JWTZ Wakanusha taarifa za kuibiwa Kifaru

JWTZ Wakanusha taarifa za kuibiwa Kifaru

Nasikia tatizo ni mgogoro wa ardhi, kwa hiyo jeshi wakaweka vifaru vyao ambavyo havitumiki mpakani kuwatisha wananchi.

Wale wananchi wakatafuta trecta na kukivuta kile kifaru njr ya sehemu kilipo kuwepo sijui kama nia yao ilikua ni kutafuta chuma chakavu au ni mwendelezo wa mgogoro.

Jeshi waeleze ukweli na sio kuleta vitisho[emoji30]
Ukweli ni kwamba kuna mgogoro wa ardhi na kesi ipo mahakamani kile kifaru kilikua eneo la range/kinatumika kama object katka range na ni scraper kwa,kifupi
 
MIMI NIMEJARIBU KUJIULIZA HAYA MASWALI
SWALI LA KWANZA
Kikosi namba 83kj kipo au nacho ni cha uzushi???

SWALI LA PILI
Kijiji cha Tondoroni ambacho wananchi wake takribani 20 wanatuhumiwa kuiba hicho kifaru,hicho kijiji kipo au nacho ni cha kuzusha???

SWALI LA TATU
Mahakama ya mwanzo Kibaha na Hakimu aliyetajwa kusikiliza kesi hiyo ni robots au wapo???

SWALI LA NNE
Hao watuhumiwa 20 waliotajwa kuhusika na kesi hiyo wapo kweli au nao ni uzushi???

SWALI LA TANO
Jeshi limesema kilichoibwa ni screpa tu,je kesi iliyopo mahakamani imeandikishwaje wizi wa screpa ya jeshi au kifaru cha jeshi?????

NB
KAMA HII HABARI IPO KWELI NA SIO UZUSHI
Waandishi wa gazeti la Dira nao wana makosa kwani walipaswa wafikirie wanaandika kitu gani na kutakuwa na madhara gani kwa usalama wa taifa .....????
Kiuhalisia wameleta mstuko kwenye jamii,wananchi wametilia shaka uweledi wa jeshi,wamelidhalilisha jeshi na nchi kwa ujumla...
HATA KAMA HABARI NI YA UKWELI KUNA HAIKUPASWA IANDIKWE VILE AS LONG AS USALAMA WA TAIFA UNAHUSIKA....

Nimejaribu tu kufikiria na akili zangu za asubuhi

Umeshasema Mwandishi wa Habari.
Ulitaka aandikaje kwenye hiyo kesi ya watuhumiwa 20. Walio kamatwa ?

Ikumbukwe kuwa mwandishi anaakili pia kwani unataka kuniambia kuwa alikuwa hajuwi kuwa anaandika Habari ya JWTZ. Tuwaache wakapigwe mikwara tu yaishe Ila kuna walakini ndani yake
 
Nasikia tatizo ni mgogoro wa ardhi, kwa hiyo jeshi wakaweka vifaru vyao ambavyo havitumiki mpakani kuwatisha wananchi.

Wale wananchi wakatafuta trecta na kukivuta kile kifaru njr ya sehemu kilipo kuwepo sijui kama nia yao ilikua ni kutafuta chuma chakavu au ni mwendelezo wa mgogoro.

Jeshi waeleze ukweli na sio kuleta vitisho[emoji30]
Umeeleza vzur sana hv unafikiri na mwandishi nae angeandika kama ww kungekuwa na ukakasi?
 
Umeshasema Mwandishi wa Habari.
Ulitaka aandikaje kwenye hiyo kesi ya watuhumiwa 20. Walio kamatwa ?

Ikumbukwe kuwa mwandishi anaakili pia kwani unataka kuniambia kuwa alikuwa hajuwi kuwa anaandika Habari ya JWTZ. Tuwaache wakapigwe mikwara tu yaishe Ila kuna walakini ndani yake
INAWEZEKANA HILO TUKIO LIPO,LAKINI NAMNA ALIVYOLIANDIKA NDO TATIZO......HAKUFIKIRIA IMPACT YA ATAKACHOANDIKA...IMPACT HIYO NINAYOIZUNGUMZIA MIMI NI KWA JAMII......
JIULIZE NI WANGAPI TULIOSOMA ILE HABARI NA KUANZA KULITILIA SHAKA JESHI KUWA HALIKO MAKINI MPAKA LINAFIKIA HATUA YA KUIBIWA KIFARU AU WE HUKUJIULIZA HILI SWALI???
 
Kuna uzito tofauti ukisema gari limeibwa na scrapper ya gari imeibwa achilia mbali kifaru
mkanganyiko umeongezwa na msemaji wa jeshi, ukweli kuna vifaru vya ukubwa wa land Rover kwa ajili ya ambush za mjini hiki kikiwa chuma chakavu kinawezwa kubebwa, kama bado ni mali ya jw; kimeibwa! shida ni kauli ya msemaji ukiitafakari sana ameshindwa kuweka msisitizo kwenye ukweli kwamba ni chuma chakavu kwa kuwa eneo lao la range hawalilindi na linafikika na raia kitu kinachozua suala la usalama kwa pande zote mbili kitu ambacho wao watatakiwa wawajibike.
 
Nasikia tatizo ni mgogoro wa ardhi, kwa hiyo jeshi wakaweka vifaru vyao ambavyo havitumiki mpakani kuwatisha wananchi.

Wale wananchi wakatafuta trecta na kukivuta kile kifaru njr ya sehemu kilipo kuwepo sijui kama nia yao ilikua ni kutafuta chuma chakavu au ni mwendelezo wa mgogoro.

Jeshi waeleze ukweli na sio kuleta vitisho[emoji30]

asante mkuu

Jeshi waache ubabe wa kijinga
 
Watanzania bwana daaaa.! Kama hujui kitu kaa kimya..magazeti na waandishi wetu ndio hao
 
NAMSHUKURU SANA MWANDISHI WA HABARI HII KWANI AMEWASAIDIA WALE WANAKIJIJI 20 WALIOBAMBIKIZIWA KESI NA JESHI!
Walau wataanza kupumua. Kuna watu walikula pesa zao za fidia wakatka kutumia uanajeshi kudhulumu raia wanyonge. Ni vema ikaundwa Tume ya Kuchunguza hii Tuhuma. Nitashangaa sana kama Bwana Jaffo utawaacha solemba wananchi wako.
 
Hapa ndio unapoweza kuthibitisha kuwa waandishi wetu na vyama vyao hawawezo kufikiri nje ya bahasha za kaki.

Suala hili lingeweza kuwatambulidha umuhimu wao katika jamii kwa kushikamana na kusimama imara kutetea taaluma yao. Kama kuna chembe ya heshima iliypbaki kwao.

Nimeisikia kauli ya vitisho ya jeshi inayosbazwa kwenye mitandao ya kijamii lakini mm inachokiona na kusikia kupitia vyombo vya habari ni masikitiko.

Vituo Vingi vya redio na runinga hats magazeti wanaendelea kupiga muziki na kuchapisha taarifa zisizokuwa na mashiko huku taaluma yao ikinyongwa.

Mpaka sasa sijaona kosa LA mwandishi na hats gazeti lakini hats kama lipo kauli za vitisho zinazoyolewa na madhaamana wa jeshi sio za kiungwana.

Ningetamani kuona waabdishi wakitudisha heshima yao kwa kupinga kauli hizi.wapi jukwaa LA wahariri, wapi MCT, wapi ile taasisi ya abubakar karsan na hata vilabu vya waandishi?
 
Siku ataponyongwa mwandishi ndio utasikia hizo taasisi zinakurupuka, kwa hili tukio wanatakiwa waonyeshe mshikamano kwa kuripoti ukweli na uhalisia wa tukio.
 
Siku ataponyongwa mwandishi ndio utasikia hizo taasisi zinakurupuka, kwa hili tukio wanatakiwa waonyeshe mshikamano kwa kuripoti ukweli na uhalisia wa tukio.

Mkuu wanajitambua?Tumesahau ya mwangosi? Naona wako busy na matamSha, makobfamano na safari zilizoandaliwa na mashirika
 
Mkuu wanajitambua?Tumesahau ya mwangosi? Naona wako busy na matamSha, makobfamano na safari zilizoandaliwa na mashirika
Huu ni wakati wa kuonesha mshikamano. Kuna kila dalili za waandishi kuogopeshwa na kupoteza ujasiri wa kuhoji katika kutafuta habari.
 
Naomba mwenye habari kamili ya hiyo taarifa kutoka kwenye hilo gazeti aiiweke hapa nasi tuweze kuisoma yote.
kuna watu sita walifikishwa kortini kwa wizi wa hicho kifaru, sasa jeshi wanabisha nini? Basi hao watuhumiwa wafutiwe kesi na waiburuze mahakamani serikali kwa kuwasingizi, kuwatesa, kuwapotezea muda na kuwachafulia jina, na walipwe fidia nene
 
NAAMINI JW WANGE KAA KIMYA, WENGI TUNGEIPA HABARI HII UZITO MDOGO. KUKANUSHA NAONA KUMETOA NAFASI YA WENGI KUDADASI. LAKINI NI VEMA WATU NA HASA WANDISHI WAKAJUA NINI MAANA YA SIRI ZA SERIKALI, NA UPI MPAKA WA KUZIANIKA.
Mkuu, kifaru kuibiwa ni siri ya serikali? Unajua kingeenda kutumika vipi?
 
Bado nina ukakasi mkubwa na huyo aliyeendesha hicho kifaru! Hawezi kuwa mwananchi wa kawaida hata kidogo...ni mtu mwenye know how na vifaru na mambo ya kijeshi
Na hata hao waliokamatwa inawezekana kabisa hawahusiki hata kidogo
Napata picha ya kuogofya kuwa inawezekana kulikuwa na dalili za uasi kwenye kambi husika, na kwa kuanzia zilianza kuondoka silaha nyingine kabla ya hiyo kubwa... huu si mpango wa mtu mmoja
Inawezekana kabisa pia kuna kitu kilitokea kikavuruga mipango yote na kifaru kikatelekezwa kijijini na wananchi wakauziwa jumba bovu
Habari kwenye gazeti inamalizia kuwa nov mwaka jana walikuja wanajeshi wakakipaki karibu ya mwanakijiji mmoja kisha wakaondoka ndipo kesho yake walipokuja polisi kuwakamata kwa kosa la kuiba kifaru,lengo lao kuwabambikia kesi ili jeshi wajihalalishie uhalali wa kuchukua eneo lao la kijiji,mwisho wa kunukuu
 
Yaani hii story imekaa sehemu nyeti halafu inachekesha sana, Yaani kifaru cha Jeshi letu imara kimeibwa, acheni masihara ha hah ha ha ha
 
Back
Top Bottom