KADA CCM: Rais Magufuli ameacha mtafaruku Zanzibar

KADA CCM: Rais Magufuli ameacha mtafaruku Zanzibar

Pole km hujaelewa. Ila mtamuelewa tu soon!
Teh teh teh teh teh!! Mwana salama lkn!! Pole sana vijana hawana nidhamu. Nakukumbukaga sana hadi naogopa kujibu utumbo wa hapa jamii forum (huwa naogopa sana hekima zako naamua kuwa mpole/dhaifu hapa jamii forum [emoji23] [emoji23] [emoji23])
 
Pole km hujaelewa. Ila mtamuelewa tu soon!

Teh teh teh teh teh!! Mwana salama lkn!! Pole sana vijana hawana nidhamu. Nakukumbukaga sana hadi naogopa kujibu utumbo wa hapa jamii forum (huwa naogopa sana hekima zako naamua kuwa mpole/dhaifu hapa jamii forum [emoji23] [emoji23] [emoji23])
Nakumbuka sana busara zenu japo ndo hivyo tena. Huwa hata mimi natamani kupashana nao kwa lugha za kuudhi lkn nakikumbuka baadhi ya wanajamii forum wenye busara kama Mwana hadi naogopa na kukubali yaishe tu. Hbr za siku dada mwana.
 
Anandika Chilumba (yule mpiga zumari wa JPM)
Matamshi aliyoyatoa Ndugu Rais leo hapa Unguja sikuyatarajia yatoke kwenye kinywa cha mkuu wa nchi, Haya yanamwagia mafuta kwenye moto.

Suala kama la pensheni au matibabu ya mtu aliyewahi kuwa Kiongozi ni la kisheria siyo hiyari ya mtu, Yaan hata umfumanie na mkeo Sheria inakutaka usaini na apewe. Mengine mmalizane wenyewe.

Na kwa kuwa Tumesema siasa zimeisha Basi tujitahidi kuzimaliza kweli, sare za vyama, vijembe na maneno ya ngebe kwenye mikutano ya serikali inawagawa raia.
Siku zijazo wasio wana CCM wanaweza kuacha kuhudhuria mikutano ya Kiongozi mkuu wa nchi kwa sababu wanajihisi wanyonge na wakiwa.

Tuzungumze Maendeleo, kufanya kazi na kubadili maisha yetu, hawa Wakosoaji na wapinzani watakuwepo daima, kuwashambulia katika jukwaa lililolipiwa kodi na watu wote ikiwemo wao si jambo la kiungwana.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, Hotuba za Ndugu Rais katika ziara yake visiwani hazijanivutia wala kusisimua. Zimeiacha Zanzibar katika mtafaruku ule ule au mkubwa zaidi.

☝☝☝☝
Waswahili husema _"kenge huwa hasikiagi hadi damu imtoke masikioni"_. Masikio ya Chilumba yameanza kuonesha dalili za damu
naona munashangaa bure tu jina limesibu
 
kaja day out zanzibar anakwambia nitaifanya zenji iwe kama ulaya, piga mipasho kama kopakopa, anakwambia nilitaka kulala Pemba lakini mhhhhhh!!! ahahahaha
 
Ccm Zanzibar wamepongeza huyu anayeiponda ni nani na watamchukulia hatua gani? SIS (STAY IN SLEEP)
 
hapana Mkuu, chanzo ni yule alietakiwa apewe tunzo akishirikiana na wenye bunduki na mizinga. wewe, mimi na huyu aliekwenda kuropokwa pale wote tunajua nini chanzo. Munapoongea mjuwe kama mnaongea na binadamu tuliopewa akili ya kuchanganua mambo. Hicho ulichokiandika hapo juu ni afadhali ungekaa kimya tu maana kinakudharaulisha bure!!

Kumdharau mtu ni hiari ya anayeamua kufanya hivyo, hatuzungumzii chanzo hapa tunazungumzia tabia ya unapokosa madaraka unaitumia jamii kwa kuijengea chuki miongoni mwao. lengo ni kuogofya na kulazimisha kuungwa mkono na watu wasiokuwa na imani nawe kwa lazima wawe upande wako. Ingalikuwa ni chanzo kila mtu anamtazamo wake, wako wanaoamini chanzo ni Maalim, kama angalifuata sheria za uchaguzi asingalijitangazia ushindi na kumkwaza Kiongozi wa tume jinsi ya kutangaza mshindi. Hata angalikuwa ameshinda Maalim tayari matokeo yalishatiwa najisi. Mbali na hilo bado nafasi ya suluhu aliitupa kwa jeuri au kudanganywa na wafuasi/wapenzi wenye malengo yao, alikimbilia Dar na kutangazia dunia amejitoa na hatashiriki. kwake suluhu atangazwe Mshindi. Katika mkwamo wa namna hii njia pekee hata kama sio kutangazwa na Jecha, ilikuwa ni kurudia uchaguzi vingenevyo kungalikuwa na ombwe la uongozi. Kwa mtu mwenye uhakika na Ushindi alioupata angalikubali kuingia kwenye mtanange wa marudio, bado ama watu walewale wakamshauri vibaya au kwa chuki zake akajitoa, hii ni hasara kwa chama. Hakina muwakilishi hata mmoja. Tume imeshatangaza mshindi, Serikali ya umoja wa kitaifa imekufa, Baraza la Wakilishi hakuna wa kuwasemea angalikuwa Masihi ni kusema "Yamekwisha" Hakuna njia ya mkato hata uwatoe muhanga wafuasi wake. Imebaki miaka mitatu wa nne ni kampeni tena wa kupambana naye si Shein tena.
 
Back
Top Bottom