Just thinking Aloud... JE PROF. MWANDOSYA ANASTAHILI PONGEZI?

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
24,898
11,292
Wanajamii,

Moja ya matatizo makubwa sana yaliyokua yanatusumbua hata wakazi wa mijini ni upatikanaji wa maji...

Matatizo yali-range from mifumo, sources, usafi wa maji, mfumo wa malipo na hata namna ya kusimamia matumizi ya maji nk

For the first time, this year silisikii hili kuwa tatizo.... hasa mijini; na hata kwa vijijini naona muamko mkubwa sana wa watu au sekta binafsi kubeba majukumu

Je, haya tunayoyaona ni juhudi za prof, au ni juhudi za mfumo uliojengwa kwa muda sasa??... Majibu yatasaidia sana kuangalia na sekt anyingine

Ta
 
Nadhani tunahitaji uchangiaji wenye facts zaidi katika hili badala ya kutanguliwa ushabiki na mapenzi, ili tuweze kutambua mahitahitaji yetu halisi ni yapi, na what are our capabilities na kwa njia zipi.
 
ʞontɹact Sniper;2310096 said:
Nadhani tunahitaji uchangiaji wenye facts zaidi katika hili badala ya kutanguliwa ushabiki na mapenzi, ili tuweze kutambua mahitahitaji yetu halisi ni yapi, na what are our capabilities na kwa njia zipi.
Ni kweli kabisa...

nadhani mleta mada hajaonyesha ushabiki, bali amehoji changes zote zile nani apewe credits?
 
Fungua bomba lako 80% of the time utapata maji-hiyo ndiyo fact.
 
Bodo inawezekana mtoa mada hujazunguka, vijijini maji hakuna na hata maeneo ambayo kunapitika na kuna mito mikubwa karibu mfano Kyela hawana maji ya bomba! Hata mijini maji hakuna ni tatizo sugu pita maeneo ya Kibaha (kutoka mlandizi mpaka ubungo) maji ni tatizo. So mimi siafiki kama kuna changes mkuu!
 
binafsi sijaelewa mtoa hoja ka-base wapi katika kujenga hoja yake au umetumia lugha ya kitendawili? maana kama ni maji ni kuwa tatizo bado ni kubwa. maana hoja yako ni kama tatizo la maji ni historia (based on the red highlight below:

.....................................................
Moja ya matatizo makubwa sana yaliyokua yanatusumbua hata wakazi wa mijini ni upatikanaji wa maji...

Matatizo yali-range from mifumo, sources, usafi wa maji, mfumo wa malipo na hata namna ya kusimamia matumizi ya maji nk

For the first time, this year silisikii hili kuwa tatizo....
 
Ishu ya maji bado ni tatizo sana! Hii kuto sikia kelele ujue ishu ya umeme ime take cove kwa muda! Ila maji bado ni tatizo sugu! Huku sinza tumeshazoe maji ya madumu ya bomba cjui mpaka Yesu arudi?
 
issue ya maji watu wameamua kujitafutia soln zao (Kuchimba visima na kuuziana), lakini shida ya maji bado ni kubwa mno
watu wako kimya wanaangalia tatizo lililo kubwa kwa sasa nchini (umeme na mafuta)
 
Kwetu Kipunguni watu hata hawajui kwamba duniani kuna maji ya DAWASCO. Wanatusaidia wanaochimba visima binafsi.
 
Baba, ungefanya hata kautafiti kadogo kabla hujaandika. Mijini gani unazungumzia? Umekwenda maeneo ya ubungo na kimara? Umekwenda Mbezi juu na Goba? Vijiji unavyovisemea ni vya wapi? Rudi mezani ukachambue upya.
 
Utafiti wako umeufanyia wapi? Mimi nipo Mazimbu Morogoro, nina wiki tatu sijaona bomba langu kutoa maji. Hali ni hiyohiyo sehemu nyingi za nchi. Kila siku wbunge wanalalamika kuwa majimbo yao hayana maji. Wewe unakaa oysterbay halafu unaleta hoja za kupakana mafuta.
 
Back
Top Bottom