Jumanne nyeusi kwa Rais Magufuli inakuja

Ukiwa muajiriwa una uhakika wa mshahara na hautoona utofauti wowote. Kwa wafanya biashara ndio wanajua hali halisi ya uchumi.
Mfanyabiashara ndio anajua hali ya uchumi wa nchi ukoje na sio muajiriwa anaetegemea mshahara wa mwisho wa mwezi.
Nenda kariakoo ukaulize hali ya biashara ikoje ndio utajua.
Kuna watu ni narrow mindedness, yaani yeye akiona mshahara tu, anadhani we are doing better economically. Kwa mawazo haya tutaendelea kuwa taifa la Wadanganyika kwa karne nyngne zijazo.
Tumekuwa subjective wa ushabiki wa kivyama na kuondoa hali ya objectivity katika fikra zetu. No concrete argument

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesema Tanzania wajinga ni wengi kuliko werevu. Hivyo jipe Moyo maana utakashfiwa sana.

Umefanya a splendid analysis, but JF of nowadays is full of retarded guys
 
Kuwa wazi ni nini anachofanya kinaua uchumi. Mimi naona juhudi kubwa za kuinua uchumi;
  1. Kupunguza kodi kwenye mazao ya Kilimo ili kuinua uzalishaji wa Kilimo
  2. Kudhibiti wizi kwenye pembejeo za kilimo na kudhibiti viwatirifu feki ili kuongeza tija ya kilimo
  3. Kutoa elimu bure mpaka sekondari na kuongeza bajeti ya mikopo elimu ya juu. Faida ya elimu inajulikana kwa uchumi wa Tanzania.
  4. Kuongeza bajeti ya madawa na kusimamia huduma bora mahospitalini
  5. Kusimamia uwajibika wa sekta ya umma kwa kiasi kikubwa.
  6. Kudhibiti rushwa na uhujumu uchumi
  7. Kuongeza kupatikana kwa huduma ya maji na umeme kwa watanzania wengi zaidi.
  8. Kusimamia UKUSANYAJI WA KODI kwa mujibu wa Sheria. Na hapa najua ndiyo chanzo cha tatizo kwa walalamikaji wasio makini.
  9. Kujenga barabara za lami.
  10. Kujenga reli SGR
  11. Kujenga fly over nk
  12. Kununua ndege ili kurahisisha usafiri ndani ya nchi na nje ya nchi hivyo kukuza utalipia.
  13. Kuhimiza na kusimamia uchumi wa viwanda ili kuongeza ajira na kukuza uchumi.
Na matokeo ya haya yote ni kuimarika kwa uchumi. Vigezo vinavyokubalika vya kiuchumi vinaonyesha uchumi wetu unafanya vizuri. Tz nimiongoni mwa nchi chache duniani zenye uchumi unakuwa kwa kasi. Mfumo wa bei umepungua kwa kiasi kikubwa.

Tatizo ninalo liona mimi ni watu ambao walikuwa hawana mazoea ya kulipia kodi kubanwa kulipa kodi. Hakuna nchi yeyote iliyoendelea ambayo hawasimamii ukusanyaji wa kodi, ikiwemo nchi uliyotolea mfano.
Badala ya kuendeleza siasa za kupinga kila kitu na kujenga hofu katika Jamii, tuwe wakweli kwa kutambua nia ya dhati na kuchangia kiustaarabu kwenye sera, sheria, mipango na utekelezaji wake.
 
Umetumia muda mwingi kuandika mambo mengi ambayo hayana uhusiano kabisa, sasa Tanzania itakuwaje na anguko la Uchumi? Uchumi upi huo uliokuwa nao TZ mpaka ipate anguko la uchumi?

Nchi ya GDP ya chini 45 Billion (US) tu na watu zaidi ya milioni 40, halafu unaongelea anguko la uchumi kana kwamba sasa hivi kuna kupanda kwa uchumi au kumeshawahi kuwepo na Uchumi mkubwa hadi uongelee anguko la Uchumi?
utawajua tu wajunga alionena mkiki
 
Majizi sasa hivi yanahangaika sana.Wanakuja na mifano mingine hata haina uhusiano.Kama kuiba ni lazima mwemde mkajiibie wenyewe katika yale ambayo mlishakwapua.Mambo ya Marekani hapa ni ngojera.Ngojeni serikali ifanye kazi.
 
Umetumia muda mwingi kuandika mambo mengi ambayo hayana uhusiano kabisa, sasa Tanzania itakuwaje na anguko la Uchumi? Uchumi upi huo uliokuwa nao TZ mpaka ipate anguko la uchumi?

Nchi ya GDP ya chini 45 Billion (US) tu na watu zaidi ya milioni 40, halafu unaongelea anguko la uchumi kana kwamba sasa hivi kuna kupanda kwa uchumi au kumeshawahi kuwepo na Uchumi mkubwa hadi uongelee anguko la Uchumi?
Maskini hafirisiki maana hana kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ANGUKO LA UCHUMI KWA TAIFA LA MAREKANI (1929~1933)

Aliyeitwa Herbert hoover aliyekuwa na miezi nane tu kwenye uongozi wake kutokana na kutokujuwa vema nini maana ya urais wa marekani uchumi ukaanguka, siku ambayo wao waliyoitaja kama jumanne nyeusi hali ilikuwa mbaya zaidi 0.75 walipoteza ajira.

Sababu kubwa ya Herbert Hoover kushindwa ni kufa kwa ununuzi wa hisa (New york stock exchange) ambayo ilipelekea watu kuchukuwa pesa zao kwenye mabenki na kufirisika kitendo ambacho kilipelekea wamerikani kumkataa rais HERBERT HOOVER.

View attachment 441037
Utawala wa herbert hoover ni wazi mambo yalionekana kuwa mabaya katika maeneo mengi muhimu kwa uchumi wa Marekani. Ni wamarekani ndio waliyofahamu kuwa Hoover mambo kwake alikuwa mabaya lakini kwa Tanzania mambo tofauti sio kama watu makini hawapo la, ni wajinga wengi sana kuliko watu makini na ndio sababu kubwa ambayo CCM wanayotumia.

View attachment 441038
Rais Herbert Hoover.

Mwaka 1929 akaja mkombozi wa uchumi wa marekani rais Franklin Delano Roosevelt na kauli yake "The only thing we have to fear is fear itself".

View attachment 441043

Mipango madhubuti ya rais Franklin delano roosevelt baada ya kuwa rais mwaka 1929

1. Nafuu(Relief): Alitoa pesa kusaidia wazee wasio na ajira.

2. Akafanya mabadiliko katika sector tofauti tofauti miongoni ni mabenk akazipa mitaji ili kurejesha matumaini kwa wananchi kutunza hela zao kwenye mabenk.

3. Rais franklin alitoa ajira kwa vijana.

4. Kutengeneza uhusiano mzuri wa wafanya kazi na waajiri wao ili kuteta ufanisi wa kazi hatimae marekani ikawa kubwa tena kwa uchumi.

View attachment 441059
The only thing we have to fear is fear itself.

View attachment 441060
It is common sense to take a method and try it. If it fails, admit it frankly and try another. But above all, try something.

RAIS JOHN POMBE MAGUFULI.

View attachment 441063

Utawala wa rais John Pombe Magufuli una zaidi ya mwaka moja na miezi kadhaa madarakani. Kama taifa, hatuwezi kuendelea na fungate (honeymoon) ya utawala wake wakati ni wazi mambo yanaonekana kuwa mabaya katika maeneo mengi muhimu kwa uchumi wa Tanzania.

Ufike wakati sasa tuanze kizungumzia mambo mazito yanayotukabili kama taifa.

Magufuli atambue kuwa hata Mungu mwenyewe alianza na mwanga

"Mungu akasema, iwe nuru, ikawa nuru. Mungu akaiona nuru na giza. Mungu akaiita nuru mchana, na giza akaiita usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya kwanza"

Ni maneno kutoka katika kitabu cha mwanzo(1: 3~5)

Tunatakiwa kufikiria kwamba tunaweza kuumizwa na tunaweza kujiumiza wenyewe, Magufuli anatakiwa kuambiwa kuwa safari yake ni ngumu katika uchumi.

Note: Magufuli utashi wa kisiasa ni muhimu katika kuendesha taifa.

Mipango ya rais Herbert ni sawa na mipango ya Magufuli.

Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu.

By mr mkiki
Kumbe wenye akili badompo, very good analysis huyu kichaa anatupoteza na wanachelewa kumgundua
 
Huyu Dalali na yeye mnamuamini?
Hashim Rungwe : "Tatizo la Rais ni kuonyesha tabia zake kuliko utendaji wake, kuna mambo ambayo anatakiwa kuyafanya na familia yake au rafiki zake yeye anayafanya kwenye taasisi ya Urais"
 
IMG_20170813_150427.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ANGUKO LA UCHUMI KWA TAIFA LA MAREKANI (1929~1933)

Aliyeitwa Herbert hoover aliyekuwa na miezi nane tu kwenye uongozi wake kutokana na kutokujuwa vema nini maana ya urais wa marekani uchumi ukaanguka, siku ambayo wao waliyoitaja kama jumanne nyeusi hali ilikuwa mbaya zaidi 0.75 walipoteza ajira.

Sababu kubwa ya Herbert Hoover kushindwa ni kufa kwa ununuzi wa hisa (New york stock exchange) ambayo ilipelekea watu kuchukuwa pesa zao kwenye mabenki na kufirisika kitendo ambacho kilipelekea wamerikani kumkataa rais HERBERT HOOVER.

View attachment 441037
Utawala wa herbert hoover ni wazi mambo yalionekana kuwa mabaya katika maeneo mengi muhimu kwa uchumi wa Marekani. Ni wamarekani ndio waliyofahamu kuwa Hoover mambo kwake alikuwa mabaya lakini kwa Tanzania mambo tofauti sio kama watu makini hawapo la, ni wajinga wengi sana kuliko watu makini na ndio sababu kubwa ambayo CCM wanayotumia.

View attachment 441038
Rais Herbert Hoover.

Mwaka 1929 akaja mkombozi wa uchumi wa marekani rais Franklin Delano Roosevelt na kauli yake "The only thing we have to fear is fear itself".

View attachment 441043

Mipango madhubuti ya rais Franklin delano roosevelt baada ya kuwa rais mwaka 1929

1. Nafuu(Relief): Alitoa pesa kusaidia wazee wasio na ajira.

2. Akafanya mabadiliko katika sector tofauti tofauti miongoni ni mabenk akazipa mitaji ili kurejesha matumaini kwa wananchi kutunza hela zao kwenye mabenk.

3. Rais franklin alitoa ajira kwa vijana.

4. Kutengeneza uhusiano mzuri wa wafanya kazi na waajiri wao ili kuteta ufanisi wa kazi hatimae marekani ikawa kubwa tena kwa uchumi.

View attachment 441059
The only thing we have to fear is fear itself.

View attachment 441060
It is common sense to take a method and try it. If it fails, admit it frankly and try another. But above all, try something.

RAIS JOHN POMBE MAGUFULI.

View attachment 441063

Utawala wa rais John Pombe Magufuli una zaidi ya mwaka moja na miezi kadhaa madarakani. Kama taifa, hatuwezi kuendelea na fungate (honeymoon) ya utawala wake wakati ni wazi mambo yanaonekana kuwa mabaya katika maeneo mengi muhimu kwa uchumi wa Tanzania.

Ufike wakati sasa tuanze kizungumzia mambo mazito yanayotukabili kama taifa.

Magufuli atambue kuwa hata Mungu mwenyewe alianza na mwanga

"Mungu akasema, iwe nuru, ikawa nuru. Mungu akaiona nuru na giza. Mungu akaiita nuru mchana, na giza akaiita usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya kwanza"

Ni maneno kutoka katika kitabu cha mwanzo(1: 3~5)

Tunatakiwa kufikiria kwamba tunaweza kuumizwa na tunaweza kujiumiza wenyewe, Magufuli anatakiwa kuambiwa kuwa safari yake ni ngumu katika uchumi.

Note: Magufuli utashi wa kisiasa ni muhimu katika kuendesha taifa.

Mipango ya rais Herbert ni sawa na mipango ya Magufuli.

Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu.

By mr mkiki
 
Kama mtu huwezi kujua umasikini nini na mzunguko wake basi kuelewa economic development and growth is hardest thing to understand.

"Mimba ikikomaa mtoto huzaliwa na kupewa jina jipya"
 
Hapa kuna hoja. Watanzania wasomi na wasio wasomi tuna taarifa kidogo sana kuhusu uchumi na maendeleo katika taifa letu.

Uchumi wetu haujawahi kusimama, siku zote umelala kama sio kuwa shimoni kabisa.

Umaskini uliyojimbia mizizi kwenye kaya zetu unatoa ushuhuda kuwa uchumi wetu hauwezi kuanguka bali kufa kabisa.

Badala ya kutafuta namna ya kila raia kujua kuwa hali ya uchumi wetu ni mbaya sana na tunapaswa kufanya kazi kwa weledi ili tuweze kuuinua uchumi kutoka ulikolala, tunafanya kazi ya kuwapumbaza kwa sifa nyingi na kujifanya wakombozi wa wanyonge.

Hakuna mtu yeyote anayeweza kuwakomboa wanyonge, bali wanyonge wenyewe.
Kiongozi bora anaweza kuwasaidia wanyonge kujikomboa.

Landson Tz
 
Ulitakiwa useme ni Mambo gani unayaona hayapo vizuri kwa utawala huu.

Kwa sababu, Mishahara analipa kama kawaida, yeye anataka kodi yake tu halali ilipwe.

Labda useme kwamba, Rais alegeze masharti ya kuweka fedha kwenye Bank Binafsi ili watu na makampuni wakope, hapa Rais anaweza kukaa na jopo lake na kuandaa utaratibu mzuri wa kuzitoa Fedha BOT na kuzipeleka kwenye Mabank binafsi huku BOT ikizi-monitor lakini Bank nazo lazima zidai kwanza madeni yao toka kwa waliowakopesha.

Mimi sioni tatizo lolote juu ya Utawala wa JPM Zaidi ya kusikia malalamiko ya watu kuwa hakuna pesa mifukoni.

Rafiki huoni kwa sababu hutaki kuona au??
1. watu wamevunjiwa nyumba zao bila FIDIA huku wakiwa na zuio la mahakama Mkononi, huoni tuu?

2. Huoni wafanyakazi wa umma hawapandi madara kwa kuwa eti kuna uhakiki?

3. Huoni KODI za ajabu ajabu zinazotozwa na TRA hadi watu wameshindwa wameamua kufunga maduka K'Koo, pita K'Koo leo utaelewa ninachomaanisha. Duka la bidhaa za kawaida mtaani tulikuwa tunalipa sh elfu 70, leo hii unatakiwa kulipa laki 3??

4. Huoni Wakuu wa Wilaya wakitumia vibaya madaraka yao bila kukemewa? Viongozi hasa wa upinzani wanawekwa ndani kila kukicha eti kwa kuwa mkuu huyo anamamlaka ya kuweka ndani masaa 48, huoni tuu, Bulaya, Mdee, walikuwa na makosa gani ya kuhatarisha usalama wa raia? Huoni tuu

5. Nani anamamlaka ya kuvuzuia shughuli za vyama vya siasa ambazo ziko halali kikatiba? Hali iko je ? Huoni tuu!!

6. Watu wametekwa, wengine wamepotea kabisa hadi leo, Vitu vya radio vinavamiwa, Ofisi za wanasheria zinalipuliwa usiku, nani umesikia akikemea vitendo hivi kwa DHATI ya moyo??

7. Watanzania wananyang'anywa mashamba yao waliyomilikishwa kwa kufuata taratibu zote, kwani ardhi imekwisha?? Mazao, mboga vinafyekwa kwenye bustani ya Mbowe ni sawa? Vitendo hivi vinajenga chuki, Huoni tatizo hapo?

Yapo mengi sana yanayotia dowa Utamaduni wetu wa kindugu ambayo lazima yaangaliwe vema. Hapo sijataja matumizi ya fedha za umma kwa kuzingatia sheria za fedha; utumbuaji usiyozingatia sheria unavyoiletea serikali mazigo wa kulipa mishahara kwa waliotumbuliwa na waliopewa nafasi n.k
 
Kumlinganisha Rais Hoover na kuanguka kwa uchumi wakati wa kipindi chake na Rais Magufuli katika kipindi chake hiki cha kurekebisha uchumi ni kutoitendea haki historia.

Nina mashaka inawezekana mtoa post hukusoma somo la Historia katika elimu yako. Kama ungelisoma, ungelijua sababu za kuanguka uchumi enzi za Hoover.

Vilevile, ungelijua na kuoanisha hatua alizochukua Rais Roosevelt kupitia kauli mbiu yake ya 'NEW DEAL' kufufua uchumi zinafanana na za Rais Magufuli kupitia kauli mbiu yake ya 'HAPA KAZI TU'.
Unapokosoa uweke maoni yako basi ili tujue wewe unaelewa nini ua unataka tujue nini?? Aaahh!!
 
Franklin Delano Roosevelt he was stricken with polio at the age 39 ila mgonjwa huyu wa polio alifanya vitu vikubwa kuliko bwana yule mpiga push up kama pono

Misingi aliyoiweka Delano marekani matunda yake yanaonekana mpaka Leo aliweza kupigana vita ya uchumi ilyo kuwa imeikumba dunia 1929-1933..great depression Kwa marekani,economic slump Britain ,die crises for German

Sasa hili limister miguvu with hollowhead + gubashitelism onyoo kama vijampo

Don't mind me
 
Hivi mtu anaposema kwamba mambo kila sehemu ni mabaya huwa anazingatia vitu gani? Naomba kufahamishwa hilo kwanza. Pili lini Tanzania ilikuwa na uchumi mkubwa mpaka kupelekea mtu /kikundi cha watu kusema uchumi unashuka? Au ndiyo kusema kwamba mtu hana sera za kuandika anaamua kuandika utumbo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiwa muajiriwa una uhakika wa mshahara na hautoona utofauti wowote. Kwa wafanya biashara ndio wanajua hali halisi ya uchumi.
Mfanyabiashara ndio anajua hali ya uchumi wa nchi ukoje na sio muajiriwa anaetegemea mshahara wa mwisho wa mwezi.
Nenda kariakoo ukaulize hali ya biashara ikoje ndio utajua.
Ni lini mfanyabiashara akasema ukweli??? Tuwe wakweli ss wafanyabiashara wa Tz hatuna mazoea ya kulipa kodi stahili tumezoea ujanjaujanja tu sasa tunapolazimishwa tutimize wajibu wetu ndio vita yote hii Inaanza!!!!!!!!!!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom