Jussa, Mbenne wabunge wapya!

Jussa, Mbenne wabunge wapya!

Well, kunaweza kuwa na maoni tofauti.

Hata hivyo sisi kama TPN tunapenda kumpa hongera dada Janet Mbene. Toka August 2007 amekuwa ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya TPN na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwezeshaji.

Alishiriki kikamilifu katika kufanikisha Kongamano la Wanataaluma wa Ndani na Nje ya Nchi lililofanyika December 2009 na mambo mengine mengi.

Janet, imefika zamu yako sasa kushika bendera ya TPN, kama baadhi ya walio kutangulia. Tunaomba usituangushe.

TPN imekuwa na bahati ya kuwa na viongozi ambao ni wanachama na mashabiki wa TPN bila kujali itikadi, dini, rangi wala jinsia zao.
 
...kwa muda mchache uliobaki ....uwakilishi atakaotoa kwa miezi hii michache..SIO VALUE FOR MONEY kwa kodi zetu..atapata kiinua mgongo pia...bora angemchagua baada ya uchaguzi!

Mkuu PM,

PM Rais wetu haangalii "Value for Money" kwa kodi zetu. Yeye amelipa fadhila kwa kutumia kodi zetu...hivyo mpaka sasa hivi lengo lake kwa mlengwa limetimia kwa 100%.

Hilo la kumteua baada ya uchaguzi ni la awamu nyingine...labda nalo atapewa kwa juhudi zake nyingine...tutajua wakati huo ukifika.
 
Rais Jakaya Kikwete amewateua Ismail Jussa Ladhu wa CUF na Janet Zebedayo Mbene wa CCM kuwa wabunge, uteuzi huo unaanza mara moja.

Jussa ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CUF wakati Janet Mbene ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Masaki kwa tiketi ya CCM

PM

Huu ni ufujaji wa pesa za walipa kodi ni miezi michache tu kabla ya uchaguzi yaani rais mzima anateua watu wake kishkaji kishkaji ili wale pesa ya walipa kodi lakini hawataweza kufanya lolote katika kipindi hiki hadi uchaguzi. AIBU!
 
si tumemkumbusha juzi hapa (last week) kuwa ni mvivu kuchagua hadi ameshindwa kujaza nafasi mbili za ubunge zilizosalia.... Finally kaamua kujaza ili asionekane mvivu mvivu.

rais wetu si mvivu ...ana kazi nyingi sana...anafanya kazi kuanzia za wakuu wa wilaya hadi rais....acha majukumu yake kama mwanamume...hata ikitokea ameanguka anguka msiwe mnashangaa sana ...ratiba jamani ....kali sana...

mnajuwa kuna tofauti kati ya being busy WITH OUTCOMES and being busy for nothing ...hili msijali sana!!
 
uteuzi wa jussa ni sahihi sana..kichwa hicho
 
Nadhani uteuzi huu umefanywa kama maandalizi ya kumuwezesha mama huyo kuchukua Jimbo moja Dar. La sivyo sioni sababu ya kuongeza mbunge yeyote muda huu. Ni gharama zisizo na maana kabisa.
 
Janet Mbene akiwa pamoja na viongozi wengine wa TPN katika hafla ya kutunisha mfuko wa TPN November 2007, Viwanja vya Karimjee

i1764_TPNcrew.JPG


Janet Mbene (Kushoto)

i1765_TPNwithsitta.JPG


Janet Mbene (Wa tatu toka kulia)
 
i1766_JanetTPN.JPG


Akiwa na Viongozi Wenzake wa Kamati ya Utendaji.

i1767_JanetTPNkazini.JPG


Akiendesha Kikao Cha Kamati ya Uwezeshaji ya TPN
 
Wouldn't be surprised JK akimteua Sheikh Yahya Hussein kuwa mbunge,kisha kumpa unaibu Waziri wa Afya (kitengo cha ndumba).
 
Huyu Presidaa hayuko siriasi hata kidogo, kwa nini anawateua wakati muda wa bunge unaelekea kuisha?
 
Huyo mama miaka ya nyuma alikuwa anafanya kazi NBC alikuwa bi mdogo wa Balozi wetu wa kudumu umoja wa mataifa Dr.Augustin Mahiga amemzalia watoto wawili!zama zake alikuwa bomba haswa!Zama hizo balozi alikuwa Mkurugenzi wa usalama wa taifa!
 
Huyu dada ni active sana katika mambo mengi, nadhani anastahili. Cha muhimu awe mzalendo katika kutetea maslahi ya wananchi.
 
People wamehate, inawezekana anataka kumpa jimbo la kawe jamani. Masaki is in Kawe, and she might be a replacement for Ritha Mlaki perhaps au anania nae nyingine. Anaweza akapewa jimbo fasta by xmas akawa Waziri mkuu Mwanamke. Unajua bora huyu mama apewe hayo marupurupu, at least ana elimu solid and she seems to have initiative. Sijui performance yake iko vipi lakini mara mia huyu kuliko Sofia Simba et al. Mimi sitaki comment sana manajua this is not the end game unless ni shoriii..lol. Lakini ngoja tuone, asingemuelevate bila plan. Masaki ndio kwa wenyewe ati..lazima ataula 2nd Term JK edition. U dig!

Kinyambiss 2020.
 
Well, kunaweza kuwa na maoni tofauti.

Hata hivyo sisi kama TPN tunapenda kumpa hongera dada Janet Mbene. Toka August 2007 amekuwa ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya TPN na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwezeshaji.

Alishiriki kikamilifu katika kufanikisha Kongamano la Wanataaluma wa Ndani na Nje ya Nchi lililofanyika Decembe 2009 na mambo mengine mengi.

Janet, imefika zamu yako sasa kushika bendera ya TPN, kama baadhi ya walio kutangulia. Tunaomba usituangushe.

TPN imekuwa na bahati ya kuwa na viongozi ambao ni wanachama na mashabiki wa TPN bila kujali itikadi, dini, rangi wala jinsia zao.

Kumbe bado hamumjui Janet Zebedayo Mbene sawa sawa,Huyu mama akiwa NBC alipora benki na kukimbilia Nairobi Kenya,RB ya kutafutwa kwake ipo police central Dar Es Salaam Tangu hapo amekuwa mtu wa kuranda randa tu hadi alipohitimisha ajira yake pale Oxfam akaanza kujihusisha na siasa za CCM,Siyo wa kihivyo mnavyomjua ana vibwanga zaidi ambavyo asingesitahili kabisa kuingia mjengoni.
 
Back
Top Bottom