Walichofanya ilikuwa ni kuzuia kile wenyewe wanachoita mapinduzi yaliyolenga kumtoa Mbatia kwenye kiti chake. Sasa wamechelewa. Nafasi pekee ya kumdhibiti Kafulila ilikuwa kumsamehe pale alipokwenda kulamba viatu vya Mbatia. Sasa hivi wakimsamehe watakuwa wamemrahisishia njia yake ya kubeba uenyekiti. Na wakishilkilia uamuzi wa kumfukuza ndiyo anaaondoka na chama. Kuna somo kwa vyama vyetu hapa.haya ndiyo matokeo ya kukurupuka katika maamuzi hivi hakukuwa adhabu nyingine zaidi ya kumfukuza uanachama
Hata hivyo ni bora kabla hajachukua uamuzi huo James Mbatia angefanya utafiti/uchunguzi nini ingegekuwa impact ya kumfukuza chamani David
Chama bado kina nafasi ya kulitatua tatuzo hili ndani ya siku 14 walizo mpa au kupitia mahakama