Ni uchaguzi wa waadilifu dhidi ya genge la wahuni - Lowassa anawakilisha genge la wasaka madaraka

Kubwajinga

JF-Expert Member
Jan 23, 2008
2,194
297
Ni uchaguzi wa waadilifu dhidi ya genge la wahuni

Lowassa anawakilisha genge la wasaka madaraka kwa manufaa binafsi

  1. KWA muda mrefu kikundi cha wahuni kilijaribu na kufanikiwa kupoka madaraka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Watu hawa walitaka kujijengea "syndicate" ya kuongoza nchi, humo walikuwamo watu kadhaa na hasa wafanyabiashara akiwamo Edward Lowassa na yeye ndiye aliyekuwa msanifu wa genge hilo. Baada ya hapo, genge hili lilijipenyeza kwenye maeneo yote nyeti ya nchi yetu.

  2. Mwaka huu wana CCM tumekataa upumbavu huu wa kudhani urais na uongozi unaweza kununuliwa kama nyanya. Tumekataa na tumehakikisha katika ile "syndicate" au genge la wahuni hakuna kati yao ambaye anaiona Ikulu kwa tiketi ya CCM. Imewauma sana, huyu bosi ndio kaenda Ukawa na wako waliobaki CCM, tutashughulika nao kimkakati, lakini kwanza ni lazima tupate Rais mwadilifu ambaye atatusaidia kazi ya pili ya kusafisha ufisadi. Kazi ya kwanza imekuwa kuwanyima dhamana ya urais kupitia CCM.

  3. Hapa CCM wanapaswa kwa kweli kujitoa kimasomaso kwa kuuvunja mtandao na kuwanyima tiketi ya urais kupitia chama hicho, kwa hakika haukuwa uamuzi rahisi. Genge sasa limehamishia mapambano kutoka kambi ya upinzani. Utagundua hoja ya ufisadi ilishamiri sana na ndio maana kipindi fulani Ukawa waliunga mkono kazi yetu ya Katiba Mpya ambayo lengo lake lilikuwa kuja kuua "syndicate" au genge la wahuni, leo Ukawa hawana tena uhalali (legitimacy) wa kukemea ufisadi maana ufisadi umetamalaki kati na juu yao.
​
Hebu tafakari mtu kama ndugu yangu na kaka yangu Said Kubenea kwa kazi yote aliyofanya miaka nenda rudi ya kupinga mafisadi na ufisadi, mpaka akashambuliwa, juzi alijisikiaje pale Kawe (Dar es Salaam) aliponyoshwa mkono juu na Edward Lowassa kutambulishwa kama mgombea ubunge? Dhamira yake ilimweleza nini? Na Lowassa hakusita kumpiga kijembe kwamba huyu alikuwa machachari sana kwenye media sasa apunguze, hivi Kubenea amejiuliza Lowassa alimaanisha apunguze nini na kwa faida ya nani?

Mimi mpaka vituo viwili vya televisheni kubwa nchini vimekataa nisikaribishwe kwenda kwenye vipindi kwa maelekezo ya wamiliki. Je, kukataliwa kwangu ni kwa faida ya nani? Mbona kama ni siasa kila siku kwenye TV hizo wadau wa Ukawa wanajimwaga vilivyo? Je, mimi tatizo langu ni nini? Wengine walifurahia TCRA kutoa tamko la kukataza watu kwenda kwenye vipindi vya moja kwa moja, na wengi walisema mitandaoni wamenikomesha mimi, hivi mimi nikikomeshwa ni kwa faida ya nani?

TCRA walilazimisha kwamba ili uruhusiwe kushiriki kwenye vipindi vya moja kwa moja ni lazima uwe mwakilishi wa vyama vya siasa. Mimi nikasema kwa hakika ningemwambia Kinana, Katibu Mkuu wa CCM angenipa barua ili niendelee kushiriki. Lakini nikasema hivi wanaoruhusiwa kushiriki ni wanasiasa peke yake? Je, uchaguzi ni haki uhodhiwe na wanasiasa pekee? Nikaendelea kujiuliza hivi Uchaguzi Mkuu wanaotakiwa kujadiliana zaidi ni wananchi wanaochagua ili kutoa dhamana au wale wanaoomba kuchaguliwa ili kupewa dhamana? Nikasema mbona Katiba inasema kuna uhuru wa kuweka mawazo hadharani, je haki ya kutoa mawazo hayo ina ukomo wakati wa uchaguzi?

Nikafunga safari kwenda TCRA nikawauliza maswali hayo na namshukuru Mungu aliwapa busara kubwa na baadaye walitoa tamko kubatilisha katazo lao la awali. Lakini nikajiuliza zaidi kwa nini hata wale wadau wa asasi za kiraia hawakuoneshwa kukasirishwa na kitendo kile cha TCRA? Nikasema hata watu wote wakisimama mimi nitaendelea kudai haki na kweli katika nchi yangu.

Leo siwezi kwenda kwenye TV mbili kubwa na wamiliki wameweka msimamo, kwa nini? Wale wanaofurahia mimi kukataliwa je, wanapata faida gani? Mbona mimi nikionana na vijana na wadogo zangu ambao wako katika vyama vya upinzani nawapa moyo na kuwaambia watende sawa sawa na dhamira zao njema na kwamba walitizame taifa kwanza? Najiuliza je, tatizo langu ni nini? Au sijitambui (naïve)?

Nitasema kweli daima na fitina kwangu mwiko na nitatumia elimu yangu kwa manufaa ya wananchi wa taifa langu, mimi kama Mtanzania maneno hayo ni msingi. Kwa nini leo baadhi ya watu wamenigeuka, watu ambao walifurahia nilipowaambia pale Ubungo Plaza na pale Mlimani City kwamba maslahi binafsi yana hatarisha mustakabali wa taifa letu. Nilikwenda mbali na kuwataja watu hao na Watanzania baadhi na wengi wakanifurahia sana na kunipongeza.

Mbona leo naendelea kuwasema watu wale wale na baadhi ya Watanzania wananiona nimegeuka? Kwa nini waliniamini kipindi kile na wakijua mimi ni CCM na nilikuwa nawasema baadhi ya wana CCM na leo nikiwa bado CCM naendelea na kazi ile ile ya kuwasema watu ambao wanataka kutununua ili waendeleze genge la kihuni mbona watu wanasema mimi ni kigeugeu? Ina maana Watanzania wamepigwa upofu, ina maana wasomi wetu wamepigwa upofu, ina maana wazee wetu ambao wameuishi umri wamepigwa upofu, na kama tumepigwa upofu wako wapi viongozi wetu wa dini, je mmetuombea? Naendelea kutafakari.

Siku moja nilikaa na viongozi wawili wa CCM, mmoja akasema nadhani mchakato wa Katiba ni lazima kabla ya kura ya maoni tujenge muafaka na kufanya maridhiano ili kila sauti ya Mtanzania isikilizwe. Kiongozi mwenzake mdogo kidogo kwa cheo akabisha sana na akasema ni lazima twende kwenye kura ya maoni kwa sababu tendo la Katiba kwa lilipofika ni kama maji yanayomwagwa kutoka katika bilauri kwamba ni lazima yafike chini.

Nikamtazama na kumkazia macho na nikamweleza wacha na mimi nizungumze kama mwana CCM. Nikawaomba niwaeleze historia ndogo ya namna nipo nilipo. Nikasema nianzie kwenye Katiba, nikawaambia unajua mimi nilikuja Tume ya Katiba nikiwa simfahamu mtu yeyote isipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano? Nikawaeleza mimi sikumfahamu mzee Warioba, Jaji Ramadhani, mzee Butiku, Dk. Salim wala Profesa Kabudi na wengineo, sikumfahamu hata mmoja.

Nilikuwa namfahamu Rais Kikwete tu. Alipotupa kazi na akatuagiza tuwasikilize Watanzania na watakachosema ndicho ambacho tukiandike, tulifanya hivyo kwa unyenyekevu mkubwa kwa Watanzania.

Hata pale ambapo Rais alionekana kutoka na msimamo tofauti na wetu nilibaki kuwaambia Watanzania kwamba Tanzania njema itajengwa na Watanzania wenyewe. Aidha niliendelea kusema kundi la watu ambao wanajulikana liliteka na kushinikiza CCM kutoka na msimamo ule. Hatukuishia pale tuliokuwa wajumbe wa Tume ya Katiba tulifanya mahojiano kwa kuzungumza na wadau mbalimbali, wabunge, viongozi wastaafu, watu mashuhuri ili kuelewa tatizo lilikuwa wapi.

Mahojiano haya ya chini chini yalinipa fursa ya kuonana na wabunge wengi wa CCM na wa upinzani na wote walikiri kwamba "Bwana Mkubwa amekataa" na tulipozidi kuhoji hoji tulikuja kukutana na wapambe wake ambao walisema "tatizo lenu mmedhoofisha urais na kwamba Kikwete anataka kuondoka ameweka masharti na kanuni ngumu za uongozi hilo haliwezekani" wakaendelea kusema "yeye (Kikwete) aende na sisi tubaki na madaraka yale yale au zaidi na tuwe na mamlaka kama aliyonayo sasa katika nchi".

Wapambe hawa tulizungumza nao kwa maana ya kuwapa elimu ya Rasimu ya Warioba na wakawa wanatuuliza "kwa hiyo ninyi (Tume ya Katiba) mnashauri ‘Mkubwa' achukue urais wa Tanzania au urais wa Tanganyika?" Tukasema achukue ya Muungano, wakasema "je itahusisha madini, gesi na ardhi"? Tukasema hapana, wakaendelea kuuliza "je, akichukua ya Tanganyika atakuwa na uwezo wa kusafiri nje ya nchi kama Rais Kikwete na kupigiwa mizinga 21"? Tukasema hapana, mmoja wao akasema; "anhaaa hapo ndio mnapokosea, sisi tunataka zote za Tanganyika na Muungano ziwe pamoja", kwa kusema hivyo walikuwa wanamaanisha serikali mbili.

Hatukuchoka, tukafanya utaratibu na tukaenda kumuona "Bwana Mkubwa" yaani Edward Lowassa, tulikutana ofisini kwake Mikocheni (Dar es Salaam). Ili kuweka uwazi katika mkutano ule tulijumuisha pia wawakilishi watatu wa asasi za kiraia na makamishna wawili, mimi nikiwa mmojawapo, tulikuwa na kikao ambacho hakikupungua saa mbili.

Ni katika kikao kile nilithibitisha kwamba aliyebuni mkakati wa kuikataa Rasimu ya Warioba kwa CCM alikuwa Edward Lowassa, tena akaonesha kufurahishwa na Rais Kikwete kama Mwenyekiti wa Chama kuzomewa katika vikao vya Chama na hatimaye Rasimu aliyoipeleka katika Chama kukataliwa. Nilijiuliza sana mimi kama kiongozi kijana, tafsiri yake ni nini? Huyu ni mwana CCM na anafurahia Mwenyekiti wake kudhihakiwa na kutupiwa Rasimu yake katika kikao? Leo najiuliza kama alikuwa na dhamira ya kuikubali rasimu ya Warioba kama anavyojinasibu sasa katika majukwaa akiomba kura kupitia Ukawa kwa nini alikaa kimya wakati Mwenyekiti wake akidhihakiwa?

Kibaya zaidi Lowassa anapoomba kura na kutumia hoja ya Katiba amekuwa akitumia neno "Mamlaka Kamili" ili kuwafurahisha baadhi ya Watanzania waishio Zanzibar. Mimi nilikuwa Tume na huko tulikubaliana Mamlaka kamili kwa Zanzibar na Tanganyika ni kuvunja Muungano.

Huyu Lowassa nilipoongea naye alisema Zanzibar ipewe kila kitu isipokuwa Ulinzi tu, tukamweleza kufanya hivyo ni kuvunja Muungano, hakuonesha kuelewa. Hata tulipomwambia unajua kwamba kwa madaraka yako na wakati unasimamia ujenzi wa shule za kata, hukupata kujenga hata shule moja Zanzibar, akaonesha kushangaa na kutokumbuka ilikuwaje kipindi hicho.

Nikawaeleza iliyokuwa Tume ya Katiba iliwahi kumwita hata mzee Kingunge aje tujadiliane kuhusu Rasimu ya Warioba na alipokuja aliwatukana wajumbe wa Tume pamoja wageni wengine waalikwa akiwemo Profesa Abdul Sherrif kutoka Zanzibar, nilipoona anamuunga mkono Lowassa sasa namwelewa na ndio maana katika mkutano wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere nilidiriki kusema Mungu akinipa umri mrefu na kufikia uzee namwomba Mungu nisiwe kama wazee wa namna hii.
Nasema tena, kama mzee Kingunge na Lowassa walikataa katukatu maoni ya wananchi ambayo sio tu yalikuwa yanaleta mabadiliko bali mageuzi ya kimfumo, je haya mabadiliko wanayoyahubiri majukwaani msingi wake ni upi? Kwa nini tunatumia wananchi wetu kukosa taarifa kuwahadaa?

Nikamwambia yule kiongozi mdogo, unadhani ni kazi rahisi mimi kama kijana mdogo kusimama kidete kutetea maoni ya wananchi? Nilijua aliyekuwa na maslahi katika kutupilia maoni ya wananchi hakuwa Kikwete bali Edward Lowassa ambaye amekuwa akiutafuta urais wa kifalme. Kuthibitisha hilo nilimtamka kwa jina mara kadhaa Edward Lowassa kwamba hafai kuwa Rais wa Tanzania.

Na kwangu mimi nilikuwa najiuliza hata kupitia CCM ambako mimi ni mwanachama, iweje mtu ambaye anakosa kuheshimu Watanzania wanapotoa maoni yao ya Katiba akawa ni mtu ambaye atasimama ili wampe dhamana ya kuwa Rais wao. Mimi nilimkataa tangu CCM na nilipoona CCM kama vile wanachelewa, mimi (Polepole), mzee Butiku na mzee Warioba tulifanya mdahalo na tukaweka msimamo kama Lowassa atapewa tiketi ya kugombea urais kupitia CCM basi sisi watatu tusingejitoa bali tungepiga kampeni ya kusema CCM isichaguliwe.

Nikaendelea kumwambia hili la Katiba mbaya wake tunamjua katika chama na alijaribu kuhonga watu mara kadhaa ili kutimiza lengo lake. Ni lazima tujenge muafaka wa kitaifa kwanza, ili tusikilize na kujumuisha sauti za Watanzania wengi, ili Katiba mpya ibebe Utanzania wetu na sio kundi moja.

Namshukuru Mungu, kiongozi yule mdogo ni muelewa haraka akasema muafaka ni kitu muhimu, hilo linawezekana na ni kwa maslahi ya Watanzania wote sema tu kipindi kile kiligubikwa na ushindani wa kisiasa, ila sasa ni muhimu tukaja pamoja kama taifa na kabla ya Kura ya Maoni hili liwekwe sawa kwanza. (Mwisho wa kunukuu kikao changu na viongozi wa CCM).

Uhalisia huu ndio umefanya mzee Joseph Sinde Warioba kupiga kampeni ya Chama Cha Mapinduzi na kumuunga mkono Dk. John Magufuli. Ila kitu kimoja napenda kuwaeleza Watanzania kuna maadui ndani ya CCM na nje ya CCM na hasa hasa wale ambao wako chini ya "syndicate" au lile GENGE la WAHUNI ambalo linafanya kila jitihada ili mgombea wa CCM asiye na makundi na asiye na msalie mtume na wezi, wabadhirifu na mafisadi asifanikiwe. Maadui hawa wako radhi mwana mtandao mwenzao (aliyeondoka CCM na kwenda Ukawa) apewe dhamana ya urais wa nchi yetu ili waendelee kutunyonya kwa maslahi yao, kumbuka mtu mwenye tuhuma za ufisadi hawezi kushughulika na wenzake wengi wenye tuhuma nzito nzito za ufisadi.

Ikumbukwe Ukawa huu sio Ukawa ule ambao mimi na mzee Butiku na mzee Warioba tulifanya nao kazi pamoja, si hawa. Hawa Ukawa wa sasa ni watu wenye uchu wa ajabu wa madaraka na kwamba wako tayari kumtumia mtu mwenye nasaba zote na ufisadi ili awafikishe Ikulu. Sikiliza kwa umakini hata kauli zao ni za vitisho, wanatisha watu, wanalazimisha ushindi na tayari wameshasema kama uchaguzi ukiwa huru na wa haki basi ni ushindi kwa Ukawa, kwani wao ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi? Wameshasema kinyume na ushindi wao ambao wamekwishajitamkia hata kabla ya wananchi kupiga kura basi watatumia nguvu ya umma kuichukua Ikulu. Nauliza kutumia nguvu ya umma kuchukua Ikulu maana yake nini.? Kauli hizi ni za kuzitafakari sana sana sana.

Kama mimi ni masikini na ninayeheshimu utu wangu na nikaambiwa mwabudu shetani ili niwe tajiri, nitakataa na kutunza utu wangu kama ambavyo Bwana Yesu alikataa kumwabudia shetani kwa sababu hizohizo.

Hivi sielewi hawa wanachama wa Chadema ambao wamekubali kumeza matapishi yao wenyewe, wanapataje amani mioyoni mwao wanapojua mgombea urais wao ndio yule mtu waliyesema ni fisadi kwa zaidi ya miaka minane. John Mnyika alisema anao ushahidi wa ufisadi wa Lowassa, Mbowe alisema anashangaa vibaka wanachomwa moto na Lowassa ameachwa anadunda mtaani, Mchungaji Msingwa aliyesema anayemkubali Lowassa akapimwe akili na Godbless Lema yeye alisema ni baraka kwa Mungu kumzomea fisadi Lowassa. Hawa leo wanapataje uthubutu wa kusimama katika jukwaa moja na Lowassa na tena wakainuliwa mikono akiwanadi.

Mimi nilijiapiza wale waliokataa maoni ya wananchi sitaki urafiki nao hata leo, na Lowassa ni mfano mmoja, Mbatia ni mfano mwingine. Na niko tayari kuendelea kuunga mkono mabadiliko chanya yaliyofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuuvunja na kuwanyima urais kupitia CCM wala rushwa na wautakao uongozi wa nchi yetu kwa kigezo cha fedha zao.

Hii ndio CCM ya kweli, CCM ya wakulima na wafanyakazi, CCM inayochukia rushwa katika uongozi na sasa tumeanza na urais na baada ya urais tutawashukia kama moto ulao wabaya wote waliosalia. CCM ambayo haishurutishwi na matajiri wanaotaka kututengenezea viongozi ikiwemo nafasi ya urais.

Mwandishi wa makala haya Humphrey Polepole, ni msomaji wa gazeti la Raia Mwema. Anapatikana kwa namba 0786146700

Chanzo: Raia Mwema
 
Lowassa ni superPower amefanya kampeni mara 4 katika uchaguzi wa mwaka huu,kura za mjini na vijijini anazo za kutosha,kumbuka huyu alikuwa ccm miezi 4 iliyopita.
 
Imani yetu kwa Lowassa haiwezi kupunguzwa na viandiko uchwara kama hivi.
Kwaherini CCM.
 
Hivi slaa angegombea uraisi CCM mngesema lipi?

Ndio maana CCM walimtema LOWASSA ili wasihangaike kumtetea madhambi yake. Dr. Slaa angeweza kushinda ki-urahisi sana, ila Mbowe hakuwa anaamini mageuzi masafi maana yeye mwenyewe sio msafi.
 
"Ni katika kikao kile nilithibitisha kwamba aliyebuni mkakati wa kuikataa Rasimu ya Warioba kwa CCM alikuwa Edward Lowassa, tena akaonesha kufurahishwa na Rais Kikwete kama Mwenyekiti wa Chama kuzomewa katika vikao vya Chama na hatimaye Rasimu aliyoipeleka katika Chama kukataliwa."

Ulithibitishaje? Kwa yeye kukataa mtazamo wenu? Aliwezaje kuwa na nguvu kubwa ya ushawishi ya kila mccm hadi Raisi kuwafanya wapinge mitazamo yenu? Ndie alimtuma aliempiga Warioba? Katika kuhoji huko Magufuli hamkumuhoji? Nini msimamo wake? Inamaana ccm yote imehongwa na Lowasa kupinga rasimu yenu? Na unaposema amehonga watu ccm mbona hao walohongwa huwataji? Wao hawagombei viti vingine vya uongozi? Huoni kama huwatendei Watanzania haki kwa kutotaja hao wengine kama unavyomtaja Lowasa na mbatia maana wataendelea kuwachagua pia!? Katika kumpinga Lowasa, kigezo ni kuikataa rasimu na ufisadi...je, mgombea wa ccm yeye hana kashfa za ufisadi (refer PPRA report), hiyo unaiongeleaje? Na je rasimu yenu anaikubali? Lakini je, ni Lowasa ndie aliandaa katiba pendekezwa kisha akawapa bunge? Ile katiba pendekezwa iliandaliwa na nani? Ni Lowasa ndie alimshawishi Kikwete kuinadi siku ile na akaandaa shamrashamra zile kumkabidhi Kikwete na yenu akaiweka kapuni? Kwanini Kikwete played along yet anajua Lowasa anataka azomewe ili yeye awe Raisi as u claim? Inamaana Kikwete is that much naive?

Sasa naelewa kwanini mahali pengine unakataliwa..jibu ni rahisi tu...uko biased!

Unapoamua kuusaidia umma wa Watanzania, hasa kama msomi hupaswi kuegemea upande mmoja au kutafuta kupenda kote, hilo ni kosa.

Ulichotakiwa kufanya ni kuwaweka wagombea wote mezani...chambua wote mazuri na mabaya yao wote, then simama pembeni MPE mtu Uhuru wa kuamua anamtaka nani kwa mizani sawa.

Ila unatumia nguvu nyingi sana inayoonekana wazi kwenye maneno kumpongeza mmoja bila vigezo na kumdhoofisha mwingine kwa vigezo vyepesi, na hii ni rahisi kwako kwasababu wengi Watanzania huwa hawana tabia ya kuhoji.

Chagua ground ya kusimamia, aidha uwe mwanaccm kabisa, ukitetee chama kwa mazuri na mabaya yake, ili usomeke mpinzani shupavu. Au uwe muelimisha rika usie na upande wowote kama as as I zingine nchini, kwasababu hoja zako zinaupande kwa kujua au kutokujua.

Unapodai kwamba kauli za Ukawa ni za kichochezi, wamejihakikishia ushindi na wao sio tume...unaweza kuwa sawa ila ulipaswa kukemea kauli hizo hizo na upande wa Pili, is unless wao ni tume, mfano "hatutakubali ushindi wetu kuhojiwa na mtu yeyote" wao nani aliwaambia wameshinda? Ila sijakusikia umetoka kumpinga.

Well, katika hotuba yako kuna mengi ya kujifunza na kuwa makini usiwe benders, ila mtazamo wangu...

Lowasa anaweza asiwe chaguo sahihi kabisa kwa Tanzania kama mnavyojitahidi kutuelewesha, lakini kwa candidates waliopo, he is the best option we have.

Why? Simple...makundi yaliyo nyuma yao, is unless ututajie majina ya hilo genge ili tujue wako wapi wengine ili tuone tunachagua wapi.

On the other hand, Magufuli might be the perfect candidate for the Presidential election, but kwa hali ilivyo, he is not the right option.

Pamoja na yooote yanayojiri, ni ushindani wa kisiasa, na mwanasiasa bora hushinda kwa kutumia vzr "opportunities and timing" na hapo ndio Lowasa alipowazidi kete.

Hapa tz tulipofikia, wengi wa watanzania wanahitaji "progress/mabadiliko-genge la wahuni" kuliko "perfection/magufuli-uadilifu".....

Its all about opportunities and timing in this game, that's why inaitwa politics! Iko tofauti na dini, ndio maana unaona Slaa hakuweza mix vyote. You choose whom to serve coz lazma somewhere mzani utaelemea mahali. U can't be both. Mifano mizuri tunayo Getrude Rwakatale mzani ulielemea church over politics, Late Mtikila..Msigwa etc...

So kuliko kutumia muda mrefu kumchambua mtu ambae he is a politician, tumia muda huo kuset ground yako vzr kama msomi/mchambuzi wa hoja.

Gudluck.
 
Binadamu anayeweka imani yake kwa binadamu mwenzake ambaye ni mchafu, huyo amefilisika kiakili.

Tatizo tunavijana wengi wanaostahili kuwa hospital za vichaa. Chama kina maamuzi mawili- leo lowasa fisadi kesho lowasa safi, hapo mwendawazimu ni nani?
 
Vijana tunazidiwa na wazee kufikiri! Inashangaza sana watu waliokuwa wakitoka nje ktk sakata la lichimondi wakiacha kujadili mambo ya msingi kwa kumtuhumu Lowasa leo anakuwa msafi tena. Kweli nchi ya wenda wazimu hii.
 
Ni uchaguzi wa waadilifu dhidi ya genge la wahuni

Lowassa anawakilisha genge la wasaka madaraka kwa manufaa binafsi

  1. KWA muda mrefu kikundi cha wahuni kilijaribu na kufanikiwa kupoka madaraka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Watu hawa walitaka kujijengea "syndicate" ya kuongoza nchi, humo walikuwamo watu kadhaa na hasa wafanyabiashara akiwamo Edward Lowassa na yeye ndiye aliyekuwa msanifu wa genge hilo. Baada ya hapo, genge hili lilijipenyeza kwenye maeneo yote nyeti ya nchi yetu.

  2. Mwaka huu wana CCM tumekataa upumbavu huu wa kudhani urais na uongozi unaweza kununuliwa kama nyanya. Tumekataa na tumehakikisha katika ile "syndicate" au genge la wahuni hakuna kati yao ambaye anaiona Ikulu kwa tiketi ya CCM. Imewauma sana, huyu bosi ndio kaenda Ukawa na wako waliobaki CCM, tutashughulika nao kimkakati, lakini kwanza ni lazima tupate Rais mwadilifu ambaye atatusaidia kazi ya pili ya kusafisha ufisadi. Kazi ya kwanza imekuwa kuwanyima dhamana ya urais kupitia CCM.

  3. Hapa CCM wanapaswa kwa kweli kujitoa kimasomaso kwa kuuvunja mtandao na kuwanyima tiketi ya urais kupitia chama hicho, kwa hakika haukuwa uamuzi rahisi. Genge sasa limehamishia mapambano kutoka kambi ya upinzani. Utagundua hoja ya ufisadi ilishamiri sana na ndio maana kipindi fulani Ukawa waliunga mkono kazi yetu ya Katiba Mpya ambayo lengo lake lilikuwa kuja kuua ?syndicate? au genge la wahuni, leo Ukawa hawana tena uhalali (legitimacy) wa kukemea ufisadi maana ufisadi umetamalaki kati na juu yao.
​
Hebu tafakari mtu kama ndugu yangu na kaka yangu Said Kubenea kwa kazi yote aliyofanya miaka nenda rudi ya kupinga mafisadi na ufisadi, mpaka akashambuliwa, juzi alijisikiaje pale Kawe (Dar es Salaam) aliponyoshwa mkono juu na Edward Lowassa kutambulishwa kama mgombea ubunge? Dhamira yake ilimweleza nini? Na Lowassa hakusita kumpiga kijembe kwamba huyu alikuwa machachari sana kwenye media sasa apunguze, hivi Kubenea amejiuliza Lowassa alimaanisha apunguze nini na kwa faida ya nani?

Mimi mpaka vituo viwili vya televisheni kubwa nchini vimekataa nisikaribishwe kwenda kwenye vipindi kwa maelekezo ya wamiliki. Je, kukataliwa kwangu ni kwa faida ya nani? Mbona kama ni siasa kila siku kwenye TV hizo wadau wa Ukawa wanajimwaga vilivyo? Je, mimi tatizo langu ni nini? Wengine walifurahia TCRA kutoa tamko la kukataza watu kwenda kwenye vipindi vya moja kwa moja, na wengi walisema mitandaoni wamenikomesha mimi, hivi mimi nikikomeshwa ni kwa faida ya nani?

TCRA walilazimisha kwamba ili uruhusiwe kushiriki kwenye vipindi vya moja kwa moja ni lazima uwe mwakilishi wa vyama vya siasa. Mimi nikasema kwa hakika ningemwambia Kinana, Katibu Mkuu wa CCM angenipa barua ili niendelee kushiriki. Lakini nikasema hivi wanaoruhusiwa kushiriki ni wanasiasa peke yake? Je, uchaguzi ni haki uhodhiwe na wanasiasa pekee? Nikaendelea kujiuliza hivi Uchaguzi Mkuu wanaotakiwa kujadiliana zaidi ni wananchi wanaochagua ili kutoa dhamana au wale wanaoomba kuchaguliwa ili kupewa dhamana? Nikasema mbona Katiba inasema kuna uhuru wa kuweka mawazo hadharani, je haki ya kutoa mawazo hayo ina ukomo wakati wa uchaguzi?

Nikafunga safari kwenda TCRA nikawauliza maswali hayo na namshukuru Mungu aliwapa busara kubwa na baadaye walitoa tamko kubatilisha katazo lao la awali. Lakini nikajiuliza zaidi kwa nini hata wale wadau wa asasi za kiraia hawakuoneshwa kukasirishwa na kitendo kile cha TCRA? Nikasema hata watu wote wakisimama mimi nitaendelea kudai haki na kweli katika nchi yangu.

Leo siwezi kwenda kwenye TV mbili kubwa na wamiliki wameweka msimamo, kwa nini? Wale wanaofurahia mimi kukataliwa je, wanapata faida gani? Mbona mimi nikionana na vijana na wadogo zangu ambao wako katika vyama vya upinzani nawapa moyo na kuwaambia watende sawa sawa na dhamira zao njema na kwamba walitizame taifa kwanza? Najiuliza je, tatizo langu ni nini? Au sijitambui (naïve)?

Nitasema kweli daima na fitina kwangu mwiko na nitatumia elimu yangu kwa manufaa ya wananchi wa taifa langu, mimi kama Mtanzania maneno hayo ni msingi. Kwa nini leo baadhi ya watu wamenigeuka, watu ambao walifurahia nilipowaambia pale Ubungo Plaza na pale Mlimani City kwamba maslahi binafsi yana hatarisha mustakabali wa taifa letu. Nilikwenda mbali na kuwataja watu hao na Watanzania baadhi na wengi wakanifurahia sana na kunipongeza.

Mbona leo naendelea kuwasema watu wale wale na baadhi ya Watanzania wananiona nimegeuka? Kwa nini waliniamini kipindi kile na wakijua mimi ni CCM na nilikuwa nawasema baadhi ya wana CCM na leo nikiwa bado CCM naendelea na kazi ile ile ya kuwasema watu ambao wanataka kutununua ili waendeleze genge la kihuni mbona watu wanasema mimi ni kigeugeu? Ina maana Watanzania wamepigwa upofu, ina maana wasomi wetu wamepigwa upofu, ina maana wazee wetu ambao wameuishi umri wamepigwa upofu, na kama tumepigwa upofu wako wapi viongozi wetu wa dini, je mmetuombea? Naendelea kutafakari.

Siku moja nilikaa na viongozi wawili wa CCM, mmoja akasema nadhani mchakato wa Katiba ni lazima kabla ya kura ya maoni tujenge muafaka na kufanya maridhiano ili kila sauti ya Mtanzania isikilizwe. Kiongozi mwenzake mdogo kidogo kwa cheo akabisha sana na akasema ni lazima twende kwenye kura ya maoni kwa sababu tendo la Katiba kwa lilipofika ni kama maji yanayomwagwa kutoka katika bilauri kwamba ni lazima yafike chini.

Nikamtazama na kumkazia macho na nikamweleza wacha na mimi nizungumze kama mwana CCM. Nikawaomba niwaeleze historia ndogo ya namna nipo nilipo. Nikasema nianzie kwenye Katiba, nikawaambia unajua mimi nilikuja Tume ya Katiba nikiwa simfahamu mtu yeyote isipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano? Nikawaeleza mimi sikumfahamu mzee Warioba, Jaji Ramadhani, mzee Butiku, Dk. Salim wala Profesa Kabudi na wengineo, sikumfahamu hata mmoja.

Nilikuwa namfahamu Rais Kikwete tu. Alipotupa kazi na akatuagiza tuwasikilize Watanzania na watakachosema ndicho ambacho tukiandike, tulifanya hivyo kwa unyenyekevu mkubwa kwa Watanzania.

Hata pale ambapo Rais alionekana kutoka na msimamo tofauti na wetu nilibaki kuwaambia Watanzania kwamba Tanzania njema itajengwa na Watanzania wenyewe. Aidha niliendelea kusema kundi la watu ambao wanajulikana liliteka na kushinikiza CCM kutoka na msimamo ule. Hatukuishia pale tuliokuwa wajumbe wa Tume ya Katiba tulifanya mahojiano kwa kuzungumza na wadau mbalimbali, wabunge, viongozi wastaafu, watu mashuhuri ili kuelewa tatizo lilikuwa wapi.

Mahojiano haya ya chini chini yalinipa fursa ya kuonana na wabunge wengi wa CCM na wa upinzani na wote walikiri kwamba ?Bwana Mkubwa amekataa? na tulipozidi kuhoji hoji tulikuja kukutana na wapambe wake ambao walisema ?tatizo lenu mmedhoofisha urais na kwamba Kikwete anataka kuondoka ameweka masharti na kanuni ngumu za uongozi hilo haliwezekani? wakaendelea kusema ?yeye (Kikwete) aende na sisi tubaki na madaraka yale yale au zaidi na tuwe na mamlaka kama aliyonayo sasa katika nchi?.

Wapambe hawa tulizungumza nao kwa maana ya kuwapa elimu ya Rasimu ya Warioba na wakawa wanatuuliza ?kwa hiyo ninyi (Tume ya Katiba) mnashauri ?Mkubwa? achukue urais wa Tanzania au urais wa Tanganyika?? Tukasema achukue ya Muungano, wakasema ?je itahusisha madini, gesi na ardhi?? Tukasema hapana, wakaendelea kuuliza ?je, akichukua ya Tanganyika atakuwa na uwezo wa kusafiri nje ya nchi kama Rais Kikwete na kupigiwa mizinga 21?? Tukasema hapana, mmoja wao akasema; ?anhaaa hapo ndio mnapokosea, sisi tunataka zote za Tanganyika na Muungano ziwe pamoja?, kwa kusema hivyo walikuwa wanamaanisha serikali mbili.

Hatukuchoka, tukafanya utaratibu na tukaenda kumuona ?Bwana Mkubwa? yaani Edward Lowassa, tulikutana ofisini kwake Mikocheni (Dar es Salaam). Ili kuweka uwazi katika mkutano ule tulijumuisha pia wawakilishi watatu wa asasi za kiraia na makamishna wawili, mimi nikiwa mmojawapo, tulikuwa na kikao ambacho hakikupungua saa mbili.

Ni katika kikao kile nilithibitisha kwamba aliyebuni mkakati wa kuikataa Rasimu ya Warioba kwa CCM alikuwa Edward Lowassa, tena akaonesha kufurahishwa na Rais Kikwete kama Mwenyekiti wa Chama kuzomewa katika vikao vya Chama na hatimaye Rasimu aliyoipeleka katika Chama kukataliwa. Nilijiuliza sana mimi kama kiongozi kijana, tafsiri yake ni nini? Huyu ni mwana CCM na anafurahia Mwenyekiti wake kudhihakiwa na kutupiwa Rasimu yake katika kikao? Leo najiuliza kama alikuwa na dhamira ya kuikubali rasimu ya Warioba kama anavyojinasibu sasa katika majukwaa akiomba kura kupitia Ukawa kwa nini alikaa kimya wakati Mwenyekiti wake akidhihakiwa?

Kibaya zaidi Lowassa anapoomba kura na kutumia hoja ya Katiba amekuwa akitumia neno ?Mamlaka Kamili? ili kuwafurahisha baadhi ya Watanzania waishio Zanzibar. Mimi nilikuwa Tume na huko tulikubaliana Mamlaka kamili kwa Zanzibar na Tanganyika ni kuvunja Muungano.

Huyu Lowassa nilipoongea naye alisema Zanzibar ipewe kila kitu isipokuwa Ulinzi tu, tukamweleza kufanya hivyo ni kuvunja Muungano, hakuonesha kuelewa. Hata tulipomwambia unajua kwamba kwa madaraka yako na wakati unasimamia ujenzi wa shule za kata, hukupata kujenga hata shule moja Zanzibar, akaonesha kushangaa na kutokumbuka ilikuwaje kipindi hicho.

Nikawaeleza iliyokuwa Tume ya Katiba iliwahi kumwita hata mzee Kingunge aje tujadiliane kuhusu Rasimu ya Warioba na alipokuja aliwatukana wajumbe wa Tume pamoja wageni wengine waalikwa akiwemo Profesa Abdul Sherrif kutoka Zanzibar, nilipoona anamuunga mkono Lowassa sasa namwelewa na ndio maana katika mkutano wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere nilidiriki kusema Mungu akinipa umri mrefu na kufikia uzee namwomba Mungu nisiwe kama wazee wa namna hii.
Nasema tena, kama mzee Kingunge na Lowassa walikataa katukatu maoni ya wananchi ambayo sio tu yalikuwa yanaleta mabadiliko bali mageuzi ya kimfumo, je haya mabadiliko wanayoyahubiri majukwaani msingi wake ni upi? Kwa nini tunatumia wananchi wetu kukosa taarifa kuwahadaa?

Nikamwambia yule kiongozi mdogo, unadhani ni kazi rahisi mimi kama kijana mdogo kusimama kidete kutetea maoni ya wananchi? Nilijua aliyekuwa na maslahi katika kutupilia maoni ya wananchi hakuwa Kikwete bali Edward Lowassa ambaye amekuwa akiutafuta urais wa kifalme. Kuthibitisha hilo nilimtamka kwa jina mara kadhaa Edward Lowassa kwamba hafai kuwa Rais wa Tanzania.

Na kwangu mimi nilikuwa najiuliza hata kupitia CCM ambako mimi ni mwanachama, iweje mtu ambaye anakosa kuheshimu Watanzania wanapotoa maoni yao ya Katiba akawa ni mtu ambaye atasimama ili wampe dhamana ya kuwa Rais wao. Mimi nilimkataa tangu CCM na nilipoona CCM kama vile wanachelewa, mimi (Polepole), mzee Butiku na mzee Warioba tulifanya mdahalo na tukaweka msimamo kama Lowassa atapewa tiketi ya kugombea urais kupitia CCM basi sisi watatu tusingejitoa bali tungepiga kampeni ya kusema CCM isichaguliwe.

Nikaendelea kumwambia hili la Katiba mbaya wake tunamjua katika chama na alijaribu kuhonga watu mara kadhaa ili kutimiza lengo lake. Ni lazima tujenge muafaka wa kitaifa kwanza, ili tusikilize na kujumuisha sauti za Watanzania wengi, ili Katiba mpya ibebe Utanzania wetu na sio kundi moja.

Namshukuru Mungu, kiongozi yule mdogo ni muelewa haraka akasema muafaka ni kitu muhimu, hilo linawezekana na ni kwa maslahi ya Watanzania wote sema tu kipindi kile kiligubikwa na ushindani wa kisiasa, ila sasa ni muhimu tukaja pamoja kama taifa na kabla ya Kura ya Maoni hili liwekwe sawa kwanza. (Mwisho wa kunukuu kikao changu na viongozi wa CCM).

Uhalisia huu ndio umefanya mzee Joseph Sinde Warioba kupiga kampeni ya Chama Cha Mapinduzi na kumuunga mkono Dk. John Magufuli. Ila kitu kimoja napenda kuwaeleza Watanzania kuna maadui ndani ya CCM na nje ya CCM na hasa hasa wale ambao wako chini ya ?syndicate? au lile GENGE la WAHUNI ambalo linafanya kila jitihada ili mgombea wa CCM asiye na makundi na asiye na msalie mtume na wezi, wabadhirifu na mafisadi asifanikiwe. Maadui hawa wako radhi mwana mtandao mwenzao (aliyeondoka CCM na kwenda Ukawa) apewe dhamana ya urais wa nchi yetu ili waendelee kutunyonya kwa maslahi yao, kumbuka mtu mwenye tuhuma za ufisadi hawezi kushughulika na wenzake wengi wenye tuhuma nzito nzito za ufisadi.

Ikumbukwe Ukawa huu sio Ukawa ule ambao mimi na mzee Butiku na mzee Warioba tulifanya nao kazi pamoja, si hawa. Hawa Ukawa wa sasa ni watu wenye uchu wa ajabu wa madaraka na kwamba wako tayari kumtumia mtu mwenye nasaba zote na ufisadi ili awafikishe Ikulu. Sikiliza kwa umakini hata kauli zao ni za vitisho, wanatisha watu, wanalazimisha ushindi na tayari wameshasema kama uchaguzi ukiwa huru na wa haki basi ni ushindi kwa Ukawa, kwani wao ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi? Wameshasema kinyume na ushindi wao ambao wamekwishajitamkia hata kabla ya wananchi kupiga kura basi watatumia nguvu ya umma kuichukua Ikulu. Nauliza kutumia nguvu ya umma kuchukua Ikulu maana yake nini.? Kauli hizi ni za kuzitafakari sana sana sana.

Kama mimi ni masikini na ninayeheshimu utu wangu na nikaambiwa mwabudu shetani ili niwe tajiri, nitakataa na kutunza utu wangu kama ambavyo Bwana Yesu alikataa kumwabudia shetani kwa sababu hizohizo.

Hivi sielewi hawa wanachama wa Chadema ambao wamekubali kumeza matapishi yao wenyewe, wanapataje amani mioyoni mwao wanapojua mgombea urais wao ndio yule mtu waliyesema ni fisadi kwa zaidi ya miaka minane. John Mnyika alisema anao ushahidi wa ufisadi wa Lowassa, Mbowe alisema anashangaa vibaka wanachomwa moto na Lowassa ameachwa anadunda mtaani, Mchungaji Msingwa aliyesema anayemkubali Lowassa akapimwe akili na Godbless Lema yeye alisema ni baraka kwa Mungu kumzomea fisadi Lowassa. Hawa leo wanapataje uthubutu wa kusimama katika jukwaa moja na Lowassa na tena wakainuliwa mikono akiwanadi.

Mimi nilijiapiza wale waliokataa maoni ya wananchi sitaki urafiki nao hata leo, na Lowassa ni mfano mmoja, Mbatia ni mfano mwingine. Na niko tayari kuendelea kuunga mkono mabadiliko chanya yaliyofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuuvunja na kuwanyima urais kupitia CCM wala rushwa na wautakao uongozi wa nchi yetu kwa kigezo cha fedha zao.

Hii ndio CCM ya kweli, CCM ya wakulima na wafanyakazi, CCM inayochukia rushwa katika uongozi na sasa tumeanza na urais na baada ya urais tutawashukia kama moto ulao wabaya wote waliosalia. CCM ambayo haishurutishwi na matajiri wanaotaka kututengenezea viongozi ikiwemo nafasi ya urais.

Mwandishi wa makala haya Humphrey Polepole, ni msomaji wa gazeti la Raia Mwema. Anapatikana kwa namba 0786146700

Chanzo: Raia Mwema

Ni uchaguzi wa mafisadi wa nyumba za serikali,malipo hewa ya makandarasi na kivuko chakavu dhidi ya mafisadi wa Richmond
 
Back
Top Bottom