Kafulila aifunika KIGOMA

haya ndiyo matokeo ya kukurupuka katika maamuzi hivi hakukuwa adhabu nyingine zaidi ya kumfukuza uanachama

Hata hivyo ni bora kabla hajachukua uamuzi huo James Mbatia angefanya utafiti/uchunguzi nini ingegekuwa impact ya kumfukuza chamani David

Chama bado kina nafasi ya kulitatua tatuzo hili ndani ya siku 14 walizo mpa au kupitia mahakama
Walichofanya ilikuwa ni kuzuia kile wenyewe wanachoita mapinduzi yaliyolenga kumtoa Mbatia kwenye kiti chake. Sasa wamechelewa. Nafasi pekee ya kumdhibiti Kafulila ilikuwa kumsamehe pale alipokwenda kulamba viatu vya Mbatia. Sasa hivi wakimsamehe watakuwa wamemrahisishia njia yake ya kubeba uenyekiti. Na wakishilkilia uamuzi wa kumfukuza ndiyo anaaondoka na chama. Kuna somo kwa vyama vyetu hapa.
 
David Kafulila anadhuriwa kwa sababu ameona na kusema alichoona. Kama akina Mbatia na wafuasi wake, especially wale wabunge wawili wa Ksl, watakamilisha azma yao, nccr itakuwa imejifuta Kigoma, nadhani na pahali pengine. Kafulila ni kijana masikini ila ambaye hategwi kwa pumba kama wenzake. His way of thinking transcend far more than his colleagues.

Sasa huyu Mbatia, schoolmate wangu, mseminari mwenzangu ameshindwa kusoma alama za nyakati, anaiua nccr ili kuijenga ccm, HATUDANGANYIKI!
 
Kafulila ni jembe........................anaonyesha kuwa vijana tunaweza.ubunge hauna maana kuzidi mawazo yako.kafulila hafikirii kwa kutumia tumbo.anasimamia anachokiamini,ipo siku jamii itamwelewa.
 
David Kafulila aliyeenguliwa ubunge na chama chake NCCR alipokelewa kwa kishindo kama mfalme jimboni kwake na wananchi

Wakati huko CUF - DAR
kwenye mkutano wa ndani walinzi wa wa chama waliwachapa vibao wajumbe na baadhi kujeruhiwa

Source magazeti ya leo via RFA

Kuna mpuuzi mmoja juzi alidanganya umma hapa eti Kafulia alitumuliwa na wenyeji wa Kigoma
 
Slaa ni kiongozi mzuri sio kwa sababu ya upadre,kwani mapadre wangapi wanafanya mambo ya kijinga.Usimchafue na kumgombanisha Rais wetu ajae na waislamu,busara muhimu
 
Baadhi ya madiwani, wenyeviti wa serikali za vijiji kupitia NCCR Mageuzi katika Jimbo la Kigoma Kusini pamoja na wanachama, wamesema watajiuzulu nyadhifa zao zote za serikali na kurudisha kadi za chama hicho ikiwa mbunge wa jimbo hilo, David Kafulila, atavuliwa uanachama na kupoteza ubunge. Walitoa tamko hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Nguruka, wilayani Kigoma, baada ya kumkaribisha Kafulila na makamishna wa NCCR-Mageuzi kutoka mikoa ya Kigoma, Ruvuma na Dodoma.
Akizungumza kwa niaba ya wenyeviti hao wa vijiji, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyangabo, Kata ya Nguruka, Simon Katenza, alisema hawakubaliani na hatua iliyochukuliwa na Halmashauri Kuu (NEC) ya NCCR-Mageuzi ya kumvua uanachama mbunge wao.
“Mheshimiwa mbunge, utambue kuwa sisi wenyeviti wa vijiji na vitongoji tuko nyuma yako. Hatukubaliani na hili. Na ikiwa unapoteza ubunge basi tutakwenda wote utakakoelekea. Haiwezekani uchaguliwe na maelfu ya watu eti watu wasiozidi hamsini waje wakuondoe. Hatukubaliani,” alisema.

w9VYhFvdoQvaQAAAABJRU5ErkJggg==

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, akihutubia mamia ya wananchi katika Kijiji cha Nguruka wilayani Kigoma ikiwa ni mkutano wake wa kwanza tangu chama chake cha NCCR-Mageuzi kilipotangaza


Diwani wa Kata ya Kandaga, Francis Kumbo, alisema wako tayari kuachia madaraka waliyonayo ikiwa hatua ya kumvua uanachama Kafulila itafikiwa na kwamba wamesikitishwa na hatua ya chama hicho chenye mizizi katika jimbo hilo kutowasikiliza wananchi wanasemaje juu ya mbunge wao.
Katika Jimbo la Kigoma Kusini, NCCR-Mageuzi inaongoza vijiji nane na ina madiwani wanne katika Kata za Nguruka, Itebula, Mganza na Kandaga.
Naye Kamishna wa NCCR-Mageuzi Mkoa wa Kigoma, Bakari Nyamcha, alisema ikiwa Kafulila atavuliwa uanachama atatembea mkoa mzima kuhakikisha chama hicho kinafutika.
Nyamcha ambaye ni mjumbe wa NEC alisema wamefanya kazi kubwa kuhakikisha chama kinapata wabunge mkoani, lakini juhudi zao zinaonekana ni balaa kwenye NCCR-Mageuzi hivyo kuliko kuendelea kuwa kwenye chama hicho ni bora kikafutika na kwa kuwa wao ndio wamekuwa wakifanya kazi ya kukieneza chama siku zote watapita kila kijiji kukifuta na kuwapa wafuasi wao mwelekeo mpya.
Akihutubia maelfu ya wananchi katika viwanja hivyo, Kafulila ambaye aliingia kwa maandamano, aliwaambia wananchi kuwa pamoja na kuomba radhi kwa mdomo na maandishi hakusikilizwa na ndio sababu alikwenda mahakamani kwa kuwa hakukuwa na namna nyingine ya kufanya katika kulipatia ufumbuzi suala hilo.
“Ndugu wananchi, kwa suala hili liko mahakamani na sipendi kuingilia uhuru wa mahakama. Lakini nilifanya jitihada za kuhakikisha mnaendelea kuwa na mwakilishi baada ya uamuzi wa Halmashauri Kuu. Lakini sikusikilizwa. Hivyo njia pekee ya kulinda kura zenu mlizonipa mwaka juzi ni kwenda mahakamani,” alisema Kafulila.
Aliongeza: “Tunataka kura za wananchi ziheshimiwe. Hivyo. mahakama ilitoa uamuzi wa chama kutoendelea na hatua zaidi dhidi yangu. Kwa hiyo, mimi bado ni mbunge, nitaendelea kutimiza majukumu yangu kama mbunge. Hivyo, msiwe na hofu wala mashaka,” alisema kafulila.

Alisema pamoja na kesi iliyoko mahakamani, baadhi ya wananchi wa jimbo hilo wiki hii watafungua kesi nyingine ya kikatiba juu ya suala hili.
“Hivi tunavyoongea, baadhi ya wananchi wako Dar es salaam. Watafungua kesi na hii itakuwa ya kihistoria. Kwa kuwa itakuwa kesi ya kwanza. Suala kubwa ni kuona inakuwaje kiongozi anachaguliwa na maelfu ya watu halafu watu wachache wanaweza kukaa na kumwondoa bila hata waliomchagua kujulishwa wala kushirikishwa,” alisema Kafulila.
Katika mkutano huo, Kafulila aliambatana na Kamishna wa Mkoa wa Ruvuma, Henri Mapunda, na Kamishna wa Mkoa wa Dodoma, Kayumbo Kabutari, ambao walipewa karipio kali na NEC ya chama hicho wakati Kafulila na wenzake walivuliwa uanachama.

Makamishna hao walieleza katika mkutano huo kuwa kudai haki kumewaponza, lakini wataendelea kufanya hivyo hadi chama kitakapokuwa katika misingi imara.
CHANZO: NIPASHE

Sasa kumekucha ndo kwanza asubuhi........
 
Kafulila kachaguliwa na Wananchi wa Kigoma ,Mbatia wa MArangu Kilema na mamluki wake wa Daslam wakiongozwa na yule Katibu nimemsahau jina wanatoa wapi mamlaka ya kumfukuza??

ndio maana tunataka katiba mpya ya wananchi sio ya JK na Mafisadi wake
 
Mimi naisubiri kwa hamu sana hiyo kesi ya kikatiba. Kama wakiifungua na mahakama ikazingatia maslahi ya wananchi, basi hii tabia ya viongozi wa vyama vya siasa kushindwa kuwavumilia wenye mitazamo na yao itakoma.

Na hoja ya kuwa na mgombea huru inazidi kuonekana umuhimu wake ili kuondoa mianya ya udikteta kwenye vyama vya siasa.
 
Chama Cha Chadema kinaonekana kimekomaa kisiasa kwa kuwavumilia wanachama wenye mlengo wa kushoto kama Shibuda.
 
Akina Mbatia nao wafanye mikutano kama kweli wanawaheshimu wananchi.Waende jimbo la Kigoma kusini wakawaeleze wananchi juu ya uamuzi wao ule waone cha mtema kuni
 
Hivi Kafulila haruhusiwi kuapply upya uanachama wa NCCR-Mageuzi?
 
Mimi naisubiri kwa hamu sana hiyo kesi ya kikatiba. Kama wakiifungua na mahakama ikazingatia maslahi ya wananchi, basi hii tabia ya viongozi wa vyama vya siasa kushindwa kuwavumilia wenye mitazamo na yao itakoma.

Na hoja ya kuwa na mgombea huru inazidi kuonekana umuhimu wake ili kuondoa mianya ya udikteta kwenye vyama vya siasa.

na nivigumu kuamini hiyo mahakama, sijui ni lini ilitenda haki tangu ilivyovamiwa na wanasiasa.
 
Kama ni wafuatiliaji wa hali ya kisiasa nchini Tanzania, pia kufanya summary ya wachangiaji humu JF, utapata clue kuwa ZITO anamkakati wa kuwania uongozi wa juu CHADEMA ili kujiweka sawa mbio za urais, hii ni baada ya kufeli mkakati wa kumwengua MBATI nccr!

TATIZO ni kauli za Dr slaa kipindi kile wanamtimua KAFULILA kuwa huyu Bw mdogo alikuwa sisimizi aliyekuwa anataka kuivuruga cdm,
na akasema ama kafulila aondeke au yeye Slaa aondoke!

sasa ZITO amesuka mpango, slaa ale matapishi yake...je slaa atakubali?

elewa kuwa viongozi wa nccr waliohamia cdm kule arusha juzi ni mkakati!

elewa kule jimboni kigoma viongozi wanapiga debe kuwa watahamia chadema, ikimaanisha wanamfuata kafulila....sasa je ...slaa atampokea kafulila cdm?

Well n' good YOTE SIASA! THE TIME WILL TELL, BUT ASAP!

 
Kama ni wafuatiliaji wa hali ya kisiasa nchini Tanzania, pia kufanya summary ya wachangiaji humu JF, utapata clue kuwa ZITO anamkakati wa kuwania uongozi wa juu CHADEMA ili kujiweka sawa mbio za urais, hii ni baada ya kufeli mkakati wa kumwengua MBATI nccr!

TATIZO ni kauli za Dr slaa kipindi kile wanamtimua KAFULILA kuwa huyu Bw mdogo alikuwa sisimizi aliyekuwa anataka kuivuruga cdm,
na akasema ama kafulila aondeke au yeye Slaa aondoke!

sasa ZITO amesuka mpango, slaa ale matapishi yake...je slaa atakubali?

elewa kuwa viongozi wa nccr waliohamia cdm kule arusha juzi ni mkakati!

elewa kule jimboni kigoma viongozi wanapiga debe kuwa watahamia chadema, ikimaanisha wanamfuata kafulila....sasa je ...slaa atampokea kafulila cdm?

Well n' good YOTE SIASA! THE TIME WILL TELL, BUT ASAP!

Ama kweli mmeamua kuwa kazini! Tunajua fedha za MKONO ndo zinafanya kazi kila sehemu ila elewa ZITTO sio maarufu ki-hivyo kama unavyotaka wana-JF tuamini. Ukweli ni kwamba mbinu zote tunazijua hivyo mpe salam kuwa jamaa wameshtukia issue anazotaka kuzifanya. Utata wake hajauanza leo na huyo Dogo Kafulila bora achague kazi za kufanya mbona zipo nyingi sana hapa Tanzania. Siasa zimemshinda Kafulila anatumika na ZITTO na hata wewe mtoa mada kama umetumwa umetukosa!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom