Jumanne nyeusi kwa Rais Samia inakuja

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
ANGUKO LA UCHUMI KWA TAIFA LA MAREKANI (1929~1933)

Aliyeitwa Herbert hoover aliyekuwa na miezi nane tu kwenye uongozi wake kutokana na kutokujuwa vema nini maana ya urais wa marekani uchumi ukaanguka, siku ambayo wao waliyoitaja kama jumanne nyeusi hali ilikuwa mbaya zaidi 0.75 walipoteza ajira.

Sababu kubwa ya Herbert Hoover kushindwa ni kufa kwa ununuzi wa hisa (New york stock exchange) ambayo ilipelekea watu kuchukuwa pesa zao kwenye mabenki na kufirisika kitendo ambacho kilipelekea wamerikani kumkataa rais HERBERT HOOVER.

herbert hoover.jpg

Utawala wa herbert hoover ni wazi mambo yalionekana kuwa mabaya katika maeneo mengi muhimu kwa uchumi wa Marekani. Ni wamarekani ndio waliyofahamu kuwa Hoover mambo kwake alikuwa mabaya lakini kwa Tanzania mambo tofauti sio kama watu makini hawapo la, ni wajinga wengi sana kuliko watu makini na ndio sababu kubwa ambayo CCM wanayotumia.

heho_hoover_london_treaty_1930.jpg

Rais Herbert Hoover.

Mwaka 1929 akaja mkombozi wa uchumi wa marekani rais Franklin Delano Roosevelt na kauli yake "The only thing we have to fear is fear itself".

32_franklin_d_roosevelt.jpg

Mipango madhubuti ya rais Franklin delano roosevelt baada ya kuwa rais mwaka 1929

1. Nafuu(Relief): Alitoa pesa kusaidia wazee wasio na ajira.

2. Akafanya mabadiliko katika sector tofauti tofauti miongoni ni mabenk akazipa mitaji ili kurejesha matumaini kwa wananchi kutunza hela zao kwenye mabenk.

3. Rais franklin alitoa ajira kwa vijana.

4. Kutengeneza uhusiano mzuri wa wafanya kazi na waajiri wao ili kuteta ufanisi wa kazi hatimae marekani ikawa kubwa tena kwa uchumi.

Franklin_D_Roosevelt_Quotations.jpg

The only thing we have to fear is fear itself.

Quote-Franklin-D.-Roosevelt.png

It is common sense to take a method and try it. If it fails, admit it frankly and try another. But above all, try something.

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

NCHI KUKOPA Vs DENI LA TAIFA.
Ubaya wa jambo hili hauwezi kuonekana na watu wajinga.

Job Ndugai alisema mkopo wa fedha wa Sh1.3 trilioni kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) ili kukabiliana na athari za kiuchumi za COVID-19 (ambazo walizipeleka kusikoonekana), malipo na riba ya mkopo huo ni Sh10 trilioni.

Hakuna Binadamu yoyote ambaye anasema kukopa ni KOSA. Tatizo la Rais SAMIA hajui mambo haya.
-Mikopo wako wa aina gani?
-Masharti yake je?, yapo vipi?
-Dhamana yake ni nini?
-Mikopo hiyo kwa shughuli gani?
-Shughuli hizo zina tija kwa raia?

Utawala wa Magufuli na Samia kwa miaka 7 umekopa zaidi ya utawala wowote hapa Tanzania.

UMEME NA MAJI NCHINI
Mgao wa umeme ni mkali sana chini ya utawala wa Samia Suluhu Hassan na January Yusuf Makamba.

Mgao wa maji ni mkali sana chini ya utawala wa Samia Suluhu Hassan na Aweso.

UMASIKINI WA MAWAZO NI UMASIKINI KUPITA UMASIKINI WOTE- BY J.K.NYERERE (R.I.P)

Hawa CCM wamekufa kimawazo , lakini ni sisi Raia ndio tutaweza kuliweka Taifa salama.

Utawala wa rais SAMIA una zaidi ya miaka na miezi kadhaa madarakani. Kama taifa, hatuwezi kuendelea na fungate (honeymoon) ya utawala wake wakati ni wazi mambo yanaonekana kuwa mabaya katika maeneo mengi muhimu kwa uchumi wa Tanzania.

Ufike wakati sasa tuanze kizungumzia mambo mazito yanayotukabili kama taifa.

Mamia atambue kuwa hata Mungu mwenyewe alianza na mwanga

"Mungu akasema, iwe nuru, ikawa nuru. Mungu akaiona nuru na giza. Mungu akaiita nuru mchana, na giza akaiita usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya kwanza"

Ni maneno kutoka katika kitabu cha mwanzo(1: 3~5)
Tunatakiwa kufikiria kwamba tunaweza kuumizwa na tunaweza kujiumiza wenyewe, Samia anatakiwa kuambiwa kuwa safari yake ni ngumu katika uchumi.

Note: Magufuli utashi wa kisiasa ni muhimu katika kuendesha taifa.
Mipango ya rais Herbert ni sawa na mipango ya Samia na Nchemba.

By mr mkiki
 
Uchumi wanaouendesha hangaya na madelu unaning'inia kwenye ncha, haishangazi ajira mpya na maslahi ya watumishi kusimama kubana wagebill ili zibaki pesa za kutosha kulipa madeni na kwa ajili ya wao kulamba asali.........tafsiri yake ni kwamba huduma muhimu za kijamii ikiwemo afya na elimu zitadorora kwani watumishi hawatoshi na waliopo morale ipo chini kutokana na maslahi duni, umaskini na ufukara unaenda kutamalaki kwenye jamii maana hakuna ajira wala pesa kwenye mzunguko, zimeenda kulipa madeni.......kumbuka kwamba sekta binafsi ni kama imekufa na hivyo haina nguvu kubwa ya kusukuma uchumi.​
 
E6403BCB-9306-45DF-935D-F89CB6E6234C.jpeg

Duru za kisiasa zimebainisha kuwa Kauli zenye matamshi makali kutoka kwa aliekua Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai zinashangaza kutokana na taswira aliyoijenga kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita akiwa hajawahi kukinzana na aliyekuwa rais wa nchi hiyo John Magufuli aliyefariki dunia Machi 2021 na kulifanya Bunge kuonekana kukosa nguvu itokanayo na mamlaka yake ya Kikatiba ya kuisimamia na kuishauri serikali.

Kwa kipindi hicho cha zaidi ya miaka mitano Bunge lilidhibitiwa na uongozi wa Magufuli kupitia uongozi wa Bunge na kwa kiasi kikubwa kuwafanya wabunge kutokuwa huru vya kutosha kushauri, kukosoa na kupendekeza mambo ya uendeshaji wa taifa hilo.

Ifahamike chanzo cha mjadala huu ni mkopo uliopokewa na serikali kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) wa shilingi trilioni 1.3 ambazo zimeelekezwa kutekeleza miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, vituo vya afya na huduma nyinginezo.

NUKUU:
Kama walidhani kutakuwa kuna kusimamishwa miradi ili wapate la kusema, halipo. Kuna jitihada za kutuvunja moyo kwenye mkopo, hakuna nchi isiyokopa, tutakopa tumalize miradi ya maendeleo ili tuendelee kwa sababu ukikopa unajenga sasa kwa haraka na kuharakisha maendeleo na mikopo hii ni ya miaka 20 kwahiyo tutakopa na tutalipa taratibu," alisema Rais Samia”

Hali hii inaweza kuongeza wasiwasi juu ya uhalisia wa tarakimu za kiuchumi zilizoko hadharani dhidi ya kile kinachoongelewa na viongozi wawili hawa. Hali hii sio nzuri sana kwa mitaji tunayovutia kutoka nje na kwa ndani inaweza kuwa kichocheo cha kuhamishwa mitaji.

"Jambo lingine ni kusambaa kwa taarifa mbaya juu ya uchumi nje ya uchumi wetu. Katika uchumi hali hiyo tunaita 'Narrative Economics. Kauli za hawa viongozi hadharani zinasambaa duniani na kuleta wasiwasi kwa taasisi za fedha.

Miaka kati ya 2012-2017 ilionekana kuwa kampuni zilitumia migogoro ya aina hii kwenye mataifa zaidi ya 8 kubaini ukweli tofauti na taarifa walizokuwa wanapata. Hii inaweza kuhalalisha hoja ya nchi za magharibi kwamba nchi zenye urafiki na China kiuchumi zina kasumba ya kutokutoa takwimu za kweli kuhusu madeni ya taifa."
 
Mnamuandama mama wa watu bure tu pamoja na comred madelu, tupeni records za tawala zote, je ni tawala ipi deni lilikua Kwa kushuka chini? Nchi hii tangu utawala wa Nyerere deni limekuwa likipanda at progress form, mjue pia kulinganisha vitu Kwa uwiano, population inaongezeka na ukubwa wa serikali pia unaongezeka so kama hivyo vitu vinaongezeka automatically na deni lazima liongezeke.
 
Wewe Ni mpotoshaji unayetamani serikali yetu ishindwe lakini kwa bahati mbaya Ni kuwa utashindwa mwenyewe na propaganda zako hizo za kizamani.

Tuletee na kutuwekea hapa ushahidi wako wa kinyaraka unaonyesha mkopo wa Tlioni moja riba take Ni Tlioni kumi,Naomba utuwekee hapa maana Hilo tu linefufisha hoja zako zote za mchongo na zisizo na nguvu ya kiuhalisia au kitakwimu.

Suala la ajira kwa vijana,Hapa sijajuwa unaishi wapi maana naona huna Takwimu sahihi ya kinachoendelea nchini mwetu,kwa sababu inafahamika kuwa mh Rais wetu mpendwa mama Samia alipoingia madarakani alitoa maelfu ya ajira kwa vijana Katika secta zote zikiongozwa na secta ya Elimu na Afya zilizokuwa na idadi kubwa ya nafasi za ajira, ajira hizi kwa pamoja katika secta zote ziliffikia Elfu 42.

Lakini pia mh Rais Amejenga miradi mbalimbali katika secta ya Elimu na Afya iliyosaidia kutoa ajira mbalimbali kwa vijana na watu mbalimbali ambao wote walikuwa Ni wazawa na hivyo kufanya fedha hizo kubaki mikononi mwa watanzania na kuingia mitaani na hivyo kusisimua uchumi wetu,

Mh Rais pia alitoa mabillioni ya Ruzuku katika mafuta na mbolea,mfano katika kilimo alitoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini na hivyo kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni na hivyo kuchochea uzalishaji wa mazao mbalimbali ,Ambayo kwa kiasi kikubwa yatachangia hata ukuaji wa secta ya viwanda kwa kuwepo kwa malighafi ya kutosha,lakini pia kumsaidia mkulima kujipatia kipato na hivyo kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wa watumishi wa umma namo mh Rais amefanya kazi kubwa Sana kwa kuboresha maslahi yao,maeneo ya kazi,kulipa malimbikizo ya madeni,kiwaongezea mishahara na malupu lupu mbalimbali,mfano ni ongezeko la 23% ya mshahara hasa kwa watumishi wa kipato Cha chini. Jambo ambalo liliongeza na kuchochea molari ya kufanya kazi kwa watumishi wa umma.

Mh Rais pia ameweja mazingira mazuri kwa secta binafsi ambapo Sasa Hali Ni nzuri na ndio sababu unasikia kila Siku biashara na uwekezaji unaongezeka badala ya kupungua, Biashara mpya zinafunguliwa kila Siku na kila Kona.

Kuhusu mikopo pia serikali yetu imekuwa Ina kopa na kuwekeza maeneo yenye tija,mfano reli ya kisasa itakayosaidia ubebaji wa mizigo mingi na hivyo kufungua fursa za kibiashara na u humi wetu,lakini pia kufanya bandari yetu kuwa bize muda wote na hivyo kuongeza mapato,lakini pia kusaidia Barabara zetu kutoharibika mapema kutokana na kupitishwa kwa mizigo mizito, na kuongezeka kwa mapato pia hasa kupitia bandari yetu ya Dar.

Pia mradi wa bwawa la Nyerere ukamilikaji wake utakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa letu kwa kuwa itasaidia upatikanaji wa umeme wa kutosha na kwa Bei nafuu,Hali itakayo saidia ongezeko la viwanda vya aina mbalimbali hapa nchini,lakini pia kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi kwa vijana hasa maeneo ya vijijini.

Habari za mgao wa umeme na maji,hapa bila Shaka ulikuwa usingizini,maana kwa Sasa Hali Ni njema Sana na hakuna hayo au changamoto hizo ,maana ilikuwa Ni kwa kipindi kifupi tu kilichokuwa kimetokana na changamoto ya ukame,lakini kwa Sasa serikali yetu imejipanga vyema na Hali IPO Kama kawaida huku watu wakiendelea na kazi
 
ANGUKO LA UCHUMI KWA TAIFA LA MAREKANI (1929~1933)

Aliyeitwa Herbert hoover aliyekuwa na miezi nane tu kwenye uongozi wake kutokana na kutokujuwa vema nini maana ya urais wa marekani uchumi ukaanguka, siku ambayo wao waliyoitaja kama jumanne nyeusi hali ilikuwa mbaya zaidi 0.75 walipoteza ajira.

Sababu kubwa ya Herbert Hoover kushindwa ni kufa kwa ununuzi wa hisa (New york stock exchange) ambayo ilipelekea watu kuchukuwa pesa zao kwenye mabenki na kufirisika kitendo ambacho kilipelekea wamerikani kumkataa rais HERBERT HOOVER.

herbert hoover.jpg

Utawala wa herbert hoover ni wazi mambo yalionekana kuwa mabaya katika maeneo mengi muhimu kwa uchumi wa Marekani. Ni wamarekani ndio waliyofahamu kuwa Hoover mambo kwake alikuwa mabaya lakini kwa Tanzania mambo tofauti sio kama watu makini hawapo la, ni wajinga wengi sana kuliko watu makini na ndio sababu kubwa ambayo CCM wanayotumia.

heho_hoover_london_treaty_1930.jpg

Rais Herbert Hoover.

Mwaka 1929 akaja mkombozi wa uchumi wa marekani rais Franklin Delano Roosevelt na kauli yake "The only thing we have to fear is fear itself".

32_franklin_d_roosevelt.jpg

Mipango madhubuti ya rais Franklin delano roosevelt baada ya kuwa rais mwaka 1929

1. Nafuu(Relief): Alitoa pesa kusaidia wazee wasio na ajira.

2. Akafanya mabadiliko katika sector tofauti tofauti miongoni ni mabenk akazipa mitaji ili kurejesha matumaini kwa wananchi kutunza hela zao kwenye mabenk.

3. Rais franklin alitoa ajira kwa vijana.

4. Kutengeneza uhusiano mzuri wa wafanya kazi na waajiri wao ili kuteta ufanisi wa kazi hatimae marekani ikawa kubwa tena kwa uchumi.

Franklin_D_Roosevelt_Quotations.jpg

The only thing we have to fear is fear itself.

Quote-Franklin-D.-Roosevelt.png

It is common sense to take a method and try it. If it fails, admit it frankly and try another. But above all, try something.

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

NCHI KUKOPA Vs DENI LA TAIFA.
Ubaya wa jambo hili hauwezi kuonekana na watu wajinga.

Job Ndugai alisema mkopo wa fedha wa Sh1.3 trilioni kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) ili kukabiliana na athari za kiuchumi za COVID-19 (ambazo walizipeleka kusikoonekana), malipo na riba ya mkopo huo ni Sh10 trilioni.

Hakuna Binadamu yoyote ambaye anasema kukopa ni KOSA. Tatizo la Rais SAMIA hajui mambo haya.
-Mikopo wako wa aina gani?
-Masharti yake je?, yapo vipi?
-Dhamana yake ni nini?
-Mikopo hiyo kwa shughuli gani?
-Shughuli hizo zina tija kwa raia?

Utawala wa Magufuli na Samia kwa miaka 7 umekopa zaidi ya utawala wowote hapa Tanzania.

UMEME NA MAJI NCHINI
Mgao wa umeme ni mkali sana chini ya utawala wa Samia Suluhu Hassan na January Yusuf Makamba.

Mgao wa maji ni mkali sana chini ya utawala wa Samia Suluhu Hassan na Aweso.

UMASIKINI WA MAWAZO NI UMASIKINI KUPITA UMASIKINI WOTE- BY J.K.NYERERE (R.I.P)

Hawa CCM wamekufa kimawazo , lakini ni sisi Raia ndio tutaweza kuliweka Taifa salama.

Utawala wa rais SAMIA una zaidi ya miaka na miezi kadhaa madarakani. Kama taifa, hatuwezi kuendelea na fungate (honeymoon) ya utawala wake wakati ni wazi mambo yanaonekana kuwa mabaya katika maeneo mengi muhimu kwa uchumi wa Tanzania.

Ufike wakati sasa tuanze kizungumzia mambo mazito yanayotukabili kama taifa.

Mamia atambue kuwa hata Mungu mwenyewe alianza na mwanga

"Mungu akasema, iwe nuru, ikawa nuru. Mungu akaiona nuru na giza. Mungu akaiita nuru mchana, na giza akaiita usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya kwanza"

Ni maneno kutoka katika kitabu cha mwanzo(1: 3~5)
Tunatakiwa kufikiria kwamba tunaweza kuumizwa na tunaweza kujiumiza wenyewe, Samia anatakiwa kuambiwa kuwa safari yake ni ngumu katika uchumi.

Note: Magufuli utashi wa kisiasa ni muhimu katika kuendesha taifa.
Mipango ya rais Herbert ni sawa na mipango ya Samia na Nchemba.

By mr mkiki

Maneno meeeengi lakini ujinga tuu..

Nchi zenye madeni makubwa wala.hazijafikia huko.ije kuwa Tanzania ambayo haijafikia hata nusu ya uwezo wake Wa kukopa?

Kati ya Nchi hizo zenye madeni makubwa ipi imepata hiyo Jumanne nyeusi? 😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom