Kaa kimya

Kaa kimya

Ukimya ni hazina iliyofichwa. Ukimya unaturuhusu kutazama, kufikiria, kuelewa, na kuunganishwa na hekima yetu ya ndani. Wakati mwingine ni muhimu kunyamaza ili kupata majibu na kugundua mitazamo mipya na maono mapya. Sikiliza ukimya na utaona yote ambayo unaweza kujifunza na kujisahihisha.

~ Nyamaa, kaa kimya, katikati ya kilele cha hasira, kaa kimya,
~ Ikiwa maneno yako yanaweza kuharibu urafiki. kaa kimya.
~ Ikiwa maneno yako yatamchukiza mtu, kaa kimya,
~ Ikiwa huwezi kuongea bila kupiga kelele, kaa kimya,
~ Kama huna ukweli wote, kaa kimya.
~ Wakati unahisi kukosolewa, nyamaza.
~ Ikiwa maneno yako yanatoa maoni yasiyofaa.

Ukimya siku zote ni bora kuliko maneno yasiyo na maana.

Kaa kimya! Ukimya ni hekima, Ukimya ni tafakuri, Ukimya ni kujitathmini.

Good morning Tanganyika .
Kama humu kuna "classmate" wangu wa Chuo, atakumbuka kisa tulichosimuliwa na Mwalimu wetu wa Sociology, Yusufu Ramadhani.

Kwamba, Msomi mmoja, katika Moja ya tafiti zake, alijifanya Sangoma anayetatua changamoto za ndoa. Mmoja wa wateja wake alikuwa ni mwanamke aliyekuwa akimtuhumu mumewe kuwa alikuwa akimgombeza mara kwa mara.

Lakini huyo Sangoma fake, baada ya kumhoji huyo mama kwa kina, alibaini kuwa huenda yeye ndiye chanzo cha tatizo, alikuwa kidomo domo. Alijua akimsaidia katika hilo eneo, tatizo litaisha.

Alimpatia dawa. Alichukua maji na kuchanganya na magome ya miti yasiyo na madhara mwilini mwa binadamu na kumpatia.

Alimwelekeza kuwa, mumewe atakapoanza kugomba, aijaze hiyo dawa kinywani na kuiacha mdomoni hadi jamaa atakapoacha kugomba. Kwa uaminifu ulioshiba, mwanamke alifuata maelekezo yote.

Wiki chache baadaye, alirejea kwa "Sangoma" wake kumpa mrejesho. "

"Dawa" ilifanya kazi kwa asilimia mia Moja. Aliamini kwamba "dawa" imemdhibiti mumewe kumbe yeye ndiyo kawekewa speed governor kinywani.

"Sangoma" alivyomwelekeza kujaza "dawa" kinywani, alijua asingeweza kujibizana na mumewe "kimiminika" kikiwa kimejaa kinywani. Kwa hiyo hata ugomvi ukizuka, ungefifia kwa kukosa ushirikiano.

Kongole kwako mkuu Mshana Jr. kwa somo zuri.
 
Maneno ya Mungu yanasema amelaaniwa yeye amtegemeaye mwanadamu na kumfanya kinga yake
Hata wazazi wetu nao wanadamu tuliwategemea hata wanao wanakutegemea wewe kana mchungaji wao ili uwalee
Alitoka huko huko kwenye uchawi, Ana mengi ya kukufunza
 
Dawa" ilifanya kazi kwa asilimia mia Moja. Aliamini kwamba "dawa" imemdhibiti mumewe kumbe yeye ndiyo kawekewa speed governor kinywani.
 
Hata wazazi wetu nao wanadamu tuliwategemea hata wanao wanakutegemea wewe kana mchungaji wao ili uwalee
Alitoka huko huko kwenye uchawi, Ana mengi ya kukufunza
Asante nimekuelewa vema
 
Kama humu kuna "classmate" wangu wa Chuo, atakumbuka kisa tulichosimuliwa na Mwalimu wetu wa Sociology, Yusufu Ramadhani.

Kwamba, Msomi mmoja, katika Moja ya tafiti zake, alijifanya Sangoma anayetatua changamoto za ndoa. Mmoja wa wateja wake alikuwa ni mwanamke aliyekuwa akimtuhumu mumewe kuwa alikuwa akimgombeza mara kwa mara.

Lakini huyo Sangoma fake, baada ya kumhoji huyo mama kwa kina, alibaini kuwa huenda yeye ndiye chanzo cha tatizo, alikuwa kidomo domo. Alijua akimsaidia katika hilo eneo, tatizo litaisha.

Alimpatia dawa. Alichukua maji na kuchanganya na magome ya miti yasiyo na madhara mwilini mwa binadamu na kumpatia.

Alimwelekeza kuwa, mumewe atakapoanza kugomba, aijaze hiyo dawa kinywani na kuiacha mdomoni hadi jamaa atakapoacha kugomba. Kwa uaminifu ulioshiba, mwanamke alifuata maelekezo yote.

Wiki chache baadaye, alirejea kwa "Sangoma" wake kumpa mrejesho. "

"Dawa" ilifanya kazi kwa asilimia mia Moja. Aliamini kwamba "dawa" imemdhibiti mumewe kumbe yeye ndiyo kawekewa speed governor kinywani.

"Sangoma" alivyomwelekeza kujaza "dawa" kinywani, alijua asingeweza kujibizana na mumewe "kimiminika" kikiwa kimejaa kinywani. Kwa hiyo hata ugomvi ukizuka, ungefifia kwa kukosa ushirikiano.

Kongole kwako mkuu Mshana Jr. kwa somo zuri.
 
Kabla ya kukaa kimya...ni muhimu kujifunza namna ya Kusubiri, Kutulia na Kunyamaza.

Note; ni Mungu pekee ndiye huwafundisha watu Kunyamaza, Kusubiri na kutulia...kabla hawajamanifest kukaa kimya
Kuna mafunuo makubwa sana ya kiroho kwenye utulivu
 
Ukimya ni hazina iliyofichwa. Ukimya unaturuhusu kutazama, kufikiria, kuelewa, na kuunganishwa na hekima yetu ya ndani. Wakati mwingine ni muhimu kunyamaza ili kupata majibu na kugundua mitazamo mipya na maono mapya. Sikiliza ukimya na utaona yote ambayo unaweza kujifunza na kujisahihisha.

~ Nyamaa, kaa kimya, katikati ya kilele cha hasira, kaa kimya,
~ Ikiwa maneno yako yanaweza kuharibu urafiki. kaa kimya.
~ Ikiwa maneno yako yatamchukiza mtu, kaa kimya,
~ Ikiwa huwezi kuongea bila kupiga kelele, kaa kimya,
~ Kama huna ukweli wote, kaa kimya.
~ Wakati unahisi kukosolewa, nyamaza.
~ Ikiwa maneno yako yanatoa maoni yasiyofaa.

Ukimya siku zote ni bora kuliko maneno yasiyo na maana.

Kaa kimya! Ukimya ni hekima, Ukimya ni tafakuri, Ukimya ni kujitathmini.

Good morning Tanganyika .

Kutoka 14:14
"BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya."

Kukaa kimya au kunyamaza ni muda ambao mwili na nafsi (akili, utashi na hisia) hutulia, ndiposa roho huweza kusikia ya ulimwengu wa roho ikiwemo sauti nyororo ya Mungu Baba au Roho Mtakatifu, na kisha kusema nawe kwa upole na kwa amani.

Aghalabu tunajikuta tunasema hivi: "Niliamua kusafiri lakini roho yangu ilisita sana kuondoka. Kwa kuwa sikutulia au sikukaa kimya ili kuisikiliza vizuri, nikakurupuka tu, lakini mbele ya safari nikapata ajali mbaya!"

Heri tungekuwa tunatulia, tunakaa kimya au tunanyamaza kwanza na kuisikiliza vizuri roho isikiacho na/au isemacho, kamwe tusingekuwa tunakurupuka na kufanya maamuzi yasiyo sahihi au kukosa hekima.

Je, unataka kusikia sauti nyororo ya Mungu Baba au Roho Mtakatifu moyoni au rohoni mwako? Je, unataka kufanya maamuzi sahihi na ya hekima? Tulia! Kaa kimya! Nyamaza!
 
Tunapenda kukaa kimya kwa ajili ya hayo uliyoandika ila huwa tunatakiwa tuongee ili ushiriki wetu uonekane tumeongea jambo. Umekaa kimya kikaoni huchangii mada, mwenyekiti wa kikao au wajumbe wanakuuli mbona huongei umekaa kimya tu? Na hapo hujanyoosha mkono kuomba kuchangia hoja. Ni kama huwa tunalizimishwa tuongee sisi wapenda kukaa kimya
Kukaa kimya si kuwa bubu, la hasha! Bali ni kuwa msikivu, kutafakari na kisha kusema yanayofaa. Kukaa kimya ni kama kufanya utafiti kwanza, kuchambua na kutafakari, ndiposa utoe hoja au ripoti.
 
Sawa lakini kanisa la kweli sio jengo kama wengi wanavyodhani
Ni kweli kabisa, kanisa ni kusanyiko la wana wa Mungu. Si jengo la ibada wala si madhehebu (taasisi za kidini), yanayoanzishwa na watu na kusajiliwa na mamlaka za duniani. Kanisa ndilo huenda kwenye jengo la ibada.

Na kwa mantiki hiyo, kiuhalisia wana wa Mungu hawaendi kanisani maana wao ndio kanisa! Aidha, kanisa ni mwili wa Yesu Kristo, waumini ni viungo vyake, kila kimoja na kazi yake au karama yake. Na ifahamike kuwa mwasisi wa kanisa ni Yesu Kristo mwenyewe, si watu!
 
Nimefafanua
~ Nyamaa, kaa kimya, katikati ya kilele cha hasira, kaa kimya,
~ Ikiwa maneno yako yanaweza kuharibu urafiki. kaa kimya.
~ Ikiwa maneno yako yatamchukiza mtu, kaa kimya,
~ Ikiwa huwezi kuongea bila kupiga kelele, kaa kimya,
~ Kama huna ukweli wote, kaa kimya.
~ Wakati unahisi kukosolewa, nyamaza.
~ Ikiwa maneno yako yanatoa maoni yasiyofaa.
Sawa brother
 
Ni kweli kabisa, kanisa ni kusanyiko la wana wa Mungu. Si jengo la ibada wala si madhehebu (taasisi za kidini), yanayoanzishwa na watu na kusajiliwa na mamlaka za duniani. Kanisa ndilo huenda kwenye jengo la ibada.

Na kwa mantiki hiyo, kiuhalisia wana wa Mungu hawaendi kanisani maana wao ndio kanisa! Aidha, kanisa ni mwili wa Yesu Kristo, waumini ni viungo vyake, kila kimoja na kazi yake au karama yake. Na ifahamike kuwa mwasisi wa kanisa ni Yesu Kristo mwenyewe, si watu!
kwa mantiki hiyo, kiuhalisia wana wa Mungu hawaendi kanisani maana wao ndio kanisa! Aidha, kanisa ni mwili wa Yesu Kristo, waumini ni viungo vyake, kila kimoja na kazi yake au karama yake. Na ifahamike kuwa mwasisi wa kanisa ni Yesu Kristo mwenyewe, si watu!
 
Back
Top Bottom