (kama anavyopenda kuitwa) pamoja na mambo mengine anaandika.

“…opposition parties perform several important functions. These include; promoting responsible and reasoned debate. Opposition parties hold the government to account for its commissions or omissions. Parties present a viable alternative to the incumbent government by designing alternative ideas, principles and policies for governing society. Should the party in power let the voters down, the ‘government-in-waiting’ takes over the reign of power – through free and fair elections.”

Kiza anendelea kuandika; “Parties act as a training ground for future leaders, parties strengthen the culture of democracy within the party and the political community in general (by, for example, promoting open debate during delegates’ conferences, promoting intra-party democratic elections and ensuring accountable use of party finances). Parties work with the Electoral Commission, the mass media and civil society organizations to monitor and improve the quality of voter registration, civic education and electoral transparency.

Tasfri (sio rasmi) ya maneno ya Kiiza
...vyama vya upinzani vinafanya kazi kadhaa muhimu. Hizi ni pamoja na; kukuza mijadala na hoja zenye kuleta uwajibikaji. Vyama vya upinzani vinaiwajibisha serikali katika maelekezo na makosa yake. Vyama vinajinadi kama mbadala unayofaa na fanisi dhidi ya serikali iliyoko madarakani katika kubuni mawazo, kanuni na sera mbadala zenye kuongoza umma. Kama itatokea chama tawala kikawaangusha wapiga kura, 'serikali inayosubiri' huchukua madaraka kupitia chaguzi huru na za haki.

Sasa nikirejea kwenye hoja yangu, ukisoma hayo maandiko na mengine mengi tu, hakuna hata moja linalosema kuwa AJENDA KUU YA UPINZANI NI UFISADI. Hivyo kwa wanaotumia maneno kama hayo ya Ndg Kafulila pale wanapoamua kuondoka upinzania, ama wanaamua kudanganya ama hawajui wajibu/agenda kuu ya upinzani ni nini.

Ni vema watoe sababu zengine lakini sio sababu zisizo na mashiko na tena ni MFU kama hizo za aina ya Ndg Kafulila. Lakini pia ukisoma maandiko hayo, na mengine mengi ambayo sikuyanukuu, hakuna mahali panasema njia ya upinzani kuiunga mkono serikali iliyoko madarakani ni kuondoka upinzani na kujiunga chama tawala, kama ingelikuwa ni hivyo. Basi upinzani na wajibu wake utakuwa hauna maana.

Mimi nadhani ni sahihi sana kwa wewe unaona vyuma vimekaza na unaona njia rahisi ni kukimbilia chama tawala, basi ondoka tu, USIUPOTOSHE UMMA. Au kama umeshindwana na wenzio ndani ya chama na ukaona njia sahihi ni wewe kuachana nao, basi ondoka tu, ukipenda kimya kimya au kwa kelele lakini USIUPOTOSHE UMMA. Na kama umeahidiwa CHEO, PESA nk basi we nenda tu kachukue lakini USIUPOTOSHE UMMA.

NAOMBA KUWASILISHA

Dickson Ng’hily
European Zone Coordinator – ACT Wazalendo
22/11/2027
Shukrani kwa andiko lako nimejifunza zaidi na kuelewa nini maana ya upinzani,ila inasikitisha kuona huyo jamaa kwa kipindi chote hicho hakuwa anajua maana ya upinzani,ok ni aina ya viongozi tulionawo sijui ni njaa.
 
Nyie mnaojisema ni wapinzani huku mnakimbia kimbia tu bila sera mtakufa hivi karibuni. Achana na mchapo ya mitaani kama mnataka mfike mnakotaka.

Kwa hali iliyowazi kabisa. Upinzani unawayawaya sana.
 
kafulila ni mbabaishaji ,lets wait and see uko anapoelekea nn kitatokea daaaaah siasa za bongo bana
 
Kafulila tangu amnadi lowasa nilimdharau sana
 
Ambacho Chadema hawajagundua bado ccm wanawawangia mchana na usiku wenyewe wakiwa wamelala usingizi, ccm iko busy kushawishi wanachadema wote wenye ushawishi kuhamia ccm wakija kushtuka wote wameiacha hapo ndipo hata Mbowe atajivua uanachama. Yote haya yakitokea tutakuwa tumerasimisha na kubariki udikteta maana hata katiba ikibadilishwa kuongeza miaka ya urais kwa mfano kutakuwa hakuna wa kupinga... baada ya hapo itafuata miaka mingi ya kulia na kusaga meno...mark my words. Cuf imemalizwa, Chadema na Act vinamalizwa kwa mpigo, Nccr ni kama haipo. Wake up and smell the coffee. Magufuli is swating the opposition like flies.

Uko sahihi sana ingawa hakuna CHADEMA inachoweza kufanya kuzuia CCM/serikali inayotumia hazina ya taifa na nguvu za dola kuua upinzani zaidi ya kutegemea mshikamano wa wananchi wote kupinga hujuma hiyo inayolielekeza taifa kwenye mfumo wa udikteta kamili.

Na NAKUHAKIKISHIA CCM/serikali ikifanikiwa kuua upinzani makini nchini, watakaolia na kusaga meno si CHADEMA, NCCR, ACT na CUF pekee bali hata wana-CCM wenyewe. Tena hao ndio watalia zaidi huku wakisakamwa na aibu ya kuendekeza uovu na ujinga usiomithilika. Kwa kifupi hakuna atakayekuwa salama nchini. Soma historia ya Hitler alipoanzia hadi kuishia. Hakuanza kama mtu wa ovyo ovyo.

Yaliyowapata Nape na Lissu ni kidokezo tu cha mwelekeo wa hiyo CCM inayojengwa leo hii kwa kuua sauti makini ya upinzani (voice of objective dissent). Tusisahau kuwa sauti ya upinzani husaidia hata ndani ya chama tawala. Magufuli mwenyewe alifurahia harakati za Kafulila kuhusu Escrow acc scandal. Leo yeye hataki kabisa sauti ya aina hiyo isikike kwenye utawala wake kiasi cha kutumia pesa za umma na nguvu ya dola kuzima upinzani. It’s up to all Tanzanian’s to wake up and smell the coffee!
 
mafisadi wanafugwa ndani ya ccm wakiacha ufisadi wanahama chama hivyo Kafulila ameamua kuwafuata hukohuko kabla awajaacha tabia yao ya ufisadi,lakini cha kujiulisa ataweza kuwafungulia mdomo au na yeye atasubiri mpaka waame chama ndio aseme?
 
Mleta mada yuko mbioni kuhamia CCM. Ni suala LA muda tu
 
Kweli kabisa . Chama hakiwezi kununuliwa na LOWASA halafu kikaendelea kuufanya UFISADI kuwa ajenda kama zamani.

Lowasa hakunnua chama bali ni wajinga pekee waliokariri propaganda za CCM kuwa Lowasa kanunua chama, wale mbumbu mpaka lao wanaamini hilo lakini Wajanja kuliko ww huko huko CCM wanajua Richmond ni ya kikwete na Ufisadi upo huko huko CCM na ajenda ya Ufisadi ipo chadema bali vyama vya upinzani hawapo huru hawaruhusiwi kufanya mikutano mikubwa ya wazi ili waibue Ufisadi wa ununuzi wa ndege, ujenzi wa reli, chato Airport, michango ya rambirambi, vibali vya Sukari, kivuko cha Dsm -Bagamoyo,

Pesa inayochotwa hazina kwenda kwa Lipumba kwa ajili ya kudhoofisha upinzani huko CCM kwako kuna wizi wa kutisha ndiyo maana mmezibwa midomo kwa vitisho vya kuvuliwa uanachama wa CCM na mnazuia mikutano ya Upinzani kuwabambikia kesi kuwakomoa ili wasipate nafasi ya kuanika Ufisadi wenu.
 
Upinzani sio mahali salama.....well and good. Angeondoka na mkewe basi.
 
mafisadi wanafugwa ndani ya ccm wakiacha ufisadi wanahama chama hivyo Kafulila ameamua kuwafuata hukohuko kabla awajaacha tabia yao ya ufisadi,lakini cha kujiulisa ataweza kuwafungulia mdomo au na yeye atasubiri mpaka waame chama ndio aseme?
Kwani kafulila anaweza nini? Kesi ya ubunge alipigwa chini na wakili wa kijijini huko CCM kavutwa kwenda kumalizwa kisiasa kwa werema bado anamtambua kama Tumbili na CCM wanamjua kuwa ana Majungu sana watakaa nae kwa tahadhali kubwa sana hatakuwa huru akiwa CCM kwa kifupi kafulila ndiyo kapotea kisiasa.
 
Amefulia kama jina lake kwa hiyo anasaka nafasi ya uteuzi, amechelewa sana kwani ndani ya zizi amekatika mkia.
 
Back
Top Bottom