JWTZ na Polisi wategua Bomu ndani ya chumba cha NMB Bank Shinyanga

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Polisi Mkoa, Janeth Magomi, Kilipuzi hicho kilipatikana kwenye chumba maalum kinachotumiwa na wateja wa Fedha Nyingi (Bulk) na mtuhumiwa mkuu amekamatwa

Kamanda Magomi amesema mkoba uliokutwa na kilipuzi hicho ulisafirishwa hadi Kambarage Police Barracks ambapo wataalam wa Mabomu kutoka JWTZ walifika na kuufyatua kwa haraka.

Tukio hilo lilifanyika Septemba 17 muda wa saa 7 mchana.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi amesema Afande: Ni kwamba majira ya saa saba mchana katika benki ya NMB Manonga hapa Shinyanga, aliingia mteja(mhalifu) anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 60+ akiwa na briefcase yenye rangi nyeusi na koti kubwa lenye rangi ya kijivu, akakaa sehemu ambako wateja wanaochukua pesa nyingi(bulk cash) huwa wanakaa.

Akiwa hapo alijifanya kama vile anajaza fomu za benki, ndipo akaliweka lile koti chini na juu yake akiweka ile briefcase, inaonekana kwenye hilo koti kulikuwa na chupa ya petrol, ndipo akaimwagia ile petrol kwenye lile koti na kulipiga kiberiti na kuondoka, moto ule ulidhaniwa kuwa ni wa kawaida, ndipo wafanyakazi wa benki wakafanikiwa kuuzima kwa fire extinguisher, kisha wakatoa taarifa polisi juu ya ajali hiyo.

Wakati huo mimi nilikuwa hapa maeneo ya kituoni, ndipo nikaondoka na A/INSP Lutufyo, SGT Nale, na baadae wakaja CPL Najim na FC Kalungwa. Tulipofika bank, tulikuta pia maafisa wa zimamoto nao wamefika, lakini tulipo asses tukio, tuliona kwamba tukio hilo linaashiria vitendo vya kigaidi, kwani tulipatwa na wasiwasi kuwa ile briefcase ni bomu lililowahiwa kabla halijalipuka.

Hivyo tulianza kukusanya baadhi ya vielelezo tulivyoviona eneo hilo, ambapo tulichukua sampuli ya kimiminika(petrol), vipande viwili vya mti mbichi, na koti, pia tulipiga picha eneo hilo. Baadae kwa umakini tulilivuta kwa kamba lile koti juu yake ikiwa ile briefcase hadi nje.

Lakini pia tulijiridhisha kuwa kwa moto ule uliozimwa ndiyo ulikuwa detonator ya lile bomu, hivyo kwa umakini tulilichukua na kuliweka kwenye gari hadi katika kiwanja cha mpira cha Kambarage Police Barracks, hapo tulimuimba ACP Mwakagonda awasiliane na maafisa wa jwtz kuja kutusaidia.

Ndipo walipokuja majira ya saa kumi jioni wakiwa na vifaa vya kulipulia bomu na kufanikiwa kulipua bomu hilo. Mtawanyiko wa bomu ulikwenda umbali wa mita 41. Usawa wa ardhi.

Baada ya mlipuko huo, tulianza kukusanya vielelezo kwa kuvipiga picha na kuvuhufadhi, baadhi ya vielelezo hivyo ni. Mbolea, vipande vya mfuko wa sulphate, tambara la shati, chanuo, mabaki ya dumu la ujazo wa lita tano, mabaki ya briefcase, pamoja na sampuli zingine ndogondogo sampuli hizo tumezihifadhi ofisini huku tukisubiri wataalamu wa milipuko kutoka forensic hq.

============================

Police in collaboration with the Tanzania People’s Defense Forces on Saturday September 17, have defused a bomb that was planted inside NMB Bank, Shinyanga branch.

The bomb, which if it had exploded would have caused serious damage including loss of life and property, was found in a special area used by bulk cash customers.

Shinyanga Regional Police Commander, Janeth Magomi has confirmed the incident, adding that key suspect has already been arrested by the Police.

"We have already arrested the suspect and the bomb has already been detonated by TPDF experts before it could harm anyone," said Commander Magomi on phone.

She did not, however, say what type of explosive the officers had found at the scene of crime.

Witnesses say the incident took place at around 1:00pm at NMB Manonga Shinyanga branch, after a person estimated to be around 60 years old entered with a black briefcase and a long gray coat.

One of the witnesses, Janeth Ernest, said the man was sitting in the Bulk customer section and while he was there, he pretended as if he was filling out bank forms, then he removed the jacket and put it on the briefcase.

"He later removed a bottle of what appeared to be petrol and poured its contents on the coat then lit it and left the scene immediately,” she said.

The bank’s staff made effort to turn out the fire and later informed police who arrived almost immediately.

One of the bank’s employees who spoke on condition of anonymity said that initially had not paid attention to the briefcase because they thought the owner had come to either deposit or withdraw large sums.

“But after extinguishing the fire we became suspicious of the black brief case and that was when we called the police,” said the employee.

The briefcase was later transported to Kambarage Police Barracks where experts from TPDF arrived and immediately detonated it.

THE CITIZEN
 
Polisi,wapewe mafunzo,namna ya kutegua mabomu,la sivyo,kila lindo awepo askari wa JWTZ mmoja.
 
Polisi,wapewe mafunzo,namna ya kutegua mabomu,la sivyo,kila lindo awepo askari wa JWTZ mmoja.
Na sio kila askari wa JWTZ anaweza kutegua Bomu,kutakuwa na kikosi maalum hivyo watakuwa wachache,haohao askari polisi waanze kukaa kwa akili tu waache kutumia nguvu hovyo vinginevyo watamalizika
 
Lakini, yawezekana alipata inspiration kutoka kwa yule binti aliewapigia simu zimamoto ili kutest kama wako active. Maybe na huyu mzee alikua anachek if bombu skwadi wapo active....
 
Katika watu wapumbavu na wachafu duniani na hawa waislamu pori hovyo kabisa. Shule hamna kichwani akili hamna basi yapoyapo tuu kama mazuzu. Majitu ya hovyo kabisa.
 
Bomu la kienyeji hilo ama namna gani. Na kwanini libebwe ndio likalipuliwe, ndio taratibu za sappers wa bongo zilivyo?
 
Back
Top Bottom