Marian Schools huduma ya chakula, usafi ni ovyo sana

Muite

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
2,348
4,807
Nimefuatilia kwa muda mrefu ubora wa shule za Marian hasa Marian Girls iliyopo Bagamoyo nikagundua kuwa ubora wao upo kwenye Masomo tu. Kuhusu huduma ya chakula ni duni sana Kulinganisha na Fedha wazazi wanazolipa ni mwendo wa harage mwanzo mwisho, chakula wanachokula hakina tofauti na wanachokula Tabora boys.

Pili ni kuhusu suala la USAFI, kwa kweli Marian girls wanatakiwa kuhakikisha Mazingira ya wanafunzi yanaendana na sifa ya Shule, kiukweli mazingira hayaridhishi hasa mabwenini na kwenye vyoo.

Halafu pamoja na kwamba watoto wanatakiwa kufundishwa usafi lakini isiwe ndio shule imefanya hao watoto kuwa ndio resources za kufanyia kazi, mzazi anapoamua kulipa fedha nyingi kwa ajili ya mtoto mjue pia anategemea kuwa maisha yake ya shuleni yatapata urahisi fulani, hii ya kuwatumia watoto 100% kusafisha vyoo sio sahihi, ni kwanini msiajiri watu kama wanavyofanya Precious blood, Bright future nk.

Kumbe ndio maana watu wanasema Marian haina kitu kikubwa zaidi ya umaarufu tu.
 
Halafu pamoja na kwamba watoto wanatakiwa kufundishwa usafi lakini isiwe ndio shule imefanya hao watoto kuwa ndio resources za kufanyia kazi, mzazi anapoamua kulipa fedha nyingi kwa ajili ya mtoto mjue pia anategemea kuwa maisha yake ya shuleni yatapata urahisi fulani, hii ya kuwatumia watoto 100% kusafisha vyoo sio sahihi

Joannah
 
Ndo shule za shirika la holy ghost fathers zilivyo, nimesoma mojawapo. Wanahamasisha sana kwenye kujitegemea nakumbuka kuna kipindi tulikua hadi tunamenya ndizi...

Hawadekezi mkuu niliposoma kulikua na viziwi nao walikua wanapigishwa kazi kama kawaida

Kwenye chakula sawa maarage kwa sana, ila sio kibaya kama cha kayumba aisee, wewe unachukia tu maharage. Halafu unashiba, usiposhiba unaenda kwa father lazima ushibe...
 
Back
Top Bottom