Juliana Shonza ni hatari kuliko tunavyodhani

Juliana Shonza ni hatari kuliko tunavyodhani

nan umeona anahangaika nae? Anzia juu kusoma utaelewa. Mnataka kutuaminisha km yeye ni tishio, labda kwenu. Somen alama za nyakati, msilete ushabiki wa kisiasa tu.

Zipo post nyingi tu majuha wenzako kaa chini uzisome ndio utakapojua mnahangaika naye

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Napenda kuamini maneno ya Membe wakati fulani akisema kuwa wananchi wanabadilika ndani ya saa 24. Na hii inatokea kwa pande zote; yani hasi na chanya hivyo ni vyema kuchukua tahadhari mambo yasijegeukia upande hasi
 
Mbona kauli ni za kijuha? Tangu lini juha akafanyiwa tahadhari?

Chama
Gongo la mboto DSM

Kama juha hafanyiwi tahadhari mpe bunduki yenye risasi kisha mchekeechekee.
 
Juliana shonza ni mtu mwenye madhara madogo sana katika CDM. Kama Nape kazunguka tanzania nzima na mwisho amechoka lakini aibu haikumkosa. Who is juliana mpaka upate wasi kaka? Wanaanchi wamechoka na hawako tayari kusikiliza upuuzi wake na chama chake. wanachotaka ni kupata chama ambacho kitakuwa mkombozi wa taifa zima na si mkombozi wa matumbo ya familia chache tu kama ilivyo kwa chama twawala(CCM)
 
Awe makini tu hasikae karibu au kuwa kwenye room moja na Mwigulu, maana hatakubali kukatiza hivi hivi....Uliza ya Igunga. Kama ana mchumba duh kaliwa. Naamini Mwigulu anachekelea akiwa na moja yake kichwani baada ya kuona Shonza amerudi kwao.
 
Mkuu amini usiamini Nyerere akifufuka sasa hivi moja kwa moja atajiunga CHADEMA, maana ndio wenye sera murua za kiukombozi, hawezi kujichanganya na mafisadi CCM!!!
Hii ni kweli mkuu...sidhani kama yule mzee anaweza kuvumilia uozo uliomo ndni ya CCM kwa sasa.....
 
nyerere akifufuka akaipigia debe ccm akaruhusu watu wamuulize maswali kumi tu kuhusiana na uchafu wa ccm atakufa tena muda huo huo bila kujibu hata moja .big up
Ha ha ha mkuu umenichekesha sana...eti atakufa tena..dah.....
 
Ahsante kutujuza hayo na nivyema kutokudharau ushauri. To my opinion, watanzania walichokutana nacho utawala huu hawatajari tena uzuri wa mtu. I guess iyo ni mojawapo ya lessons learnt. Pili, timing ya masalia na jinsi walivyoondoka cdm haiwezi kuwa na impact yoyote kwa cdm. In fact imekuwa ni aibu kwa ccm- na mitego yao ya kizamani ktk kuangamiza upizani.

CCM wameshindwa kujua njia sahihi ktk siasa kuwa ni transparency and accountability. Kama hawawezi kulitambua ili njia itakayo salia kwao nikutumia utawala wa kimabavu/jeshi ili waendelea kulinda mali zao walizojichumia kwa njia zisizo halali na kuendeleza utawala wa kifamilia.
 
Kajitu kadogo kasikojulikana kataweza wapi kukata kisiki cha mpingo kwa kisu?kama wenye shoka wenyewe wameshindwa.
 
kwa sasa chadema inakubaliwa na watanzania wengi sana,huyu Juliana kaenda ccm kujimaliza,atajuta kama Nakaaya
 
Bado nasisistiza kina Shonza si wa kupuuzwa. Wako wengi hao na uharibifu ni rahisi zaidi kuliko ujenzi.
 
Hana uwezo! Hivi Tambwe Hiza yuko wapi???? Huyu dada kapotea njia. Angekuwa ametoka kivyake na si kwa kufukuzwa labda angekuwa na kitu kidogo. Kufukuzwa inaleta maswali mengi!!!!!!!!!! Kwa nini kafukuzwa!!! Je tuhuma alizonazo zina mahusiano yeyote na kule alikokimbilia!!! Kama jibu ni ndio, kwanini aaminike kwa kile anachokisema? Kama jibu ni hapana, je anauwezo wa kujenga hoja kuwashawishi watu vinginevyo???
 
Huyu Binti ni kama Joka La Kibisa tuu wala hana hata Sumu Msiogope Mtu yeyote anayetoka Upinzani na Kuhamia CCM amekufa Kisiasa kule anaenda kula tuu
George Saitoti aliwahi kumtukana Eugine Wamalwa Kuwa yeye ni Kahaba wa kisiasa baada ya kuwa na uanachama wa vyama7 tofauti ni wakati huo huo ni Waziri kwenye Serikali kuu sasa huyu Binti ni kitu kidogo sana hii kulalamika huku ndo kunaendelea kuimpandisha Chart kijinga
 
Wakuu nimekuwa nikifuatilia mtiririko wa matukio tangu kuibuliwa kwa hoja ya masalia hadi kufukuzwa na hatimaye kufikia hatua ya kuhamia chama tawala baadhi ya masalia akiwepo Juliana na Mwampamba. Kuibuka kwa ile hoja ni jambo ambalo japo lilijadiliwa sana, chanzo chake ni tata. Waliohamia CCM ni wawili; Juliana na Mtela lakini anayesikika zaidi ni huyu dada. Awali alisema yeye bado ni BAVICHA na hautambui utenguzi uliofanyika. Mara tukasikia yuko CCM na kapokelewa na Rais! Akiwa yeye na mwenzake. Mara anatoa kauli kuwa yeye ni mzawa wa Ubungo na yuko tayari kupambana na Mnyika.

Niseme tu kwamba kazi aliyotumwa sio kwamba ameikamilisha. Ndio kwanza inaanza. Huyu ni Delila. Ni mzuri wa sura na umbo lakini ana akili ya nyoka. CHADEMA itambue yafuatayo;
1. Safari ya Juliana kuzunguka Tanzania nzima kueneza sumu dhidi ya chadema ndio imeanza.
2. Juliana ni hatari kuliko Mwigulu na Nape.
3. Juliana ana hasira za kweli (japo ni kwa upuuzi wake) juu ya CHADEMA na viongozi wake.
4. Juliana atakachoomba toka CCM kwa ajili ya kuikandamiza cdm atapewa. Kumbuka huyu ni Delila.
5. Watu watavutika kumsikiliza huyu binti kwa kuwa ni mwanamke na ana mvuto. Atajenga huruma kwa wavivu wa kufikiri na wepesi wa kusahau.
6. Kwa bahati mbaya kila atakachosema sasa na baadaye kitakuwa habari, hivyo athari yake si ndogo.

CHADEMA watambue sasa kuwa hawajaondoa tatizo bali wamezaa tatizo. Wamezaa si kwa kosa lao bali wakati mwingine inatokea tu. Wajipange katika kudhibiti athari zitakazotokana na kauli za huyu msichana. Historia isijeandikwa kupitia sumu ya huyu mtoto na kamwe asipuuzwe. Harakati zake kipindi cha masalia na PM7 dhidi ya CHADEMA zinajulikana, nazo zilikuwa za faragha na ziliathiri chama. Sasa hizi za hadharani nazo zikipuuzwa si balaa?

Mkuu uko sahihi lakini mimi ninamaono tofauti kidogo. Kwa mtu mwenye uelewa mdogo juu ya Siasa za Tanzania ataweza kudanganyika. Nionavyo mimi Tanzania sasa hivi watu wanauelewa mpana sana. CCM wametuhadaa kwa wakati fulani lakini sasa pamoja na masalia haya wananchi wanajua huyu binti yuko katika kuchumia juani na kuwa karibu na Mh JK kwa jina la kukiangamiza chama cha CHADEMA jambo ambalo ni kinyume chake. Mimi kila anapokitusi Chama cha CHADEMA ndiyo kwanza ananiimarisha. Anakipaisha zaidi tofauti na anavyodhani.
"Mwanamke mpumbavu hubomoa ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe" Biblia
 
Mtoa mada umevurugwa, unataka kuuaminisha umma kuwa,kutolewa kwa shonza cdm ni kukiua chama, uhatari wa shonza unaupima kwa yeye kupokelewa na rais ccm?

Mada nyingine ni kuleta uchuro tu humu ndani, nachokiona nikuwa,shonza ataenda kuwa chakula ya wakubwa na kutajwa tajwa kwake kutawafanya maccm wenye uchu na utupu watake kumjua kiundani zaidi.
 
Ni tahadhari maana hata mbuyu ulianza kama mchicha.
Tahadhari sawa, lakini umemu-overstimate sana yule binti.

Unajua wapumbavu ni workshop ya Ibilisi, so kwa vile yeye ni mpumbavu watatmtumia kwa mambo ya kipumbavu tu....take it from me. Swali ni je utaogopa mpumbavu akifanya upambvu wake?
 
Tahadhari sawa, lakini umemu-overstimate sana yule binti.

Unajua wapumbavu ni workshop ya Ibilisi, so kwa vile yeye ni mpumbavu watatmtumia kwa mambo ya kipumbavu tu....take it from me. Swali ni je utaogopa mpumbavu akifanya upambvu wake?
labda nikuulize. Kwa yale yote aliyokuwa akiongea yana hekima? Kuna sababu ya kutoyahofia?
 
Back
Top Bottom