Jussa, Mbenne wabunge wapya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jussa, Mbenne wabunge wapya!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Feb 10, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,618
  Likes Received: 23,709
  Trophy Points: 280
  Raisi Jakaya Kikwete amehitimisha uteuzi wa wabunge 10 wa kuteuliwa na rais kwa kumteua Bw. Ismail Jussa Ladhu, wa CUF na Janet Mbene wa CCM kuwa wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Uteuzi huu, umetangazwa live jioni hii bungeni mjini Dodoma, na Spika wa Bunge, Mhe. Samweli Sitta wakati akikamilisha mjadala wa Richmond.

  Jussa ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CUF na msungumzaji mzuri kwenye medani za media. Janet Mbene ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Masaki kwa tiketi ya CCM, na huku ndiko ziliko nyumba za waheshimiwa mawaziri na wenzetu waliojaliwa neema.

  Wabunge hawa, wataapishwa kesho Bungeni Dodoma.
   
 2. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Rais Jakaya Kikwete amewateua Ismail Jussa Ladhu wa CUF na Janet Zebedayo Mbene wa CCM kuwa wabunge, uteuzi huo unaanza mara moja.

  Jussa ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CUF wakati Janet Mbene ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Masaki kwa tiketi ya CCM

  PM
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,301
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Kuongeza gharama kwa walipa kodi! Watafanya nini muda huu uchaguzi OCT! Kaweka rekodi kuchagua jamaa wa CUF.

  Sijui kama ni Mbene huyu nime-mgoogle!

  Janet Mbene -
  [​IMG]

  She joined the Board in May 2006. She is a professional banker and holds a Masters Degree in Economics from University of New England, Armidale New South Wales, Australia. She has a Bachelor of Arts in Economics from University of Dar es Salaam and an Advanced Diploma in banking from Institute of Finance in Dar es Salaam. She is a Company Director and Lead Consultant SIA Limited and a member of Fair Competition Tribunal Tanzania and the Advisory Board Faculty of Business at Tumaini University in Dar es Salaam. She is also a founder member of the Association of Women Economists in Tanzania among others.
   
 4. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Huu si ndio mwaka wa mwisho kwa Bunge? hao watafanya kazi gani?
   
 5. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #5
  Feb 10, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,753
  Trophy Points: 280
  Unajua bunge la Nigeria lilimuidhinisha Jonathan kuwa Rais baada ya kuona amar yardua amekosa uongozi thabiti.Wametumia neno "kukosa uongozi thabiti",hivi sisi kweli tunao?

  Nwei,hongera wateule!
   
 6. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  huyu mbene sio mke wa professor anayemfagilia kikwete kila siku??????????
   
 7. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  mkuu unakuwa kama hujui!!!!!!!!! si kuchukua ngawira za mwishomwisho aka kiinua mgongo kwa kazi ya miezi minne?????????
   
 8. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hajaweka rekodi, alianza Mkapa ambaye alimteua Hamad Rashid. Inashangaza kwamba wabunge wa majimbo ukomo umewekwa kwamba nafasi ikiwa wazi chini ya mwaka mmoja kuelekea uchaguzi hakuna kujazwa lakini wa kuteuliwa na Rais wakati wowote anaweza kujaza kisiasa kuelekea kwenye uchaguzi.

  Janet Mbene aliwahi kugombea ubunge wa bunge la Afrika ya Mashariki akashindwa

  PM
   
 9. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  mama ameruka kwa kasi ya ajabu, kutoka serikali ya mtaa hadi dodoma, kaaaaaazi kweli kweli...
   
 10. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndiye yeye amewahi kuwa kwenye bodi ya SID nk

  PM
   
 11. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #11
  Feb 10, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  [​IMG]

  Ms Janet Mbene - Working in Zimbabwe Now.
  Chaiperson Kenya Commercial Bank

  Naona ni huyu na hapa kama Miss sijui ana mume ama laa, ni muhimu kujua hili.​
  ni fellow wa Synergos Announces 2009 Senior Fellows

  Janet Mbene (Zimbabwe)​
  , Executive Director, MWENGO, a private voluntary association based of nongovernmental organizations in East and Southern African countries that focus on gender, children and youth, trade, land distribution, the environment and social justice.
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,301
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160


  Mmmmmhh hili nalo niangalizi, mambo ya fadhila!
   
 13. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #13
  Feb 10, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,681
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Wananchi tutegemee nini katika uteuzi huu?? wateule hawa kwa muda mfupi wa ubunge uliobaki watawafanyia nini watanzania? Anyway, jichukulieni chenu kwa muda huo baadae laleni mbele.
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,618
  Likes Received: 23,709
  Trophy Points: 280
  Mode, naomba iunganisha hii thread na ile nyingine, its coincidential duplicate!.
   
 15. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #15
  Feb 10, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mhh kukubali kuuzwa kwa ile Masaki Beach huu ndio ujira wake? just thiking aloud..
   
 16. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #16
  Feb 10, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 9,285
  Likes Received: 2,988
  Trophy Points: 280
  imebaki miezi 5 au 6 rais avunje bunge ...uteuzi huu wa nini..bora wa jussa naweza kuita kuwa ni sahihi kisiasa..as gesture ya kukubali hatua ya karume na seif...unajuwa jussa ndiye mshika mkoba wa seif..miaka yote[PS] ...sasa huyu mama kuna motive gani..kama ni fadhila ...si ingetosha kumwambia ahsante na amteue mwaka 2010 mwishoni ..akishaapishwa ....kama rais awamu ya pili????
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Feb 10, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  Si tumemkumbusha juzi hapa (last week) kuwa ni mvivu kuchagua hadi ameshindwa kujaza nafasi mbili za ubunge zilizosalia.... finally kaamua kujaza ili asionekane mvivu mvivu.
   
 18. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #18
  Feb 10, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Je huyu Mama na yeye si ataondoka na marupurupu yote kama wabunge wengine tu...haijalishi ameteuliwa lini.??!!

  Lengo la uteuzi sio kwenda bungeni kuwakilisha wananchi. Lengo ni kulipa fadhila....sasa nani wa kusema huwezi kulipa fadhile kwa sababu imebakia miezi michache bunge kuvunjwa?
   
 19. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #19
  Feb 10, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 9,285
  Likes Received: 2,988
  Trophy Points: 280
  ...kwa muda mchache uliobaki ....uwakilishi atakaotoa kwa miezi hii michache..SIO VALUE FOR MONEY kwa kodi zetu..atapata kiinua mgongo pia...bora angemchagua baada ya uchaguzi!
   
 20. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,794
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  Hahaaa! Huyu anapata mkpo siju ruzuku ya shngingi na makitu mengine yanayohusiana na ubunge.
  Sisi bana! Mi wakinipa pingu tu, achilia mbali bunduki, nafunga mtu kwenye high tention posts za kihansi.

  Nggggrrrrr!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...