Na Buberwa Kaiza: Mradi usiokamilika wa mageuzi nchini Tanzania

conductor

JF-Expert Member
May 29, 2013
718
569
Mparanganyiko wa NCCR haukuishia kwa kuundwa UMD au kuondoka kwa Chief Abdallah Said Fundikira, bali uliendelea kuwepo. Kati ya Desemba 1991 na Februari 1992, Bwana James Mapalala (Rip) pia aliacha NCCR na kuanzisha Chama Cha Wananchi (CCW) - Mapalala akiwa Mwenyekiti na Katibu Mkuu wake akiwa Dr. Alec Chemponda (RIP). Mch. Christopher Mtikila (Rip) aliacha NCCR pamoja na Mwinjilisti Kamara Kusupa, mlokole Mwigandoshi, na Bwana Mahinbo Kaoneka, na kisha kuanzisha Chama Cha Democrasia (CCD) - Kaoneka akiwa Mwenyekiti, Kusupa Katibu Mkuu, na Mch. Mtikila akiwa 'Mlezi'. Viongozi wa CCD waligombana na mlezi wa chama chao, na kisha Mch. Mtikila alitangaza kubadilisha CCD kutoka Kiswahili kuwa Kiingereza, yaani Democratic Party (DP), na kuwaachia Kusupa na Kaoneka CCD yao. Ni wakati huo KAMAHURU walijitenga na NCCR kinyemela, kuungana na CCW na kisha kuunda chama cha The Civic United Front (CUF). Mwenyekiti akiwa James Mapalala na Katibu Mkuu mzee Khamis Mloo (Rip), Seif Sharif Hamad (Rip) akiwa Makamu Mwenyekiti (Zanzibar).

Hata hivyo, NCCR (Kamati) iliendelea kutandaa (networking) kupitia njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kusambaza machapisho (Tunachotaka Sasa, Upinzani Siyo Uadui, Sera ya UZAWA) na kujitangaza kupitia magazeti ya Radi (likimilikiwa na Ndimara Tegambwage), Mfanyakazi, Motomoto, Heko, Mshindi, Wakati ni Huu, Michapo, Family Mirror, na kadhalika, na kutembelea watu maarufu wenye mwelekeo wa kimagharibi kwa lengo la kuwashawishi, kuunga mkono, au kujiunga na NCCR. Miongoni mwa watu waliotembelewa walikuwa ni pamoja na Bwana Wilfrem Mwakitwange (aliyekuwa mmiliki wa Rungwe Oceanic Hotels & Resort), Bwana Hillal Mapunda (aliyekuwa mhadhiri wa Chuo Cha Siasa [Chama] Kivukoni), Mzee Mushendwa (mfanyabiashara aliyekuwa akiishi Morogoro), Daktari Walid Amani Kabourou (wakati akiwa likizo akitokea Marekani alikokuwa akiishi), Bwana Edwin Mtei, na wengineo. Aidha, kupitia Prince Bagenda, Daktari Ringo Willy Tenga, waandishi wa habari Mbena Mwanatongoni (huyu sijui mahali aliko kwa sasa) na Anthony Ngaiza (tunaye hapa jukwaani), Professa Mwesiga Baregu (Rip) na Mashaka Nindi Chimoto (Rip), NCCR ilianzisha asasi ya kiraia ya African International Group of Political Risk Analysis (PORIS) ikiwa na dhima ya kuimarisha umahiri wa jamii ya kiraia (civic competence) kwa Watanzania, na kueneza dhana ya mageuzi ya kisiasa miongoni mwa Watanzania.

Februari 1992, NCCR (Kamati) ilibaini mwelekeo wa kisiasa nchini ulikuwa wa kuanzisha vyama vya siasa licha ya kutokuwepo kwa mwongozo wa kisheria. Kamati ilikuwa na hofu kuwa baadhi ya wana-Kamati (rogue elements) wangeweza kujitangazia isivyo rasmi kuwa NCCR ni chama chao, hali ambayo ingesababisha mtafaruku kiasi cha kuua matokeo chanya ya kazi ya Kamati iliyokuwa imefanyika kwa miezi minane.

Aidha, ni wakati huo Tume ya Jaji Mkuu Francis Nyalali ilikuwa imetoa ripoti na kupendekeza kwa Serikali kuwa Tanzania ianzishe mfumo wa siasa za ushindani wa vyama vingi. Serikali ya Rais Mwinyi na Chama Cha Mapinduzi chini ya Katibu Mkuu Horace Kolimba (RIP) iliitikia (echoed) mapendekezo ya Tume ya Nyalali. Serikali ilitangaza Tanzania kuingia siasa za ushindani wa vyama vya siasa kuanzia Julai/1992.

Februari 15/1992, wana-Kamati walikaa na kukubaliana rasmi kuwa NCCR ibadilike kutoka Kamati ya Mageuzi ya Katiba na kuwa chama cha siasa lakini kwa kubakiza jina la NCCR na kisha kuongeza mbele yake maneno MAGEUZI. Hivyo jina la chama likawa The National Convention for Construction and Reform (NCCR-Mageuzi). Kabla ya hapo, wakati wa mashauriano, wajumbe walikuwa wamependekeza chama kipya kiitwe Chama Cha Demokrasia na Maendeleo. Hata hivyo, hofu ya kuachwa kwa jina la 'NCCR' kisha lije kutekwa na watu wenye nia mbaya na ku-water-down matokeo chanya ya kazi zake ilipelekea muafaka kuwa maneno 'DEMOKRASIA NA MAENDELEO' yabaki, ila yawekwe na kuonekana katikati ya Chata ya Chama.

Mara baada ya NCCR-Mageuzi kutangazwa kuwa chama - Mabere Marando akiwa Mwenyekiti, Prince Bagenda akiwa Katibu Mkuu, Mashaka Chimoto akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Ndimara Tegambwage akiwa Katibu wa Habari, Uchochezi na Uhamasishaji - chama kilienea nchi nzima kwa haraka sana, kikibebwa hususan na wanafunzi na wahadhiri wa Chuo Kikuu. Chama kiliunda na kuimarisha kamati za mikoa yote nchini. Chama kilipata misaada ya hali na mali kutoka kwa viongozi na watu mabalimbali - akina Gulam (huyu ni mtoto wa Mama Kero, Mhindi aliyezaliwa na kukulia Bukoba), Dr. Alex Khalid (RIP) mmiliki wa Makondeko Holdings, Dr. Tenga, Prince Bagenda, Ndimara Tegambwage na Watanzania wengine waliokuwa wakiishi nje na ndani ya nchi. Mtanzania mmoja, Patrick Bamukunda (RIP), alijitolea gari lake na yeye mwenyewe kuendesha viongozi wa NCCR-Mageuzi muda wote na mahali popote ambapo wangetaka kwenda kwenye kazi za Chama. Wanafunzi kutoka vyuoni walifanya kazi za kueneza NCCR-Mageuzi kwa kujitolea.

Mwezi Machi/1992 uongozi wa NCCR-Mageuzi ulimkaribisha Mzee Edwin Mtei kujiunga na chama hicho. Prince Bagenda akiambatana na James Mbatia, walikwenda kwa Mzee Mtei, nyumbani kwake USA River, Arusha wakiwa na ujumbe rasmi wa chama kumkaribisha Mzee Mtei kujiunga na NCCR-Mageuzi. Mzee Mtei alitaka kwanza apelekewe andiko la Sera na Katiba ya NCCR-Mageuzi asome kwanza kabla ya kufanya uamuzi wa kujiunga na chama hicho. Alipendekeza nyaraka hizo zipelekwe nyumbani kwake Dar es Salaam na kwamba baada ya kuzisoma angeitisha mkutano kukutana na uongozi wa NCCR-Mageuzi kujadili way forward. Nyaraka zote ziliandaliwa na kuwasilishwa kwake kama zilivyopendekezwa.

KUNAKO Mei/1992, baada ya kusoma andiko la Sera na Katiba ya NCCR-Mageuzi, Mzee Mtei aliwaita viongozi wa NCCR-Mageuzi na kukutana nao nyumbani kwake Dar es Salaam. Ilikuwa wakati wa mkutano huo Mzee Mtei aliwaambia viongozi wa NCCR-MAGEUZI kuwa hakuridhia maombi ya kujiunga na NCCR-Mageuzi. Mzee Mtei aliwaambia viongozi hao kama ninavyonukuu "Vijana kuna watu wengi wenye 'means and substance' wanataka mimi nianzishe chama. ...kwa hiyo, nitaanzisha chama, ninawashauri mvunje chama chenu, niwakaribishe mje kujiunga kwenye chama changu," mwisho wa kunukuu. Marando alimjibu Mzee Mtei kwa kumwambia kuwa chama cha NCCR-Mageuzi kimekwisha kuanzishwa na kuwepo, hivyo hawakuwa tayari kuvunja chama hicho. Kwamba Mzee Mtei aendelee na jitihada zake za kuanzisha chama chake ila akisha 'kunyeshewa mvua' kama wao, 'wangekutana wakati wa wakijikinga mvua'.

