Kabwe Vs. Wangwe - kisa cha mafahali wawili?

Kabwe Vs. Wangwe - kisa cha mafahali wawili?

Hawa jamaa hawajui kuwa kila neno na tendo la mwanasiasa mbele ya jamii linachukuliwa kwa mapana na marefu,kwa hiyo hakuna mambo binafsi au ya taasisi/chama so long as you want to be a public figure.Mpaka 2010 mtakuwa mmejichora sana kiasi kwamba mtakuwa hamna jipya mbele ya jamii na jamaa atawapiga bao kirahisi sana!
 
kama mh. wangwe kayasema haya nadhani hii ni zaidi ya tofauti ya mtazamo wa hoja ya kukua kwa uchumi! kwa mtazamo wangu hizi ni risasi zilizolengwa kummaliza mtu na ni vyema wakuu wa chadema wakakaa pamoja na kuwekana sawa

Wangwe ampinga Zitto

2007-12-26 10:26:41
Na Simon Mhina

...Akizungumza na Nipashe jana, Bw. Wangwe, ambaye pia ni Mbunge wa Tarime kupitia chama hicho, alisema kama kauli hiyo ina ukweli, ni ya kusikitisha na kushangaza kwa vile inaonekana kwamba Bw. Zitto amedandia gari la CCM.

`Mimi ndio maana wakati mwingine huwa nasema, kuna sababu gani kudandia gari la CCM kwa nyuma? Gari liko wazi kama mtu umelipenda unalipanda sio kudandia dandia, utavunjika mguu bure,` alisema Bw. Wangwe...

...Zitto kasema hivyo, basi ana lake jambo, na huo ni msimamo wake binafsi,``alisisitiza.

http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2007/12/26/105044.html

naona mstari wa mpambano umechorwa mchangani
 
Hiyo ndiyo Tanzania Yetu! Kila sector haiko makini, uandishi wa habari ndio maroroso matupu! Kila mwandishi ni reporter wa [uchumi, mazingira, elimu, afya, utalii, technology,afya, etc] sasa kila habari ikitoka inahitaji na wewe uwe na diplom ya uandishi ndio uielewe.. au ukaze macho mithili ya mjusi aliyebanwa mlango.
Infact both are right only Wangwe ana tatizo la mawailiano.
 
..Niliwahi kuuliza hapa kama mtetezi wa suala la Madini muda wote amekuwa Mwanasheria Tundu Lissu, imekuwaje Raisi amteue Zitto Kabwe ktk kamati ya Madini?

..Na kwanini Watanzania haswa wana Jambo Forums wanataka wawakilishwe na Zitto Kabwe wakati wanaelewa he is not as competent as Tundu Lissu?

..Ndiyo yale yale ya Kikwete wakati wa uchaguzi. Tuliuliza sana JK amefanya jambo gani la maana kiasi cha kustahili kuwa Raisi hakuna aliyekuwa na jibu.
 
Kafara,
Katika siasa kama mnagombania kiti mjomba madongo kama haya unarusha tu. na wala sii kosa kabisa kwa mtu kusifia kitu kisha ukapingwa singi na mwanasiasa mwengine wa Chama chako. Tazama US ndani ya demokratic wapo watu wanaounga mkono swala la Iraq na wengine wanapinga na kila siku hurushiana madongo kuhusu msimamo wa mtu fulani. Tena wao basi wapo viongozi wanaojulikana kuwa wana baadhi ya sera zinazokubatia upande wa pili yaani wanakubaliana na Republican hali yeye ni Demokratic ama vise verse.
Tatizo kubwa letu sisi ni kwamba siasa ni WATU na kuwa chama kimoja ni sawa na kuwa pacha ama ndoa hali hata huko kuna kutokubaliana.
Hadi sasa sioni kabisa mahala penye kuleta utata kwetu sisi zaidi ya kuwa Wangwe katumiwa kutoa taarifa ile ili kummaliza Zitto. Na sisi tumeshindwa kuelewa hadi sasa kuwa hili sakata la Zitto na Wangwe nini hasa chimbuko lake.
Je, Ni Obama na mama Clinton wakitafuta kura za wananchi? kwa sababu info zao hazina tofauti wala uongo isipokuwa zimeundwa.
 
