Juu ya DOWANS: Mwakyembe ashangaa kutaka kulipa matapeli

Ni kwa nini Ngeleja, Werema na Pinda walikurupuka na kusema Dowans lazima walipwe? Kuna mkono wao hapo au kuna mkono wa mkubwa wao fulani ambaye wanamuabudu kama Mungu wao.

Hakuna kufanya kazi kwa mazoea tena. Kama vichwa vyao vimejaa uyoga that's too bad. Watanzania tumeamka.
 
Ndugu zangu wana JF, samahani kwa kusema ukweli.

Dowans tutawalipa mapesa hayo, CCM iko na itaendelea kuwepo madarakani.
Tumepiga kelele za EPA (133Billion Tshs), wezi wanajulikana na ushahidi upo je nini kimefanyika mpaka leo?.
Hamuoni kwamba wezi wa EPA ama wahusika wakuu wa EPA ndiyo wahusika wakuu wa Dowans?. Kama tulishindwa kuwachukulia hatua za kisheria katika suala la EPA 133 billion Tshs tutawezaje kuwachukulia hatua katika suala la dowans la 94 billions Tshs tu?. Mambo haya yanawezekana hapa Tanzania tu.
 
...inauma sana watanzania wenzangu! pamoja na neema yote hii ambayo Mungu ametupa ya kuwaumbua CCM na kutuonyesha ni kwa jinsi walivyo mabaradhuli, bado kuna mingese kama Zomba inaendekeza u-chama (specifically u-CCM)!!! Hakyamungu, ningejua physical adress yako wewe Zomba, ningekutafuta nikufanyizie!!! Mnatuletea man-made poverty kisha unaleta utani kwenye issue sensitive kama hii!!!??? Maku we!!
 
...inauma sana watanzania wenzangu! pamoja na neema yote hii ambayo Mungu ametupa ya kuwaumbua CCM na kutuonyesha ni kwa jinsi walivyo mabaradhuli, bado kuna mingese kama Zomba inaendekeza u-chama (specifically u-CCM)!!! Hakyamungu, ningejua physical adress yako wewe Zomba, ningekutafuta nikufanyizie!!! Mnatuletea man-made poverty kisha unaleta utani kwenye issue sensitive kama hii!!!??? Maku we!!

Njoo Kariakoo, Mtaa wa Livingstone, kati kati ya mtaa wa Mafia na Kariakoo, kuna Baa bubu inaitwa Pajero, opposite yake, utakuta vijana wamekaa (kijiwe) waulize nataka kumuona Mzee Zomba, utanipata. Jitayarishe vizuri lakini, nisije nikakufanyia wewe.

Utani? mimi sina utani, nasema kweli na kweli tupu. Nionyeshe post yangu moja yenye utani kwenye hii issue.

Kama unataka kulijuwa jiji, njoo ntembelee. Anuani zote nimeshakupa hapo.
 
Wakati yote haya yakiendelea Mkuu wa Nchi kakaa kimya kabisa bila kutia neno kitu ambacho kinastaajabisha sana. Kikwete ni bora ujiuzulu tu maana kama kiongozi wa nchi hata siku moja hujafanya maamuzi yaliyoweka mbele maslahi ya Tanzania na Watanzania siku zote umelala kitanda kimoja na mafisadi.
 
Sasa
[*]Kwanini Serikali Inalipa Kipaumbele "Dowans" Wakati Wastaafu Wengi Hawajalipwa Miaka Mingi Sasa na Pia Wizara Nyingi Hakuna Pesa (Elimu na Afya)? Serikali Inatoa Wapi Pesa?
[/LIST]



TEHEHEHEHHEH!!!
Yote tisa, Kumi ni hapa:
Wastaafu wa lililokuwa shirika la EAC wameshalipwa??????? KAMA BADO - KWANINI?????? DOWANS wana umuhimu zaidi kwanini???
 
Ukisikia mawakili pumba ndio hao. Kesi imeamuliwa ICC na mahakama ya hapa ni kusajili maamuzi, wangepinga huko ICC na si hapa, mahakama ya Tanzania haina mamlaka ya kufuta maamuzi ya ICC.

Wanajitafutia umaarufu lakini hawana kesi ya kushinda katika hili. Wangeshinda ingekuwa tu Dowans hawatimiza masharti ya mkataba.

The only way out ni kutangaza kuwa hatuwalipi Dowans na kuwalipa chini ya uvungu. Otherwise ya LONRHO na Nyerere yatajirudia.

Tunaomba uweke wazi taaluma yako kwanza, na sikuwahita wenzako MAWAKILI PUMBA. Maana sisi wengine si wanasheria hivyo kama unasema wasemacho wanaharakati ni pumba twambia ni pumba kivipi? na nini kingefanyika? na je wakili yeyote alikuwa anaruhusiwa kushirika ktk usuluhishi nauliza hivi kwa sababu umeeleza hivi ktk post yako "wangepinga huko ICC na si hapa, mahakama ya Tanzania haina mamlaka ya kufuta maamuzi ya ICC".
Tupapie ufafanuzi wa kisheria kuhusu huu mgogoro, Usisahau kutueleza taaluma yako na kiwango chako cha elimu kama 1degree, 2degree au Phd
 
Genge la Wezi wa Kimataifa....lililopasishwa na serikali yetu............kwenye kamari.....hawa tunawaita ma-high rollers.........waka-bet maximum....Tanzania tukaibuka kichwa kichwa..................daahh inauma sana
 
Pasco said:
ilichofanya (ICC) ni kuidhinisha tuu vipengele vya mkataba ambao walikubali uamuzi wake ni wamwisho, hauna rufaa wala hauhojiwi na mamlaka yoyote!
Kwa waliosoma hukumu wanajua wapi tuliposhikwa! Tafsiri ni kwamba kukataa hukumu ya ICC ni kupoteza wakati; muhimu ni kuikataa Serikali iliyopitisha mkataba na Kampuni hewa!
 
Yaani nin hasira na hii kodi ninayokamuliwa kila mwezi halafu inaishia kulipa matapeli badala ya kuboresha maisha..agrrrr
 
Dk. Mwakyembe alisema ana shauku ya kujua ni kwa namna gani serikali imepoteza kirahisi kesi hiyo, ambayo alisema hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa digrii ya sheria angeweza kuisimamia na kushinda.

Napenda kumsikia Zitto na hoja yake jamaa watakamata mali za Tanzania nje!
 
Kwa ufupi ni kuwa endapo Dowans watalipwa kama ilivyoamuriwa na serikali ya JK; na wakalipwa na ikajulikana wamelipwa fedha hizo basi Sitta na Mwakyembe watapaswa kujiuzulu nafasi zao katika Baraza la Mawaziri mara moja. It is as simple as that.

Wanatakiwa wajiuzulu sasa hivi. Kumbuka Rais mwenyewe na Waziri Mkuu wake katika hotuba zao wamesema waziwazi kuwa malipo kwa Dowans hayakwepeki. Sasa wanafanya nini humo serikalini. Waje huku waungane na wanaharakati wa Femact na JF. Huwezi kuukata mti ulioukalia. Ukitaka kuukata vizuri shuka chini, shika shoka then uushughulikie. Siasa za kimaslahi na kinafika Tanzania zinachosha na kuzesha!
 
Kazi kweli kweli halafu hili la TANESCO pia inabidi liangaliwe maana nimekuwa nikijiuliza hizo hela za kulipa hawa jamaa zitatoka wapi


Unajiuliza pesa zinatoka wapi wakati umepandishiwa bill ya umeme?!! Ni wewe ndio unalipa ndugu yangu, huo ndio ukweli wenyewe.
 
Dr Mwakyembe atueleze yale yaliyofichwa na kamati yake ili kuiepushia aibu serikali!
 
Hakuna kuwalipa hawa watu. Halafu nyie mliopewa dhamana ya WaTZ hivi mnafikiri bado 2ko vipofu kama zamani.? Someni majira ya nyakati na mwache kabisa wizi na ufisadi raia tukichachamaa mtakosa kwa kukimbilia. Mbona hamna kabisa machungu na nchi yenu au nyinyi sio waTz nini.!!
 
Waarabu wametutesa sana , lakini babu zetu waliwatimua , kwanini mwaarabu mmoja rostam aziz anayumbisha serikali????

Kosa la mwakyembe hapa ni kushindwa kumutaja hadharani mapema wakati anamufahamu sasa umefika wakati wa kumwondoa farao
 
Serikali ya jakaya mlisho kikwete imewekewa alama ya x kwa ajili ya kubomolewa , kama anataka abomoe mwenyewe kama alivyo anza kubomoa makamba , lasivyo tingatinga linakuja!!!!
Utawala wa rias jakaya kikwete umefika mwisho!!!
Kikwete ataondolewa madarakani kabla ya laurent wa ivory coast!!!
Mwakyembe na sitta wakijiuzulu ni lazima waende upinzani na kinachofuata ni maandamano makubwa ya kumung'oa kikwete madarakani
 
Wakati wote nilikua nikijiuliza mzee mzima wamembana mbavu sana nini au tayari kakatiwa kitu kidogo? Mpaka dakika hii hewala!! Acha ninywe kwanza chai ndio nirudi mezani kusoma vizuri hii taarifa muhimu.

i was thinking exactly the same, though i kept quite to be VOCAL about Mwakyembe,
nikasema au ndio unaibu waziri kawa kimya, imani ilitaka kunitoka, maana hata CDM
trust him, ila sasa we hope nin YULEYULE Mwakyembe, hajabadilika, thanks God,
anajua TAIFA LAKE linamhitaji sana, BIG UP.
 
Sababu zilizokupelekea kusema Dowans si kampuni halali ni zipi? Haijasijiliwa? Haina wenyewe? Haina bodi? Haijafanya kazi iliokubaliana na Tanesco? Sijakuelewa, naomba fafanuwa.

It is In-human!!
If Nyerere was living, He would not let these happen. He is GONE (RIP Father of Nation). I know we can, every one should start to make changes!!!!!!
 
Back
Top Bottom