Wiki moja baadaye Mzee Edwin Mtei akiwa na marafiki zake; Bob Makani (RIP), Edward Barongo (RIP), Mzee Brown Ngwilulupi (RIP) na wengineo, wakiwa wamevaa suti na suruali zikining'inia kwenye suspenders, waliitisha Press Conference pale Motel Agip, Dar es Salaam, kutangaza kuanzishwa kwa chama kipya kikiitwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Ukweli wa kihistoria ni kuwa Mzee Mtei na wenzake hawakufanya mental work hata kidogo bali walitumia jina, Sera na Katiba ya NCCR-Mageuzi kuanzisha Chadema.

Daktari Walid Amani Kabourou (Rip)

“....Hitoria ya Dr. Walid Amani Kabourou, katika siasa za upinzania hapa nchini haikuanzia Chadema, la hasha.

Mwaka 1992, akiwa safarini kwenda USA, Dr. Kabourou alipitia ofisi ya makao makuu ya NCCR-Mageuzi, mtaa wa Mchikichi Dar es Salaam, alinunua kadi (sikumbuki namba yake) ya NCCR-Mageuzi na kujiunga na chama hicho. Kisha alikutana na kujadiliana na viongozi wa chama hicho; Mabere Marando, Prince Bagenda, Ndimara Tegambwage, na Mashaka Nindi Chimoto (RIP).

Mwaka 1993 vilitokea vifo vya Mhe. Mbano na Mhe. Stephen Kibona aliyekuwa waziri wa fedha wakati huo. Kwa hiyo, kulikuwa na majimbo mawili - Ileje na Kigoma mjini - yaliyofanya uchaguzi mdogo kwa wakati mmoja.

Katika jitihada za kutafuta wagombea, kwa kuwa wakati huo Chadema hakikuwa na watu zaidi ya old guards wake akina Bob Makani (RIP), Edward Barongo (RIP), na wengineo, Mwenyekiti wa chama hicho, Mzee Edwin Mtei, alisafiri hadi USA kumfuata Dr. Walid Amani Kabourou. Mzee Edwin Mtei alimwambia Dr. Kabourou ujumbe wa uongo kuwa vyama vya NCCR-Mageuzi na Chadema vilikuwa vimekubaliana kugawanya majimbo - kwamba NCCR-Mageuzi kiweke mgombea jimbo la Ileje wakati Chadema kikiweka mgombea katika jimbo la Kigoma mjini. Kwamba safari ile alikuwa ametumwa na uongozi wa NCCR-Mageuzi (Mabere Marando) ampelekee ujumbe Dr. Kabourou ahamie Chadema ili aweze kugombea ubunge jimbo la Kigoma mjni; kisha akampatia kadi ya Chadema.

Ni bahati mbaya kuwa tangu awali siasa za upinzania nchini Tanzania zimeendelea kujengwa kwenye misingi ya uongo. Na ni uongo huo uliopelekea safari ya Dr. Walid Amani Kabourou kujiunga na Chadema.

Kamati ya Utendaji ya NCCR-Mageuzi ilipokaa iliamua na kumuagiza Mwenyekiti Mabere Marando apige simu kwa Dr. Kabourou kumtaarifu kuwa chama kilikuwa kimemteua aje kugombea ubunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Dr. Kabourou alibaki midomo wazi na kumwambia Marando kuwa tayari alikuwa ameingia makubaliano/amesaini fomu za Chadema kugombea ubunge kupitia chama hicho [baada ya kuelezwa kuwa kulikuwa na makubaliano baina ya Chadema na NCCR-Mageuzi.....

Kitabu Cha Historia ya Mageuzi nchini kinakuja ukikisoma utajua mengi kuhusu mradi usiokamilika wa mageuzi nchini Tanzania.

Note: Mimi conductor nimekopi na kupaste sina hati miliki ya kubadirisha chochote. Zaidi nimeongeza picha hiyo tu.
FB_IMG_1677475035824.jpg
 
Dah!
What a coincidence, it's as if you're writing an obituary to one of those opposition parties!

Ahsante sana mkuu 'conductor' kwa mchango wako huu wakati huu.

Naona kama historia inajirudia muda si muda.
 
aisee safari ilikuwa ndefu sana kumbe! Chama cha upinzani kuzaliwa, kukua, kukomaa hadi kushika dola is not sport kabisa.
 
Dah!
What a coincidence, it's as if you're writing an obituary to one of those opposition parties!

Ahsante sana mkuu 'conductor' kwa mchango wako huu wakati huu.

Naona kama historia inajirudia muda si muda.
Chadema imeandikiwa "obituary" tokea 2013 na Mzee wassira ila tupo hapa ni 2023 nadhani umepata mrejesho kutoka mikutano inayoendelea. Ni hivi unlike NCCR, Chadema kina misingi imara na watu makini ndio maana licha ya migogoro ila Bado uongozi upo intact na motisha ipo juu sana.

FqI8zlAX0AE3AA-.jpeg
 
Nimemkumbuka Mtikila, alikuwa na kanda zake amejirekodi, zinauzwa kimagendo. Ukikamatwa nayo unafunguliwa mashitaka ya uchochezi m
 
Chadema imeandikiwa "obituary" tokea 2013 na Mzee wassira ila tupo hapa ni 2023 nadhani umepata mrejesho kutoka mikutano inayoendelea. Ni hivi unlike NCCR, Chadema kina misingi imara na watu makini ndio maana licha ya migogoro ila Bado uongozi upo intact na motisha ipo juu sana.

View attachment 2535565
We nawe mgumu kuelewa....
Sasa picha ya nini?.. kwani mnashindana ktk kila kitu
 
Kwa andiko hili, nimetambua kabisa CHADEMA ya sasa na ACT Wazalendo wanapoteza au wanatupotezea muda kwa kujua au kwa kutokujua. Hiyo mikakati na watu wa kimkakati waliokuwa nao NCCR, hivi vyama vya sasa havijakaribia hata. Na bado NCCR-Mageuzi, mageuzi yakawashinda.
 
Mkuu ndio maana tukisema Mbowe ni Mwamba muwe mnaelewa. Uongozi wake ni wa busara kuliko mihemko.

Angekua mwingine chama kingepasuka enzi za mgogoro na wangwe, mgogoro wa BAVICHA 2013, waraka wa Zitto, ama kuondoka kwa Slaa.

Lakini Kwa umahiri wake aliweza handle hayo masuala na chama kikavuka bila mpasuko.

Kingine Mbowe anatumia narrow management yes ni chama Cha kidemokrasia ila Kuna narrow structure kwahiyo yeyote anayevuruga utaondoka mwenyewe ila inner core itabaki intact!!
 
1. How?
2. Kwanini alibadili katiba ili awe mwenyekiti wa milele?
3. Kwanini amekikumbatia chama kama mali yake? Yeye ndio anaamua nani awe nani?
4. Je, composition ya maafisa wa chama(sekretariat ya chama) pale makao makuu ikoje?
5. Je, mfumo wa kuajiri wa CHADEMA ukoje? Kwanini wanashindwa kuiga kwa CCM?
6. Kwanini wakati wakiwa juu(their prime time), 2005-2020: Hawakuweza kujenga ofisi za chama nchi nzima?
7. Sekretariat za mikoa za chadema ziko wapi? Ni mikoa mingapi ina sekretariat? Ni wilaya ngapi zina sekretariat?
8. Mikakati na utekelezaji wa elimu ya uraia kwa wanachama na wananchi ziko wapi? Hata tu kuomba kipindi katika TV za hapa nchini, hakuna.
Hata kufika Clouds au kipindi cha dk 45 cha ITV hakuna!
Can a political party grow automatically?
 
Kabla sijakujibu embu jiulize umesema NCCR ilikua na Kila kitu ambacho Chadema Haina Sasa na wewe umeongeza list ya mambo 8 hapo kwamba Chadema haina.

Sasa jiulize kivipi hayo yote Chadema hatuna ila Bado hatujapotea kama NCCR? yaani unadai hatuna ofisi, hatuna sekretarieti, hatuna media n.k ila chama hakijafa je huoni mpaka hapo Chadema ni tofauti na NCCR yaani ukiwa na resources ila ukakosa uongozi imara basi hakuna chama kitakua.

Na ndio maana nikasema mpe credit Mbowe kwamba licha ya kuwa Hana hizo rasilimali tajwa ila Bado amekisimamisha Chadema kuwa hapo kilipo Leo!!
 
Mimi nilichojifunza vyama vya siasa ni kiini macho na kupumbaza watu Ila viongozi wengi wa upinzani wengi ni maagent wa serikali na ni Wana CCM damu. Vyama vya upinzani= CCM A, CCM B, CCM C, ........=CCM lengo ni kuwaaminisha ngozi nyeupe kuwa tuna demokrasia ya ushindani ya vyama vya siasa ili tupewe mamisaada.
 
Bado sijajua ni kwa nini Mungu aliwafanya watu wachache zaidi waelewe mambo in deep and in real sense!
lengo ni kuwaaminisha ngozi nyeupe kuwa tuna demokrasia ya ushindani ya vyama vya siasa ili tupewe mamisaada.
 
Chadema imeandikiwa "obituary" tokea 2013 na Mzee wassira ila tupo hapa ni 2023 nadhani umepata mrejesho kutoka mikutano inayoendelea. Ni hivi unlike NCCR, Chadema kina misingi imara na watu makini ndio maana licha ya migogoro ila Bado uongozi upo intact na motisha ipo juu sana.

View attachment 2535565
Ninacheka tu mkuu 'zitto junior', kwa mtu kama wewe kutumia picha kama hizi kuwa ushahidi wa chama kukubalika.

SAWA, niseme CHADEMA ilikuwa inakwenda vizuri sana; hasa ilipokuwa inapitia kwenye tanuru la moto moto wa Magufuli.

Samia kaja kaimwagia barafu. Ni sahihi kabisa kusema hapa kwamba haijulikani kutatokea nini baada ya barafu hii kuyeyuka na kuona kilichobaki mahala pa CHADEMA.
 
Mkuu ndio maana tukisema Mbowe ni Mwamba muwe mnaelewa. Uongozi wake ni wa busara kuliko mihemko.

Angekua mwingine chama kingepasuka enzi za mgogoro na wangwe, mgogoro wa BAVICHA 2013, waraka wa Zitto, ama kuondoka kwa Slaa.

Lakini Kwa umahiri wake aliweza handle hayo masuala na chama kikavuka bila mpasuko.

Kingine Mbowe anatumia narrow management yes ni chama Cha kidemokrasia ila Kuna narrow structure kwahiyo yeyote anayevuruga utaondoka mwenyewe ila inner core itabaki intact!!
Nilisema "nanyamaza", kusubiri wakati useme, lakini inalazimu nitoe duku duku la mwisho hapa, pamoja na kwamba nitakuwa narudia niliyokwishasema mara kadhaa humu humu JF.

CCM anayoitamani Samia, na CHADEMA anayoipigania Mbowe; hakuna tofauti kati yao.

Lililobaki ni jinsi gani watakavyounganisha juhudi zao na kuendelea mbele.

Kazi kubwa ipo kwa Samia, kuondoa takataka zote za Magufuli, pamoja na ukoko mwingi uliokwishagandamana huko miaka na miaka.
Mbowe sasa hivi anatumia turufu ya maumivu yake na ya wenzake waliyoyapata miaka yote hii. Wanachama wa chama hicho, wengi wao sasa hivi hawajui chama kinakokwenda; lakini wanalazwa usingizi kwa matumaini, kwamba "maridhiano' ndiyo yanayosababisha hali ipoe, na yakishatimia chama kitaendelea kwa misingi yake waliyoielewa wao toka zamani.

Sina hakika kama kati yao waliwahi kudhani kwamba wangeweza kuwa pamoja na CCM katika jambo lolote. Sasa tusubiri tu kuona 'shock' watakayoipata baadhi yao mambo yakishakuwa wazi.
Nisilolielewa, ni nani atakuwa mkbwa kati ya mwenzie, lakini hapana shaka Samia atakuwa amewakaribisha CHADEMA, kwa hiyo ndiye atakayekuwa kinara.

Yote haya yatategemea mafanikio ya Samia kuyaangamiza yanayomkabiri huko ndani ya CCM.
Na huko CHADEMA itakuwaje?
Sioni wengi wenye msimamo wa kumkabili Mbowe.

Lakini swali litakuwa: Bado CHADEMA itabaki kuwa ile ile inayojaza nyomi hizi? Au itakuwa inaelekea kwenye u-NCCR au u-TLP?

Nimemaliza. Sidhani kuwa nitarudia tena kuyasema haya.
 
Tatizo la mageuzi Tanzania lilianza kwa kufutwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1967, wakati pia mfumo wa vyama vingi unarejeshwa mwaka 1992 wanazi wengi na vigogo wa chama tawala walikubali kwa shingo upande tu.
Kinachohitajika sasa kuleta mageuzi ya kweli ni kubadilisha katiba ina favour utawala wa chama kimoja iakisi mfumo wa vyama vingi.
Mparanganyiko wa NCCR haukuishia kwa kuundwa UMD au kuondoka kwa Chief Abdallah Said Fundikira, bali uliendelea kuwepo. Kati ya Desemba 1991 na Februari 1992, Bwana James Mapalala (Rip) pia aliacha NCCR na kuanzisha Chama Cha Wananchi (CCW) - Mapalala akiwa Mwenyekiti na Katibu Mkuu wake akiwa Dr. Alec Chemponda (RIP). Mch. Christopher Mtikila (Rip) aliacha NCCR pamoja na Mwinjilisti Kamara Kusupa, mlokole Mwigandoshi, na Bwana Mahinbo Kaoneka, na kisha kuanzisha Chama Cha Democrasia (CCD) - Kaoneka akiwa Mwenyekiti, Kusupa Katibu Mkuu, na Mch. Mtikila akiwa 'Mlezi'. Viongozi wa CCD waligombana na mlezi wa chama chao, na kisha Mch. Mtikila alitangaza kubadilisha CCD kutoka Kiswahili kuwa Kiingereza, yaani Democratic Party (DP), na kuwaachia Kusupa na Kaoneka CCD yao. Ni wakati huo KAMAHURU walijitenga na NCCR kinyemela, kuungana na CCW na kisha kuunda chama cha The Civic United Front (CUF). Mwenyekiti akiwa James Mapalala na Katibu Mkuu mzee Khamis Mloo (Rip), Seif Sharif Hamad (Rip) akiwa Makamu Mwenyekiti (Zanzibar).

Hata hivyo, NCCR (Kamati) iliendelea kutandaa (networking) kupitia njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kusambaza machapisho (Tunachotaka Sasa, Upinzani Siyo Uadui, Sera ya UZAWA) na kujitangaza kupitia magazeti ya Radi (likimilikiwa na Ndimara Tegambwage), Mfanyakazi, Motomoto, Heko, Mshindi, Wakati ni Huu, Michapo, Family Mirror, na kadhalika, na kutembelea watu maarufu wenye mwelekeo wa kimagharibi kwa lengo la kuwashawishi, kuunga mkono, au kujiunga na NCCR. Miongoni mwa watu waliotembelewa walikuwa ni pamoja na Bwana Wilfrem Mwakitwange (aliyekuwa mmiliki wa Rungwe Oceanic Hotels & Resort), Bwana Hillal Mapunda (aliyekuwa mhadhiri wa Chuo Cha Siasa [Chama] Kivukoni), Mzee Mushendwa (mfanyabiashara aliyekuwa akiishi Morogoro), Daktari Walid Amani Kabourou (wakati akiwa likizo akitokea Marekani alikokuwa akiishi), Bwana Edwin Mtei, na wengineo. Aidha, kupitia Prince Bagenda, Daktari Ringo Willy Tenga, waandishi wa habari Mbena Mwanatongoni (huyu sijui mahali aliko kwa sasa) na Anthony Ngaiza (tunaye hapa jukwaani), Professa Mwesiga Baregu (Rip) na Mashaka Nindi Chimoto (Rip), NCCR ilianzisha asasi ya kiraia ya African International Group of Political Risk Analysis (PORIS) ikiwa na dhima ya kuimarisha umahiri wa jamii ya kiraia (civic competence) kwa Watanzania, na kueneza dhana ya mageuzi ya kisiasa miongoni mwa Watanzania.

Februari 1992, NCCR (Kamati) ilibaini mwelekeo wa kisiasa nchini ulikuwa wa kuanzisha vyama vya siasa licha ya kutokuwepo kwa mwongozo wa kisheria. Kamati ilikuwa na hofu kuwa baadhi ya wana-Kamati (rogue elements) wangeweza kujitangazia isivyo rasmi kuwa NCCR ni chama chao, hali ambayo ingesababisha mtafaruku kiasi cha kuua matokeo chanya ya kazi ya Kamati iliyokuwa imefanyika kwa miezi minane.

Aidha, ni wakati huo Tume ya Jaji Mkuu Francis Nyalali ilikuwa imetoa ripoti na kupendekeza kwa Serikali kuwa Tanzania ianzishe mfumo wa siasa za ushindani wa vyama vingi. Serikali ya Rais Mwinyi na Chama Cha Mapinduzi chini ya Katibu Mkuu Horace Kolimba (RIP) iliitikia (echoed) mapendekezo ya Tume ya Nyalali. Serikali ilitangaza Tanzania kuingia siasa za ushindani wa vyama vya siasa kuanzia Julai/1992.

Februari 15/1992, wana-Kamati walikaa na kukubaliana rasmi kuwa NCCR ibadilike kutoka Kamati ya Mageuzi ya Katiba na kuwa chama cha siasa lakini kwa kubakiza jina la NCCR na kisha kuongeza mbele yake maneno MAGEUZI. Hivyo jina la chama likawa The National Convention for Construction and Reform (NCCR-Mageuzi). Kabla ya hapo, wakati wa mashauriano, wajumbe walikuwa wamependekeza chama kipya kiitwe Chama Cha Demokrasia na Maendeleo. Hata hivyo, hofu ya kuachwa kwa jina la 'NCCR' kisha lije kutekwa na watu wenye nia mbaya na ku-water-down matokeo chanya ya kazi zake ilipelekea muafaka kuwa maneno 'DEMOKRASIA NA MAENDELEO' yabaki, ila yawekwe na kuonekana katikati ya Chata ya Chama.

Mara baada ya NCCR-Mageuzi kutangazwa kuwa chama - Mabere Marando akiwa Mwenyekiti, Prince Bagenda akiwa Katibu Mkuu, Mashaka Chimoto akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Ndimara Tegambwage akiwa Katibu wa Habari, Uchochezi na Uhamasishaji - chama kilienea nchi nzima kwa haraka sana, kikibebwa hususan na wanafunzi na wahadhiri wa Chuo Kikuu. Chama kiliunda na kuimarisha kamati za mikoa yote nchini. Chama kilipata misaada ya hali na mali kutoka kwa viongozi na watu mabalimbali - akina Gulam (huyu ni mtoto wa Mama Kero, Mhindi aliyezaliwa na kukulia Bukoba), Dr. Alex Khalid (RIP) mmiliki wa Makondeko Holdings, Dr. Tenga, Prince Bagenda, Ndimara Tegambwage na Watanzania wengine waliokuwa wakiishi nje na ndani ya nchi. Mtanzania mmoja, Patrick Bamukunda (RIP), alijitolea gari lake na yeye mwenyewe kuendesha viongozi wa NCCR-Mageuzi muda wote na mahali popote ambapo wangetaka kwenda kwenye kazi za Chama. Wanafunzi kutoka vyuoni walifanya kazi za kueneza NCCR-Mageuzi kwa kujitolea.

Mwezi Machi/1992 uongozi wa NCCR-Mageuzi ulimkaribisha Mzee Edwin Mtei kujiunga na chama hicho. Prince Bagenda akiambatana na James Mbatia, walikwenda kwa Mzee Mtei, nyumbani kwake USA River, Arusha wakiwa na ujumbe rasmi wa chama kumkaribisha Mzee Mtei kujiunga na NCCR-Mageuzi. Mzee Mtei alitaka kwanza apelekewe andiko la Sera na Katiba ya NCCR-Mageuzi asome kwanza kabla ya kufanya uamuzi wa kujiunga na chama hicho. Alipendekeza nyaraka hizo zipelekwe nyumbani kwake Dar es Salaam na kwamba baada ya kuzisoma angeitisha mkutano kukutana na uongozi wa NCCR-Mageuzi kujadili way forward. Nyaraka zote ziliandaliwa na kuwasilishwa kwake kama zilivyopendekezwa.

KUNAKO Mei/1992, baada ya kusoma andiko la Sera na Katiba ya NCCR-Mageuzi, Mzee Mtei aliwaita viongozi wa NCCR-Mageuzi na kukutana nao nyumbani kwake Dar es Salaam. Ilikuwa wakati wa mkutano huo Mzee Mtei aliwaambia viongozi wa NCCR-MAGEUZI kuwa hakuridhia maombi ya kujiunga na NCCR-Mageuzi. Mzee Mtei aliwaambia viongozi hao kama ninavyonukuu "Vijana kuna watu wengi wenye 'means and substance' wanataka mimi nianzishe chama. ...kwa hiyo, nitaanzisha chama, ninawashauri mvunje chama chenu, niwakaribishe mje kujiunga kwenye chama changu," mwisho wa kunukuu. Marando alimjibu Mzee Mtei kwa kumwambia kuwa chama cha NCCR-Mageuzi kimekwisha kuanzishwa na kuwepo, hivyo hawakuwa tayari kuvunja chama hicho. Kwamba Mzee Mtei aendelee na jitihada zake za kuanzisha chama chake ila akisha 'kunyeshewa mvua' kama wao, 'wangekutana wakati wa wakijikinga mvua'.

Wiki moja baadaye Mzee Edwin Mtei akiwa na marafiki zake; Bob Makani (RIP), Edward Barongo (RIP), Mzee Brown Ngwilulupi (RIP) na wengineo, wakiwa wamevaa suti na suruali zikining'inia kwenye suspenders, waliitisha Press Conference pale Motel Agip, Dar es Salaam, kutangaza kuanzishwa kwa chama kipya kikiitwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Ukweli wa kihistoria ni kuwa Mzee Mtei na wenzake hawakufanya mental work hata kidogo bali walitumia jina, Sera na Katiba ya NCCR-Mageuzi kuanzisha Chadema.

Daktari Walid Amani Kabourou (Rip)

“....Hitoria ya Dr. Walid Amani Kabourou, katika siasa za upinzania hapa nchini haikuanzia Chadema, la hasha.

Mwaka 1992, akiwa safarini kwenda USA, Dr. Kabourou alipitia ofisi ya makao makuu ya NCCR-Mageuzi, mtaa wa Mchikichi Dar es Salaam, alinunua kadi (sikumbuki namba yake) ya NCCR-Mageuzi na kujiunga na chama hicho. Kisha alikutana na kujadiliana na viongozi wa chama hicho; Mabere Marando, Prince Bagenda, Ndimara Tegambwage, na Mashaka Nindi Chimoto (RIP).

Mwaka 1993 vilitokea vifo vya Mhe. Mbano na Mhe. Stephen Kibona aliyekuwa waziri wa fedha wakati huo. Kwa hiyo, kulikuwa na majimbo mawili - Ileje na Kigoma mjini - yaliyofanya uchaguzi mdogo kwa wakati mmoja.

Katika jitihada za kutafuta wagombea, kwa kuwa wakati huo Chadema hakikuwa na watu zaidi ya old guards wake akina Bob Makani (RIP), Edward Barongo (RIP), na wengineo, Mwenyekiti wa chama hicho, Mzee Edwin Mtei, alisafiri hadi USA kumfuata Dr. Walid Amani Kabourou. Mzee Edwin Mtei alimwambia Dr. Kabourou ujumbe wa uongo kuwa vyama vya NCCR-Mageuzi na Chadema vilikuwa vimekubaliana kugawanya majimbo - kwamba NCCR-Mageuzi kiweke mgombea jimbo la Ileje wakati Chadema kikiweka mgombea katika jimbo la Kigoma mjini. Kwamba safari ile alikuwa ametumwa na uongozi wa NCCR-Mageuzi (Mabere Marando) ampelekee ujumbe Dr. Kabourou ahamie Chadema ili aweze kugombea ubunge jimbo la Kigoma mjni; kisha akampatia kadi ya Chadema.

Ni bahati mbaya kuwa tangu awali siasa za upinzania nchini Tanzania zimeendelea kujengwa kwenye misingi ya uongo. Na ni uongo huo uliopelekea safari ya Dr. Walid Amani Kabourou kujiunga na Chadema.

Kamati ya Utendaji ya NCCR-Mageuzi ilipokaa iliamua na kumuagiza Mwenyekiti Mabere Marando apige simu kwa Dr. Kabourou kumtaarifu kuwa chama kilikuwa kimemteua aje kugombea ubunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Dr. Kabourou alibaki midomo wazi na kumwambia Marando kuwa tayari alikuwa ameingia makubaliano/amesaini fomu za Chadema kugombea ubunge kupitia chama hicho [baada ya kuelezwa kuwa kulikuwa na makubaliano baina ya Chadema na NCCR-Mageuzi.....

Kitabu Cha Historia ya Mageuzi nchini kinakuja ukikisoma utajua mengi kuhusu mradi usiokamilika wa mageuzi nchini Tanzania.

Note: Mimi conductor nimekopi na kupaste sina hati miliki ya kubadirisha chochote. Zaidi nimeongeza picha hiyo tu.
View attachment 2535345
 
Back
Top Bottom