Kafulila aifunika KIGOMA

kafulila ni shujaa.anateswa na kile anachokiamini alichoamua kuwaambia viongozi wake kuwa wanakosea.


Hana ushujaa wowote. Yule kijana si mstaarabu,kiongozi gani hasiyejua yapi ya kusema,wapi na wakati gani? Kama ulisikiliza kauli ya nccr juu ya kulazimika kwao kumfukuza chama kafulila usingemwita shujaa. Nina mashaka na uelewa wako juu ya uendeshaji vyama. Migogoro ni kitu cha kawaida katika chama mara kwani inaonyesha hali ya kutofautiana juu ya jambo fulani,suala la kafulila ni ukosefu wa nidhamu tu, hivyo hafaiii, si wa kutetea.
 
Kosa la kafulila ni kuungana na chadema kutoka nje!! alimkera m/kiti wake maana mbatia ni ccm na kafulila alionyesha u-chadema badala ys u-ccm!!
uchadema ni mdudu gani huyo? au kuwa mkweli, kupinga ufisadi, kutetea wanyonge (uanaharakati kwa ujumla)...
 
vigezo na masharti kuzingatiwa wakuu ndani ya nccr mimi ninavyoona!
 
David Kafulila aliyeenguliwa ubunge na chama chake NCCR alipokelewa kwa kishindo kama mfalme jimboni kwake na wananchi

Wakati huko CUF - DAR
kwenye mkutano wa ndani walinzi wa wa chama waliwachapa vibao wajumbe na baadhi kujeruhiwa

Source magazeti ya leo via RFA
[/QUOTE
kama ushujaa ni kuropoka ovyo basi ni shujaa.kafulila ni mpumbavu tu anayetaka sifa na madaraka.atadanganya watu wa kwao tu lakini sio watu wenye akili zao.
 
Hao waliompokea hawajui sababu ya yeye kufukuzwa!!!!!!!!!!!!!!
 
Watu tujikite kwenye hoja za msingi,........
Watanzania wenzangu mbona tunakuwa wepesi wa kusahau tunakimbila kwenye hoja zisizo na mashiko,...watu wanalalamika kafulila kaonewa,..kwangu mie hainingii akilini,....
Ilikuwaje jamaa akaomba msamaha kama kweli alikuwa anapigania haki yake kwenye chama,....??
Je mtu akivunja taratibu na kanuni hata kama ni jembe aachwe tuh,....?????
Ifike mahala tusiwe washabiki leo hii nchi hii imeoza sababu kuu ni ushabiki na kubebana kusiko na msingi, tuanchoilalamikia ccm ni hiko hiko,...!!!!
Mie nasema kama kafulila alivunja kanuni na taratibu a chama chake alistahili adhabu,....la sivyo kama ndiyo hivyo tusitegemee jipya hata kama kitaingia chama gani cha upinzania madarakani,...!!!!
Kama tutashindwa fata sheria za chama tuh za nchi sizani kama tutaweza,...
 




Na Jacob Ruvilo na Datus Boniface

ZIARA ya Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila, ambaye juzi alipokewa kama mfalme jimboni hapa, imechukua sura mpya baada ya njama za kutaka kuzuia mikutano yake kwa kutumia Jeshi la Polisi kukwama.


Habari za kuaminika zimeonyesha kuwa viongozi wawili walioagizwa na uongozi wa NCCR-Mageuzi Taifa kuwashawishi madiwani na viongozi wa wilaya kutoshiriki mapokezi wala mikutano yake, walinusurika kupewa kipigo kiasi cha kukimbilia polisi ambako inadaiwa wamefungua mashtaka ya kutishiwa maisha.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kafulila aliliambia Tanzania Daima kwa njia ya simu kutoka Kigoma kuwa uongozi wa juu wa chama hicho ulileta mamluki kutoka Dar es Salaam kwa lengo la kuzuia na kuuvuruga mkutano wa hadhara na kuwashawishi madiwani na wanachama kutohudhuria mkutano huo.


“Ni kweli walitumwa watu, lakini kabla ya kufikia hatua hiyo, tayari madiwani na wanachama waliishaitisha mkutano, hivyo walipojaribu walifukuzwa na baadhi ya wafuasi wangu na kutoka eneo la tukio, lakini naelezwa kwamba wameenda kituo cha polisi (hakukitaja) kufungua jalada la kutishiwa maisha.”


Tukio hilo limezidi kuwasha moto ndani ya chama hicho ambapo karibu viongozi wote wametishia kuchoma moto kadi na bendera za chama na kuhamia chama kingine cha upinzani ikiwa Mwenyekiti wa Taifa, James Mbatia, na kundi lake hawatafuta uamuzi wa kumvua uanachama mbunge wao.


Katika tamko la pamoja walilotoa jana, viongozi mbalimbali wa NCCR-Mageuzi ngazi ya jimbo, kata na matawi wakiwemo baadhi ya madiwani, walisema wako tayari kujiuzuru nafasi zao ikiwa chama hicho taifa kitakataa kusikiliza uamuzi wao wa kutaka Kafulila
arejeshewe uanachama.


Madiwani karibu wote wa kata za jimbo hilo, kamishina wa mkoa wa chama hicho na viongozi wengine walisema kwa sasa wanangoja maamuzi ya Mahakama Kuu juu ya hatima ya mbunge wao.


Hata hivyo, wameonya kuwa hata kama mahakama itaunga mkono hatua za chama ngazi ya taifa kumvua uanachama Kafulila, watatangaza
kuachana na chama hicho.


Katika mikutano ya hadhara iliyofanyika mjini Nguruka na Uvinza, Diwani wa Kata ya Itebule Shukuru Chiza, Diwani wa Kata ya Nguruka, Abdallah Massanga, na Diwani Kata ya Kandaga Francis Kumbo walisema hawana haja ya kuendelea na nyadhifa zao kama chama hakitaamua vinginevyo.


Naye Kamishna wa chama hicho mkoa wa Kigoma, Bakari Nyamcha, na Mwenyekiti wa Kata ya Kahawa, Iddi Issa, walisema watachukua hatua nzito ya kukusanya kadi za wanachama wote, bendera na mali zingine na kuvichoma moto ikiwa Mbatia na wenzake watashikilia uamuzi wao waliouita wa kidikteta.


Walisema pamoja na mbunge wao kuwa na kasoro kadhaa lakini kwa kuwa aliomba radhi kwa maneno na maandishi katika kikao, alipaswa kusamehewa na si kumvua uanchama hatua ambayo mbali na kumuathiri mbunge huyo, imewaumiza sana wananchi wa jimbo hilo kwa kuwa wana imani kubwa na mwakilishi wao bungeni.


”Tumefanya kazi kubwa, hatukulala usiku na mchana tukimpigania Kafulila na chama, sasa tumepata lakini watu wachache wanafikia maamuzi mabaya bila kujali haki ya wananchi zaidi ya elfu ishirini na tano waliomchagua bila kujali itikadi ya vyama,” alisema mmoja wa viongozi hao akiitikiwa na wenzake.


Nao makamishna wa chama hicho mkoa wa Ruvuma, Henry Mapunda, na Kayumbo Kabutale kutoka Mkoa wa Dodoma, ambao wameambatana na mbunge katika ziara hiyo, walisema wanachotaka ni mabadiliko ya uongozi yatakayoleta changamoto ya demokrasia katika chama hicho kuanzia ngazi ya taifa na si kufanya chama kuwa taasisi ya mtu.


Walisema mapambano ya kupigania haki ya demokrasia katika chama hicho watayafanya bila kukoma kwa njia za haki kwa misingi iliyowekwa na chama.


Akizungumza katika mikutano yake mbalimbali, Kafulila ambaye ziara yake imeteka akili za watu wengi ambao wanafurika katika mikutano hiyo, alisema licha ya tamko la Halmashauri Kuu kumvua uanachama, bado yeye ni mbunge halali kwa sasa kutokana na uamuzi wa Mahakama Kuu Tanzania hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo kutokana na kesi ya msingi.


Aliwaomba wananchi wa jimbo hilo kutulia na kungoja maamuzi ya mahakama huku akiwataka washirikiane vema katika kuwajibika kwa kazi ili kuchochea maendeleo ya jimbo.


Aliwashukuru wananchi kwa kumuombea dua wakati wote wa matatizo yake na kwamba ataendelea kuwatumikia kwa moyo wake wote kwa maslahi ya Kigoma Kusini na mkoa wote wa Kigoma.


Aliongeza kuwa ataendelea kufanya mikutano kadhaa ya hadhara katika vijiji vya Malagarasi, Mtego wa Noti na Nguruka kama njia moja ya kutetea na kuwawakilisha wananchi.


Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila alifika jimboni kwake Jumamosi ya wiki hii na kupokewa kwa shangwe kubwa na wananchi ambao waliandamana wakiwa wamebeba mabango yaliyokuwa na ujumbe tofauti yakimlenga Mbatia na wajumbe wa kikao kilichomvua uanachama mbunge huyo.


”Karibu mbunge shujaa msema kweli tutakuunga mkono kokote utakakokwenda kwa nia ya kudai haki za wanyonge,” ilikuwa ni moja ya sehemu ya ujumbe uliokuwa katika mabango mengi yaliyobebwa na wananchi hao.

 
Padri Mmoja sawa na masheikh ubwabwa 1000!!

udini,upumbavu na ujinga vimekujaa! Huna hata chembe ya busara. Inaonesha unafanya vizuri kazi ya bwana yako ibilisi. Mkiristo safi hawezi kashifu dini ya Muislam sababu Muislam anaabudu Mungu kama wakristo wanavyo abudu! Wewe ni freemason na unaabudu shetani ndio maana unaleta fitna za udini ili waislam na wakristo wagombane upate faida wewe na BWANA yako shetani. Tumekutambua wewe kijakazi wa shetani.
 
siku hizi utaratibu wa picha umeenda wapi? huyu MALAGARASI, atupe picha ya matukio tulinganishe propaganda zake na msimamo wa watata wa KIGOMA, uvinza na Nguruka
 
haya ndiyo matokeo ya kukurupuka katika maamuzi hivi hakukuwa adhabu nyingine zaidi ya kumfukuza uanachama

Hata hivyo ni bora kabla hajachukua uamuzi huo James Mbatia angefanya utafiti/uchunguzi nini ingegekuwa impact ya kumfukuza chamani David

Chama bado kina nafasi ya kulitatua tatuzo hili ndani ya siku 14 walizo mpa au kupitia mahakama
 
Pole sana Mbatia. Watu wa aina hii si wa kukurupukia kufukuza. Waachie kamba ndefu wajinyonge nayo wenyewe.
 
Back
Top Bottom