Jumatano ya majivu

Jumatano ya majivu

Maria hebu nambie, Jumatano ya majivu ndo maandalizi ya Majilio au? Nimepata kipaimara siku nyingi sana, nshasahau.
 
Mateso yake bwana YESU yalitokana na dhaambi zetu.... dah hii nyimbo inanikumbusha mbaaali sana na hiki kipindi ni muhimu sana kwetu sisi wakristo. Ahsante MR aka ticha kwa kutukumbusha, MUNGU akujaalie na akupe siku njema
 
Ibara St, Theresa Arusha
1. Asubuhi 12.15 asubuhi
2. Mchana Saa 6.00
3. Jioni Saa 10.00
 
Larueni mioyo yenu na si mavazi yenu, msijionyeshe kuwa mmefunga ili msije kuwa kama wale wanafiki, ni muda muafaka wa kutafakari mwenendo wa maisha yako, kila la kheri wakristo wenzangu!!!!
 
we maria umetubu madhambi yako ya huko chini kabisa hadi uwatakie wadau kwaresma njema?
 
tujitahidi tukapake majivu kwa wale wakristo jamani pia kipindi hiki ni cha mfungo na kutenda mema kwa wenye matatizo tuwasaidie na kuwaombea walau kila mmoja wetu awe na muda wa kushiriki ibada na kushirikiana na wengine kwa mfungo!
Napenda kuwatakia wakristo wenzangu wote wa JF Jumatano njema ya majivu.
Kwarezma njema wapenzi
Mr




 
Last edited by a moderator:
MR twende zetu St. Joseph kwa Fr. Mansuetus (sijui bado yupo pale yule) tukapake majivu.:wink2:
Hayupo siku waliishamuamisha siku nyingi yuko Fr. Edwin Kigomba na mwingine aliyekuwa paroko wa Kibaha
 
Kwa wale ambao awakufanikiwa kupaka majivu asubuhi na wapo posta,kutakua na misa jioni st.joseph ambayo itaongozwa na kadinali.
 
Asante na mimi ndo natoka huko ubarikiwe nawe

"Funga Jumatano ya Majivu usile nyama siku ya Ijumaa Kuu"

Finest amri ya kanisa ya ngapi tena hii?
 
Ubarikiwe sana Mpendwa MR na wana JF wote
 
He kumbe leo ni J5 ya majivu, hawa jamaa huku bush hakuna anayesali wala kuswali ati wako busy!
 
mfungo wa kwaresma ndio unaaza........... ILA USIFUNGE KWA KUWA HUNA PESA YA KULA MCHANA MAOMBI YAKO HAYATAKUWA NA TIJA
 
ni kipindi cha toba kutafakari wapi umekosea toka kwaresma iliyopita na mwisho kujirekebisha. Asante rm kwa kukumbusha wengi kwaresma njema wote
 
Back
Top Bottom