Hana akili vipi...???
Acha kutumia lugha za maudhi...mbona jamaa katiririka vizuri acha wivu na uvivu wa kufikiri... Suala la uchumi kushuka/kupanda ni la kutafakari binafsi sio kusingizia GDP....
Wajinga ni wengi na watu makini ni wachache.. Suala la kushuka au kupanda kwa uchumi ni kujumlisha/kutoa na kulinganisha tuu sio mpaka mzungu aje akufundishe ndo uelewe.. Ndo maana jambo la msingi ww unaleta mzaha...
!Mwaka huu mtatabiri kila kitu.. na bado namba mtazisoma..
"Ni kiburi cha ovyo mtu kuropoka yale anayoyaona kuwa ya kweli bila kujali matatizo yatakayowapata wananchi. Maana hakuna hata mmoja wetu anayejua ukweli wote; tunaweza tukagundua sehemu mpya ya ukweli, lakini hatuna haki ya kujidai kwamba tunajua zaidi " - Nyerere, Feb 29th,1968ANGUKO LA UCHUMI KWA TAIFA LA MAREKANI (1929~1933)
Aliyeitwa Herbert hoover aliyekuwa na miezi nane tu kwenye uongozi wake kutokana na kutokujuwa vema nini maana ya urais wa marekani uchumi ukaanguka, siku ambayo wao waliyoitaja kama jumanne nyeusi hali ilikuwa mbaya zaidi 0.75 walipoteza ajira.
Sababu kubwa ya Herbert Hoover kushindwa ni kufa kwa ununuzi wa hisa (New york stock exchange) ambayo ilipelekea watu kuchukuwa pesa zao kwenye mabenki na kufirisika kitendo ambacho kilipelekea wamerikani kumkataa rais HERBERT HOOVER.
View attachment 441037
Utawala wa herbert hoover ni wazi mambo yalionekana kuwa mabaya katika maeneo mengi muhimu kwa uchumi wa Marekani. Ni wamarekani ndio waliyofahamu kuwa Hoover mambo kwake alikuwa mabaya lakini kwa Tanzania mambo tofauti sio kama watu makini hawapo la, ni wajinga wengi sana kuliko watu makini na ndio sababu kubwa ambayo CCM wanayotumia.
View attachment 441038
Rais Herbert Hoover.
Mwaka 1929 akaja mkombozi wa uchumi wa marekani rais Franklin Delano Roosevelt na kauli yake "The only thing we have to fear is fear itself".
View attachment 441043
Mipango madhubuti ya rais Franklin delano roosevelt baada ya kuwa rais mwaka 1929
1. Nafuu(Relief): Alitoa pesa kusaidia wazee wasio na ajira.
2. Akafanya mabadiliko katika sector tofauti tofauti miongoni ni mabenk akazipa mitaji ili kurejesha matumaini kwa wananchi kutunza hela zao kwenye mabenk.
3. Rais franklin alitoa ajira kwa vijana.
4. Kutengeneza uhusiano mzuri wa wafanya kazi na waajiri wao ili kuteta ufanisi wa kazi hatimae marekani ikawa kubwa tena kwa uchumi.
View attachment 441059
The only thing we have to fear is fear itself.
View attachment 441060
It is common sense to take a method and try it. If it fails, admit it frankly and try another. But above all, try something.
RAIS JOHN POMBE MAGUFULI.
View attachment 441063
Utawala wa rais John Pombe Magufuli una zaidi ya mwaka moja na miezi kadhaa madarakani. Kama taifa, hatuwezi kuendelea na fungate (honeymoon) ya utawala wake wakati ni wazi mambo yanaonekana kuwa mabaya katika maeneo mengi muhimu kwa uchumi wa Tanzania.
Ufike wakati sasa tuanze kizungumzia mambo mazito yanayotukabili kama taifa.
Magufuli atambue kuwa hata Mungu mwenyewe alianza na mwanga
"Mungu akasema, iwe nuru, ikawa nuru. Mungu akaiona nuru na giza. Mungu akaiita nuru mchana, na giza akaiita usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya kwanza"
Ni maneno kutoka katika kitabu cha mwanzo(1: 3~5)
Tunatakiwa kufikiria kwamba tunaweza kuumizwa na tunaweza kujiumiza wenyewe, Magufuli anatakiwa kuambiwa kuwa safari yake ni ngumu katika uchumi.
Note: Magufuli utashi wa kisiasa ni muhimu katika kuendesha taifa.
Mipango ya rais Herbert ni sawa na mipango ya Magufuli.
Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu.
By mr mkiki
AsanteHii ni analogy nzuri sana. Kuweka kumbukumbu sawa ni kwamba Rais Rooservelt aliingia madarakani mwaka 1933.
Rais Rooservelt ndiye alikuwa muasisi wa utaratibu wa tathmini ya siku 100 za rais kukaa madarakani. Katika siku zake 100 madarakani, Rooservelt alipeleka miswada 13 ya sheria bungeni.
Mabadiliko makubwa aliyoyasimamia Rooservelt aliyapa jina "The new deal", ikiwa ni pamoja na kuachana na sera za uchumi zilizotokana na nadharia za Adam Smith (Classical Economic Theory) ambazo zilikiwa zinajali tu matajiri na wawekezaji na akakumbatia nadharia za kiuchimi za John Keynes zilizosisitiza serikali kuratibu shughuli za kiuchumi ili manufaa ya kustawi kwa uchumi yawanufaishe wote.
Ni wakati wa urais wa Rooservelt ndipo taasisi imara za kiuchumi (kama CMSA, FCC, nk) zolipoanzishwa huko Marekani na kuliwezesha hili taifa kuwa kinara duniani kiuchumi.
Haya yaliwezekana kwa Rooservelt kwa kuwa alikuwa na muongozo wa imani ya kiikadi kisiasa, pamoja na mrengo wa kiuchumi, ambavyo vilimpa dira ya kufanya aliyoyafanya na kufanikiwa.
Hizi sifa Magufuli hana. Ni vyema akatumia zaidi washauri wake wa kiuchimi na kuachana na kutafuta umaarufu. Awe strategist zaidi.
YaniSifa za mtu asiyeweza kujifunza
1.Kutokuwa na kumbukumbu aka historia
2.Kiburi
3.kupenda sifa (huwexi kuuliza utaonekana dhaifu)
4.kuwamiongoni mwa wajinga kuliko wewe
5. Kuwa miongoni mwa wanafiki
Pole sana....Ina maana nchi inavyoangamia ktk Hali ya kawaida huoni...au mwenzetu uko stockhomUlitakiwa useme ni Mambo gani unayaona hayapo vizuri kwa utawala huu.
Kwa sababu, Mishahara analipa kama kawaida, yeye anataka kodi yake tu halali ilipwe.
Labda useme kwamba, Rais alegeze masharti ya kuweka fedha kwenye Bank Binafsi ili watu na makampuni wakope, hapa Rais anaweza kukaa na jopo lake na kuandaa utaratibu mzuri wa kuzitoa Fedha BOT na kuzipeleka kwenye Mabank binafsi huku BOT ikizi-monitor lakini Bank nazo lazima zidai kwanza madeni yao toka kwa waliowakopesha.
Mimi sioni tatizo lolote juu ya Utawala wa JPM Zaidi ya kusikia malalamiko ya watu kuwa hakuna pesa mifukoni.
Upata hela ya kulaUchumi unaomaanisha ni upi? Maana siye wenye maisha ya chini tunaona mambo yanaenda tu hela ya kula hatukosi, sasa wanaolia wengi ni wale waliozoea kupata hela ambazo hawakuzistahili na ndo maana matumizi yake yalikuwa ya kutapanya, mfano watu walikuwa na nyumba ndogo wanazihudumia kwa kila kitu Magufuli kaja kawabana wote wamerudi njia kuu. Sasa michepuko lazima iseme uchumi kwa sababu walizoea kulishwa. Hakuna uchumi utakaotetereka tupige kazi kwa bidii.