Mimi naamini ni wakati wa watanzania kuamka na kutaka mabadiliko,Msaliti wa chama cha upinzani chenye nguvu si msaliti wa chama hicho bali ni msaliti wa watanzania wote
Hebu tuangalie historia:
CDM ni chama cha tatu cha upinzani kuibuka kuwa na nguvu kisiasa ,ilianza NCCR-Mageuzi mwaka 1995,wakatokea wasaliti chama kikaanguka,tukadhani imeanguka NCCR.
Ikafuatia CUF wakatokea wasaliti CUF ikaangua uchaguzi mkuu 2000 japo mbinu za vitu vya ncha kali zilitumika.
Na katika kuanguka kwa vyama hivyo tunaoendelea kuumia ni sisi watz wa hali ya chini,mara hii ni CDM nayo nionavyo mimi mbinu chafu zimeanza ili nayo ianguke.
Hivi watz kwa nini tusishtuke tukasema hapana kwa wasaliti wanaotaka tuendelee kuteseka huku wao wakila maisha.
Tusitegemee mabadiliko ya msingi kama hatutabadilisha serikali iliyoko madarakani,na kuibadilisha ni kukiunga mkono chama cha upinzani chenye nguvu na mvuto kwa taifa zima.
Juliana sonza ni mmoja ktk mamilioni ya watz,tuchukulie ni unyasi mmoja umedondoka kutoka paa la nyumba iliyoezekwa na nyasi,ni muda muafaka wa kusema 'No' kwa Juliana sonza kama tunavyosema hivyo kwa magonjwa ya ukimwi ili taifa letu lisonge mbele.
JULIANA AMEOMBA MSAMAHA KWA MAFISADI!! KWANGU HII INAMAANISHA:ALIKUWA AMEPOTEA ALIPOAMUA KWENDA KUPIGANIA WATANZANIA,SASA AMERUDI ILI KUWAPONZA WATANZANIA.Huu si wakati wa kucheka ni wakati wakuonyesha msimamo wa kupingana na fikra za ubinafsi uliovaa ngozi za kijamaa.
........
Mifano hufundisha zaidiLakini mbuyu sio mchicha.
Hata kama ni juha hawezi kupuuzwa katika wakati kama huu. Atasikilizwa na majuha wenzie watakaomwamini. Mwisho wake ni upotoshaji.Kama angekuwa hana lolote msingehangaika naye!
Chama
Gongo la mboto DSM
Unategemea madhara yaonekane kama mafuriko. Siasa haiko hivyo ndugu. Propaganda zinakula ufahamu wa watu kama kansa.Mkuu, binafsi ninaona kwamba anatapataap tu na hana lolote. Labda ungesema kwa mifano, ni lipi alilolisema mpaka sasa limekiuwa na athari kwa CDM?
Huyo ni mchumia tumbo tu, anajua kwa kuwa CCM wanapenda ushabiki wanaweza wakampa pesa za kuzunguka TZ kuelezea wanachofikiria kitaweza kuibomoa CDM.
Wakuu nimekuwa nikifuatilia mtiririko wa matukio tangu kuibuliwa kwa hoja ya masalia hadi kufukuzwa na hatimaye kufikia hatua ya kuhamia chama tawala baadhi ya masalia akiwepo Juliana na Mwampamba. Kuibuka kwa ile hoja ni jambo ambalo japo lilijadiliwa sana, chanzo chake ni tata. Waliohamia ccm ni wawili; Juliana na Mtela lakini anayesikika zaidi ni huyu dada. Awali alisema yeye bado ni bavicha na hautambui utenguzi uliofanyika. Mara tukasikia yuko ccm na kapokelewa na Rais! Akiwa yeye na mwenzake. Mara anatoa kauli kuwa yeye ni mzawa wa Ubungo na yuko tayari kupambana na Mnyika.
Niseme tu kwamba kazi aliyotumwa sio kwamba ameikamilisha. Ndio kwanza inaanza. Huyu ni Delila. Ni mzuri wa sura na umbo lakini ana akili ya nyoka. Chadema itambue yafuatayo;
1. Safari ya Juliana kuzunguka Tanzania nzima kueneza sumu dhidi ya chadema ndio imeanza.
2. Juliana ni hatari kuliko Mwigulu na Nape.
3. Juliana ana hasira za kweli (japo ni kwa upuuzi wake) juu ya cdm na viongozi wake.
4. Juliana atakachoomba toka ccm kwa ajili ya kuikandamiza cdm atapewa. Kumbuka huyu ni Delila.
5. Watu watavutika kumsikiliza huyu binti kwa kuwa ni mwanamke na ana mvuto. Atajenga huruma kwa wavivu wa kufikiri na wepesi wa kusahau.
6. Kwa bahati mbaya kila atakachosema sasa na baadaye kitakuwa habari, hivyo athari yake si ndogo.
Chadema watambue sasa kuwa hawajaondoa tatizo bali wamezaa tatizo. Wamezaa si kwa kosa lao bali wakati mwingine inatokea tu. Wajipange katika kudhibiti athari zitakazotokana na kauli za huyu msichana. Historia isijeandikwa kupitia sumu ya huyu mtoto na kamwe asipuuzwe. Harakati zake kipindi cha masalia na PM7 dhidi ya cdm zinajulikana, nazo zilikuwa za faragha na ziliathiri chama. Sasa hizi za hadharani nazo zikipuuzwa si balaa?
Hata kama ni juha hawezi kupuuzwa katika wakati kama huu. Atasikilizwa na majuha wenzie watakaomwamini. Mwisho wake ni upotoshaji.
mtu mmoja hawezi kuyumbisha chama cha watu milioni 40 banaaa
Kama angekuwa hana lolote msingehangaika naye!
Chama
Gongo la mboto DSM
Ni tahadhari maana hata mbuyu ulianza kama mchicha.
Majuha wapo ccm. Kuondoka kwa huyu binti ni faraja yenye tahadhari
Wakuu nimekuwa nikifuatilia mtiririko wa matukio tangu kuibuliwa kwa hoja ya masalia hadi kufukuzwa na hatimaye kufikia hatua ya kuhamia chama tawala baadhi ya masalia akiwepo Juliana na Mwampamba. Kuibuka kwa ile hoja ni jambo ambalo japo lilijadiliwa sana, chanzo chake ni tata. Waliohamia ccm ni wawili; Juliana na Mtela lakini anayesikika zaidi ni huyu dada. Awali alisema yeye bado ni bavicha na hautambui utenguzi uliofanyika. Mara tukasikia yuko ccm na kapokelewa na Rais! Akiwa yeye na mwenzake. Mara anatoa kauli kuwa yeye ni mzawa wa Ubungo na yuko tayari kupambana na Mnyika.
Niseme tu kwamba kazi aliyotumwa sio kwamba ameikamilisha. Ndio kwanza inaanza. Huyu ni Delila. Ni mzuri wa sura na umbo lakini ana akili ya nyoka. Chadema itambue yafuatayo;
1. Safari ya Juliana kuzunguka Tanzania nzima kueneza sumu dhidi ya chadema ndio imeanza.
2. Juliana ni hatari kuliko Mwigulu na Nape.
3. Juliana ana hasira za kweli (japo ni kwa upuuzi wake) juu ya cdm na viongozi wake.
4. Juliana atakachoomba toka ccm kwa ajili ya kuikandamiza cdm atapewa. Kumbuka huyu ni Delila.
5. Watu watavutika kumsikiliza huyu binti kwa kuwa ni mwanamke na ana mvuto. Atajenga huruma kwa wavivu wa kufikiri na wepesi wa kusahau.
6. Kwa bahati mbaya kila atakachosema sasa na baadaye kitakuwa habari, hivyo athari yake si ndogo.
Chadema watambue sasa kuwa hawajaondoa tatizo bali wamezaa tatizo. Wamezaa si kwa kosa lao bali wakati mwingine inatokea tu. Wajipange katika kudhibiti athari zitakazotokana na kauli za huyu msichana. Historia isijeandikwa kupitia sumu ya huyu mtoto na kamwe asipuuzwe. Harakati zake kipindi cha masalia na PM7 dhidi ya cdm zinajulikana, nazo zilikuwa za faragha na ziliathiri chama. Sasa hizi za hadharani nazo zikipuuzwa si balaa?
Unategemea madhara yaonekane kama mafuriko. Siasa haiko hivyo ndugu. Propaganda zinakula ufahamu wa watu kama kansa.
Ni tahadhari maana hata mbuyu ulianza kama mchicha.
Mwogope Mungu wewe. Wavivu ni hao wanaotaka madaraka kwa njia za mkato na wakikosa basi wanaanza kumwaga sumuMleta Mada ni mvivu wa kufikiri, yaani Juliana Shonza kwa mawazo yako anaweza kumshawishi! Wewe ni mmoja wao wa masalia au ni magamba!