Justice For Mnyika

mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,223
4,681
Wadau wote wa demokrasia na maendeleo tuungane kwa pamoja kupigania haki ya mpambanaji wetu John Mnyika.

Mnyika amekuwa kimya sana tangia ujio wa Lowassa na team yake ndani ya UKAWA. Inasemekana Mnyika akufurahishwa na mapokezi ya Lowassa na team yake kwenye chama na alifanya busara ya kukaa kimya.

Mnyika ni mpambanaji wa ufisadi na amekuwa akiunga mkono mtu yoyote anayewasulubu mafisadi.


Ila kinachosikitisha ni jitihada zinazofanywa kumpoteza kwenye ulingo wa kisiasa na kundi hovu.

Kundi ilo limefanikiwa kumpora nafasi aliyoandaliwa kumrithi Dr Slaa na sasa linaendelea kumzima kwa njia "spiritual" na kimafia.

Wadau tupaze sauti zetu kumlilia Mnyika maana taifa linapoteza hazina muhimu sana sababu ya tamaa za watu za pesa na madaraka.

Tulimpoteza Chacha Wangwe tusikubari kumpoteza Mnyika.

#BringOurMnyikaBack
 
Mnyika anajiandaa kujiunga na CCM...... Maana Chadema siku hizi wamekumbatia mafisadi....
 
Nilikuwa mfuasi mkubwa wa staili ya siasa za John Mnyika mpaka nilithubutu kumtabiria kwamba kama itatokea Rais akatoka nje ya CCM basi angelikuwa Mnyika. Lakini ghafla Chadema ilipompokea Lowassa, John Mnyika naye alibadilisha staili ya siasa zake, akaja na staili mpya ya Hero to Zero ndani ya Chadema.
 
Nilikuwa mfuasi mkubwa wa staili ya siasa za John Mnyika mpaka nilithubutu kumtabiria kwamba kama ni Rais itatokea Rais akatoka nje ya CCM basi angelikuwa Mnyika. Lakini ghafla Chadema ilipompokea Lowassa, John Mnyika naye alibadilisha staili ya siasa zake, akaja na staili mpya ya Hero to Zero ndani ya Chadema.
Mkuu Mnyika apendezwi na namna mambo yanavyoenda kwenye chama. Siku akitoa ya moyoni mtamuita msaliti maana Mnyika awezi uongo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom