Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Wakuu,

Nani ana jukumu la kuweka mazingira ya shule safi? Ni walimu, wanafunzi au watu maalum wa kufanya usafi?

Shule hasa za serikali wanafunzi ndio huwa wanakuwa na jukumu la kufanya usafi kwenye mazingira ya shule kwa kufagia uwanja, ofisi za walimu, kusafisha vyoo na hata wakipewa adhabu zinakuwa za kusafisha ama kulima kwenye maeneo ya shule na wakati mwingine huambiwa kufanya usafi hata kwenye nyumba za walimu.

Jambo hilo limekuwa likileta msuguano kati ya wazazi na walimu, na tukio la hivi karibuni mzazi kaenda kumpiga mwalimu sababu ya kumchapa mwanafunzi aliyekataa kudeki darasa.

Sasa je, nani ana jukumu la kufanya usafi kwenye mazingira ya shule?
 
Hilo ni jukumu la wanafunzi maana ni sehemu ya kujifunza pia, wazazi wa siku hizi ni changamoto sana mtoto akifanyashwa usafi kidgo mbio kwenda kusema kwa Baba/mama na li mzazi linakuja mbio mbio kutukana walimu, unakuta toto la kike Lina miaka 13 lakin haliwez kuosha vyombo, kufua Wala kusafisha chumba chake.
 
Kufagia uwanja, madarasa na kudeki, kumwagilia bustani ni jukumu la WANAFUNZI!
Kusafisha vyoo kwa shule za msingi watafute watu MAALUM!
Kusafisha vyoo shule za sekondari na Advance ni jukumu la WANAFUNZI!
Kuosha vyombo vya walimu ni jukumu la WALIMU wenyewe..

Walimu wanaboa vyombo vyao vya kulia wanawatoa wanafunzi madarasani waoshe.
 
Wanafunzi ndiyo wanatakiwa kufanya usafi kwani ile ni sehemu ya elimu kwa huku kwetu.

Kwani usafi unachukua masaa mangapi ukizingatia idadi ya wanafunzi shuleni?

Kitu ambacho sikubaliani nacho ni kutumia wanafunzi kuwatumikia walimu, lakini kwa shuleni tu na waendelee kufanya usafi.
 
Sidhani kama tatizo lilikua mwanafaunzi kutokufanya usafi, lilikua ni mwalimu kuzidisha adhabu

Kuna shule ya private nilisoma tulikua tunalima, tunamenya ndizi za kupika, usafi wa mazingira yote tulikua tunafanya. Mimi hadi mikate nimeoka. Ila tulikua hatuzidishiwi adhabu, hakukua na malalamiko.

Walimu wasitumie mabavu, iwe kama kuwaelimisha.
 
Duh!! Mzazi kampiga Mwalimu kisa mwanae amepewa kazi ya kusafisaha mazingira halafu kesho toto kama hili likiwa halina nidhamu halimuheshimu wala kumsikiliza mtu yoyote kutokana na malezi mabovu alioyapata kutoka kwa wazazi wake mnashangaa
Mimi miaka ya themanini wakati nasoma sio usafi tu tulikuwa tunalima mpaka mashamba ya shule
 
Kufagia uwanja, madarasa na kudeki, kumwagilia bustani ni jukumu la WANAFUNZI!
Kusafisha vyoo kwa shule za msingi watafute watu MAALUM!
Kusafisha vyoo shule za sekondari na Advance ni jukumu la WANAFUNZI!
Kuosha vyombo vya walimu ni jukumu la WALIMU wenyewe..

Walimu wanaboa vyombo vyao vya kulia wanawatoa wanafunzi madarasani waoshe.
Hivi wewe upo nyumbani bint mkubwa wazazi wakisha kula vyombo waoshe wenyewe hivi wewe unaona inaingia akilini hiyo?
Tatizo kubwa kizazi hiki hakina heshima wala maadili kutokana na huu ukisasa uliopachikwa jina la haki sawa
 
Unamtoa mtoto darasani aje kuosha vyombo vyako wewe!? Uniform zilowe kipindi darasani kimpite?
Muda wa mapumziko aache kwenda kula na kurefresh mind akae akuoshee wewe vyombo!
Kwani kwao hafanyi kazi?
Utakuta mtoto yupo darasani mwalimu anamuita eti kaninunulie chips!
Mkiendelea na tabia zenu za kipuuzi mtaendelea kupigwa na wazazi wenye hasira kaliii.
 
Kufagia uwanja, madarasa na kudeki, kumwagilia bustani ni jukumu la WANAFUNZI!
Kusafisha vyoo kwa shule za msingi watafute watu MAALUM!
Kusafisha vyoo shule za sekondari na Advance ni jukumu la WANAFUNZI!
Kuosha vyombo vya walimu ni jukumu la WALIMU wenyewe..

Walimu wanaboa vyombo vyao vya kulia wanawatoa wanafunzi madarasani waoshe.
Naunga mkono hoja. Kuna shule ya msingi maeneo ya karibu na Gongo la Mboto Msambarauni nadhani kama sijakosea. Aisee vyoo vya ile shule vinatoa harufu ya mkojo kali sana. Hadi unashangaa watoto wanawezaje kutumia hivi vyoo? Usalama wao kwa upande wa magonjwa kama UTI ukoje?
 
Walimu wa shule za msingi hawajali watoto kabisaaaa, sanasana hizi shule za vichochoroni!
Niliposoma mimi tulikua tunachangia hela kila mwezi ya kufanyiwa usafi chooni kila mtu aliweza kuafford sababu ni Tsh200 kila mwezi.
 
Wakuu,

Nani ana jukumu la kuweka mazingira ya shule safi? Ni walimu, wanafunzi au watu maalum wa kufanya usafi?

Shule hasa za serikali wanafunzi ndio huwa wanakuwa na jukumu la kufanya usafi kwenye mazingira ya shule kwa kufagia uwanja, ofisi za walimu, kusafisha vyoo na hata wakipewa adhabu zinakuwa za kusafisha ama kulima kwenye maeneo ya shule na wakati mwingine huambiwa kufanya usafi hata kwenye nyumba za walimu.

Jambo hilo limekuwa likileta msuguano kati ya wazazi na walimu, na tukio la hivi karibuni mzazi kaenda kumpiga mwalimu sababu ya kumchapa mwanafunzi aliyekataa kudeki darasa.

Sasa je, nani ana jukumu la kufanya usafi kwenye mazingira ya shule?
Hausigeli
 
Back
Top Bottom