Moshe Dayan
JF-Expert Member
- Feb 10, 2008
- 815
- 698
Moshe Dayan najua when it comes to mambo ya JWTZ uko very deep.
Swali langu kwako ni hili, kama kweli jeshi linafanya reform na kuanza kuajiri wasomi wengi lakini kwa utaratibu wa jeshi hao wasomi lazima wafaulu shughuli ya monduli, na huko monduli ndiko kunatuhumiwa kuwa na matrainer wanoko hasa wale wa vteo vya chini.
JWTZ inafanya juhudi gani kuondoa huo unoko/uonevu ili wataalamu/waomi hao watumie taaluma zao kwa manufaa ya jeshi na nchi kwa ujumla.
Na kwa nchi zilizoendelea wasomi wanaojiunga na majeshi wanakuwa treated ''kinyaninyani'' kama mnavyowafanyia monduli?
Comrade, nidhamu haijengwi kwa kumbembeleza mtu..., hata kama wewe ni msomi wa kiwango cha juu, kama umeamua kuingia jeshi, kwanza we train you to be a commander.., lazma kwanza uwe mjeshi mzuri umeiva na mwenye nidhamu then ukifaulu,, unapewa sasa kitengo chako kufatana na elimu ulonayo,
Nasisitiza, monduli unafundishwa kwanza kuwa commander then ukifaulu, MMJ wanakupangia kazi,, kazi ya wakufunzi monduli ni moja tu, kukupika uive.na pale ndio unakutana na watu wana roho mbaya shetani mwenyewe anawaogopa, tena anayekutesa ni corporal ambae siku chache mbeleni atakusalute,,
pale unajengwa utimamu wa akili na mwili na pia wanaitoa ile roho flani ya kahuruma ka asili.., huwezi kwenda kwny battle unamuona adui unaanza kufkiria nikimuua familia yake itapata tabu! Au unaanza kufkiria amri ya mungu usiue,, ww unakua kamanda ambae hujaiva,,
Nakubaliana na ww kuna mazoezi huwa yanazidi kipimo lakn pia yana faida kwa utimamu wa mwili kwa mfano monduli kuna "exercise chomoka" hii ni kukimbia 48kms,,, je, majeshi ya kisasa bado yanafanya haya mambo? Lakn jiulize wht if ulitekwa umefanikiwa kutoroka, kama hukupewa stamina ya namna hii utafika mbali??
Na ukitaka kujua kwamba wanajeshi wana stamina pamoja na wengine kua na vitambi.., kila wiki kila kikosi kina siku ya mazoezi na utaona watu wazima na vitambi vyao lakn wanakimbia na wanafanya mazoezi mengine vzr tu, nadhani wengi wenu mnaoishi near barracks hua mnaona
Mwisho wa siku hata tuki-modernize jeshi kinachohitajika ni nidhamu, utimamu wa mwili na akili, comrade, katika hayo mazoezi ya kinyaninyani kuna faida zake pia..., look at things from a positive side!
Last edited by a moderator: