BabaDesi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2007
- 6,032
- 3,944
Ni kweli usemacho Abednego but je wabunge wa Tanzania wote wanakubalika kwa matendo na maneno yao? Nijuavyo Mama Mbene amerudi nchini siku za karibuni (kama sikosei ) alikuwa Swaziland au Botswana.
Hapa sitetei kuwa yeye ni msafi sana (since simjui kihivyo) but ninajaribu kusema kuwa tusimpime kwa kipimo ambacho kikitumika kwa wabunge waliopo kitatoa majibu sawa kwa wote!! Unless uvilete hivyo vimbwanga tuanzekuvichambua ili tuone ni kwa kiwango gani vimevizidi vile vya wabunge wenzie mjengoni.
...mmm, mOne, unaniangusha. tayari Abednego ameishataja kimbwanga kimojawapo cha mama kuwa alichori kwenye Benki yetu na kukimbilia Kenya. Kama tunafahamu hili, kama ni kweli na lina ushahidi, ni halali kumuingiza mjengoni kwa vile tu walio wengi mjengoni humo nao wana vimbwanga vyao??
Si ingekuwa vema kuwa kwa vile tumefahamu kimbwanga cha mama huyu basi tumpunguze kabisa kuingia mjengoni na sio kumuongeza humo kwa vile tu tayari mjengoni kuna wana vimbwanga wenzake tayari??