Kafulila Asipotoshe Umma

Kafulila Asipotoshe Umma

Grace Mugabe hafai ni mtu Hatari sana lakini hakuna mabaya yasiyo na mwisho ipo simu watafeli na kupata Aibu kubwa

Na leo Grace Mugabe hajui hata kesho yake nia aibu.
 
Aliyenunua kivuko cha Dsm-Bagamoyo aliwahi kuwajibika? Aliyeuza nyumba za serikali akajiuzia nyumba kibao kienyeji tena zingine akagawa kwa mdogo wake na Zingine kwa hawala huku akizaa na Shemeji yake kinyume cha maadili je? Aliwajibika? Zile bilion 252 zilipotea wizara ya ujenzi kwa kuwalipa makandarasi hewa ni nani aliwajibika? Kuzuiwa kwa ndege Canada ni nani wa kuwajibika?
Kwaiyo unashauri wapinzani waachane na mijadara ya ufisadi kwakuwa kuna mafisadi hawakuwajibika?? Waiwajibishe serikali kwenye mambo gani?
 
Chukua mfano wa Patrobas unadhani angepewa jukumu gani zaidi ili abaki kwenye chama? Mwenyekiti wa Taifa wa Youth wing??? Halafu useme hawapewi majukumu? Ukweli ni kuwa wameahindwa majukumu.
Upinzani hakuna fursa ya uteuzi sababu hawana serikari fursa ya katambi ilkuwa ya juu na zaidi ya hapo haina maslahi kwani ruzuku yenyewe ni ndogo na hawana biashara yeyote ndio maana zito anatembeza bakuli
Chukua mfano wa Patrobas unadhani angepewa jukumu gani zaidi ili abaki kwenye chama? Mwenyekiti wa Taifa wa Youth wing??? Halafu useme hawapewi majukumu? Ukweli ni kuwa wameahindwa majukumu.
 
Kwa NYALANDU mlishangilia hasaaa,!!!!
Na wana CCM walikaa Kimyaaa,,!!!!!
Kwa KAFULILA POVU zinawamiminika kama wagonjwa wa VIFAFA
Thread imeshushwa kisomi hasa mpaka quotes za wasomi zimewekwa, lakini majibu ya mwana CCM ndio haya. Siku polisi wakiachana na CCM sijui nguzo yenu itakuwa nini.
 
Ambacho Chadema hawajagundua bado ccm wanawawangia mchana na usiku wenyewe wakiwa wamelala usingizi, ccm iko busy kushawishi wanachadema wote wenye ushawishi kuhamia ccm, Chadema wakija kushtuka wote wenye ushawishi wamejivua uanachama hapo ndipo hata Mbowe naye atajivua uanachama...mwisho wa upinzani. Yote haya yakitokea tutakuwa tumerasimisha na kubariki udikteta maana hata Katiba ikibadilishwa na kuongeza miaka ya urais, kwa mfano, kutakuwa hakuna wa kupinga... baada ya hapo itafuata miaka mingi ya kulia na kusaga meno, mark my words! CUF imemalizwa, Chadema na ACT vinamalizwa kwa mpigo, NCCR ni kama haipo. Magufuli is swatting the opposition like a buffalo swatting flies, wake up and smell the coffee!
Day dreaming.Linganisha leo mikutano ya CCM na CDM. Siri kuu ya kuua upinzani ni kuifanya Tanzania iwe first world economy; na hata huko first world kuna upinzani, kwa hiyo ndoto yako haiwezekani.
 
Huyu alipokosa ubunge alichanganyiikiwa,pesa yote ikaisha,akawa utegemezi kwa mkewe.Mkewe akienda bungeni jamaa anajikunyata tuu kama paka na pia mama akawa anamkazia kiaina si unajua mke ana pesa mume hana.Jamaa akahisi labda chama kinampa kiburi akachukia ,baba Jesca alipomtangazia hela kidogo na uwezekano wa UDC ,jamaa akaufyata bila fyoko fyoko.Hata hivyo usije ukamwamini mtu wa Kigoma hata kama ni baba au mama yako.
 
Hivi hii CCM ya akina Chenge ndio inapambana na ufisadi? Hebu mtupatie mfano halisi wa jinsi CCM inavyochukia na kupambana na ufisadi. Maana wengine tunaona kabisa kwamba CCM ni himaya ya ufisadi na mafisadi.
 
Opposition parties hapa Africa ni tofauti unavyofikiria wewe. Kwenye Demokrasia kuna mazuri yanayofanywa na chama tawala inatakiwa opposition parties waunge mkono na serikali inapokosa waikosoe. Nchi nyingi za ulaya huwezi kuona chama cha upinzani kinatoa kejeli na matusi kwa kiongozi aliyeko madarakani.
Reuters)
Obama’s family leaves Italy
Read Less
First lady Michelle Obama left Italy with her daughters, Malia and Sasha, as well as her mother, Marian Robinson. During their stay the Obama family visited the Milan Expo.
June 21, 2015 | 5:41 PM EDT
Mfano wa hapo juu familia ya Rais Obama walienda Italia kutembea kwa gharama ya walipa kodi wa Marekani lakini hakuna kiongozi wa chama cha upinzani alitoa tamko la kulalamika. Hapa serikali imejenga Airport Chato ambayo ipo Tanzania imekuwa tatizo kubwa. Kwa msimamo na speed ya serikali ya awamu ya tano Opposition parties Tanzania zitakufa natural death.
Kujenga Airport sehemu yoyote Tanzania bila kufuata sheria na kanuni za nchi ni kiashiria cha ufisadi.
 
dalaber:
1. Wewe unafurahia kinachofanywa na CCM?
2. Hicho kinachofanywa na CCM kuwashawishi kwa namna yoyote wanachama na viongozi wa upinzani kuhamia CCM kina faida kwa Taifa?
3. Hivi tukiwa na Bunge la chama kimoja tu Taifa litanufaika au litapata hasara?
4. Kwa nini hii nguvu isitumike kuwaletea maendeleo wananchi?
gani
 
Kujenga Airport sehemu yoyote Tanzania bila kufuata sheria na kanuni za nchi ni kiashiria cha ufisadi.
Muanze kuchunguza huo Ufisadi wa mamilioni za fedha za ruzuku kwanza
 
Kama kinachosemwa ni kweli basi tumefika pabaya kama Taifa. Inasemekana vyombo vya moto vinafika kwa mwanachama au kiongozi wa upinzani na kumwambia achague moja, ama yamkute ya Lissu na Ben Saanane au ahamie CCM awe salama.
 
Ufisadi gani unatikomezwaa?? Mbona mm sioni?? Yaan nchi hii ufisadi ni ule wa IPTL tena waharifu ni wawili tu ??
 
Kwa hiyo Kafulila pamoja na kuwa mtunga sheria kwa miaka kadhaa hajajua vyombo vya kisheria vya kupambana na rushwa na ufisadi nchini? Toka lini upinzani ni chombo cha kisheria cha kupambana na ufisadi? Mbona tumetangaziwa hivi karibuni kwamba kuna chombo maalumu cha kisheria cha kupambana na mafisadi na ufisadi,kinaitwa Mahakama ya mafisadi. Kwani Kafulila yeye anajua kuwa hicho chombo ndio upinzani au hicho chombo kimeundwa na upinzani? Sasa badala ya kuwahoji watu husika analaumu upinzani, kwa nini na kwa lipi?
 
Huyu tangu ikanushwe na mkuu wa nchi kuwa walimwita tumbili ndio watakaokuwa tumbili amevimba kichwa akiamini kuwa CCM ni chama kinachopambana na ufisadi!AMEPOTOKA!

Ufisadi haujengwi na mtu unajengwa na MFUMO.Ktk tuhuma zote za ufisadi zilizotikisa nchi hazikufanywa na watu kwa majina yao zilifanywa na watu kwa dhamana zao na dhamana hizo zilitokana na vyama vyao,

Kwa kauli yake anataka kutuaminisha kwamba chama cha siasa kikishapambana na ufisadi ndiyo kitakuwa kimemaliza kazi?

Hivi mwanasiasa tena wa chama cha upinzani nyakati hizi unashindwa kuhoji Wapi Ben Saanane,Nani alimwua Alphonce Mawazo,Nani Alimpiga risasi Tundu Lissu,Nani kazuzia mikutano ya vyama vya siasa,Mani kazuia Bingu live?
 
Nikiwa kama miongoni mwa watu nisiowapenda kabisa CCM namuunga mkono Kafulila aende tu CCM sababu alizotoa ni ukweli mtu.

"UPINZANI UMEPIGWA GANZI AJENDA YAO KUU KWA SASA SIO UFISADI TENA" Ndio! Nani mwenye ujasili wa kuongelea ufisadi kwa hari iliyopo sasa? tunachoweza kuongelea kuhusu ufisadi sasa ni ule unaoishia ngazi tu ya halmashauri na tukizidi sanaaa uw@ziri na si zaidi ya hapo vinginevyo tunakuwa tunajihukumu kutangulia mbele za haki, tukionewa huruma ni nyuma ya nondo miaka 5 au million 7 sasa sisi wengine hata laki hatuna tutaponea wapi?

Eti Kafulila hana kazi nyingine? Inamaana anategemea siasa tu?
Hivi ni taasisi ipi ikotayari kumuajiri kazi mfia chama wa upinzani, hiyo taasisi haijipendi?
Eti anashindwa hata kujiajili? Acheni unafiki, ulishaona wapi mfanyabiashara ama mjasiliamali anapeperusha bendela ya chadema kijiweni ama nyumbani kwake labda zamani na wengi walijuta.

Ooh mbona mimi ninafanya biashara na ni chadema?
Hapo lazima uchadema wako uwe ni wa jf tu na si wa kujionesha hadhalani kama alivyokuwa Kafulila na wenzake.

Mnataka mtangaziwe na nani kuwa sasa tuko mfumo ule wa kabla ya mwaka 1992. Na kuzibitisha hilo 2020 tutaachiwa vibunge viwili tu vya kuidanyanyia Dunia na sitashangaa wabunge wengi wa chadema wakijivua uwanachama kabla ya 2020 na kugombea tena kupitia sehemu salama.

Tusidanganyane tulikofikia mmtu yoyote anayepinga bila kujificha yale yanayoendelea hapa njaa itamtafuna mpaka atakapo salim amri.
 
Ulimuelewa lakini hapo juu au ulitoka kavu? Ni kweli ni ujinga ulikuwa unaimbwa eti ajenda ya upinzani ni ufisadi!
Kweli kamanda.
Wajinga bado hawajui kuwa baada ya chama kununuliwa tumebadili gia. Siku hizi agenda ni kusubiri matukio na kupinga mabadiliko yanayofanywa na Magu kurejesha maliasili kwa watanzania.


Wajinga wanashabikia eti sasa hivi tuwe tunagawana mapato na ACACIA 50/50.
Sie werevu hatutaki hay tunataka tushitakiwe ili tudaiwe mabilioni na Bombadier ziendelee kukamatwa.

Waache wajinga waendelee na Ajenda ya UFISADI tuliyoikacha mara tu kamanda Mbowe alipofika bei na kamanda LOWASA.
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Nadhani mleta mada ametoa shule ya jumla kwa watu wasio na uelewa kama Kafulila ambao hawajui dhana ya chama cha upinzani.

Agenda ya chama cha upinzani haiwezi kuwa ni hiyo hiyo wakati wote bali hutegemea serikali ya wakati huo inafanya nini dhidi ya wananchi wake. Kwa sasa naamini agenda ya udikteta ni yenye nguvu kuliko zote. Wananchi wengi wanaonja mateso ya udikteta/maamuzi ya mtu mmoja kuliko kitu kingine chochote.

well said. Lakini hii mi kwa mtazam wako. kwa mtazamo wa Kafulila na wengine wanao share muono mmoja wanaona UFISADI BADO ULIPASWA KUA AGENDA KUU YA WAPINZANI na inawashangaza kwanii uko kimy kwenye hili.ndio maana wanaamua kufuata wanachokiamini so nafikiri sio busara kwa makamanda kuwatukana au kuwakejeli eti tu kwasababu wanaamini kitu tofauti na wao kwa sasa!
wee unaamini udikteta ni agenda yenye nguvu wao wanaamini zao la kila baya ni ufisadi na wameamua kufuata wanachokiamini...
ni haki yao ya kidemokrasia..waachwe.
 
Awali ya yote naomba kuchukua nafasi kumshukuru Mwenyezi Mungu kutujalia zawadi ya uzima tulio nao.

Bila kupoteza muda, napenda kusema kuwa nimemsikia Ndg Kafulila kupitia (voice note) akithibitisha kuwa ndiye aliyetoa tamko la kujiengua toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Kimsingi sina tatizo na yeye kutoka kwani ni HAKI yake kikatiba kufanya maamuzi aliyoyafanya na hivyo sina PINGAMIZI lolote katika hilo.

Ndg Kafulila anasema kupitia tamko lake kuwa ataujulisha umma ni chama gani atajiunga nacho hivi karibuni, kitu ambacho binafsi naona hakina haja kwani tayari maudhui ya andiko lake yanabainisha ni chama gani atajiunga nacho.

Sasa kama sina tatizo na Ndg Kafulila ku-exercise haki yake kikatiba, kwanini natoa maoni yangu kuhusiana na suala lake la yeye kuondoka Chadema?

Nimeamua kutoa maoni yangu kutokana na ukweli kuwa SIKUBALIANI na hoja kuu ya Ndg kafulila kuwa UPINZANI SIO TENA JUKWAA SALAMA LA KUENDESHA VITA DHIDI YA UFISADI. Adai hii imetokana na vyama vya upinzani kupigwa ganzi (japo hajasema nani kavipiga ganzi na kwanini avipige ganzi) na hivyo UFISADI SIO TENA AJENDA KUU YA UPINZANI.

Labda nisema tu kuwa Ndg Kafulila ni ama kaamua kupotosha umma kwa makusudi au hajui ni nini maana ya VYAMA VYA UPINZANI, lakini pia hajui AJENDA KUU ya vyama hivyo nchini! Kifupi tu ni kwamba, UFISADI haujawahi kuwa na kamwe hauta kuwa AJENDA KUU ya vyama vya upinzani si tu kwa Tanzania, bali duniani pote. Hii inatokana na tafsri ya upinzani lakini pia wajibu wake katika Demokrasia ya mfumo wa vyama vingi duniani.

Naomba nitumie maandiko kadhaa kulithibitisha hili nisemalo, nitaanza na mmoja wa wanasiasa wakongwe na machachari nchini New Zealand, na huyu sio mwingine ila ni Dakta Donald Thomas Don Brash. Dakta Brash alipata kuwa Gavana wa Benki Kuu ya New Zealand, Kiongozi wa Kambi Rasmi Bungeni, Kiongozi wa vyama vya National Party na ACT Party kwa nyakati tofauti. Yeye aliwahi kusema, naomba nimnukuu;

“The Opposition’s main role is to question the government of the day and hold them accountable to the public…. Opposition represents an alternative government, and is responsible for challenging the policies of the government and producing different policies where appropriate.”

Naomba nitoe tafsiri (sio rasmi) Kazi kuu ya upinzani ni KUHOJI serikali iliyoko madarakani na kuifanya iwajibike kwa umma….Upinzani unawakilisha serikali MBADALA na unawajibika kutoa changamoto kwenye sera za serikali na hivyo kutoa sera tofauti/mbadala pale inapowezekana.

Dakta Brash anaongeza kusema, namnukuu; “…one of the most important jobs of the Opposition is to constantly question the Government. Any Government has to remain answerable to the public at all times, and a good Opposition can put the spotlight on serious issues and have them resolved quickly”.

Tafsiri (sio rasmi) Moja ya kazi muhimu za upinzani ni kuendelea kuhoji serikali bila kuchoka, Serikali yeyote inapashwa kuendelea kuwajibika kwa umma muda wote, na upinzani mzuri unaweza kumulika/kuibua mambo na hivyo kurekebishwa kwa haraka.

Lakini pia kwa mujibu wa Taasisi ya Kidemokrasi ya Afrika (Africa Democratic Institute) inasema wajibu wa upinzani katika Demokrasia ni mkubwa sana. Taasisi hii inabainisha baadhi ya kazi/wajibu wa upinzania kuwa ni pamoja na:-

To hold governments accountable (Kuiwajibisha Serikali);
To serve as a credible alternative to the ruling government (Kuwa mbadala wenye kuaminika/thabiti dhidi ya serikali inayotawala);
To promote and stimulate debates in parliament (Kukuza na kuchochea mijadala bungeni);
To be a training ground for future leaders (Kuwa eneo la mafunzo kwa viongozi wa baadaye);

Kwa upande mwingine, mwandishi Sheetal Kumari wa India, anaandika kama ifuatavyo:-
The Opposition parties play a very significant role in a democracy as representatives of the people…to safeguard their interests….The opposition act as watch dog’ of a the system.

Tafsiri (sio rasmi) Vyama vya upinzani vina jukumu muhimu sana katika Demokrasia kwa kuwa wawakilishi wa watu/umma ili kulinda maslahi yao….Upinzani ni mlinzi katika mfumo.

Sio hao tu, pia msomi Julius Kiiza, PhD; kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, katika ‘pepa’ yake ya Wajibu wa Upinzani katika Demokrasia, Kiiza (kama anavyopenda kuitwa) pamoja na mambo mengine anaandika.

“…opposition parties perform several important functions. These include; promoting responsible and reasoned debate. Opposition parties hold the government to account for its commissions or omissions. Parties present a viable alternative to the incumbent government by designing alternative ideas, principles and policies for governing society. Should the party in power let the voters down, the ‘government-in-waiting’ takes over the reign of power – through free and fair elections.”

Kiza anendelea kuandika; “Parties act as a training ground for future leaders, parties strengthen the culture of democracy within the party and the political community in general (by, for example, promoting open debate during delegates’ conferences, promoting intra-party democratic elections and ensuring accountable use of party finances). Parties work with the Electoral Commission, the mass media and civil society organizations to monitor and improve the quality of voter registration, civic education and electoral transparency.

Tasfri (sio rasmi) ya maneno ya Kiiza
...vyama vya upinzani vinafanya kazi kadhaa muhimu. Hizi ni pamoja na; kukuza mijadala na hoja zenye kuleta uwajibikaji. Vyama vya upinzani vinaiwajibisha serikali katika maelekezo na makosa yake. Vyama vinajinadi kama mbadala unayofaa na fanisi dhidi ya serikali iliyoko madarakani katika kubuni mawazo, kanuni na sera mbadala zenye kuongoza umma. Kama itatokea chama tawala kikawaangusha wapiga kura, 'serikali inayosubiri' huchukua madaraka kupitia chaguzi huru na za haki.

Sasa nikirejea kwenye hoja yangu, ukisoma hayo maandiko na mengine mengi tu, hakuna hata moja linalosema kuwa AJENDA KUU YA UPINZANI NI UFISADI. Hivyo kwa wanaotumia maneno kama hayo ya Ndg Kafulila pale wanapoamua kuondoka upinzania, ama wanaamua kudanganya ama hawajui wajibu/agenda kuu ya upinzani ni nini.

Ni vema watoe sababu zengine lakini sio sababu zisizo na mashiko na tena ni MFU kama hizo za aina ya Ndg Kafulila. Lakini pia ukisoma maandiko hayo, na mengine mengi ambayo sikuyanukuu, hakuna mahali panasema njia ya upinzani kuiunga mkono serikali iliyoko madarakani ni kuondoka upinzani na kujiunga chama tawala, kama ingelikuwa ni hivyo. Basi upinzani na wajibu wake utakuwa hauna maana.

Mimi nadhani ni sahihi sana kwa wewe unaona vyuma vimekaza na unaona njia rahisi ni kukimbilia chama tawala, basi ondoka tu, USIUPOTOSHE UMMA. Au kama umeshindwana na wenzio ndani ya chama na ukaona njia sahihi ni wewe kuachana nao, basi ondoka tu, ukipenda kimya kimya au kwa kelele lakini USIUPOTOSHE UMMA. Na kama umeahidiwa CHEO, PESA nk basi we nenda tu kachukue lakini USIUPOTOSHE UMMA.

NAOMBA KUWASILISHA

Dickson Ng’hily
European Zone Coordinator – ACT Wazalendo
22/11/2027
Mkuu kwa hiyo Ufisadi siyo ajenda ya upinzani?? Kwanini kabla ya watuhumiwa wa ufisadi kuhamia upinzani Ufisadi ilikuwa ajenda ya upinzani?? Ukinijibu maswali yangu hayo kwa ufasaha then nitakuelewa!!
 
Shida wanasiasa wengi wanategemea siasa Kama ndiyo njia ya kujiingizia hela tu
Wakitoswa kwenye nafasi zao wanapigika
Garama ya maisha zinawashinda.....

Ova
 
Back
Top Bottom