Juliana Shonza, Mtela Mwampamba wahamia CCM...

Juliana Shonza, Mtela Mwampamba wahamia CCM...

Tuache ubishi, hii issue ni SCUD kwa CHADEMA. Ni pigo la shoka. Vumilieni , pengine CHADEMA wamrubuni Nape ku-even the score!!!!
Kaka hapo hakuna Jeraha CDM. Bali ni Jeraha kwao kwa vile walichopania kufanya hakijafanikiwa 100%. Ndio maana unawaona wapo na nyuso za majonzi wakati walitakiwa kuwa na furaha kwa sababu wanalazimisha mioyo yao kufanya vile wasivotaka. Sisi wenzine humu ni Wakali wa kuwasoma mambulula kama hao.
 
Taarifa zilizopatikana muda huu ni kwamba JUliana Shonza na Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la mbozi mashariki(MTELA ALLAM MWAMPAMBA) wamehamia CCM NA KUPOKELEWA NA MWENYEKITI WA CCM TAIFA RaisKIKWETE Tukio la kuwapokea vijana hao limefanyika Dodoma mbele ya Rais wa nchi (MWENYEKITI WA CCM TAIFA) Mh. Jakaya Mrisho Kikwete. Vijana hao ambao wameteka mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kwa muda mrefu sasa, Wamepewa nafasi ya kutoa ushuhuda wa kile kinachofanyika ndani ya CHADEMA. Kila mmoja ametoa ushuhuda wake kadri alivyotendewa na yanayotendeka ndani ya CHADEMA. Mapokezi yao yamekuwa makubwa sana kutokana na kuunganishwa na shughuli zingine za kichama zinazomalizika muda si mrefu. Taarifa zaidi itakujia nikifanikiwa kupata VIDEO nitaiweka, Dr J.Kikwete awapokea rasmi muda huu,,!!
543667_10200318953750526_1713528751_n.jpg
​
Sasa mbona wamenunaa kwani wamelazimishwa? Pole yao bora wangeenda CHAUMA!!
 
Wana bodi
Hapa hakuna cha Scud kwa Chadema. If anything ni Scud kwa CCM. Sababu hizi hapa:

-Chadema walimfukuza Shonza kwa madai ya kutumiwa na CCM. Sasa Shonza kahamia CCM. Mwenye credit ni Chadema siyo CCM.

-Muda mwingi CDM imedai kuwa CCM inapandikiza mgogoro ndani ya CDM. CCM wamekuwa wanakana. Shonza na mwenzake wameenda CCM. Hapa CCM kakamatwa ugoni. Kwa maneno mengine CCM ni sponsor wa "umalaya" huu wa kisiasa.

-Inaeleweka na kukubalika mwana CCM kuhamia upinzani na huo si "umalaya" wa Kisiasa. Haikubaliki na haieleweki kwa mpinzani kuhamia CCM. Kwa hili Shonza si makini, CCM si makini, lakini CDM ni smart.

-Kazi ya kupokea wanachama wanaohamia vyama vingine baada ya kusaliti vyama vyao, huachiwa makada wadogo isipokuwa kama anayehama ni nyangumi wa siasa. JK kumpokea Shonza ameshusha hadhi yake iliyokuwa imebaki ndani ya chama. Usaliti wa Shonza hauwezi kuishia CDM. Wasaliti hupokelewa na makada waliowatuma, siyo Mwenyekiti wa chama labda kama aliwatuma yeye kusaliti.

Wengine ongezea sababu nyingine maana ni nyingi mno. Kwa hili CDM wameramba dume na hata CCm wamewapa credit bila kujua.
 
Mahitaji ya tumbo yanapozidi uwezo wa kufikiri. Hawa vijana sidhani kama kweli wanaipenda CCM kiasi hiki au kuichukia CDM kiasi cha kuihama. Tatizo hapa ni tumbo aka njaaa kali.
Baada ya kujiunga CCM nini kifuatacho ITV? Mwampamba atagombea ubunge na mwenyekiti wa chama wa mkoa wa Mbeya bw. Zambi? Au ndoo ndoto zake za kuwa mbunge amezizika rasmi?
 
Makamanda, japo ni mara chache kucoment humu, lakini leo imenibidi sana baada ya kuona mnatumia sana TAFSIDA kuhusu Juliana na Mwampamba. Hawa siyo kwamba wamehamia CCM ni kwamba leo wamejionesha rasmi kuwa siku zote wao ni CCM na walikuwa wanafanyia kazi CCM ila baada ya Maombi ya watanzania kuzidi juu ya wale wanaokihujumu chama kuumbuka, imebidi waondoke haraka kabla hawajaumbuka. Ni kama unavyomwombea mgonjwa mwenye mapepo, kuna wakati mapepo yanagoma mapaka kuwe na moto wa ziada, hawa wameshindwa maombi ya nguvu ya umma. wamekimbia na washindwe na kulegea. Muda kidogo tu, ukombozi utapatikana.
Taarifa zilizopatikana muda huu ni kwamba JUliana Shonza na Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la mbozi mashariki(MTELA ALLAM MWAMPAMBA) wamehamia CCM NA KUPOKELEWA NA MWENYEKITI WA CCM TAIFA RaisKIKWETE

Tukio la kuwapokea vijana hao limefanyika Dodoma mbele ya Rais wa nchi (MWENYEKITI WA CCM TAIFA) Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.

Vijana hao ambao wameteka mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kwa muda mrefu sasa, Wamepewa nafasi ya kutoa ushuhuda wa kile kinachofanyika ndani ya CHADEMA. Kila mmoja ametoa ushuhuda wake kadri alivyotendewa na yanayotendeka ndani ya CHADEMA.

Mapokezi yao yamekuwa makubwa sana kutokana na kuunganishwa na shughuli zingine za kichama zinazomalizika muda si mrefu.

Taarifa zaidi itakujia nikifanikiwa kupata VIDEO nitaiweka, Dr J.Kikwete awapokea rasmi muda huu,,!!




543667_10200318953750526_1713528751_n.jpg

​
 
Mkuu Ritz
Makamanda wanatuletea zile hadithi za sizitaki mbichi hizi! Siku za karibuni walipiga debe waondoke leo wameondoka kelele haziishi! Siasa za Chadema mashaka matupu!!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Sema wamerejea kwao baada ya mission waliyotumwa ku fail. Aibu kwao na magamba wote.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
MTELA MWAMPAMBA A.K.A GANZII!!! mtu asiyejua njia hawezi kupotea njia ..njia yoyote apitayo itamfikisha sehemu aliyokusudia kufika ....FAREWELL Brother
 
Wameenda kunako wafaa, kwenye siasa chafu na majungu, msichana ukivua chupi unapewa speacial seat,uwaziri au kuingizwa cc kama ...... Huyu binti ajiandae kuhemeshwa.
 
sias ni mpira unaodunda dunda kama kitennesi mara ccm mara chadema mara cuf mar.........
 
Wamejiabisha. Yamethibitika kuwa walitumwa tena na uongozi wa juu. Hongera CDM kuwatambua mapema.Njaa kali huyo binti namuonea huruma.
 
a woman of her calibar, is poisonous!! naona kama hajafunga vizuri kifungo cha shati, kama upo karibu yake msaidie pini, maana yupo na mkulu hapo na kesho ni jumatano ya majivu!!
 
Hivi karibuni Utasikia Mtela kapigwa U.DC,wasipopewa HAWATASIKIKA KABISA.njaa mbaya.
 
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Kikwete katika picha ya pamoja na comrade Mangula,Juliana Shonza, Mwampamba na Kinana

attachment.php
 

Attachments

  • 8E9U8493.JPG
    8E9U8493.JPG
    133.6 KB · Views: 3,328
Back
Top Bottom