KADA CCM: Rais Magufuli ameacha mtafaruku Zanzibar

KADA CCM: Rais Magufuli ameacha mtafaruku Zanzibar

Watanzania tumechemka sana, ndio nikionacho mimi. Bora mipasho ya mkwere kuliko huyu na vitisho. Wahuni usema tumeingia chaka.
 
Nafahamu marais wengi, hata wa africa, baada ya uchaguzi huwa ni maridhiano, kuheshimiana, na kuungana kujenga nchi.
Nakumbuka hata Kenya, baada ya uchaguzi Uhuru alimsihi Raila maridhiano
 
Mkuu kuna kitu hakipo sawa, lazima tuseme bila kuogopa, zile sio kauli za Raisi wa nchi, tukimwacha aendelee kutoa kauli kama hizi atachafua nchi

Mkuu kuna watu hawataki kuelewa hili. Magufuli atapasua nchi hii asipoingiliwa.

Mkuu wa nchi huwezi kuongea vile. Kikwete ndio alikuwa na kasoro kubwa na mengi yamemkera lakni hakuwahi kuleta hasira katika mustakabali wa taifa. Utaifa kwanza mengine baadaye.
 
Usiogope alikuwa anawatania watani zake wa Zenj. Kiongozi mahiri hivyo hawezi kuyatoa maneno hayo from his mouth. Anaipenda nchi yake, anawapenda watu wake wote, waliomchagua na ambao hawakumchagua.
 
Ukweli sikuamini nilichokuwa nasikia jana ila kwa upande mwingine sishangai maana tabia hazianzi ukubwani. Huyu mzee toka alivyokuwa waziri alikuwa anaropoka tu sasa lipi la kushangaa. Tofauti hajielewi kuwa hivi sasa yeye ni raisi na jana ndio nimemshusha kabisa. Kuwa kiongozi ni hekima sasa wewe kama huna hekima na uvumilivu unaweza kutumia vibaya nguvu sababu unazo ila jambo moja tumepata mtu hastahili kuongoza taifa kama Tanzania ni majanga.
 
Nani alisema Chato kuna watu wenye busara... Mambo mengine siyo ya kushangaa pombe inamadhara kwenye jamii isipo nyweka kistaarabu.
 
Halafu kutwa ana take advantage ya maskini hebu atueleze mikakati yake ya kusaidia maskini maana wakati huohuo kuwasema matajiri. Vipi wewe uwapende maskini na utajiri no maana kuwapenda kuwasaidia maskini apige hatua awe na kitu kidogo. Mimi namuomba aache kurudia story zake hizo ni kama kuwadhihaki maskini tu.
 
Anandika Chilumba (yule mpiga zumari wa JPM)
Matamshi aliyoyatoa Ndugu Rais leo hapa Unguja sikuyatarajia yatoke kwenye kinywa cha mkuu wa nchi, Haya yanamwagia mafuta kwenye moto.

Suala kama la pensheni au matibabu ya mtu aliyewahi kuwa Kiongozi ni la kisheria siyo hiyari ya mtu, Yaan hata umfumanie na mkeo Sheria inakutaka usaini na apewe. Mengine mmalizane wenyewe.

Na kwa kuwa Tumesema siasa zimeisha Basi tujitahidi kuzimaliza kweli, sare za vyama, vijembe na maneno ya ngebe kwenye mikutano ya serikali inawagawa raia.
Siku zijazo wasio wana CCM wanaweza kuacha kuhudhuria mikutano ya Kiongozi mkuu wa nchi kwa sababu wanajihisi wanyonge na wakiwa.

Tuzungumze Maendeleo, kufanya kazi na kubadili maisha yetu, hawa Wakosoaji na wapinzani watakuwepo daima, kuwashambulia katika jukwaa lililolipiwa kodi na watu wote ikiwemo wao si jambo la kiungwana.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, Hotuba za Ndugu Rais katika ziara yake visiwani hazijanivutia wala kusisimua. Zimeiacha Zanzibar katika mtafaruku ule ule au mkubwa zaidi.

☝☝☝☝
Waswahili husema _"kenge huwa hasikiagi hadi damu imtoke masikioni"_. Masikio ya Chilumba yameanza kuonesha dalili za damu
Mazoea tu hayo!!! Mlizoea hotuba za kuremba kwani Seif hotuba zake zilikuwa za kujenga??? Wafuasi wake kwenye kufeka karafuu za watu wasio waunga mkono ni sahihi??? Rais yuko right kuwashughulikia wote wasiotaka amani au suluhu kwamba uchaguzi umeisha na sasa ni wakati wa kazi tu.... ubabaishaji hakuna... Rais kaza mwendo twende watakuelewa tu... Nakukumbuka wakati ukiwa unajenga barabara ya Morogoro eneo la Ubungo hadi kimara kunawatu walikuwa hawataki kupisha ujenzi huo na wakavunjiwa na barabara ikajengwa two ways unaona sasa hivi tunaona matunda ya barabara hiyo wangebembelezwa saa hizi two ways isingekuwepo!! Watu huwa hawapendi mabadiliko hasa Waafrika. Lazima walazimishwe...!!
 
Tambua hawakuanza leo haya unayoyasema, mambo haya yalikuwepo tangu na tangu, wakulima na wafugaji wanauwana kabisa sio kuchomeana nyumba na mashamba, wao wanatoana roho kabisa ulishasikia hotuba kama ile kuwaambia wafugaji na wakulima???
Wakulima na wafugaji hawapigani sababu ya siasa, hawachagizwi na watu wenye siasa za chuki. Wakulima na wafugaji ni ubabe katika jamii usilinganishe na uchochezi wa kugombea madaraka
 
Ukimsikiliza mh. Unalazimika kuwa na mawazo ya ajabuajabu, na kama unaendesha gari unaweza kugonga, naona hotuba zake zisirushwe live, kama mtafaruku uishie hapohapo kuliko kusambaa nchi nzima kwa sekunde.Baadae vyombo vya habar vichuje nin cha kulisha wananchi.
 
Wenye chuki wameambiwa ukweli, kutozikana, kutosalimiana, kuchoma karafuu hakutaleta maendelep, wala hakutavutia wawekezaji. imedhihirika dhahiri chanzo cha yote ni kiongozi wao Seif amedhihirisha kwa kutosalimiana na Shein Msibani. Ukweli sio vijembe ni ukweli unaosemwa kwa wenye chuki. Uchaguzi umekwisha na hakuna rais mwingine ni Shein mpaka 2020 huu ni ukweli, Uende mashariki uende magharibi hakuna serikali ya mpito labda kwa wenye ndoto za mchana, huo ndio ukweli. Sasa ni kazi tu

hapana Mkuu, chanzo ni yule alietakiwa apewe tunzo akishirikiana na wenye bunduki na mizinga. wewe, mimi na huyu aliekwenda kuropokwa pale wote tunajua nini chanzo. Munapoongea mjuwe kama mnaongea na binadamu tuliopewa akili ya kuchanganua mambo. Hicho ulichokiandika hapo juu ni afadhali ungekaa kimya tu maana kinakudharaulisha bure!!
 
Pole saaaaaana! Nyie ndio wale wazushi wa kufuata mkumbo fulani kasema baso. Fulani abaenda urlekeo huo bila iuuliza na wewe umooo. Indicate where is the problem. Sio kubwabwajaja tu bila kuonyesha kosa. Hebu toa mfano mmoja tu ili ' walewale' tujifunze.

Muhane tu. Dharau jwa Mkuu wa nchi ndio mbafutahia no way. Respect jwa Authority ni muhimu na ndio Rais anasisitiza!

Kiswahili tu shida. Sishindani na wewe kamwe! Rudia darasa la tatu kama nilivyowashauri....
 
Back
Top Bottom