JWTZ mpaka leo imeshindwa kuajiri wasomi wenye vipaji halisi, sababu hizi hapa...

master yako ya sheria itawekwa nyuma ya mzinga ukutane na "big bang" jeshi linahitaji wasomi wachache tu.nani kakwambia digrii zinahitajika jeshini.ha ha ha ni mimi" the war as i hav seen"
 
inaonekana kama ulifukuzwa monduli...,

kwa kifupi, pamoja na kipaji ulichonacho nidhamu ndiyo pillar ya mafunzo yako,, jeshi ni nidhamu, period! Na nidhamu ndio inaleta ufanisi kwenye uwanja wa vita, unapotoa amri mfuasi akatumbukize hand grenade kwny kifaru cha adui, hatakiwi kujiuliza hata kwa sekunde moja.., na hii nidhamu inajengwa kwenye mafunzo, ndio maana jeshini kuna adhabu za kipuuzi kabisa,, mfano unaambiwa umwagilie maua wakati mvua inanyesha,,, ukileta mambo ya logic utaona kua mkufunzi wako ni mpuuzi hana akili,,,, lakn thts part of disciplining you,, ufanye ulichoamrishwa hata kama hupendi,, na hii sio kwa jwtz tu, proffesional armies zote wana namna mbalimbali ya kufundisha nidhamu..,

Kuhusu kuajiri vipaji,,, kwa hili nakubaliana na ww kabisa kwamba japo jeshi linaajiri wasomi na siku za karibuni wanaajiri kwa wingi zaidi, ila bado kuna upungufu mkubwa sana wa wasomi wa fani mbalimbali,, lakini pia tutambue jwtz ipo kwenye transition period,,, kuna individuals ambao hawapendi kabisa hawa watoto wasomi wanaingia na kutoka na manyota fasta,, resistance kwenye change lazima iwepo, ila in general jeshi limeamua liwe dogo na la kisomi na ndio maana kwa sasa hakuna std 7 anaajiriwa wote ni form four and above unless ni mwanamichezo au ana kipaji flani cha sanaa...,

Ukiondoa isolated incidents za wakufunzi wachache kuwachukia wasomi,,, wakuu ngazi za juu wanataka jeshi dogo la kisasa na la wasomi..., na pale monduli bana ukichukiwa na wakufunzi,,, chances za kumaliza ni ndogo sana,,,

Nawaasa watakaopita interview inayokuja hivi karibuni,, pale monduli jishushe,, ni yes sir, yes staff, hata kama task ulopewa logically doesnt make sense

Sir,umeongea vema sana sir!
 
1. a.Je, ni macadet wangapi wenye elimu kubwa waliohitimu na wangapi waliofukuzwa?
b.Je, ni unadhani ni mamlaka gani inayohusika kufukuza cadet?

2. a.Je, jeshi linatengewa bajeti kiasi gani kwa ajili ya tafiti mbali mbali?
b.Je, ni yapi majukumu ya msingi ya jeshi letu? Je jeshi linayatekeleza? Ni yapi majukumu ya ziada?
c.Je, unadhani ratio ya AMO to MD (20:80) ni uwiano mbovu kiasi hicho?
d.Je, jeshi lina vikosi vingapi? Je, kuna vituo vingapi vya afya jeshini? Je unadhani madaktari wote ni vema wawe Lugalo kusubiri migomo?
e.Je, unadhani taifa limewahi kujitosheleza katika nyanja za wataalamu mbalimbali? (mf. madaktari)
f.Je unajua ni mara ngapi kikosi cha mainjinia wamejihusisha katika kuokoa maisha ya watanzania?

3. a.Je unadhani ni wakati muafaka sasa jeshi likaondoa mafunzo magumu yanayowaudhi wasomi wetu na kuweka aina ya mafunzo yatakayovutia wasomi wazuri zaidi jeshini?
b.Je, ungependekeza wakufunzi wa TMA wawe na level gani ya elimu?
c.Je, unaonaje kama jeshi litaachana na strict discipline na kuangalia zaidi elimu ya mtu?

4. Je, unadhani msingi mkuu wa jeshi lolote lile (hata kama ni insurgents) ni nini?

Ni hhayo u.

Kazi ya jeshi ni kupigana na si kingine
 
Na hayo mengine yote yapo kuwezesha jeshi lipigane, basi. Tatizo vijana wengi siku hizi wanalitazama jeshi kama ajira ya kawaida tu.

Ajira kitaan imekuwa ngumu ndomana wasomi wanaona bora twende tu jeshini ila

Jeshi ni taasisi nyingine kabisa tofauti saaaaaaaaana ni vigumu kuendeshwa kwa misingi ya watu binafsi
 
Back
Top Bottom