JWTZ mpaka leo imeshindwa kuajiri wasomi wenye vipaji halisi, sababu hizi hapa...

Moshe Dayan najua when it comes to mambo ya JWTZ uko very deep.
Swali langu kwako ni hili, kama kweli jeshi linafanya reform na kuanza kuajiri wasomi wengi lakini kwa utaratibu wa jeshi hao wasomi lazima wafaulu shughuli ya monduli, na huko monduli ndiko kunatuhumiwa kuwa na matrainer wanoko hasa wale wa vteo vya chini.
JWTZ inafanya juhudi gani kuondoa huo unoko/uonevu ili wataalamu/waomi hao watumie taaluma zao kwa manufaa ya jeshi na nchi kwa ujumla.
Na kwa nchi zilizoendelea wasomi wanaojiunga na majeshi wanakuwa treated ''kinyaninyani'' kama mnavyowafanyia monduli?

Comrade, nidhamu haijengwi kwa kumbembeleza mtu..., hata kama wewe ni msomi wa kiwango cha juu, kama umeamua kuingia jeshi, kwanza we train you to be a commander.., lazma kwanza uwe mjeshi mzuri umeiva na mwenye nidhamu then ukifaulu,, unapewa sasa kitengo chako kufatana na elimu ulonayo,
Nasisitiza, monduli unafundishwa kwanza kuwa commander then ukifaulu, MMJ wanakupangia kazi,, kazi ya wakufunzi monduli ni moja tu, kukupika uive.na pale ndio unakutana na watu wana roho mbaya shetani mwenyewe anawaogopa, tena anayekutesa ni corporal ambae siku chache mbeleni atakusalute,,

pale unajengwa utimamu wa akili na mwili na pia wanaitoa ile roho flani ya kahuruma ka asili.., huwezi kwenda kwny battle unamuona adui unaanza kufkiria nikimuua familia yake itapata tabu! Au unaanza kufkiria amri ya mungu usiue,, ww unakua kamanda ambae hujaiva,,

Nakubaliana na ww kuna mazoezi huwa yanazidi kipimo lakn pia yana faida kwa utimamu wa mwili kwa mfano monduli kuna "exercise chomoka" hii ni kukimbia 48kms,,, je, majeshi ya kisasa bado yanafanya haya mambo? Lakn jiulize wht if ulitekwa umefanikiwa kutoroka, kama hukupewa stamina ya namna hii utafika mbali??

Na ukitaka kujua kwamba wanajeshi wana stamina pamoja na wengine kua na vitambi.., kila wiki kila kikosi kina siku ya mazoezi na utaona watu wazima na vitambi vyao lakn wanakimbia na wanafanya mazoezi mengine vzr tu, nadhani wengi wenu mnaoishi near barracks hua mnaona

Mwisho wa siku hata tuki-modernize jeshi kinachohitajika ni nidhamu, utimamu wa mwili na akili, comrade, katika hayo mazoezi ya kinyaninyani kuna faida zake pia..., look at things from a positive side!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mambo ya jeshi yako hivyo hivyo matrainer wengi elimu zao ni za chini, tafuta hata record za WESTPOINT kwa jeshi la AMERICA au Loyal College UK kupitia cadet school lazima uwe harassed ili apatikane soldier mzuri especially officer ambaye ni commander wa unity!!! Mkuu tafuta training program ya majeshi mbali mbali hasa western armies!! Huwezi kupata best officers kama hujawatoa uraia ingawa mara nyingi wanapewa short courses badala ya long program!! Wataalamu wanapewa special treatment wanapomaliza course, hivyo vijana wavumilie tuu undava ili baadae wafaidi!!

Ni kweli kabisa mike...,
 
Hadith tamu kama vile naangalia movie......eeeeh hivi visa vya jeshini vyataka moyo sana.
 
Nimependa jinsi watu walivyoeleza mambo kwa kweli imenikumbusha jamiiforums ya wakati ule...

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
hahhaaha umenikumbusha mbali nilipeleka cv pale ngome upanga nika kosea geti jama alie ni pokea nikamwambia naleta barua yakuomba kazi akani jibu hili ni jeshi lina taratibu zake sio unaleta barua kama unaenda kwenye shamba la mkonge

hahahaaa,, pole sana, ni kweli, ajira ni hadi zitangazwe,, hakuna maombi ya mmoja mmoja
 
Ukiangalia mfumo mzima wa ajira utabaini yafuatayo
1. Waalimu waliopo vyuoni 90% ni kikwazo kwa wasomi wengi wanaojiunga na jeshi hilo, akitokea mwanafunzi mwenye elimu kubwa hata Phd watafanya kila mbinu wamfukuze kwa kisingizio cha utovu wa nidhamu au watacomment kuwa kafeli.

2. Trainning zao hazija base kutafuta vipaji vya kweli katika nyanja muhimu kitaifa, kama vile madaktari, Eng, nk. Mfano Nyumbu mpaka leo wameshindwa kuifanya iwe ya kizalishaji toka enzi za mwalimu. Lugalo mpaka leo hawana hata blood bank sababu wanasayansi tiba hawapo ndio maana wanashindwa kukabiliana na migomo ya MH, sababu huko wengi 80% ni AMO na CO.

3. TMA ni kikwazo kikubwa sana katika kuwapata wasomi wazuri ndani ya jeshi hilo, elimu ya rasilimali watu kwa waalimu inawezekana ikawa ni issue. So they are trying to reduce the number of students kwa visingizio vya nidhamu ambayo ukifuatilia kiundani sio nidhamu as such but ni kutojua ubaya wakumfundisha mtu at certain level na kumwachisha mafunzo. HILO N BOMU BAADAYE.

4. Mazingira dhaifu kuwawezesha wenye vipaji kubuni kwa uhuru na kutumia taaluma zao, kufanya tafiti chanya maeneo yao ya kazi, mpaka leo hatujaziona.

5. Officer aliyetokea uraiani moja kwa moja I mean those who have got a little knowledge kuwa mkufunzi, atafundisha nini kama sio kupika majungu na kukosa comfidence?

Hayo machache yaliyobainishwa hapo juu ni chanzo kikubwa cha jeshi letu kuwa kama lilivyo hivi leo.

Sina uhakika na madai yako; ila ninajua kuwa kwa muda mrefu sana aliyekuwa mkuu wa Nyumbu pale (General Mashauri) ni rafiki yangu wa siku nyingi sana tuliyejuana tangu akiwa Luteni wa Jeshi akiwa anasomea Masters in Mechanical Engineering huko Ireland; huyu ni msomi aliyeiva sana Mechanical Engineering. Nawafahamu wakuu kadhaa a hospitali ya Lugalo walipita, wote ni wasomi wa hali juu sana katika nyanja zao ama wakiwa MD au wakiwa na specialist degrees. Vile vile ninawafahamu makamanda kadhaa wa vita ya ardhini (Army) niliosoma nao shule za sekondari ambao wana elimu za juu sana za masters na zaidi ya hapo walizopata sehemu mbalimbali za dunia kama Canada, Egypt, UK, USA, South Africa na China.

Nadhani madai yako uliyoweka hapo juu siyo concrete sana, labda kama unamjua mtu mmoja tu ndani ya TPDF anayefanya unayodai, ila siyo kweli kuwa JWTZ yetu ya leo ni kama ile ya mwaka 1964 ambayo haikuwa na wasomi.
 
08_11_rk3qan.jpg

TANZANIA People's Defence Forces (TPDF) commanders push a ceremonial military vehicle during the farewell parade for retired Major Generals, Prof Yodan Kohi (left) and Salim Suleiman (right) at Abdallah Twalipo Baracks in Dar es Salaam on Wednesday August 2011.Photo by Tiganya Vincent MAELEZO

Major General(Rtd) Yodan Kohi ni mtafiti, mwanasayansi na 'brain surgeon' pia aliwahi kuwa mkurugenzi mkuu wa COSTECH COSTECH
Tujiulize kwa nini vijana wa sasa hatuwezi kuhimili mikiki ya kusotea mafunzo ya awali ya kuwa ofisa wa JWTZ? Major General (rtd) Yodan Kohi ni mmoja kati ya wasomi waliotumikia jeshi na ambao bado ni watumishi wa jeshi, je ni kwa vile hatupitii JKT?
 
Majeshi yote duniani yanataratibu zake za kiasili,

Mfano jeshi la Tanzania linapowahitaji kuajiri watu wapya, licha ya kuangalia mahitaji muhimu kwalo, cha kwanza kabisa uingiapo kambini ni kupikwa kuwa mjeshi bila kujali taaluma wala chochote!

Na hapo penye kupikwa kinachozingatiwa ni NIDHAMU yako na UVUMILI wako, BIDII yako.

Ukifeli kwa hayo huna nafasi ya kuingia Jeshini hata kama una PHD.

Hili limesaidia kubadili sera na muundo wa Usalama wa Taifa kwa kuchukua watu kutoka jeshini tofauti na zamani walipokuwa wakiokotwa urainani tu.

Jeshi la Wananchi wa Tanzania linasifika kwa mafunzo mazuri kwa wanajeshi wapya barani Afrika, hili linatokana na maeneo mazuri ya mafunzo na wataalu wanaotajwa kuwa wana ROHO mbaya duniani yaani (wasionahuruma)

Wadadisi wa mambo ya kijeshi duniani wanalitaja jeshi la Tanzania kuwa muundo na falsafa yake ni ya KISOVIETI

Linatajwa kuwa ndio jeshi lenye uwezo zaidi wa kupigana vita vya Ardhini hasa ikizingatiwa kuwa katika mafunzo maalumu ya awali, hukimbia kwa umbali wa 48km na hili hudumu kila kambi tz!

Tatizo la Viwanda vya NYUMBU na vingine ni la sera ya nchi sio ya kijeshi!

Kama serikali inashindwa kuwekeza ipasavyo katika viwanda hiki ambacho kilikuwa ni kiwanda pekee barani Afrika cha kutengeneza magari na zana za kijeshi, serikali iwajibike!

Kenya wameanzisha nao kiwanda cha kutengeneza magari ya kijeshi wakati sisi tunazidi kukiua kile cha NYUMBU!

Leo kambi ya askari wanamaji Kigamboni inajaribu kutengeneza Manowari na boti za Kijeshi na juhudi hizi zinazaa matunda!

Pia NYUMBU wameanza kuzalisha mabomu ya masafa marefu (kama yale ya gongo la mboto)

Vilevile JKT Mafinga wanajaribu kuunda redio za mawasiliano ya kijeshi zisizotumia nishati umeme (kidatu) bali zitumie nishati ya jua!

Kwahiyo mkuu nakujuza kuwa wataalamu tena waliobobea ndani ya jeshi letu wapo tena wa elimu za juu kabisa!

Jambo jema zingatia kinachomuingiza mtu jeshini sio taaluma yake bali ni:

NIDHAMU
BIDII
UVUMILIVU
UZALENDO wa KWELI
 
yani toka nimeanza kusoma huu uzi na michango ya wadau humu ndani nahisi harufu za "viroba" tu.
 
Comrade, nidhamu haijengwi kwa kumbembeleza mtu..., hata kama wewe ni msomi wa kiwango cha juu, kama umeamua kuingia jeshi, kwanza we train you to be a commander.., lazma kwanza uwe mjeshi mzuri umeiva na mwenye nidhamu then ukifaulu,, unapewa sasa kitengo chako kufatana na elimu ulonayo,
Nasisitiza, monduli unafundishwa kwanza kuwa commander then ukifaulu, MMJ wanakupangia kazi,, kazi ya wakufunzi monduli ni moja tu, kukupika uive.na pale ndio unakutana na watu wana roho mbaya shetani mwenyewe anawaogopa, tena anayekutesa ni corporal ambae siku chache mbeleni atakusalute,,

pale unajengwa utimamu wa akili na mwili na pia wanaitoa ile roho flani ya kahuruma ka asili.., huwezi kwenda kwny battle unamuona adui unaanza kufkiria nikimuua familia yake itapata tabu! Au unaanza kufkiria amri ya mungu usiue,, ww unakua kamanda ambae hujaiva,,

Nakubaliana na ww kuna mazoezi huwa yanazidi kipimo lakn pia yana faida kwa utimamu wa mwili kwa mfano monduli kuna "exercise chomoka" hii ni kukimbia 48kms,,, je, majeshi ya kisasa bado yanafanya haya mambo? Lakn jiulize wht if ulitekwa umefanikiwa kutoroka, kama hukupewa stamina ya namna hii utafika mbali??

Na ukitaka kujua kwamba wanajeshi wana stamina pamoja na wengine kua na vitambi.., kila wiki kila kikosi kina siku ya mazoezi na utaona watu wazima na vitambi vyao lakn wanakimbia na wanafanya mazoezi mengine vzr tu, nadhani wengi wenu mnaoishi near barracks hua mnaona

Mwisho wa siku hata tuki-modernize jeshi kinachohitajika ni nidhamu, utimamu wa mwili na akili, comrade, katika hayo mazoezi ya kinyaninyani kuna faida zake pia..., look at things from a positive side!

Nakuunga mkono mkuu ! Wasomi wanafikiri elimu ni kila kitu, jeshi ni nidhamu, utii na ujasiri !
 
Mkuu hilo ndilo jeshi, usiende pale Monduli kutafuta nyota ukatanguliza shahada zako, hizo zitakuja fanya kazi baadae!! Kwanza uwe discipline upate harassment ili uwe askari mzuri, mambo ya jeshi yanahitaji utii, fikiria bomu limetupwa hapo chini unaambiwa down, wewe unajishauri kwa nini si tutakuokota vipande vya nyama???? Kamanda mzuri lazima awe na discipline, hapo tutapata best soldier !!!! Pole kama ulikwenda ukashindwa kupaform, tekeleza amri maswali baadae!!!

Atafute picha moja (DVD) linaitwa "Full Metal Jacket" lina kila kitu kuhusu mafunzo na kuna kuruta mmoja anazidiwa na presha ya mafunzo mpaka anamuua Mkufunzi na kujiua mwenyewe !
 
Nimependa jinsi watu walivyoeleza mambo kwa kweli imenikumbusha jamiiforums ya wakati ule...

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

siku hizi watu wamejaa ushabiki na matusi. Ni wachache sana wanaojenga hoja ya ukweli tofauti na kile anachoshabikia yeye.
 
  • Thanks
Reactions: Wun
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom