Juu ya DOWANS: Mwakyembe ashangaa kutaka kulipa matapeli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Juu ya DOWANS: Mwakyembe ashangaa kutaka kulipa matapeli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 12, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  Tuesday, 11 January 2011

  [​IMG]

  * Ahoji uhalali wa kampuni ya kitapeli kulipwa fidia
  * Wanaharakati kwenda mahakamani kuipinga

  Na Bakari Mnkondo na Furaha Omary

  ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza suala la kampuni ya kufua umeme ya Richmond, Dk. Harrison Mwakyembe, ameibuka na kuhoji uhalali wa kampuni ya Dowans, ambayo ni ya kitapeli kulipwa fidia kwa utapeli wake.

  "Nikiwa mwanasheria ninasubiri kwa hamu maazimio ya Mahakama ya Kimataifa ya Biashara (ICC) yasajiliwe Mahakama Kuu ili kuona maamuzi ya kuilipa Dowans yalifikiwaje nataka kujua msingi wa tapeli kulipwa fidia kwa utapeli wake?" amesema.

  Alitoa maoni yake jana kuhusu sakata la Dowans baada ya kutafutwa na gazeti hili kwa muda mrefu. Hivi karibuni ICC ilifikia uamuzi wa kulitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuilipa kampuni ya Dowans sh. bilioni 97 kutokana na kuvunja mkataba kinyemela. Baada ya uamuzi huo, suala hilo lilifikishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ambaye alitoa ushauri kwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, wa kukubali serikali kuilipa Dowans endapo uamuzi wa ICC utasajiliwa Mahakama Kuu ya Tanzania.

  Kwa kauli hiyo, Dk. Mwakyembe, ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, anaungana na aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, sasa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupinga kampuni ya Dowans kulipwa kiasi hicho cha fedha.

  Akifafanua kuhusu msimamo wake wa kitaalamu, ambao alisisitiza ni tofauti na wa kisiasa, Dk. Mwakyembe alisema ana shauku ya kujua ni kwa namna gani serikali imepoteza kirahisi kesi hiyo, ambayo alisema hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa digrii ya sheria angeweza kuisimamia na kushinda.

  "Upande wa kisiasa sina tatizo wapo wa kulizungumzia, lakini kitaalamu nitalizungumzia kwa kina kwa kuwa nipo kwenye taaluma ya sheria kwa miaka 20 nikiwa mwalimu. Ningependa kujua msingi wa ICC kufanya lililo batili jana kuwa halali leo," alisema.

  Alisema kamati teule ya Bunge ilimaliza kazi kwa kutoa maazimio kadhaa, ambayo hadi sasa hakuna lililofutwa, na moja ya maazimio hayo ni kuiona Richmond ni kampuni hewa, hivyo kupendekeza ifutwe kwenye orodha ya kampuni za Tanzania na Oktoba, 2008 ilifutwa rasmi.

  Dk. Mwakyembe alisema anasubiri kuona ICC ilimuonaje mmiliki wa Dowans Holdings SA, iliyosajiliwa nchini Costa Rica, ambako serikali ya nchi hiyo ilisema haimtambui kwa kuwa hana anuani wala ofisi.

  "Kwenye kamati tulifanya utafiti wa kina na serikali ya Costa Rica ilitueleza mmiliki wa kampuni hiyo hajulikani kwa jina, ofisi, anuani ya posta wala namba za simu," alisema.

  Dk. Mwakyembe aliyewahi kuwa mwalimu wa sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema walichoambulia Costa Rica ni kutajwa jina la Bernal Zamora Arse, anayemiliki kampuni takriban 100 zenye kuishia na SA, lakini hazielezi zipo jengo gani, nyumba ama kumiliki gari au pikipiki.

  Alisema kutokana na ukweli huo, anashangazwa kuona uamuzi wa ICC ulivyofikiwa, na kuhoji fedha hizo zitalipwa kwa nani?. Dk. Mwakyembe alisema anasubiri uamuzi huo usajiliwe ili apate fursa ya kuupitia kwa kina na kuoana hatua za kuchukua kama mwanasheria.

  Wakati huo huo, wanaharakati kupitia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wanakwenda Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kupinga amri ya TANESCO kuilipa Dowans fedha hizo, wakisema haina uhalali wa kulipwa, kwa kuwa ilishafahamika kuwa Richmond iliyoirithi ni kampuni hewa.

  Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, wakili Francis Kimwaga, alitangaza hayo jana mjini Dar es Salaam, alipotoa tamko la wanaharakati kuhusu mtazamo na muitikio wa serikali kuhusu shauri hilo la Dowans. Alisema katika kesi waliyotarajia kuifungua jana, wanapinga kusajiliwa kwa uamuzi wa ICC.

  Alisema kituo hicho na mashirika mengine yanayotetea haki za binadamu, usawa wa jinsia na ukombozi wa wanawake kimapinduzi (FemAct), wameshitushwa na kusikitishwa na mtazamo na muitikio wa serikali kuhusu shauri la Dowans.

  "LHRC itafungua shauri leo (jana) Mahakama Kuu kupinga uhalali wa tuzo iliyotolewa kwa Dowans na ICC na isisajiliwe kwa kuwa mikataba ya awali ilipatikana kwa rushwa na kukiuka maslahi ya umma," alisema.

  Kwa mujibu wa Kiwanga, mwenendo wa Wizara ya Nishati na Madini kuhusu suala hilo pia unatia shaka, hususan malipo kwa Dowans.

  Alisema katika suala hilo kuna mambo ya kujiuliza, yakiwemo ya kuendeshwa kwa usiri kwa shauri hilo katika Mahakama ya ICC bila wananchi kuelezwa kilichokuwa kikiendelea tofauti na kesi ya Bi-Water dhidi ya serikali, ambapo walialikwa kama marafiki wa mahakama.

  ìIkiwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kwa taarifa ya kamati teule ya Bunge iliyoundwa Novemba 13, 2007 kikao cha 11, mkutano wa tisa), ilithibitisha Richmond ni kampuni hewa, inawezekanaje kuwa na mkataba wa kurithisha mali zake kwa Dowans?.

  "Uhalali wa kisheria wa miliki ya Dowans kwa mali za Richmond haupo, kwa nini serikali haikutaifisha mali za Richmond tangu awali?" alihoji Kiwanga.

  Aliyataja mambo mengine ya kujiuliza ni ikiwa Dowans haikurithi kwa uhalali mali ya Richmond, inawezekanaje kuwa mdai halali dhidi ya serikali kuhusu mali iliyopatikana kutokana na uhalifu, na serikali kuharakisha kuilipa Dowans kuhusu mali iliyopatikana kwa uhalifu.

  Kiwanga alihoji sababu za TANESCO kulazimishwa kuilipa Dowans wakati tangu awali ilishakataa kuhuishwa mkataba haramu wa Richmond kwa Dowans.

  Wanaharakati hao wameitaka serikali na maofisa wa umma wanaohusika na suala hilo kuzingatia maelekezo ya Katiba na waheshimu uamuzi wa Bunge kuwa, Richmond ni kampuni hewa, hivyo kuendelea kulazimisha Dowans ni kukiuka utawala wa sheria.

  Wameitaka Wizara ya Nishati na Madini kuacha kuwabebesha Watanzania mzigo wa kulipa gharama hizo kutokana na kodi wanazolipa, kwa kuwa malipo hayo yanatokana na uzembe, ubadhirifu na ufisadi.

  Kwa upande wake, Dk. Sengondo Mvungi, alisema wanakwenda mahakamani ili kupata majibu ya mambo mbalimbali, huku akisema mahakama haipaswi kusajili matapeli, ila isimame iungane na wanaharakati hao na kuwataka Watanzania kujitokeza kupinga hukumu hiyo.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Ananilea Nkya, alisema inapaswa picha za wamiliki wa Dowans ziwekwe hadharani ili Watanzania wawajue wanaolipwa fedha hizo, badala ya kutajwa majina.

  Chanzo: Uhuru
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  Utamu wa kashfa ya DOWNS sasa umeiva.......................usikose hii filamu ya bwererere
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wakati wote nilikua nikijiuliza mzee mzima wamembana mbavu sana nini au tayari kakatiwa kitu kidogo? Mpaka dakika hii hewala!! Acha ninywe kwanza chai ndio nirudi mezani kusoma vizuri hii taarifa muhimu.
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Afadhali,nawatakia kila la kheri kwa hli,kupnga 2zo hyo
   
 5. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kazi hipo...ha ha ha...atalia mtu hapa!
   
 6. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,871
  Likes Received: 11,982
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu alisema Dowans ni kaburi la JK.
   
 7. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Good
   
 8. Tekelinalokujia

  Tekelinalokujia JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Masikini Ngeleja, masikini mawaziri wa JK, full kuparanganyika. And the drama continues.
   
 9. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Hapa kazi ipo wala sio siri, hapa nimepapenda zaidi maana huyu jamaa anajua kila kitu :
  Alisema kamati teule ya Bunge ilimaliza kazi kwa kutoa maazimio kadhaa, ambayo hadi sasa hakuna lililofutwa, na moja ya maazimio hayo ni kuiona Richmond ni kampuni hewa, hivyo kupendekeza ifutwe kwenye orodha ya kampuni za Tanzania na Oktoba, 2008 ilifutwa rasmi.
  alisema walichoambulia Costa Rica ni kutajwa jina la Bernal Zamora Arse, anayemiliki kampuni takriban 100 zenye kuishia na SA, lakini hazielezi zipo jengo gani, nyumba ama kumiliki gari au pikipiki.
  Alisema kutokana na ukweli huo, anashangazwa kuona uamuzi wa ICC ulivyofikiwa, na kuhoji fedha hizo zitalipwa kwa nani?.
   
 10. n

  niweze JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasa Tutamwona Real Owner wa Dowans Holding SA Ajitokeze Kama Kweli Yeye ni Mwanamme. Watanzania Hatutoi Pesa kwa Malipo Mpaka Tujue Maswala Yafuatayo:
  1. Aliopigia Debe au Lobby On Behalf of Dowans Holding Kuingia Mkataba na Tanesco ni Nani?
  2. Dowans Ilisajiliwa Vipi au Tender Process Ilifanikishwa Vipi?
  3. Aliesaini Mkataba na Kukubali Tanesco wa Saini na Dowans ni Nani? (Najua Jibu Rostam, Lowasa na JK Hawakosi)
  4. Alichukua Uamuzi wa Kwenda ICC Badala ya Kuchallange Validity ya Mkataba wa Tanesco na Dowans ni Nani (Najua Jibu JK na Rostam wapo hapa)
  5. Utaratibu Gani Ulitumika Kumpata Arbitrator wa Kuwakalisha Chini Tanesco na Dowans?
  6. Sababu Gani JK Kakaa Kimya ICC Ilipotoa Maamuzi?
  7. Kwanini Baraza la Mawaziri Alihusishwi Kabla ya Maamuzi ya Mwisho? (Hii Process ya Malipo Inafanyiwa Ikulu)
  8. Kwanini Wizara ya Nishati na Madini na Tanesco Wana Harakisha Kuwalipa Dowans Wakati Bei ya Umeme Imepanda na Pia Hakuna Umeme Wakutosha?
  9. Kwanini Serikali Inalipa Kipaumbele "Dowans" Wakati Wastaafu Wengi Hawajalipwa Miaka Mingi Sasa na Pia Wizara Nyingi Hakuna Pesa (Elimu na Afya)? Serikali Inatoa Wapi Pesa?
   
 11. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Huyu ndio Dr. (PhD.) sasa, mtu ambaye anaweza kutofautisha siasa na professionalism yake. Nakusifu sana kwa hilo Dr. (PhD)
   
 12. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,871
  Likes Received: 11,982
  Trophy Points: 280
  Richmond ilikwenda na mtu Dowans nayo lazima iende na mtu ebo tena hii ndiyo miezi yenyewe, ukipita pale Vijana Social Hall Ilala kuna kikundi cha kina mama kinaitwa 'Tumechoka kuonewa Group' wangekuwa wanaruhusu wanaume ningejiunga nacho.
   
 13. Averos

  Averos JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 648
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  * Ahoji uhalali wa kampuni ya kitapeli kulipwa fidia

  * Wanaharakati kwenda mahakamani kuipinga

  Na Bakari Mnkondo na Furaha Omary

  ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza suala la kampuni ya kufua umeme ya Richmond, Dk. Harrison Mwakyembe, ameibuka na kuhoji uhalali wa kampuni ya Dowans, ambayo ni ya kitapeli kulipwa fidia kwa utapeli wake. ìNikiwa mwanasheria ninasubiri kwa hamu maazimio ya Mahakama ya Kimataifa ya Biashara (ICC) yasajiliwe Mahakama Kuu ili kuona maamuzi ya kuilipa Dowans yalifikiwajeÖ nataka kujua msingi wa tapeli kulipwa fidia kwa utapeli wake?î amesema. Alitoa maoni yake jana kuhusu sakata la Dowans baada ya kutafutwa na gazeti hili kwa muda mrefu. Hivi karibuni ICC ilifikia uamuzi wa kulitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuilipa kampuni ya Dowans sh. bilioni 97 kutokana na kuvunja mkataba kinyemela. Baada ya uamuzi huo, suala hilo lilifikishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ambaye alitoa ushauri kwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, wa kukubali serikali kuilipa Dowans endapo uamuzi wa ICC utasajiliwa Mahakama Kuu ya Tanzania.

  Kwa kauli hiyo, Dk. Mwakyembe, ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, anaungana na aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, sasa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupinga kampuni ya Dowans kulipwa kiasi hicho cha fedha.

  Akifafanua kuhusu msimamo wake wa kitaalamu, ambao alisisitiza ni tofauti na wa kisiasa, Dk. Mwakyembe alisema ana shauku ya kujua ni kwa namna gani serikali imepoteza kirahisi kesi hiyo, ambayo alisema hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa digrii ya sheria angeweza kuisimamia na kushinda.

  ìUpande wa kisiasa sina tatizo wapo wa kulizungumzia, lakini kitaalamu nitalizungumzia kwa kina kwa kuwa nipo kwenye taaluma ya sheria kwa miaka 20 nikiwa mwalimu. Ningependa kujua msingi wa ICC kufanya lililo batili jana kuwa halali leo,î alisema.

  Alisema kamati teule ya Bunge ilimaliza kazi kwa kutoa maazimio kadhaa, ambayo hadi sasa hakuna lililofutwa, na moja ya maazimio hayo ni kuiona Richmond ni kampuni hewa, hivyo kupendekeza ifutwe kwenye orodha ya kampuni za Tanzania na Oktoba, 2008 ilifutwa rasmi.

  Dk. Mwakyembe alisema anasubiri kuona ICC ilimuonaje mmiliki wa Dowans Holdings SA, iliyosajiliwa nchini Costa Rica, ambako serikali ya nchi hiyo ilisema haimtambui kwa kuwa hana anuani wala ofisi.

  ìKwenye kamati tulifanya utafiti wa kina na serikali ya Costa Rica ilitueleza mmiliki wa kampuni hiyo hajulikani kwa jina, ofisi, anuani ya posta wala namba za simu,î alisema.

  Dk. Mwakyembe aliyewahi kuwa mwalimu wa sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema walichoambulia Costa Rica ni kutajwa jina la Bernal Zamora Arse, anayemiliki kampuni takriban 100 zenye kuishia na SA, lakini hazielezi zipo jengo gani, nyumba ama kumiliki gari au pikipiki.

  Alisema kutokana na ukweli huo, anashangazwa kuona uamuzi wa ICC ulivyofikiwa, na kuhoji fedha hizo zitalipwa kwa nani?. Dk. Mwakyembe alisema anasubiri uamuzi huo usajiliwe ili apate fursa ya kuupitia kwa kina na kuoana hatua za kuchukua kama mwanasheria.

  Wakati huo huo, wanaharakati kupitia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wanakwenda Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kupinga amri ya TANESCO kuilipa Dowans fedha hizo, wakisema haina uhalali wa kulipwa, kwa kuwa ilishafahamika kuwa Richmond iliyoirithi ni kampuni hewa.

  Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, wakili Francis Kimwaga, alitangaza hayo jana mjini Dar es Salaam, alipotoa tamko la wanaharakati kuhusu mtazamo na muitikio wa serikali kuhusu shauri hilo la Dowans. Alisema katika kesi waliyotarajia kuifungua jana, wanapinga kusajiliwa kwa uamuzi wa ICC.

  Alisema kituo hicho na mashirika mengine yanayotetea haki za binadamu, usawa wa jinsia na ukombozi wa wanawake kimapinduzi (FemAct), wameshitushwa na kusikitishwa na mtazamo na muitikio wa serikali kuhusu shauri la Dowans.

  ìLHRC itafungua shauri leo (jana) Mahakama Kuu kupinga uhalali wa tuzo iliyotolewa kwa Dowans na ICC na isisajiliwe kwa kuwa mikataba ya awali ilipatikana kwa rushwa na kukiuka maslahi ya umma,î alisema.

  Kwa mujibu wa Kiwanga, mwenendo wa Wizara ya Nishati na Madini kuhusu suala hilo pia unatia shaka, hususan malipo kwa Dowans.

  Alisema katika suala hilo kuna mambo ya kujiuliza, yakiwemo ya kuendeshwa kwa usiri kwa shauri hilo katika Mahakama ya ICC bila wananchi kuelezwa kilichokuwa kikiendelea tofauti na kesi ya Bi-Water dhidi ya serikali, ambapo walialikwa kama marafiki wa mahakama.

  ìIkiwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kwa taarifa ya kamati teule ya Bunge iliyoundwa Novemba 13, 2007 kikao cha 11, mkutano wa tisa), ilithibitisha Richmond ni kampuni hewa, inawezekanaje kuwa na mkataba wa kurithisha mali zake kwa Dowans?.

  ìUhalali wa kisheria wa miliki ya Dowans kwa mali za Richmond haupo, kwa nini serikali haikutaifisha mali za Richmond tangu awali?î alihoji Kiwanga.

  Aliyataja mambo mengine ya kujiuliza ni ikiwa Dowans haikurithi kwa uhalali mali ya Richmond, inawezekanaje kuwa mdai halali dhidi ya serikali kuhusu mali iliyopatikana kutokana na uhalifu, na serikali kuharakisha kuilipa Dowans kuhusu mali iliyopatikana kwa uhalifu.

  Kiwanga alihoji sababu za TANESCO kulazimishwa kuilipa Dowans wakati tangu awali ilishakataa kuhuishwa mkataba haramu wa Richmond kwa Dowans.

  Wanaharakati hao wameitaka serikali na maofisa wa umma wanaohusika na suala hilo kuzingatia maelekezo ya Katiba na waheshimu uamuzi wa Bunge kuwa, Richmond ni kampuni hewa, hivyo kuendelea kulazimisha Dowans ni kukiuka utawala wa sheria.

  Wameitaka Wizara ya Nishati na Madini kuacha kuwabebesha Watanzania mzigo wa kulipa gharama hizo kutokana na kodi wanazolipa, kwa kuwa malipo hayo yanatokana na uzembe, ubadhirifu na ufisadi.

  Kwa upande wake, Dk. Sengondo Mvungi, alisema wanakwenda mahakamani ili kupata majibu ya mambo mbalimbali, huku akisema mahakama haipaswi kusajili matapeli, ila isimame iungane na wanaharakati hao na kuwataka Watanzania kujitokeza kupinga hukumu hiyo.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Ananilea Nkya, alisema inapaswa picha za wamiliki wa Dowans ziwekwe hadharani ili Watanzania wawajue wanaolipwa fedha hizo, badala ya kutajwa majina.

  Chanzo: Uhuru
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mawaziri tunaomba mzungumze kwa UJASIRI WOTE huko ndani ya baraza lenu na kuitupilia mbali mambo ya malipo ya Maruani Dowansi na ikibidi MJIUZULU TU kura tunazo hapa nje tutawarejesheni bungeni maramoja bila gharama yoyote alimradi ukatutete maslahi ya taifa letu tuipendayo.

  Chonde katika hili mkawakabili vilivyo MAFISADI wasipate pakupita na hata kwa malipo mengine yajayo yasiokua na maslahi ya nchi yetu mbele. Msiwaachie hii mitapeli ya Dowans ije ikatupore kodi zetu kiduchu ambazo hata Chanjo kwa watoto haitoshi.

  Kwanza wana jf nimepata tetesi mahala kwamba serikali haina stock ya chanjo ya watoto wala hawajaagiza na kwamba chache zilizopo zimebakisha wiki chache tu kuharibika.

  Yeyote anayeweza kuopoa vya jikoni zaidi huko wizara ya afya juu ya madai nyeti haya yanayogusa moja kwa moja UHAI WA TAIFA LA KESHO.
   
 15. O

  Ogah JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Oh oh ....wait a minute Dr............chagua moja................. Siasa au Kushika Chaki............!!
   
 16. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #16
  Jan 12, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Patamu hapa, sasa mwanaume na asimame, Umefika wakati wa mwanasheria mkuu ajiuzulu maana hana faida kwa watanzania!
  Kunguru yule kwa ufinyu wa akili yake alishapitisha walipwe!
   
 17. m

  moma2k JF-Expert Member

  #17
  Jan 12, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 953
  Likes Received: 984
  Trophy Points: 180
  Kwanini Serikali inang'ang'ania Dowans walipwe kinyemela na haraka? Udharula huu unatoka wapi? Je JK atatoa tamko baada ya kuilipa Dowans au kabla?
  NOTE WELL: wananchi tuamke, muda wa kuibiwa imepita!
   
 18. k

  kijiichake JF-Expert Member

  #18
  Jan 12, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hapatoshi! Jei kei soma alama za nyakati mambo yamewiva.
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ukisikia mawakili pumba ndio hao. Kesi imeamuliwa ICC na mahakama ya hapa ni kusajili maamuzi, wangepinga huko ICC na si hapa, mahakama ya Tanzania haina mamlaka ya kufuta maamuzi ya ICC.

  Wanajitafutia umaarufu lakini hawana kesi ya kushinda katika hili. Wangeshinda ingekuwa tu Dowans hawatimiza masharti ya mkataba.

  The only way out ni kutangaza kuwa hatuwalipi Dowans na kuwalipa chini ya uvungu. Otherwise ya LONRHO na Nyerere yatajirudia.
   
 20. n

  niweze JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tukisoma Taratibu Zenyewe za ICC Tunaona Kwamba Serikali ya JK na CCM Wamevunja Sheria za Tanzania na Kudharau Mahakama Kuu ya Tanzania. Tusome Hapa Chini Kutoka Website ya ICC:

  Arbitration
  Often the parties are from markedly different national, cultural and legal backgrounds.
  They want to avoid litigation because they fear bias by national courts, are unfamiliar with national court procedures and want to be spared damaging publicity. ICC arbitration is an attractive alternative because it is international and confidential. Usually, it is less time-consuming and less expensive than litigation.

  he Court organizes and supervises your arbitration and helps in overcoming obstacles. It does not itself resolve disputes, a task that is carried out by independent arbitrators. The Court makes every effort to ensure that the award is enforceable in national courts if need be, although in practice the parties usually comply

  Under ICC Rules, the parties can choose the arbitrators, the place of arbitration and which rules of law should apply. They can even indicate a target date for completing the arbitration and estimate approximate costs in advance in full confidence that the Court will exercise control over the choice of the arbitrators, over the procedure, over the costs and over the award

  Ukisoma Yote Haya Tutaona Jinsi Gani JK na Rostam Wameuchezea Ngoma Watanzania. Wanafikiri Hatujui Jinsi ya Kuresearch na Kupata Information Sahii. Huu Ndio Mwisho wa CCM na JK...
   
Loading...