DRC: Kabila anapanga mashambulizi dhidi ya serikali

DRC: Kabila anapanga mashambulizi dhidi ya serikali

carbohydates

Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
24
Reaction score
49
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imemshutumu rais wa zamani Joseph Kabila kwa kupanga kile ilichokiita "shambulizi pana” dhidi ya taifa hilo baada ya kuungana na waasi wa M23 na kuunda muungano wa FRN.

Akizungumza na shirika la habari la AFP siku ya Ijumaa (16.10.2026), msemaji wa serikali Patrick Muyaya, alisema Kabila ameamua kuweka wazi hatua zake za kuishambulia DRC kwa kutumia silaha.

"Kuchukua silaha kunamaanisha kuwaua Wakongo ili kujaribu kuteka maeneo ya nchi," alisema Muyaya.
Kwa mujibu wa Muyaya, kuanzishwa kwa harakati hizo mpya ni jaribio la kujipa sura mpya, lakini malengo na mbinu zinazotumiwa zinafanana na zile zilizokuwepo awali.

Hatua hiyo inafuatia tangazo la siku ya Jumatatu lililobainisha kuwa Kabila ameungana rasmi na kundi la AFC/M23 na kuongoza muungano mpya unaoitwa Front pour Refondation de la Nation (FRN) , ambalo limeelezwa kuwa muungano wa kisiasa na kijeshi.

Soma Pia: Aliyekuwa Rais wa DRC, Kabila, Kuongoza Muungano Mpya Utakaochukua Nafasi ya AFC/M23

Muungano huo umetangaza kuwa utaunganisha nguvu, rasilimali na uwezo wake ili kumaliza kile ulichokitaja kuwa utawala wa mabavu kwa kutumia njia zote, ikiwemo nguvu za kijeshi. Kabila amepewa uongozi wa FRN huku viongozi wa M23 wakiteuliwa kuwa manaibu wake.
Chanzo Dw kiswahili
 
Back
Top Bottom