Juu ya DOWANS: Mwakyembe ashangaa kutaka kulipa matapeli

Juu ya DOWANS: Mwakyembe ashangaa kutaka kulipa matapeli

Kansa ya watanzania wengi ni kupenda sana statements kama hizi, eti ndiyo shujaa huyu

alikuwa wapi wakati kesi inaendelea? alisema nini? na sasa kwa maneno yake anaweza kuzuia malipo,IF not forgets he is just like another Rostam in different shape!

Huo ndio ukweli........
 
Soma vizuri hukumu, mkataba ni baina ya Dowans na Tanesco. ICC huwezi kukiuka hukumu yao na nchi ikikataa kulipa kitachofatia ni kutolewa kwenye uanachama wa ICC, sasa sijui hapo biashara zako utafanya na nani kwani nchi nyingi na bidhaa za biashara kubwa lazima ziidhinishwe na Chemba za biashara. Hapo ndio panakuwa patamu. Hili ni pigo kubwa kwa waTanzania.

Nilisema na ninasema tena, aliyesababisha hili ni yule aliyekurupuka na kuvunja mkataba halali na si yule aliyeweka mkataba.

Ni kweli Zomba, hapo kwa RED, lakini pia huyu anayepokea si atuonee huruma? Manake ukifuatilia michango mbalimbali humu janvini inaonekana kabisa wahusika wa hiyo Dowans bado kuna mkono wa Watanzania.

Unajua Kaka zomba, kuwalipa hawa jamaa kama kweli ni stahili yao haina shida, wengi wetu kinachowaumiza ni kwa nini watanzania wengine wenye madeni hawalipwi fasta kama inavyoonekana kufanyika kwa Dowans?

Ina maana wazee wa Africa mashariki wakienda ICC watalipwa fasta? Zomba amini usiamini kama baba yako angekuwa miongoni mwa wazee wa iliyokuwa East Africa hakika usingefurahi kusikia malipo hayo ya Dowans ambayo bado yana utata.


Amini usiamini, Wapo wafanyakazi wa serikali kibao wanaoidai serikali lakini hawalipwi kisa pesa hakuna na huwa wanaridhika bila matatizo. Madai ya aina yoyote yangekuwa yanalipwa haraka kwa wadaiwa, nina amini kwa hii dowans wasingelalamika sana kwa ninavyowajua watanzania.

Lakini linapokuja hili swala la dowans na kiasi hiki cha pesa wengi nanasituka sana. Na kwa maana hiyo wanaona kama kumbe serikali ina pesa huku haitaki kutatua matatizo ya wananchi wake hasa kuweka mipango madhubuti ya Umeme usio wa Mgao.

Huo ndio msingi mkuu wa kuhoji ukichanganya na kamati ileee.
 
Rostam muda wako wa kurudi IRAN umefika we SAKARIR hii nchi siyo yako nashangaa viongozi uchwara kuendelea kumkumbatia huyu ***** umefika wakati, we are sick and tired of being driven of this man.Hey leaders cant you feel shame of embracing this guy, kazi yenu ni taarifa za ki-intelijensia kwa vitu vya manufaa kwa wananchi lakini je hivi hamna taarifa za ki-intelijensia kwa Rostam VICHEKESHOOO.
 
ICC wanamfahamu mmiliki wa Dowans & Richmond wakati Serikali ya Tanzania ndiyo pekee ulimwenguni ku-deal na kampuni tapeli (ghost co.) na kukubali kulipa kitu ambacho hakipo. Hivi kweli tuna viongozi au viroja? Watakwambia wanafuata utawala bora wa sheria.
 
Dowans: Mwakyembe Acharuka!



* Ahoji uhalali wa kampuni ya kitapeli kulipwa fidia
* Wanaharakati kwenda mahakamani kuipinga
Na Bakari Mnkondo na Furaha Omary
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza suala la kampuni ya kufua umeme ya Richmond, Dk. Harrison Mwakyembe, ameibuka na kuhoji uhalali wa kampuni ya Dowans, ambayo ni ya kitapeli kulipwa fidia kwa utapeli wake. ìNikiwa mwanasheria ninasubiri kwa hamu maazimio ya Mahakama ya Kimataifa ya Biashara (ICC) yasajiliwe Mahakama Kuu ili kuona maamuzi ya kuilipa Dowans yalifikiwajeÖ nataka kujua msingi wa tapeli kulipwa fidia kwa utapeli wake?î amesema. Alitoa maoni yake jana kuhusu sakata la Dowans baada ya kutafutwa na gazeti hili kwa muda mrefu. Hivi karibuni ICC ilifikia uamuzi wa kulitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuilipa kampuni ya Dowans sh. bilioni 97 kutokana na kuvunja mkataba kinyemela. Baada ya uamuzi huo, suala hilo lilifikishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ambaye alitoa ushauri kwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, wa kukubali serikali kuilipa Dowans endapo uamuzi wa ICC utasajiliwa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Kwa kauli hiyo, Dk. Mwakyembe, ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, anaungana na aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, sasa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupinga kampuni ya Dowans kulipwa kiasi hicho cha fedha.
Akifafanua kuhusu msimamo wake wa kitaalamu, ambao alisisitiza ni tofauti na wa kisiasa, Dk. Mwakyembe alisema ana shauku ya kujua ni kwa namna gani serikali imepoteza kirahisi kesi hiyo, ambayo alisema hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa digrii ya sheria angeweza kuisimamia na kushinda.
ìUpande wa kisiasa sina tatizo wapo wa kulizungumzia, lakini kitaalamu nitalizungumzia kwa kina kwa kuwa nipo kwenye taaluma ya sheria kwa miaka 20 nikiwa mwalimu. Ningependa kujua msingi wa ICC kufanya lililo batili jana kuwa halali leo,î alisema.
Alisema kamati teule ya Bunge ilimaliza kazi kwa kutoa maazimio kadhaa, ambayo hadi sasa hakuna lililofutwa, na moja ya maazimio hayo ni kuiona Richmond ni kampuni hewa, hivyo kupendekeza ifutwe kwenye orodha ya kampuni za Tanzania na Oktoba, 2008 ilifutwa rasmi.
Dk. Mwakyembe alisema anasubiri kuona ICC ilimuonaje mmiliki wa Dowans Holdings SA, iliyosajiliwa nchini Costa Rica, ambako serikali ya nchi hiyo ilisema haimtambui kwa kuwa hana anuani wala ofisi.
ìKwenye kamati tulifanya utafiti wa kina na serikali ya Costa Rica ilitueleza mmiliki wa kampuni hiyo hajulikani kwa jina, ofisi, anuani ya posta wala namba za simu,î alisema.
Dk. Mwakyembe aliyewahi kuwa mwalimu wa sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema walichoambulia Costa Rica ni kutajwa jina la Bernal Zamora Arse, anayemiliki kampuni takriban 100 zenye kuishia na SA, lakini hazielezi zipo jengo gani, nyumba ama kumiliki gari au pikipiki.
Alisema kutokana na ukweli huo, anashangazwa kuona uamuzi wa ICC ulivyofikiwa, na kuhoji fedha hizo zitalipwa kwa nani?. Dk. Mwakyembe alisema anasubiri uamuzi huo usajiliwe ili apate fursa ya kuupitia kwa kina na kuoana hatua za kuchukua kama mwanasheria.
Wakati huo huo, wanaharakati kupitia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wanakwenda Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kupinga amri ya TANESCO kuilipa Dowans fedha hizo, wakisema haina uhalali wa kulipwa, kwa kuwa ilishafahamika kuwa Richmond iliyoirithi ni kampuni hewa.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, wakili Francis Kimwaga, alitangaza hayo jana mjini Dar es Salaam, alipotoa tamko la wanaharakati kuhusu mtazamo na muitikio wa serikali kuhusu shauri hilo la Dowans. Alisema katika kesi waliyotarajia kuifungua jana, wanapinga kusajiliwa kwa uamuzi wa ICC.
Alisema kituo hicho na mashirika mengine yanayotetea haki za binadamu, usawa wa jinsia na ukombozi wa wanawake kimapinduzi (FemAct), wameshitushwa na kusikitishwa na mtazamo na muitikio wa serikali kuhusu shauri la Dowans.
ìLHRC itafungua shauri leo (jana) Mahakama Kuu kupinga uhalali wa tuzo iliyotolewa kwa Dowans na ICC na isisajiliwe kwa kuwa mikataba ya awali ilipatikana kwa rushwa na kukiuka maslahi ya umma,î alisema.
Kwa mujibu wa Kiwanga, mwenendo wa Wizara ya Nishati na Madini kuhusu suala hilo pia unatia shaka, hususan malipo kwa Dowans.
Alisema katika suala hilo kuna mambo ya kujiuliza, yakiwemo ya kuendeshwa kwa usiri kwa shauri hilo katika Mahakama ya ICC bila wananchi kuelezwa kilichokuwa kikiendelea tofauti na kesi ya Bi-Water dhidi ya serikali, ambapo walialikwa kama marafiki wa mahakama.
ìIkiwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kwa taarifa ya kamati teule ya Bunge iliyoundwa Novemba 13, 2007 kikao cha 11, mkutano wa tisa), ilithibitisha Richmond ni kampuni hewa, inawezekanaje kuwa na mkataba wa kurithisha mali zake kwa Dowans?.
ìUhalali wa kisheria wa miliki ya Dowans kwa mali za Richmond haupo, kwa nini serikali haikutaifisha mali za Richmond tangu awali?î alihoji Kiwanga.
Aliyataja mambo mengine ya kujiuliza ni ikiwa Dowans haikurithi kwa uhalali mali ya Richmond, inawezekanaje kuwa mdai halali dhidi ya serikali kuhusu mali iliyopatikana kutokana na uhalifu, na serikali kuharakisha kuilipa Dowans kuhusu mali iliyopatikana kwa uhalifu.
Kiwanga alihoji sababu za TANESCO kulazimishwa kuilipa Dowans wakati tangu awali ilishakataa kuhuishwa mkataba haramu wa Richmond kwa Dowans.
Wanaharakati hao wameitaka serikali na maofisa wa umma wanaohusika na suala hilo kuzingatia maelekezo ya Katiba na waheshimu uamuzi wa Bunge kuwa, Richmond ni kampuni hewa, hivyo kuendelea kulazimisha Dowans ni kukiuka utawala wa sheria.
Wameitaka Wizara ya Nishati na Madini kuacha kuwabebesha Watanzania mzigo wa kulipa gharama hizo kutokana na kodi wanazolipa, kwa kuwa malipo hayo yanatokana na uzembe, ubadhirifu na ufisadi.
Kwa upande wake, Dk. Sengondo Mvungi, alisema wanakwenda mahakamani ili kupata majibu ya mambo mbalimbali, huku akisema mahakama haipaswi kusajili matapeli, ila isimame iungane na wanaharakati hao na kuwataka Watanzania kujitokeza kupinga hukumu hiyo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Ananilea Nkya, alisema inapaswa picha za wamiliki wa Dowans ziwekwe hadharani ili Watanzania wawajue wanaolipwa fedha hizo, badala ya kutajwa majina.
CHANZO; Mwananchi
 
Sitta then Mwakyembe. Who's next? I think hawa wawili wameikataa collective responsibility ya baraza la mawaziri. Swali ni, kama hao vichwa ngumu watang'ang'ania kuwalipa Dowans, Six na Mwake watajiuzuru kwa kupinga? Najua jk (small letters) hawez wafukuza kwakuwa wana siri nzito juu yake na wengine
 
Tunaomba uweke wazi taaluma yako kwanza, na sikuwahita wenzako MAWAKILI PUMBA. Maana sisi wengine si wanasheria hivyo kama unasema wasemacho wanaharakati ni pumba twambia ni pumba kivipi? na nini kingefanyika? na je wakili yeyote alikuwa anaruhusiwa kushirika ktk usuluhishi nauliza hivi kwa sababu umeeleza hivi ktk post yako "wangepinga huko ICC na si hapa, mahakama ya Tanzania haina mamlaka ya kufuta maamuzi ya ICC".
Tupapie ufafanuzi wa kisheria kuhusu huu mgogoro, Usisahau kutueleza taaluma yako na kiwango chako cha elimu kama 1degree, 2degree au Phd

Mimi sina hizo Digirii zote ulizozitaja, lakini, ujuwe, elimu si kujifungia katika kuta nne za darasa.

Nna upeo mkubwa wa Biashara na nimeiona dunia, na hilo nnalokwambia leo lishike, hao ni Mawakili uchwara.
 
Kumekwiva sasa manake naona wanataka kujlipa wenyewe tu hapo hakuna lolote hapo
 
Ukisikia mawakili pumba ndio hao. Kesi imeamuliwa ICC na mahakama ya hapa ni kusajili maamuzi, wangepinga huko ICC na si hapa, mahakama ya Tanzania haina mamlaka ya kufuta maamuzi ya ICC.

Wanajitafutia umaarufu lakini hawana kesi ya kushinda katika hili. Wangeshinda ingekuwa tu Dowans hawatimiza masharti ya mkataba.

The only way out ni kutangaza kuwa hatuwalipi Dowans na kuwalipa chini ya uvungu. Otherwise ya LONRHO na Nyerere yatajirudia.

Thank you. Hawa kina Dr. Mwakyembe na Sitta ni mavuvuzela ya CCM tu hawana lolote.

Walidandia hoja ya ufisadi na kujidai wapiganaji kumbe hamna kitu zaidi ya kuchumia tumbo tu.
 
Wana Jf, mimi si mwanasheria lakini hii hapa chini imekaakaaje ? Hakuna kifungu kinachoweza kutunasua ? Kwa nini hela yetu na jasho letu liwanufaishe hawa wezi, matapeli na mafisadi ?

Grounds for Refusal to Enforce Arbitral Awards
Generally, a court must comply with a request to enforce an arbitration award. The grounds upon which a court can refuse to enforce an award are very narrowly defined. Generally, there are seven grounds for refusal to enforce, which fall into two categories:


1. Problems with the conduct of the arbitration itself. The party against whom enforcement is sought must furnish proof that the award is flawed due to:
a. Incapacity of a party;
b. Failure to give proper notice to a party, or the inability of a party to present his/her case;
c. The award fell outside the scope of the arbitration agreement;
d. The selection of the arbitrators violated the agreement; or, if the agreement did not address selection, the selection process violated the law; or
e. The award was set aside or annulled.
2. State sovereignty issues
a. The law of the country in which enforcement is sought prohibits arbitration on the subject matter of the issue in dispute; or
b. The recognition or enforcement of the award would be contrary to the public policy of that country.


Je, katika kuilinda na kuitetea sovereignty yetu, Mahakama yetu haiwezi kuikomalia hiyo hukumu kwa misingi hii ?
 
Jenifa umenena, hapa JF kuna watu hutazama upande mmoja tu wa shillingi, hawatazami wa pili. Hilo ndio tatizo.

Na wewe "Zombe " mbona unatazama upande wa pili tu wa shilingi hutazami upande mmoja?
 
Na wewe "Zombe " mbona unatazama upande wa pili tu wa shilingi hutazami upande mmoja?

Nambie, ni wapi amabapo sijapaona, Its Zomba, not Zombe. Toa Z uweke T, halafu ndio utanipata vizuri.
 
Jaji Werema: Ruksa kupinga malipo ya Dowans
Wednesday, 12 January 2011 21:24

Hussein Issa
SIKU moja baada ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kuwasilisha pingamizi Mahakama Kuu kutaka serikali isiilipe Kampuni ya Dowans, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, ameibuka na kusema ni ruksa. Jaji Werema aliliambia gazeti hili jana kuwa, haoni tatizo lolote kwa wanasheria hao kupinga malipo hayo mahakamani, kwani suala hilo halina madhara kwa serikali.

"Waende tu (kupinga mahakamani), kwani ni sehemu ya kazi yao na huwezi kuwazuia. Hii haina madhara yoyote kwa serikali.

Mimi nimeshaongea vya kutosha kuhusu suala la Dowans na kulifafanua sana," alisema. Jaji Werema alisema tayari amesoma hukumu hiyo na kutoa mapendekezo yake kwa wizara husika, hivyo kinachotakiwa sasa ni serikali kutekeleza mapendekezo yake sio kuendeleza mjadala. "Sikiliza. Mimi nimeshatoa maoni yangu kupitia wizara husika. Hayo maswali mnayoniuliza nikiyajibu nitakuwa sijawatendei haki wananchi," alisema Jaji Werema.

Juzi LHRC, kwa kushirikiana na wanaharakati wa haki za jinsia nchini, waliwasilisha pingamizi Mahakama Kuu kupinga malipo ya fidia ya Sh97 bilioni kwa Kampuni ya Dowans. Hata hivyo, ili malipo hayo yafanyike, kesi hiyo ilipaswa kusajiliwa Mahakama Kuu jambo ambalo sasa limeonekana kuingia doa baada ya wanaharakati hao kuweka pingamizi kuzuia mchakato huo.

LHRC walitoa tamko hilo walisisitiza kuwa, wanaungwa mkono na vyama mbalimbali visivyo vya kiserikali yakiwamo mashirika yanayotetea haki za binadamu, usawa wa jinsia na ukombozi wa wanawake (FemAct).

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Francis Kiwanga, alisema wameamua kuweka pingamizi kutokana na mikataba ya awali ya Kampuni ya Dowans kupatikana kwa rushwa na kukiuka maslahi ya umma.

"Kituo kinafungua shauri Mahakama Kuu kupinga uhalali wa tuzo iliyotolewa kwa Dowans isisajiliwe na kuwa, tuzo ya kimataifa kwa sababu mikataba ya awali ilipatikana kwa rushwa na kukiuka maslahi ya umma," alisema Kiwanga. Kiwanga alimtataja Wakili wa Kujitegemea na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Dk Sengondo Mvungi, kuwa ndiye wakili aliyeteuliwa kulisimamia shauri hilo.

"Ikiwa Bunge la Jamhuri ya Muungano kupitia Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa Novemba 13, 2007 ilithibitisha kuwa Richmond ni kampuni hewa, inawezekanaje kuwa na mkataba wa kurithisha Dowans?" alihoji Kiwanga. Kiwanga alisema Wizara ya Nishati na Madini inatia shaka kuhusu mwenendo wa suala zima la Dowans na kutaka Tanesco kukataa kulipa deni hilo.

"Uhalali wa kisheria wa miliki ya Dowans kwa mali za Richmond haupo. Ni kwanini serikali haikutaifisha mali za Richmond tangu awali? Pili ikiwa Dowans haikurithi kwa halali mali ya Richmond, inawezekanaje Dowans kuwa na madai halali dhidi ya serikali ya Tanzania?" alihoji Kiwanga.

Kiwanga alielezea shaka kwa serikali kuwa na uharaka wa kulipa deni hilo bila hata kuchukua hatua zozote za kisheria. Alihoji, "Nini hasa maslahi ya Wizara ya Nishati na Madini hasa ikizingatiwa ndio iliyoshinikiza Tanesco kukubali kuhusishwa na kuhamishwa kwa mkataba wa Richmond kwenda Dowans?"
 
Pasco;

ICC wakitoa hukumu lzm iende kwenye Mahakama Kuu ya nchi husika kusajiliwa na ndipo hapo walioshinda kesi watalipwa;Serikali kama inaona ilionewa na ina ushahidi wa madai yao inaweza ikaiambia Mahakama Kuu yake isiisajili kesi hiyo na hao DOWANS hawatalipwa!

Nchi nyingi tu duniani kwa kupitia Mahakama zake kuu zimewahi kukataza kusajiliwa kwa kesi za ICC na kutolipa wanao wadai na Tanzania inaweza fanya hivi maana DOWANS ilinunua mkataba kutoka RICHMOND kampuni ambayo Kamati teule ya Bunge iliwatangazia wa Tanzania kuwa ni ya kitapeli!

Kwa nini watanzania wawalipe hela matapeli,tuna sababu nzuri tu ya kuiambia ICC kuwa DOWANS hatuilipi maana ilichukua mkataba wa Richomond kampuni hewa isiyokuwepo duniani?
Malafyale, mimi sio mwanasheria, ila tongo tongo kwenye sheria, nimetoa.
1. Sheria ya mikataba ni independence of any interfiarance, iwe ya serikali au ya nani. Kwenye mikataba, kuna void na voidable. Void, ndio mkataba batili ambao ni sawasawa na hakuna 'void ab-initio'. Voidable ni mkataba wenye matatizo yanayorekebishika. Mkataba wa richimand sio void wala voidable, hivyo ni mkataba halali.
2. Wamiliki, ni corporate veil, na majina ni synonames, unaweza kusajili kuampuni kwa majina ya kuku na ngedere, not humans, yakionyesha ni majina ya watu halisi, ndio maana nimesema kwenye usajili, hata hayo majina mnayayaona, ni fictitious names na fictition company lakini wametekeleza mkataba. Wameleta majerereta ambayo siyo fictitious na yamezalisha umeme ambao nao sio fictitious, kinacholipwa sio kufidia kampuni feki, wala wamiliki ni kina nani, bali kufidia hizo jerereta wakiwakilishwa na dowans, nyuma yake wawepo kuku au ngedere, mkataba wa kufua umeme kwa jerereta za ukweli, umevunjwa, jenereta zimezuiliwa, lazima zilipwe!.
3.Hukumu hiyo imeidhalilisha sheria yetu ya manunuzi kwa kusema, eti sheria haijatamka bayana kama ukiukwaji wa sheria hiyo, itaifanya mikataba iwe batili!. Taratibu zimekiukwa lakini sheria haikusema itabatilisha mkataba.
4. Serikali yetu imezungukwa na wanasheria mazumbukuku wa kutupwa, baada ya richmond kushindwa kuleta umeme kwa muda ule waliokubaliana, hapa ndipo serikali ilitakiwa kuuvunjilia mbali mkataba ule na kuyataifisha majereta outright kufidia hasana waliotusababishia. Hatukufanya hivyo na hapa wahusika ndipo waliopotakiwa kuwajibishwa bila huruma, mimi nakumbuka EL akiwasisitizia Watanzania tuvute subira tuwaongeze muda.
5. Walioingia mkataba huo Tanesco nao pia ni mazumbukuku wa ajabu, kwa kukubali vipengele kibao ambavyo vinaitia pingu na kuidharau mahakama zetu kwa kuifanya ICC ndia mahakama ya hakimu mfawidhi, ndio mahakama ya hakimu mkazi, ndio mahakama kuu na hapa hapo ndio mahakama kuu ya rufani!, uamuzi wake ni wa mwisho, hauhojiwi na chombo chochote, unasajiliwa kwa utekeleji tuu ili kupata legal basis Tanzania.
 
Ni kwa nini Ngeleja, Werema na Pinda walikurupuka na kusema Dowans lazima walipwe? Kuna mkono wao hapo au kuna mkono wa mkubwa wao fulani ambaye wanamuabudu kama Mungu wao.

Hakuna kufanya kazi kwa mazoea tena. Kama vichwa vyao vimejaa uyoga that's too bad. Watanzania tumeamka.
Tatu, Ngeleja, Werema na Pinda, wote hawa ni wanasheria na wanajua wanasema nini, achilia furahisha genge!
 
Kaka umesema vizuri swala ambalo wengi tunajiuliza,

Unasema mkataba ulikuwa Illegal, NI WEWE UMESEMA au ndivyo ulivyo? Hiyo ni kwa mujibu wa maelezo kamati ya bunge iliyochunguza Richmond - Bofya hapa kwa ajili ya more details.

Kama ulikuwa ILLegal kwa nini walienda mahakamani in the first place? Inavyoonyesha kulikuwa tayari na systematic arrangements kuanzia kurithi mkataba toka Richmond mpaka kuishtaki TANESCO ICC.

Je ICC iko biased? je anajua mkataba ulikuwa illegal? Bila shaka utetezi wa mawakili controversial (Rex) wa Tanesco ulikuwa dhaifu ndiyo maana Dowans wakapangua hoja hii.

Je watetezi wa TANESCO hawakulijua hili?? Rex Attorneys hebu wasome hapa mkuu halafu uniambie!!!!!!!

Mpaka kesi imeenda ICC,ni kuwa huo mkataba ulisainiwa kwa misingi ya kimataifa, then illegality hapa inaweza kuwa questionable, au ICC credibility might be in question! Tunarudi pale pale kwenye systematic arrangements. Ni kwamba kuna kila dalili kwamba hizi avenues zote jamaa walishaziexplore kabla na ndiyo maana kukawa na vipengele vile vya kipuuzi kwenye mkataba wao na Tanesco

Au mawakili wa TANESCO walikuwa so silly kiasi cha kutoweza kugundua hilo? Rex Attorneys hebu wasome hapa mkuu halafu uniambie!!!!!!!

Mkataba ulivunjwa na bunge siyo? kwa nini TANESCO hwakuchukua zile sababu na kuziwasilisha?? Rex Attorneys hebu wasome hapa mkuu halafu uniambie!!!!!!!

Hoja ya dowans walisema ulivunjwa kwa pressure za kisiasa! could this be true? Hivi ndivyo isemavyo na Dowans!

maana tusipopata utatuzi hapa, then we have many cases ahead us in this world of globalization and every time tutakuwa tunatafutana uchawi - To be frank utatuzi wa hili ni rahisi tu kama kuna political will na matumizi ya taaluma yasiyofisadiwa- Unapoona hata mkuu wa nchi anaogopa hata kucomment kitu ambacho kimekuwa gumzo ndani ya nchi for about a month ujue tuna tatizo tena si dogo, huyo huyo mkuu alishawahi kunukuliwa kwa sifa sifaeti "amepigilia msumari wa mwisho Dowans" - That time ilikuwa kuhusu kununu ile mitambo yao at a price of Billion arobaini, leo tunatakiwa tulipe bilioni karibu 100 yuko kimyaaaaaa!

All in all JK anahusika sana tu na hili jambo na ndiyo maana linakuwa na utata kama inavyoonekana.
 
Back
Top Bottom