....and the difference is....?

Demokrasia ina entail uhuru wa kujieleza unaowekea maanani responsibility na research pamoja na kuweka pembeni personal bickering and selfish ambitions.

Domokrasia ni kimbelembele kinacho-entail "mike happy faces" zinazojisemea ovyo ili kusudi kuandikwa na magazeti, zisizoweza kujizuia kusema kabla ya kufanya research, zinazotumia kila opportunity ku-further selfish ambition rather than reaching common goals.
 
They just need to be careful with the media. It is the media that promoted Mrema and it is the same media that demoted him. Sasa akili ni nywele na kila mtu ana zake.

By the way ni kweli kwamba Zitto alisema uchumi unakua, maana report zote zinaonyesha kuwa hali ya uchumi inazidi kuwa mbaya ikiwemo kukua kwa deni la taifa.

Kwa hiyo Zitto alisema uongo, au siyo?
 
Zitto alisema uchumi unakua au uchumi katika sekta ya madini unakua? Hivi vitu viwili tofauti.
 
zitto alidaganya full stop.
msimpe ushauri wa kumpotosha kama wanavyompotosha JK.

Hakuna uchumi wa madini unaokuwa ila wanazidi kugudua sehemu nyingine zilizo na madini na kuwapa hawa nyag'au na kuzikwanywaua malighafi zetu.
 
Tatizo ni la kuchukua kipengele kidogo cha maelezo ya mtu ukakibinua miguu juu kichwa chini ili upakue yalo ujaza moyo wako!!

Wangwe, hakuelewa Zitto kaongela nini, na katoa ufafanuzi gani? hapa alipaswa kutumia hekima kwa kuto jiingiza kutoa maelezo juu ya habari ambayo hana uhakika nayo.. Lakini yeye kwa kupenda ama kutojua, akaona hiyo ndo nafasi pekee ya kupakua yaliyopo kichwani na moyoni mwake..
Mfano, Haya mambo ya kudandia gari la ccm na kuvunja miguu yana husikaje hapa??

Haya ndo yanadhihirisha kwamba kuna kitu zaidi ya maelezo ya kwenye magazeti. Wakuu wa mbadala hili jambo si la kuacha lipite, inabidi kuwa kutanisha hawa watu ili kuwapiga msasa, kila mmoja aelewe kazi kubwa iliyo mbele yake na umuhimu wake kwa nafasi aliyo nayo! Kufanya kosa.. bali kosa ni krurudia kosa. Fanyeni matengenezo kungali mapema!.
 
Mkama mbona hujajibu swali?

Concept ya kukua uchumi siyo simple ndiyo maana tunataka tupate specifics kwa analysis.

Kwa sababu kama mtu anaongelea kukua kwa uchumi katika sekta ya madini inabidi tuangalie vitu katikas context tusiwe kama Mafarisayo wanao quote only a few Psalms na kuzi-distort out of context in rhetoric to their own advantage regardless of the broader meaning.

Kwa mujibu wa maneno yako mwenyewe

Hakuna uchumi wa madini unaokuwa ila wanazidi kugudua sehemu nyingine zilizo na madini na kuwapa hawa nyag'au na kuzikwanywaua malighafi zetu.

Inawezekana kabisa unachanganya issue ya kukua kwa uchumi na wananchi kufaidika na kukua kwa uchumi huo.Kama wanazidi kugundua sehemu nyingine zilizo na madini na kuwapa hawa nyang'au at the very least kodi na royalties zinaongezeka na uchumi, angalau katika sekta hiyo, unakua.

Sasa kama royalty ya 3% iko unfair au wananchi hawafaidiki vya kutosha na kukua huku hili ni swala jingine.
 
Kafara,
Katika siasa kama mnagombania kiti mjomba madongo kama haya unarusha tu...
..Hadi sasa sioni kabisa mahala penye kuleta utata kwetu sisi zaidi ya kuwa Wangwe katumiwa kutoa taarifa ile ili kummaliza Zitto. Na sisi tumeshindwa kuelewa hadi sasa kuwa hili sakata la Zitto na Wangwe nini hasa chimbuko lake.

Je, Ni Obama na mama Clinton wakitafuta kura za wananchi? kwa sababu info zao hazina tofauti wala uongo isipokuwa zimeundwa.

nimekupata mkuu, lakini si inabidi wajitokeze hadharani kuueleza umma kwamba wanagombea kiti kimoja ili tujue kwamba hii ni mikakati ya kujijenga? tena naamini haya yana muda wake maalum.

nadhani kwao huu ni muda wa kujenga chama chao na sio kuashiria uccm wa "mgombea mwenza" au matamanio ya uccm ya "mgombea mwenza"
 
Kafara,
Mimi nimejaribu kubuni tu hilo swala la kugombea maanake inatisha kuona vita baina ya wakuu hawa na hasa kufikia Wangwe kurusha makombola mazito kama yale ya kudandia basi la CCM.
Nimeunganisha na ile ishu ya Zitto na Dr. Slaa kutaka kujiuzuru, hapo nikapata sababu kubwa ya waandishi wetu hasa hawa chini ya RA kuchora mstari, kesho utasikia wamemfuata Zitto na kusema mjomba PUTA!.. kakutukania mamako.
 
Si wote wanajenga nyumba moja? Sasa ya nini kugombea fito..........
 
Si wote wanajenga nyumba moja? Sasa ya nini kugombea fito..........

Masatu credit hapo, kuna watu hawaridhiki na "tumejenga nyumba" mpaka waonekane wao ndio "head foreman" au "engineer" of some sort.
 
Naomba niulize swali maana naona tunaenda angalau kwenye substance ya tofauti ya Zitto na Chacha kwenye suala hili. Mtu anapoamua kuchimba kisima na kutengeneza mtaro wa kuleta maji kwenye kisima hicho anaweza vipi kupima mafanikio ya kisima chake hicho?

Kama amechimba kisima halafu katengeneza mtaro na maji yanaanza kutiririka na kukijaza kisima je twaweza kusema kuwa kisima kina manufaa kwa watu wa jirani? Je mafanikio ya kisima yako katika kitendo cha kuanza kujaa maji au yapo katika kisima kilichojaa maji na watu wanakuja kuchota kunywa, kumwagilia na matumizi mengine?

Je inakuwaje kama wakati maji hayo yanatiririka toka mtoni kuingia kwenye mtaro na kabla ya kufikia kwenye kisima kuna wajanja wametengeneza mirija kunyonya maji yale kabla hayajafika kisimani? Wale walioko kisimani watakaa kwa muda mrefu kusubiri maji yajae lakini kwa vile kuna "wajanja" wanayachota huku wakiimba wimbo "kisima kinajaa" wale wa kisimani wasiulize "mbona pole pole".

Sasa ikatokea shujaa ambaye anakuja na kusema "jamani maji yananyonywa njiani" mtu huyo si atakuwa shujaa wa wanakijiji wanaongoja maji kisimani? Sasa inapotokea mjenzi wa kisima anakubali kuna tatizo na badala yake anaamua kupanua mtaro wa maji na hivyo maji mengi yanazidi kutiririka na kisima kinaanza kujaa. Lakini wakati huo huo ameamua kuziba yale matundu ya mtaro lakini waliotoboa amewahamisha na kuwaweka kwenye midomo ya kisima hicho na mirija yao ikiwa imechimbwa chini kidogo ya udongo huku maji yanayojaa kwenye kisima yanavuja kabla hajafika pomoni je wanakijiji wafurahi?

Wanakijiji wataona maji ni kweli yamejaa tena kwa wingi na yana fukuta fukuta, lakini hayafuriki. kwa hivyo wanaendela kuchota kiasi kile kile cha maji kilichopo na siyo nyongeza yake.

Hapa ndipo ilipotofauti ya nchi zetu na zile zilizoendelea. Wenzetu walioendelea maji siyo tu yamejaa kwenye kisima bali pia yamefurika kiasi kwamba wengine tunakimbilia hata pembezoni mwake na kuchota!

Sasa, kwenye suala hili la Zitto na Kabwe nadhani tofauti wanapoangalia uchumi wao wamesimama wapi? Je kwenye mtaro, kisimani, pembeni au na mirija yao?
 
Pundit
uchumi unakuwa ikiwa input is less than output kwa maana efficiecy inakuwa kubwa kuliko moja
La kujiuliza je madini yetu yanayokwenda nje yana thamani ndogo kuliko asilimia hiyo tunayopata jibu ni hapana na efficiency yake is ndogo mnooooooo hivyo tunapoteza madini na implies tunapata hasara kubwa that ist uchumi ktk sekta hiyo inakufa.

Viongozi wengi vipofu walio kama Zitto hawalioni hilo eti kwa sababu tu madini tunayachimba ardhini hivo chohote tutakachopata ni faida WRONG IDEA, hii ni sawa umerithishwa mali za baba yako za gharama kubwa wewe unaamua kuzilaguza kwa bei ya madafu eti tu kwa vile unapata chochote na wewe haikukugharimu kuzipata mali hizo.
Mr Pundit kama Mungu angekujalia kuishi miaka mingine mia hapo ndipo utakuwa shuhuda mzuri wa jinsi sekta ya madini inavyokufa.

Viongozi wengi wana miono hii mifupi badala ya mirefu na mwisho kulisukuma bara kuwa bara la giza eti uchumi unakua siku yatakapobaki mashimo na Rais wawakati huo akose cha kubinafisisha hapo ndipo mtajua uchumi ktk madini ulikuwa je kwa ku accerate au deteriorate.
Zito is something in nothing kwa kauli yake hizo

Madini inatakiwa yachukuliwe kama bidhaa iliyotafutwa na inapouzwa ithaminishwe vivyo hivyo na si kuchukulia ipo ardhini kama Zitto alivyochukulia kama hayupo anayekubali kuyanunua kwa gharama ya faida basi yakae ardhini ama kama yanauzwa kwa bei ya hasara na wakoloni wetu weusi tukubali lakini tuseme uchumi unaporomoka ktk madini kwani madini hayamei kama mmea na unachungulia kaburi

Mr Pundit ktk sekta yenye hasara kuliko zote na inayoanguka kwa mwendo wa rocketi ni sekta ya madini matokeo yake huyaoni kama nawe unachukulia madini yapo ardhini
hakuna cha madini wala utalii uchumi wake unaokua na
CHACHA was right more than enough
 
Alichokisema Zitto kama ilivyoandikwa na gazeti la UHURU la tarehe 25 Disemba 2007 Ukurasa wa mbele ni kwamba "Zitto Kabwe asema uchumi wa Tanzania umekua", "Ataka wananchi waiamini serikali". Ndani ya habari yenyewe inasema Zitto amesema wote wanasema uchumi haukui ni waongo na kwamba viongozi wa serikali wapo sawa kabisa kuwa uchumi unakua. Na alitaka wananchi wawe na imani na viongozi wa serikali. Labda hii ndio habari iliyomuamsha Chacha usingizini. Mwenye habari kamili kadiri ilivyoandikwa na UHURU atuletee hapa.

Hii ni mara ya pili kwa Zitto kutoa kauli yenye utata- mara ya kwanza alinukuliwa na gazeti la Mtanzania akisema Rais Kikwete ni kiongozi makini anayestahili kuongoza taifa la Tanzania. Hii ni baada ya kuteuliwa kwenye kamati ya madini.

Wachunguzi wa mambo wanajiuliza, kama ananukuliwa vibaya- kwanini hawiwakwanza kukanusha uzushi mpaka viongozi wenzake watoe kauli?

Chacha naye- hii si mara ya kwanza kumtuhumu Zitto, kuna nini kati yao?

Naendelea kufanya uchunguzi ikiwemo kuwahoji wenyewe Chacha na Zitto na nikipata habari kamili nitawaletea.

PM
 
Back
Top Bottom